ar
Feedback
Swahili News

Swahili News

الذهاب إلى القناة على Telegram
2 742
المشتركون
-424 ساعات
-177 أيام
-10230 أيام
أرشيف المشاركات
Rahby Netanyahu kuja na madai ya uongo dhidi ya Lebanon

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa kwenye ajali baada ya basi la abiria kampuni ya Last Bullet lililokuwa l
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa kwenye ajali baada ya basi la abiria kampuni ya Last Bullet lililokuwa likitokea Tabora kuelekea Geita kupoteza mwelekeo na kuangukia mtaroni muda mfupi baada ya kutoka Stendi Kuu ya Mabasi Tabora Mjini. Jeshi la Polisi mkoani humo limesema linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na kumsaka dereva ambaye amekimbia.

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kiswahili, siku iliyotangazwa na UNESCO ili kutambua mchango wa lugha ya Kiswah
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kiswahili, siku iliyotangazwa na UNESCO ili kutambua mchango wa lugha ya Kiswahili katika kuunganisha watu, kukuza utamaduni, elimu na mawasiliano duniani. Unadhani ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa ili Kiswahili iwe lugha yenye ushawishi mkubwa zaidi duniani? Karibu tujadiliane kwenye kipindi cha Kurunzi Live.

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Viongozi wa NATO kutoka nchi 32 wanakutana Ankara, Uturuki, kujadili matumizi ya ulinzi na ushirikiano wa k
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Viongozi wa NATO kutoka nchi 32 wanakutana Ankara, Uturuki, kujadili matumizi ya ulinzi na ushirikiano wa kijeshi. Mkutano huo unafanyika huku Marekani ikishinikiza washirika wa Ulaya kuongeza bajeti za ulinzi na kubeba jukumu kubwa zaidi la usalama wa muungano huo. Vita vya Ukraine, hali ya Mashariki ya Kati na msaada wa kijeshi kwa Kyiv ni miongoni mwa ajenda kuu za mkutano huo.

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Upepo mkali uliokumba mkoa wa Hubei nchini China umesababisha taharuki baada ya kurusha vitu hewani na kuwa
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Upepo mkali uliokumba mkoa wa Hubei nchini China umesababisha taharuki baada ya kurusha vitu hewani na kuwalazimu wakazi kutafuta usalama. Tazama jinsi hali ilivyokuwa wakati dhoruba hiyo ilipopiga eneo hilo.#kurunzi 07.07.2026

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Mhariri wa gazeti la The Standard, Alex Kiprotich, amenusurika jaribio la kutekwa na watu wenye silaha akiw
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Mhariri wa gazeti la The Standard, Alex Kiprotich, amenusurika jaribio la kutekwa na watu wenye silaha akiwa njiani kuelekea kazini mjini Nakuru, nchini Kenya. Kufuatia ya tukio hilo, Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) imetaka uchunguzi wa haraka ufanyike, ikisema tukio hilo linaibua wasiwasi kuhusu usalama wa wanahabari nchini humo. Jaribio hilo limetokea siku chache baada ya Rais William Ruto kulikosoa hadharani gazeti la The Standard, huku mashirika ya kutetea haki yakieleza wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya utekaji kwa wakosoaji wa serikali.

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ China yafanya majaribio ya kombora la kisasa la JL-3 katika Bahari ya Pasifiki, hatua iliyozua wasiwasi kwa
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ China yafanya majaribio ya kombora la kisasa la JL-3 katika Bahari ya Pasifiki, hatua iliyozua wasiwasi kwa Marekani na washirika wake. Beijing yasema zoezi hilo ni sehemu ya mafunzo ya kawaida ya kijeshi. Je, jaribio hilo linaashiria nini kwa usalama wa kanda na dunia?#kurunzi 07.07.2026

Watu 506 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DR Congo, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani
Watu 506 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DR Congo, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani. Tangu kutangazwa kwa mlipuko huo Mei 2026, watu 1,561 wamethibitishwa kuambukizwa nchini humo, huku wawili wakifariki nchini Uganda.

Trump aongea na Zelensky na Putin

Swahili Times tunakutakia Sikukuu njema ya Sabasaba.
Swahili Times tunakutakia Sikukuu njema ya Sabasaba.

#NenolaSiku
#NenolaSiku

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Mamlaka nchini Tanzania zimeimarisha usalama huku makumi ya watu wakikamatwa kabla ya maandamano yaliyopang
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Mamlaka nchini Tanzania zimeimarisha usalama huku makumi ya watu wakikamatwa kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika leo, yanayodai mageuzi ya kidemokrasia. Jeshi la Polisi limetoa onyo kali dhidi ya maandamano hayo na kuongeza operesheni katika maeneo ya kimkakati. Hadi sasa hali inaripotiwa kuwa tulivu katika maeneo mengi ya Dar es Salaam na sehemu nyingine ambako polisi wameelekeza nguvu zaidi.

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Uhispania imeonyesha uimara wake kwa kuitoa Ureno na kumaliza safari ya Cristiano Ronaldo katika Kombe la D
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Uhispania imeonyesha uimara wake kwa kuitoa Ureno na kumaliza safari ya Cristiano Ronaldo katika Kombe la Dunia. Sasa macho yote yanaelekezwa kwenye robo fainali dhidi ya Ubelgiji, mechi inayotarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa. Nani ataendelea kufukuzia ndoto ya ubingwa?

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Mchporo wa Said Michael ukionesha maadhimisho a Siku ya Kiswahili Duniani (Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Mchporo wa Said Michael ukionesha maadhimisho a Siku ya Kiswahili Duniani (Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakiwa Paris, Ufaransa kuhamasisha matumizi ya lugha ya hiyo huku lugha rasmi ya kufundishia sekondari na vyuo vikuu ikiwa ni kiingereza) Na tujadiliane kwa pamoja.

️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Maswali matano ya Mwandishi wa BBC Omary Mkambara @loko_omi kwa @ramadhani_chobwedo nyota wa TRA United ana
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Maswali matano ya Mwandishi wa BBC Omary Mkambara @loko_omi kwa @ramadhani_chobwedo nyota wa TRA United anayetamaniwa na vigogo wa Ligi Kuu Tanzania. 🎥: @frankmavura