E-PLUS MEDIA
Открыть в Telegram
1 307
Подписчики
+124 часа
-27 дней
-1330 дней
Архив постов
1 307
Mmwijaku ✍️
#FACT-Hakuna mwanamke wa rahisi rahisi na hakuna mwanaume mpumbavu. Mwanamke ambae umemfukuzia kwa takribani miezi 12 alilala na Boyfriend wake siku ya tatu tu baada ya kukutana.
Mwanamke ulielala nae wiki moja tu baada ya kuanza mahusiano nae ujue kuna mwanaume mwingine anamfukuzia mwaka wa pili huu na hajampata. Kama amekupenda na ameona quality anazozihitaji kwako usisimame na kusema 'she is CHEAP' au 'maharage ya Mbeya'.
Na kwa Wanawake: Mwanaume ambae amejipinda amekununulia Iphone au chochote kile hajawahi kumnunulia hata hereni mpenzi wake wa zamani. Kama umebahatika ujue anakupenda, usidhanie kuwa yeye ni mpumbavu, bwege au wa kumchuna.
Usimchukulie kirahisi rahisi, usimuone kama ni bwege fulani, mtu kuwa mkarimu kwako haimaanishi ni bwege. Wote tujifunze kuheshimu na kuzikubali zile jitihada zinazooneshwa na wenzetu katika mahusiano.
Ladies are not cheap and guys are not fool!!
Unakubaliana na hayo?
Toa maoni yako
1 307
Finally Madebe amefuta picha zote za aliyekuwa mkewe Chanuo, kisha ameposti video akiwa dinner na mkewe huyo mpya Kipini wakilishana kwa mahaba ya kienyeji kisha kumpa chanuo ujumbe huu.
"Sina tena namba yako kinyago cha mpapule huku nilipo nanawili, nalishwa nanenepa, nimekusahau wewe pumba hata jina lako silikumbuku".
1 307
"Samahani mke wangu, siwezi kukuletea kombe ulilotaka kama zawadi ya harusi yetu, nilijitahidi lakini haikunifanya nipate kikombe, samahani." amekaririwa akisema Sadio Mané baada ya Timu ya Taifa ya Senegal 🇸🇳 kuondolewa kwenye michuano ya AFCON 2023.
Toa maoni yako
1 307
"Mimi nataka nimwambie ndugu yangu Hassan Mwakinyo, muda ushaisha sasahivi, ule muda wa kupigizana kelele, kukwaruzana, mwisho wa siku watanzania watatuchoka sasa."
"Watanzania wanataka kukata kiu yao, mashabiki zako (Mwakinyo) wanajua wewe ni bora kuliko mimi, na mashabiki zangu (Kiduku) wanajua mimi ni bora kuliko wewe. Ni muda wakuonyeshana sasa nani ni bora."
"Watoto wakiume tuonyeshane kazi sio maneno, ooh sijui mama yako ni kungwi, sijui nini. Mapromota wapo wengi, tena Pambano nataka lifanyikie hapo nyumbani Tanga, Tanga nina wadau wananikubali sana kuliko unavyofikiria" - Twaha Kiduku, Bondia wa Tanzania.
Toa maoni yako
1 307
Baada ya tetesi kusambaa kuwa hajui kupika zaidi ya kugalauka Instagram, leo Zaiylissa amewadhihilishia Watesi wake kuwa hana jambo dogo kwenye masuala ya makuli.
Kama anavyoonekana pichani ni akiwa jikoni kwake.
1 307
Huyu hapa Dj Juma Khan, Dj maarufu anayetafsiri Filamu za kihindi, ni kwa kiasi gani unamkubali?
1 307
"Nyie mnaosema naharibu mziki wa Injili kwa kuvaa cheni na namna ya uchezaji wangu nimewasikia kilio chenu, lakini mkumbuke kuwa zamani nilikiwa naimba nyimbo za mastepu, nikiwa sina cheni lakini hazikwenda popote na hamkuzipenda. Lakini nilipotoa nyimbo nimevaa cheni na nacheza kama ninavyoonekana kwenye hizi video zangu mpya nyimbo hizo zimenitambulisha na hata nyie mlizipenda sana, sasa mnatakaje?"
"Mnataka niendelee kuimba nikiwa kwenye uzamani nyimbo zibume? Na mkumbuke kuwa mimi ndiye nilianzisha hii style mpya ya kucheza na kuvaa kujanja kwenye miziki ya Injili embu nipeni heshima yangu tafadhali"- Goodluck Gozbert
1 307
⚠️😳 "Nikilala sitaki kuashwa na simu huwa nazima. Usingizi wangu ni wa mashaka na nikilala hata mlango ukigongwa naamka na mke wangu ameshajua. Mambo ni mengi ndio maana napata usingizi wa mashaka" - Manara akihojiwa Clouds TV
1 307
⚠️😳 - "Kuna watu hawasalimiwi wala hawajibiwi salamu zao sio kwamba hawakumbukwi au wanadharauliwa hapana, tatizo ni tabia mbovu walizonazo, kuna watu hapa nje ukiwasalimia tu lazima mwishoni waombe hela, siku wakikutumia message ya salamu ujue ni shida tu ndio unataka kuliliwa" - Dr.Modest Bafite
"Please wenye tabia hizi acheni mara moja, sio vizuri, sio sawa, maisha hayataki hivyo, kuwa na tabia ya kusalimia na kusalimiwa bila kulia shida, ili siku ukikwama mtu ajue kweli umekwama, sio unakaa miezi hujasalimia, ukisalimiwa tu, mwishoni unaomba, wengine mnanyimwa sio kwamba uwezo haupo ni vile hamfai kusaidiwa" - amesema Dr.Modest Bafite
1 307
⚠️😳 Paka na mbwa warithishwa utajiri wa shilingi bilioni 7
Mwanamke wa nchini China aliyetambulika kwa jina moja la Liu ambaye umri umeenda, ameibua mshtuko na minong'ono baada ya kuwatupilia mbali watoto wake watatu ambao ni watu ili wasiweze kurithi utajiri wa dola $2.8 milioni ambazo sio chini ya shilingi bilioni 7 za Tanzania
Kwa mujibu wa South China Morning Post, sababu hasa ya Liu kufanya hivyo ameeleza kuwa katika umri wake wa utu uzima na hata alipougua watoto wake hawakumjali hata kumtembelea ila paka na mbwa wake ndio walikuwa karibu yake kumfariji ndio maana akaona awarithishe utajiri wake halafu wanae wa kuwazaa wasipate kitu,
Ingawa awali alikuwa ameandika majina ya wanae katika urithi ila alipoona hawamjali ndio akawageuzia kibao, miaka mitatu sasa imepita tangu awarishe paka na mbwa wake utajiri alionao siku akifariki
Mtalaamu wa mambo ya urithi/mirathi nchini China amesema China hairuhusu moja kwa moja wanyamwa kupewa urithi hivyo, Liu imebidi achague clinic maalum inayohusika na mambo ya paka na mbwa ili ndio isimamie utajiri huo katika kuwatunza paka na mbwa wake maisha yao yote na watoto watakaozaa, pia ameshauriwa atamfute mtu yeyote anayemuamini aweze kuwa macho kuangalia kama clinic husika itasimamia pesa vizuri zisije kuishia mikononi mwa mafisadi
Aidha, ameambiwa muda wowote anakaribishwa tena ikiwa atataka kutengue maamuzi yake utajirinwake awarithishe tena wanae
Hii si mara ya kwanza wanyama(pets) kurithishwa utajiri mkubwa ilishatokea zaidi ya mara tatu
1 307
HARMONIZE KWANGU NI UCHAFU TU "MALAIKACUTE"
Mwanadada Malaikacute Amedai Hawezi Kuwa Katika Mahusiano Na Harmonize Kwa Sababu Anamuona Msanii huyo Kama Uchafu Tu.!! 😫🙆🏽♂️
Akijibu comment ya Shabiki Ambae alitoa maoni Katika Moja ya Posti yake akimueleza kuwa Harmonize Huwa anapenda Wanawake wenye Shape Kubwa hivyo akimuona Lazima atakuwa ameisha, Jibu la Malaika Cute lilikuwa hili 👇
"Harmonize kwangu ni uchafu tu"
Toa maoni yako Hapa ✍️
1 307
MIMI NI MSANII WATATU TAJIRI TANZANIA NZIMA-BABA LEVO
Baba levo ametangaza Kuwa yeye ni msanii namba tatu Tanzania kwa kuwa na hela Nyingi.Huku pia akimshukuru Mwanamuziki pamoja na Mfanyabiashara Diamond platnumz kwa kumuwezesha kuwa tajiri .
" Mi nikipiga Hesabu Najiona ni msanii Namba tatu kwa hela Tanzania ..
Hao wasanii tulikuwa tunawaogopa hawana kitu Aiseh NJAA TUPU .
1 307
TANROAD WAANZA OPERATION FYEKA MAZAO BARABARANI
Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS) mkoa wa Tabora imeanza zoezi la kuondosha kwa kufyeka mazao yote ambayo yamelimwa na wakulima katika hifadhi za barabara.
Zoezi hilo utekelezaji wake umeanza katika maeneo ya wilaya ya Nzega na Igunga mkoani humo ambapo umefanyika ufyekaji wa mazao ikiwemo mahindi.
Meneja wa TANROADS mkoa wa Tabora Mhandisi Raphael Mlimaji, amesema hatua hiyo imefuata baada ya elimu kutolewa mara kadhaa juu ya wananchi kutotakiwa kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo katika maeneo ya hifadhi za barabara huku wengi wao wakionekana kukaidi.
1 307
Hajismanara ameeleza kwamba kama Mbunge wa sasa wa jimbo la Ilala Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu akiacha kugombea Ubunge jimbo hilo Mwaka 2025 basi yeye atagombea.
Kama Zungu atagombea mwaka 2025 basi @hajismanara ataacha kugombea Ubunge maana hawezi kugombania nafasi yoyote ile ya uongozi pamoja na kaka yake (Zungu) kwa sababu anamheshimu na kukubali uongozi wake tangu Zamani, hivyo hawezi kushindana naye.
1 307
Wadau wamehoji Imekuwaje Mchezaji Clement Mzize amecheza Mchezo siku ya jana Dhidi ya HAUSING wakati alikuwa anaumwa Ugonjwa wa RED EYES 👁️
Una maoni Gani ✍️
1 307
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk. Pindi Chana, amesema cheti cha kuzaliwa hakimpi mtu uhalali wa uraia bali ni uthibitisho wa kuzaliwa kwake.
Dk. Chana alitoa kauli hiyo baada ya kutembelea Ofisi ya Msajili wa Vizazi na Vifo (RITA) Mkoa wa Njombe kwa lengo la kuangalia hali ya uandikishaji na usajili wa watoto chini ya miaka mitano.
“Sio uthibitisho pekee na ndiyo maana cheti cha kuzaliwa hata mtoto ambaye wazazi wake wote wawili sio Watanzania ni wageni wamekuja kutalii akizaliwa Tanzania atapata cheti, hivyo katika vigezo vyetu vya kuangalia huyu ni Mtanzania ama sio, cheti cha kuzaliwa kinaweza kikatumika,” amesema Dk. Chana.
