E-PLUS MEDIA
Відкрити в Telegram
1 307
Підписники
+124 години
-27 днів
-1330 днів
Архів дописів
1 307
#HABARI Mwanamke aitwaye Bugumba Misalaba mkazi wa Kijiji cha Nyakato, Kata ya Nyanguku Halmashauri ya mji wa Geita anayedaiwa alifariki miaka mitatu iliyopita ameonekana akiwa hai kijijini hapo jambo ambalo limesababisha mshangao mkubwa miongoni mwa wananchi wa eneo hilo.
Wakizungumza ndugu mwanamke huyo wamesema ndugu yao alifariki September 15, 2020 kwa ajali baada ya kugongwa na gari akiwa kwenye baiskeli akitoka Sengerema mkoani Mwanza kumtembelea baba yake mdogo na kupelekea kifo chake palepale.
"Ni kweli dada yetu huyu Bugumba Misalaba alifariki mwaka 2020 kwa ajali eneo la Igaka na kusababisha kifo chake hapohapo ni kweli tulipata taarifa tukaenda tukakuta amefariki kweli tukamsafirisha mpaka nyumbani, tukafanya mazishi toka 2020 mpaka tarehe 1 ya mwaka huu 2024 ndiyo tukapata taarifa kuwa ndugu yetu amepatikana hapa senta tulipofika tukakuta kweli ni yeye" amesema mmoja wa ndugu yake.
Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe, alifika eneo la tukio akiambata na kamati ya ulinzi na usalama na kuwataka wananchi wa eneo hilo kuacha tabia zenye viashiria vya imani za kishirikina.
Source #EastAfricaRadio
1 307
DJ AFRO mwenyewe ndo huyu hapa
"Neno lipi unalijua lazima atamke akiwa anatafsir movie..
1 307
Kwanini???
Mwanzoni wa ule wimbo ndiyo utaelewa vizuri nini maana ya msemo, pale Bwana misosi aliposema,
(Misosi Nitoke vipi nafanya tafiti ya ndani
Sitaki ulimbukeni nataka kuuza duka
Na hawa ni baadhi ya waliopanda chati Nchini
Na huu ni upeo wangu tu
Nitoke namna gani
Nasema upeo wangu tu
Nitoke namna gani)
Hata kwa akili za Chekechea utabaini Bwana misosi katika ule wimbo ni swali ambalo anatuuliza Mashabiki, na ndiyo maana anatutajia wasanii ambao tumeshazisikia kazi zao, na yeye anauliza atoke vipi? Bahati nzuri nusu ya wasanii ambao amewataja katika ule wimbo, wamempa kampani kwa kuonekana katika ile video, lakini pia hakuwataja kwa ubaya, hata yeye Afande Sele ametajwa katika ule wimbo, Bwana misosi alisema,
(Afande mkuki moyoni
Morogoro ukamuingia) kwa namna ninavyojua mimi Afande ni jina la heshima ambalo mwanajeshi au askari yeyote anamwita mkubwa wake. Inalingana na neno la Kiingereza "Sir" Lakini ajabu Afande Sele hakuwa akijua hilo, na pia hakutaka hata kuelewa nini maana ya upeo wangu!!! Uzuri ni kwamba Bwana misosi alilijua hilo la kukosolewa na Afande Sele, Bwana misosi alikuja na majibu pale alipomwambia Afande Sele katika moja ya nyimbo zake wenye Kiitikio chenye kusema,
(Nikitunga nyimbo haina vina
We kaishi palipo na vina
Uganda Bongo na Kenya
Ninatoa Radha bila kubana)
Hakukuwa na marumbano ya muda mrefu kwa wasanii hawa wawili, lakini iliripotiwa kwenye vyombo vya habari, kuwa wawili hawa haziivi kabisa, na chanzo ilisemekana ni katika hizo nyimbo zao,
Na kama ilikuwa kweli maana yake nini???
Hapo hakuna jibu zaidi ya kusema, Afande Sele alivunja darasa ambalo alilitoa yeye mwenyewe katika wimbo wa mtazamo,
Nitoke vipi ya Bwana misosi haikuwa mbaya, na hata Mashabiki tuliipokea vizuri, na kupitia wimbo huo ambao ndiyo ulibeba jina la Albamu, ilipelekea Albamu hiyo kufanya vizuri sokoni, na jina la Bwana misosi likawa kubwa ndani na nje ya nchi, wote tuliona namna Bwana misosi alivyokuwa akifanya kazi na wasanii mbalimbali wa kutoka nje ya nchi, kama Uganda na Kenya,
Naaam Msomaji katika toleo lijalo ni zamu ya O Ten na Afande Sele, na nitagusia kuhusu Soggy Doggy, na Kama kutakuwa na nafasi nitamuunganisha na Madee,
Itaendelea
1 307
HUENDA HII IKAWA NDIYO SABABU
YA AFANDE SELE KUINGIA KWENYE BIFU NA BWANA MISOSI, SOGGY DOGGY, O TEN NA MADEE!!!
Kabla hujaanza kusoma vizuri, naomba kwanza urejee kichwa cha habari hapo juu, kielewe vizuri halafu ndiyo uendelee kusoma,
Binafsi ukija kwa mbele yangu na kunitupia swali la haraka, kutaka nikutajie wasanii watano ambao nawakubali sana,
Basi jina la Mfalme wa Rhymes (Afande Sele) litakuwa miongoni mwao,
Kwanini???
Afande ni miongoni mwa Wasanii ambao nawaelewa sana nyimbo zao, enzi za kutamba kwake kwenye gemu, Afande Sele alikuwa Balozi mzuri sana wa jamii ya watanzania,
Kwa sababu Mshikaji alikuwa anaimba nyimbo zenye kugusa jamii,
Mwenyewe katika kiitikio cha wimbo wa Ndugu Zangu anasema....
Napenda ndugu zangu
toka moyoni mwangu uuhh, siwezi idharau nchi yangu,
kutenga ndugu zangu
kwa iman yangu itakua dhambi mbele za mungu
Ndugu hao ambao Afande Sele amewaongelea katika wimbo huo, ni sisi Watanzania wenzake,
Ni wimbo mzuri sana ambao mtu ukiusikiliza unapata mambo mawili kwa wakati mmoja,
Kwanza kuelimika, wimbo huo unakuelimisha vizuri sana,
Pili burudani ambayo mtu unaipata wakati wa kuisikiliza ngoma hiyo, lakini pia Afande Sele kama binadamu ana kasoro zake, na moja ya kasoro yake kubwa, ni kupenda kuwapangia wasanii wenzake nini cha kuimba,
Kivipi???
Afande Sele anapenda kuzitoa kasoro nyimbo za wenzake, kitu ambacho alikuwa anakitaka Afande Sele kutoka kwa wasanii wenzake, watunge nyimbo zenye kugusa jamii kama vile yeye anavyofanya.
Hapa ndipo Mfalme huyo wa Rhymes anapokosea, na huenda ndiyo sababu ya kuingia kwenye bifu na baadhi ya wasanii wenzake,
Halafu kama hujui Afande Sele ni bingwa na mtaalamu kweli wa kuvunja darasa ambalo analitoa yeye mwenyewe, yaani Mshikaji anatoa wimbo uliyo na ujumbe wa kukemea jambo fulani, halafu yeye mwenyewe anakuja kutoa wimbo wa kufanya kile ambacho amekikemea katika wimbo wake wa kwanza,
Kivipi???
Nitakupa mfano ili twende sawa,
Nenda kasikilize wimbo wake wa Mtazamo, katika Verse yake Afande Sele anasema,
Asante Professor Jay
Majani na Ulamaa mmegusa n’napopataka
Nami kwenye mtazamo nina jambo nataka kuweka
Maana kila kukicha emcees wanaongezeka
Nasema very nice, yes rap kama dhehebu
Emcees kama wafuasi
Wingi wa wasanii unaonesha ni dini safi
Yaani imekubalika, waumini tuko wengi
Lakini bado nashaka
Sijapata uhakika, wote tumesadiki
Ama wengine ni fake mmetumwa kama mamluki
Maanake hamna maana
Mna-rap ili mradi rap, mistari imekosa vina
Yenye vina haina maana
Na kila mnapokaa mnapenda kusengenyana
Mnapenda kutetana na mnapenda kurumbana
Mimi naogopa sana
Kwa jinsi navyoelewa mwishoni mtatukanana
Ama inawezekana mwishoni mkaja chinjana
Na wote tunao-rap tuonekane hatuna maana
Wapi ilipo Taarab
Ilikuja kwa kishindo, hata wagumu walishausudu
Kwa ajili ya marumbano mwishoni ikafa kibudu
Shabiki piga simu, changia mawazo yako
Nani tutamlaumu, kama rap ita-cease kwa kuendekeza upuuzi
Nani tumchune ngozi, producer aliyerekodi
Ama labda DJ anaepiga kwenye kipindi
Wengi wanapenda rap, ajabu rap haiwapendi
Waungwana wanaiacha, wapumbavu hawaambiliki
Hivi kwani lazima tuwe wote wanamuziki
Mi nadhani ingetosha wengine mbaki ushabiki
Huu ni wangu mtazamo masela msijenge chuki
Hata na Majani, yoh
Unaona namna Afande Sele alivyosema, mimi nashika mistari yenye kusema,
(Mnapenda kutetana na mnapenda kurumbana
Mimi naogopa sana
Kwa jinsi navyoelewa mwishoni mtatukanana
Ama inawezekana mwishoni mkaja chinjana)
Katika mistari hiyo Afande Sele anaonekana ni kwa namna gani hafurahishwi na marumbano na kutetana, yeye ana hofu vitu hivyo huenda Baadaye watu wakaja kuchinjana,
Lakini upande wa pili kwenye wimbo wa Darubini kali, ni yeye Afande Sele anayaanzisha marumbano kwa kuwadisi Bwana misosi na O Ten, katika wimbo huo Afande Sele anamwambia Bwana misosi, "kuna vitu vya kuimba vyenye maana kila kona, na siyo nyimbo nzima anataja taja majina tu, tena kwa mistari isiyo na vina" Binafsi sijaona kosa la Bwana misosi katika ule wimbo wa Nitoke vipi,
1 307
🔰_| 𝗞𝗨𝗧𝗢𝗞𝗔 𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔 𝗦𝗖
Rais wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris Nchini Ufaransa, jana Desemba 3, 2023.
Eng Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.
Vilevile, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Eng Hersi kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa magoli 2-0.
1 307
Ameandika Bondia Hassan Mwakinyo juu ya kupigana na Bondia Twaha Kiduku
"Natukanwa sana Dm kua nimemtaka msena wa watu kwakua ameonekana ameshuka kiwango kwa siku za hivi karbuni lakini pia wanasema nimekua nikimuhofia"
"Cha kuwa kumbusha tu ni kuwa nyinyi ndio mumechelewa kujua kua uwezo wa msena wenu unafanya kazi pale akikutana na wapiganaji wa mfumo wake tu ‘ hajashuka kiwango kiasi cha kuonekana ni dhaifu ila aina ya wapiganaji anao kutana nao sasa ni standard quality ya dunia boxing skills ring IQ hawafanyi boxing ya kushindana ndio maana mnaona ame shuka lakini sio kweli’
"Mimi ni mmoja kati ya wapiganaji sirudii mfumo wa kupigana … tofauti ya mimi na hao naweza kufanya vyote I can box i can fight halafu naweza kukita ile kinoma noma 👊🏾 ikiwa utapenda tuonyeshane nani amenyonya vizuri kifua cha mama yake All in all
"Mnisamehe washabiki mlio kwazika na taarfa hii isiyo rasmi ila ningependa mjue ya kua sihofii kitu na pia sina mategeo na juu ya nilichosema ila kama hio itatokea basi itakuwa ni biashara ya kweli kweli na ndio itakua fight yake ya mwisho kucheza ngumi’ tafadhali sitegemei kupokea simu ya promoter akianza na ofa ya neno gari…."
1 307
HII HAPA SIRI INAYOFANYA BAADHI YA WANAMUZIKI WA INJILI WAKONGWE WAENDELEE KUWA JUU NA WENGINE KUDODA.
Ni wazi kuwa wanapotajwa wanamuziki wa Injili wanaofanya vizuri nyakati zote huwezi kuwaacha Bahati Bukuku, Rose Muhando, Martha Mwaipaja na Christina Shusho, hapa katikati wametokea wanamuziki wengi lakini hawa wameendelea kutajwa zaidi kwenye vinywa vya watu kwa zaidi ya miaka 10 hadi 20. Sijui ni kwanini ila nadhani ni Neema tu waliyojaaliwa.
Zamani wakati wanaanza, kazi zao zilikuwa zinasambazwa kwa njia ya kanda, tepu n.k habari zao zilikuwa zinapatikana kwenye Tv, Magazeti na Radio. Baadae Teknolojia ilikuja kubadilisha mambo ikabadili usambazaji wao wa kazi na sasa wanasambaza na kuuza kazi zao kupitia digital platforms za mitandao kama YouTube n.k
Hapa kidogo kuna utata wa kuendana na soko hili, ikumbukwe kwamba mitandao ya kijamii asilimia kubwa imejaa maovu, hata watu wanaoitumia kuna namna wamechangamka, mitazamo yao si kama ya miaka 10 iliyopita, wengi wao wanaenda zaidi na wakati kwa hivyo ili waweze kupenda kazi zako ni lazima na wewe uende kama wao wanavyotaka, hawataki kuona video za vitenge na mabazee ya Ki-nigeria, hawataki kuona una sura natural.
Wasikilizaji wa sasa wanataka kuona Mwimbaji amechachuka, amepodoka, wanataka kusikiliza nyimbo ambazo zina udunia kiasi na umungu kwa mbali, zina mdundo mzuri unaochezeka Klabu na sehemu nyingine za starehe, wanataka kuona Mwimbaji amevaa mawigi, miwani ikiwezekana hata nguo zake kidogo ziwe shagalabagala zisieleweke ni za kidini au kidunia, ndio maana sasa hivi hakuna utofauti wa video ya kidunia na kimungu, zote ziko sawa.
Sasa hapa ndipo pana mtihani na imekuwa ngumu wasanii wengi wa Injili kuuvuka, wengi wao wamejikuta wameangukia huko na ukishaangukia huko kutoka ni ngumu na asilimia kubwa utajiona upo sahihi. Ndio maana wasanii wengi wa sasa hivi hata wale wakongwe wananyoa minyoo ya ajabu, wanavaa suruali hata kwenye video zao, wanavaa nguo fupi zenye ukakasi, hata ukiangalia video zao zina ukakasi ndani yake, si Injili si Bongo Fleva.
Huenda shida si kupenda kwao, ila biashara yao inawataka wafanye hivyo. Mfano, we umetumia milioni mbili kushuti video alafu unapata hasara hata pesa yako inashindwa kurudi utafurahi? Alafu kesho unavaa kimpasuo kidogo, kasuruali kiasi, wimbo una maudhui ya kidunia kiasi alafu wimbo huo unakuingizia milioni 50 utaacha kutumia hiyo njia? Kwa akili na moyo wa kibinadamu ni ngumu sana ndio maana wengi wameangukia huko.
Kuna wachache ambao bado wanaishi kwenye misingi ya Injili, ingawa maisha yao hayawezi kuwa kama hawa walioamua kuifata dunia zaidi kwasababu huku duniani kuna pesa nyingi. Injili inapotea taratibu litabaki jina tu la Mziki wa Injili lakini Injili inayokusudiwa haitakuwepo. Ni kama walivyo wachungaji, Ule uchungaji wa kweli unapotea taratibu na pia ipo siku jina Mchungaji litaendelea kuwepo lakini ile dhamira ya uchungaji haitakuwopo.
HAPPY NEW YEAR 🙌
1 307
"Mdada wa mwaka 1990s unachukua video unatoa ulimi nje eti unajishebedua umekuwa nyoka? Haujioni kama umeshakuwa lishangazi? Mbona mnakosa aibu?"- Stong Icome
1 307
Miriam Odemba anayekadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 40 aanika muonekano wake wa mwaka 2024
1 307
🎙️ “MWAKA 2024 nitaendelea kufanya kama 2023 kuwashawishi watu. Nina furaha (kuwa Saudi Arabia) kwa sababu nilifanya uamuzi wangu binafsi kuja hapa na hakuna mtu aliyekuwa akiamini. Yaliyopita siyajali. Kwa sasa, kitu muhimu ni kwamba ligi imekuwa kubwa, wachezaji wakubwa wanataka kuja hapa kuja kucheza kwa sababu ligi imekuwa na ushindani. Dunia nzima kwa sasa inatazama ligi (ya Saudia), nawashauri tu wachezaji wakubwa waje, wanakaribishwa sana,” supastaa wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo.
1 307
PRESS || "Kwa mchezaji mwenye asili ya Tanzania na ana uwezo wa kuichezea timu ya Taifa ataitwa tu."
"Kuna wakati tumetoa uraia kwa mchezaji asiye na asili ya Tanzania "Kibu Denis" hakuna aliyezungumza sana, sasa ndio iwe kwa mjukuu wa mzee Kawawa? tena kama tumefuata sheria ya FIFA."
"Hakuna tatizo lolote na izingatiwe Tanzania haijawahi kuwa na ubaguzi, na haturuhusu hilo litokee, tulizubaa kwa Poulsen tena ni mdigo, sasa hivi anaichezea Denmark."
- Dokta Damas Ndumbaro Waziri mwenye dhamana ya michezo anazungumzia suala la wachezaji wengi wenye asili ya Tanzania kwenye timu ya Taifa.
.
.
.
