en
Feedback
Millard Ayo

Millard Ayo

Open in Telegram

BLUE BOY WA KISHUA Journalist Award winning TV/Radio Personality | Amplifaya @CloudsFMTZ |Journalist from Africa | I 💙 TIGO PESA APP | Bookings millard@millardayo.com www.youtube.com/watch?v=g3NCUIuMVI0

Show more
The country is not specifiedThe category is not specified
5 023
Subscribers
No data24 hours
No data7 days
No data30 days
Posts Archive
Mzigo mpya wa kijanja umeshuka ndani ya maduka ya @maxfashion_tz @gsmmall 🔥🔥Max Store's📍Max mlimani📍Max msasani📍Max salamander📍Arusha max TFA📍Dodoma max shoppers plaza📍Zanzibar max michenzani mall

Waziri wa OR-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwachukulia hatua za kinidhamu Watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo kuzorotesha utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za Halmashauri hiyo.Mchengewa amechukua uamuzi huo wakati wa ziara katika Wilaya ya Liwale ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Mchengerwa ameelekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa mujibu wa Kanuni ya 42 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022 inayoainisha kuwashusha vyeo, kukatwa mshahara kwa asilimia 15 kwa muda usiopungua miaka 3 pamoja na kufukuzwa kazi iwapo watabainika kufanya makosa hayo.Watumishi wanaotakiwa kuchukuliwa hatua hizo za kinidhamu ni Sisty Njau (Kaimu Mhandisi wa Wilaya), Damasi Mumwi (Mkuu wa Idara ya Maliasili), Mustafa Magembe (Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika), Vinsent Moyo (Mkuu wa Idara ya Ugavi na Ununuzi), Mohamedi Songolo (Mkuu wa Idara ya TEHAMA), Sadick Bakari Khatibu (Katibu wa Afya) pamoja na Tunu Mtamaha ambaye ni Afisa Ugavi na Ununuzi aliyehamishiwa Halmashauri ya Wilaya Kilwa.Waziri Mchengerwa pia ameelekeza kuanzia sasa Maafisa wote wenye kesi za rushwa na ubadhirifu wasihamishwe vituo vyao vya kazi mpaka mashauri yao yanapokamilika “Afisa yeyote mwenye kesi ya uhujumu uchumi au ubadhirifu wakati kesi yake ikiendelea ataendelea kuchunguzwa mienendo yake na hukumu yake ikitoka hatopewa tena jukumu la Ukuu wa Idara au Kitengo hadi mienendo yake itakaporidhisha”#MillardAyoUPDATES

Serikali imesema Jimbo la Mtama lililopo Mkoani Lindi litapewa kipaumbele katika uwekaji wa taa za barabarani ili kuruhusu usafirishaji kwa muda wote.Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema hayo leo September 18,2023 mbele ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati Rais aliposimama pamoja na Viongozi wengine kusalimia Wananchi katika Jimbo la Mtama ambalo Mbunge wake ni Nape Nnauye ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Baada ya Bashungwa kupewa nafasi ya kusalimia Wananchi na kumaliza salamu zake, Rais Samia amenukuliwa akimuuliza Bashungwa “Haujamuuliza Mh. Nape anazo taa za barabaarani?.. anasema hana taa na alikuomba” Baada ya kauli hiyo ya Rais , Waziri Bashungwa amesimama tena na kusema “Kwenye suala la taa Mh. Rais umetuelekeza Wizara ya Ujenzi, badala ya kununua vipandevipande, kwanza tuangalie standard bora ya kudumu lakini pia tuwe tuna mpango wa kufanya Bulk Procument (manunuzi ya vifaa kwa wingi) ili tukinunua kwa idadi kubwa ya taa tuwe tunapunguziwa bei, kwahiyo nikuhakikishie maelekezo yako ambayo umetupa Wizara ya Ujenzi, Mh. Nape atakuwa namba moja mzigo utakapoingia"Kuhusu ujenzi wa Barabara ya Newala - Mtama na kipanda cha Tandahimba - Mtama, Bashungwa amesema Wizara imeichukua na ipo kwenye vipaumbele kama alivyoagiza Rais Samia kuwa ifanyiwe upembuzi yakinifu.#MillardAyoUPDATES

Tayari washiriki wote 24 wameingia mjengoni hapo jana na siku ya leo itaruka show ya kwanza kutoka mjengoni.Ni mshiriki gani ambae Unatamani kujua siku yake ya kwanza ilikuwaje mjengoni??Tazama Bingwa Show Kila siku ya Jumapili hadi Ijumaa kuanzia saa 4:00 Usiku Kupitia @tv3tz Ndani Ya Kisimbuzi Cha @startimestz#TukutaneMjengoni#BingwaSeason2#NajiminiKinoma#Tv3Tanzania Katika kisimbuzi cha @startimestz CH 131 (Antena) na CH 197 (Dish)Powered By @quantuminfinity.hq @coca_cola_tanzania @startimestz @robby_one_pharmacy @matangazo.co.tz

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba amesema sasa ni wakati sahihi kwa Serikali kuweka somo linalofundisha Mila na Desturi za kitanzania Shuleni ili Watoto wakuwe na kufahamu mambo yanayohusu Jamii yao. Kishimba amesema kumekuwa na tamaduni za kigeni ambazo Watoto wamekuwa wakikuwa na kuzikuta ambazo zinapelekea kuharibu makuzi ya Watoto hasa wanaokulia Mjini na kuwafanya kuamini mambo ambayo sio ya kwao na kupelekea kuwepo kwa Wagonjwa wa Afya ya Akili kutokana na msongo wa mawazo.Kishimba amesema hayo katika mahafari ya kwanza Tanzania ya Chuo cha Waganga wa Jadi cha Modesta kilichopo Kagongwa Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga ambapo Wanafunzi zaidi ya 400 wamehitimu mafunzo ya dawa asili ya Modesta baada ya kusoma kwa mwaka mmoja na Watu zaidi ya 1000 wamehudhuria mahafari hayo “Mjini wanaugua ugonjwa wa msongo wa mawazo mbona kijijini hawaugui huo msongo wa mawazo kwanini tusiende kwao kuwauliza lazima na sisi Watu wa mile tujitetee kwasababu maisha yetu ni mazuri zaidi ila tunashambuliwa mno kuwa ni mila potofu, hapa hakuna mila potofu ni uongo kama ingekuwa ni mila potofu ng’ombe angelala nje sisi tunalala ndani?, mbona sisi wa Mjiji Wajuaji na tuna mageti na ndani hakuna chakula”#MillardAyoUPDATES

Kijana Mkacha Mohamed (35) Mkazi wa Kiteto Manyara amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki wakati akiwakimbia Askari Polisi baa
Kijana Mkacha Mohamed (35) Mkazi wa Kiteto Manyara amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki wakati akiwakimbia Askari Polisi baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi huku mwenzake Nassibu Yahaya(23) akikamwatwa akiwa na bunda 250 ambazo ni Kilo 119 za mirungi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara George Katabazi amesema tukio hilo limetokea September 17,2023 katika Kijiji cha Namelock Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.Katika tukio jingine RPC Katabazi amesema Richard Zahab (60) Mkazi wa Ngage Simanjiro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi misokoto 897 “Nitoe wito kwa Wananchi wa Manyara kuacha mara moja biashara haramu ya dawa za kulevya kwani lazima tutawakamata na kuwafikisha Mahakamani, niwaombe Wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusu uhalifu na Wahalifu ili tuweze kuzifanyia kazi na kuhakikisha tunatokomeza biashara ya dawa za kulevya"#MillardAyoUPDATES

UEFA Umerudi ⚽️⚽️⚽️, na hakuna sehemu nyingine yoyote unayoweza kupata mechi hizi isipokua @dstvtanzania.Hakikisha unalipia kifurushi chako kwa kupiga *150*53#, na Kama Huna DStv jiunge Sasa kwa ofa ya 59,000/= tu kwa kupiga 0659 070707.#SokaPromax#UCL #Unakosaje

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewasili Jijini New York nchini Marekani ambapo anatarajia kumwakilisha Rais w
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewasili Jijini New York nchini Marekani ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa (UNGA78). Makamu wa Rais ataongoza pia Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano mbalimbali inayohusu Mazingira, Uchumi, Afya, Maji, Demokrasia na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo Tanzania imealikwa na Nchi Washirika, Taasisi za kimataifa na Asasi binafsi. Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani September 21, 2023.#MillardAyoUPDATES

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Nachingwea – Ruangwa - Nanganga, sehemu ya Ruangwa – Nanganga (KM 53.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami, leo September 18, 2023.Rais amesema Serikali ya awamu ya sita imejipanga kujenga miundombinu ya Mikoa ya Kusini ili kurahisisha usafirshaji wa mazao na kukuza uchumi wa Mikoa hiyo na kuwataka Wakandarasi wakamilishe ujenzi wa barabara hiyo kwa wakati."Niwaombe Wakandarasi na Wasimamizi waende kwa kasi sana lakini nipongeze TANROADS Mkandarasi na wengine kwa hatua ambayo imeshafikia na kwetu sisi Serikali mafedha yapo tunasubiri certificate ziletwe tulipe kazi ziendelee"Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta, amesema Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ni China 15th Group kwa thamani ya Tsh. bilioni 50.3 na jumla ya Tsh. bilioni 1.1 ikiwa ni sehemu ya ongezeko la thamani na kutumika kulipa fidia ya mali na ardhi kwa Watu walioathirika na ujenzi kwa mujibu wa Sheria “Ujenzi mpaka sasa tumefikia 71% na mapaka sasa tumeshalipa jumla ya shilingi Bilioni 20.7 na zilizobaki tunaendelea kulipa kwa utaratibu uliowekwa"#MillardAyoUPDATES

Ready to hit the sports scene in style? Join the groove with @gsm.sportstz and let's turn those sports vibes up to 11! 🏀⚽️GSMSports:📍 GSM Mall Msasani📍 Gsm Sports Dodoma📍 Salamanda Tower📍 Mlimani City📍 Gsm.sports Pugu (Outlet)We're all about that OG life - Get your game on with the most authentic and original sportswear in town. 🔥💯 #OG #GSMSportsTz #GameOn"

Kufuatia uhaba wa maji katika Mji Mkuu wa Africa Kusini Johannesburg, Wasambazaji wa maji wamewataka Wakazi wa Jiji hilo na Vitongoji vyake kutumia maji kwa kiasi kwa kutumia dakika mbili kuoga na kuosha magari yao kwenye siku za wikendi pekee tena kwa kutumia ndoo huku wakiwasihi Watu kuepuka kumwagilia bustani na nyasi kwa maji safi.Kampuni ya Rand Water na Johannesburg Water ambazo zinasambaza maji zimesema matumizi makubwa ya maji kwa Wakazi wa Jiji hilo yanatatiza mfumo mzima na kusababisha maji kuzidi kupungua kwenye hifadhi yake hivyo zimewataka Watu kuokoa maji kwa kutoa pia taarifa kuhusu uvujaji wa maji.Johannesburg kwa sasa inapitia changamato ya uhaba wa maji inayotokea kila mwaka ambayo mara nyingi hutokea wakati wa kiangazi cha Afrika Kusini kati ya September na mwezi March, katika Wiki za hivi karibuni, baadhi ya Wakazi wa Jiii hilo na Taasisi kama vile Hospitali zimekosa maji na kusababisha Wananchi kupaza sauti wakieleza kutoridhika na hali hiyo.#MillardAyoUPDATES

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ‘Mcheza kwao hutunzwa’ hivyo ni lazima Serikali ipeleke maendeleo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi ili kumtunza kwa maendeleo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, kwakuwa kazi yake ya kuwatumikia Watanzania ni kubwa hivyo Serikali ni lazima ihakikishe nyumbani kwake kunakaa sawasawa.Akiongea na Wananchi wa Ruangwa leo Sept 18,2023 kwenye mkutano wa hadhara Ruangwa Mjini, Rais Samia amesema “Waswahili wanasema ‘Mcheza kwao hutunzwa’ kwanini tusimtunze Waziri Mkuu kwa maendeleo!?, lazima Serikali tumtunze Waziri Mkuu kwa maendeleo, Wadhifa wake ni Mkubwa kazi yake ni kubwa ya kushughulikia Tanzania nzima ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi ni kubwa mno lazima tuangalie nyumbani kunakaa sawasawa lazima tulete maendeleo Ruangwa”“Ruangwa ina fursa nyingi za kiuchumi yamesemwa hapa kilimo, madini, uvuvi, utalii, gesi na misitu mikubwa ya Lindi, kwa mambo yote haya ni lazima maendeleo yapatikane, Mungu ameumba Ruangwa na Mkoa wa Lindi na rasilimali zote hizi kama hazikuleta maendeleo sisi Viongozi tunapata dhambi, zimeumbwa ili zilete maendeleo na tutazitumia kuleta maendeleo ya Mkoa na Wilaya ya Ruangwa” “Mwaka huu bei ya ufuta na mbaazi ni nzuri lakini Waziri wangu huyu halali anahangaika kuipandisha bei ya korosho” #MillardAyoUPDATES

Kitu cha tambi nini..... sema AZANIA kiboko kabisa, sasa hivi hadi unga wa ngano wa kutengenezea tambi wanatusambazia.... 👏�
Kitu cha tambi nini..... sema AZANIA kiboko kabisa, sasa hivi hadi unga wa ngano wa kutengenezea tambi wanatusambazia.... 👏🏿