E-PLUS MEDIA
Открыть в Telegram
1 307
Подписчики
+124 часа
-27 дней
-1330 дней
Архив постов
1 307
Bondia @hassanmwakinyojr amewataka mapromota kuacha kumpigia simu, yeye na maeneja wake akidai kuwa hakuna promota mwenye uwezo wa kuandaa pambano na @twaha_kiduku
"Mapromota wadogo kwangu, nyie ni muhimu na mna maana kubwa sana kwangu. Lakini kwenye hili, wacheni kupiga simu kwangu na kumsumbua meneja wangu. Najua mna shauku na matumaini ya kibinadamu, lakini ukweli ni kwamba kati yenu hakuna mwenye uwezo wa kuandaa pambano hilo".
Nini maoni yako?
1 307
"Binafsi sitakuwa daraja la kumfikisha mtu kwenye hela ikiwa sina hela naifahamu thamani yangu na najua biashara ya ngumi ilivyo it’s really business na sio majarbio ya utajiri. Ikikosekana namna kabisa upo uwezekano mkubwa pia nikaliandaa mwenyewe kupitia promoshen yangu ya mwakinyo pros na bado tukapata tv ya kuonyesha ……Understood" ameandika Bondia Hassan Mwakinyo
1 307
Kama ulikua humjui vizuri Manara wacha nikufahamishe;-
K U Z A L I W A
Jina lake kamili anaitwa HAJI SANDE MANARA,
Amezaliwa January 18, 1976 nchini UHOLANZI,
Ambapo baba yake alikuwa akicheza soka huko,
Kwasasa HAJI MANARA ana umri wa miaka 48.
E L I M U
Haji Manara alianza masomo ya elimu ya msingi katika shule ya msingi MNAZI MMOJA,
Kisha akahamia na kuhitimu katika shule ya msingi BUNGEzote za jijini Dar es Salaam,
Kidato cha kwanza hadi cha nne alisoma katika shule ya secondary CHIMALA,
Huku kidato cha tano na sita akasoma katika shule ya sekondari MZUMBE iliopo mkoani MOROGORO,
Baada ya kumaliza masomo ya kidato cha tano na sita yaani A LEVEL,
Mzee SANDE MANARA alimpeleka HAJI nchini SAUDI ARABIA,
Kwa ajili ya kusomea masomo ya dini ya kiislamu,
Baadae akampeleka nchini AFRIKA KUSINI,
Huko alienda kusomea mawasiliano ya umma yaani MASS COMMUNICATIONS.
K A Z I
Baada ya kutoka AFRIKA KUSINI HAJI MANARA aliajiriwa,
Na kuwa mtangazaji katika kituo cha radio UHURU,
Tena wakati huo kikiwa moto sana miaka ya 2000,
Ambapo alikuwa akitangaza vipindi vya MICHEZO na SIASA,
Baadae akahama na aliajiriwa na kampuni ya Index international,
Haji aliendelea kufanya kazi huku akiwa mchambuzi wa soka katika vituo mbalimbali,
Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa DAR ES SALAAM,
Aliitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2010 ambapo alijiuzulu kufuatia shutuma nzito alizopewa,
Haji alituhumiwa kufanya utapeli na wizi wa magari,
Alipelekwa mahakamani baada ya kesi kusikilizwa,
Hatimae HAJI hakukutwa na hatia hivyo mahakama ikamuachia huru,
Mwaka 2014 HAJI MANARA aliajiriwa TBC kuwa mchambuzi wa soka,
Akiwa hapo alifanya kazi na watu mbalimbali,
Akiwemo marehemu THEOGENIX ALEX KASHASHA,
Ambapo moja ya kazi yao ilikua ni kuchambuzi kwenye michuano ya KOMBE LA DUNIA iliyofanyika nchini BRAZIL,
Mwaka 2015 HAJI MANARA alijiunga na klabu ya Simba sc,
Huko HAJI MANARA aliaajiriwa kuwa afisa habari,
Kazi ambayo allifanya kwa miaka 6 hadi August 2021,
Alipoomba kuondoka SIMBA SC na bodi ya wakurugenzi ya SIMBA SC ikaridhia,
Kwa sasa HAJI MANARA anafanya kazi katika klabu ya YANGA.
Cc:
Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka morogoro.
1 307
Ameandika Haji Manara, Mwanachama wa Yanga
Nikiwa kama Morani Mkuu wa huku Social Media nimeona niseme kitu na nitoe ushauri wangu kuhusu sakata la bakora zetu (siungi mkono violence)
Kiasili Sisi Wamasai sio Watu wagomvi na hatupendi shari hata kidogo, lakini tuna shida kubwa moja, hatupendi kunyanyaswa wala kuonewa hata kidogo, hatuna udhaifu katika kutetea haki zetu, TUKICHOKOZWA TUNACHOKOZEKA.
Tumeona pia katazo la kutembea na silaha zetu za jadi kwa dhana ya kulinda utamaduni wa Zanzibar, ifahamike kabila letu ni miongoni mwa makabila machache yaliyobaki duniani, ambayo yanadumisha utamaduni na mila zake, kutuzuia kwa sababu yoyote ile ni kutunyanyasa kisaikolojia!! Tunahofia mtakuja kutuzuia hata kutembea bila boxer wakati sio mambo yetu!!
Vipi hamzuii Walami wanaotembea nusu utupu kwenye mitaa ,mje mtuzuie Watanzania wenzenu? Kutembea utupu kwa Watasha ni utamaduni wa Zanzibar? Lakini utawakatazaje wakati kwao sio dhambi, iweje mtuzuie sisi Waafrika wenzenu.
Viongozi wangu nawaomba chezeni Biti ya Rais Dr Hussein Mwinyi, Biti nzuri ya Uchumi wa Buluu, Biti ambayo Sisi Wamasai tunaoishi Zanzibar tunaicheza kwa midundo yote,tunashiriki kikamilifu katika kuusapoti utalii wetu, msitufanyie hivyo tukaja kujihisi manyanyaso !!
Tunaipenda sana Zanzibar na tunaheshimu tamaduni zenu na ndio maana hata Taarabu tunaweza kuimba siku hizi, tunacheza hadi Msewe na kidumbak, tunakula urojo na mikate ya boflo, ilhali sisi chakula chetu kikuu ni Maziwa na Nyama.
Chonde Chonde tuishi kwa kuvumiliana ndugu zangu 🙏🙏
Bugati
Morani Mkuu
1 307
#HABARI Watu wawili wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuangakiwa na maporomoko ya miamba katika kijiji cha Kambeni kata ya Myamba wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na kufanya idadi ya waliofariki kutokana na athari za mvua kwenye wilaya hiyo pekee kufikia saba tangu mwezi Novemba zilipoanza kunyesha mvua kubwa.
Waliofariki ni watoto mmoja mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Myamba mwingine ni mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Kambeni, walioangukiwa na kifusi kilichotokana na kuporomoka kwa mwamba uliokuwa eneo la juu ya nyumba yao.
1 307
MAKONDA HASTAHILI KUWA MTATUZI WA SHIDA ZA WANANCHI - FELESHI
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Eliezer Feleshi, amewashangaa wananchi kujisomba kwa Paul Makonda eti kutafuta utatuzi wa shida zao. Jaji Feleshi ametaka utitiri huo wa wananchi kuacha kwenda "mahala pasipostahili"
1 307
Kwa hiyo mmefikia wapi kuhusu Maasai?
Watembee na rungu na sime au wazipumzishe majumbani?
1 307
Happy Birthday Bwana Mdogo Masantula, Pamoja Niko Safari ya Mbali lakini nikaona sio Vema kusahau kukutakia Heri katika kutimiza kwako Miaka 22.
1 307
Shabiki wa Ivory Coast,anayefahamika kwa jina la Anselme Santos ambaye ali-trend kwa kunaswa na Camera kwenye mchezo wa AFCON 2023 kati ya Senegal na Ivory Coast akizungumza na mwanadada jukwaani, ameomba msamaha kwa mke na watoto wake kwa tukio hilo ambalo amekiri alikuwa anaomba namba ya simu kwa shabiki huyo.
“Katika hali ya furaha, Nilimwambia (Yule mwanamke) ‘Nipe namba yako’. Sikumaanisha,lakini hakutaka kunipatia. Kwa hiyo sikusisitiza. Ningependa kuchukua nafasi hii kuomba msamaha kwa mke wangu na watoto wangu” — Amesema Anselme Santos katika mahojiano
1 307
⚠️😳 "Kwani kuna dhambi kupanga apartments? mimi ni mwajiriwa wa Yanga, sijawahi kusema mimi ni tajiri, naishi life standard ambayo watu wengi hawaiwezi kwa sababu hawajipangii mimi sio tajiri kabisa" - Manara akiongea Clouds TV
1 307
⚠️😳 Mwijaku amepost picha akiwa na Wema Sepetu kisha kuandika yafuatayo
"Katika kizazi cha leo, ukiondoa s3x katika mahusiano utagundua kuwa asilimia kubwa ya wanaume hawana jambo lingine la maana la kuwepo katika mahusiano.Vilevile ukiondoa pesa utagundua asilimia kubwa ya wanawake hawana jingine wanalohitaji katika mahusiano.
Bila pesa asilimia kubwa ya wanawake wataona haina haja ya kuwa katika mahusiano.Na bila s3x, utagundua kua wanaume hawaoni haja ya mahusiano.Namnukuu dada mmoja hivi, aliongea haya
"Sisi wanawake tunataka boyfriends wetu watutunze, lakini hakuna cha thamani tunachokiongeza katika maisha yao zaidi ya kuwapa s3x tu...."
Wanawake nao wanalalamika kwamba wanaume wanapenda sana s3x basi, wakishapata s3x wanawakimbia na ule upendo waliokua wakiuonesha unapoa.Ni wakati wetu sote kubadili mtazamo. Wanaume wengi siku hizi wanalalamika sana kwamba mnapenda pesa, sio wote ila baadhi yenu ni kweli mmeweka pesa kipaumbele
Na vile vile ni kweli asilimia kubwa ya wanaume wako after s3x.Tujifunze kuongeza thamani katika mahusiano...mahusiano sio kupelekeana kula bata na mafichoni Lodge bali ni kuombeana tunapokuwa down, kutiana moyo kuendelea kupambana na maisha..kusikilizana, na kupeana ushauri wenye tija, that's smart dating
Inakua ni kazi bure pale ambapo mwanaume unajua jinsi ya kutengeneza pesa lakini unapata mwanamke ambae anajua kutumia tu. Ndio maana kwenye mahusiano ni vema nyote wawili mkawa na falsafa moja kuhusiana na pesa.Vinginevyo utakua unacheza soccer safi la kushambulia, lakini defense ni dhaifu mno. Itakua ni ngumu kwa hiyo timu kushinda haitajalisha ni kwa kiasi gani inao washambuliaji makini wanaozifumania nyavu
Na mwanamke ni kama safu ya ulinzi.My wisdom; "As for you ladies, Be a Woman of virtue and purpose...Slay with sense and dignity..As for you Men, You gain more value as a man when you refuse to s3x with any woman just because she is available. The class you gain is invaluable. That's the Gentleman's Code."
1 307
Ikiwa leo ni tarehe moja mwezi wa pili, Aunty Ezekiel aachia muonekano huo wenye mfanano na Kim Kardashian.
