fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Disemba 05, 2023 ametembelea kambi ya muda walipo waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha
+2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Disemba 05, 2023 ametembelea kambi ya muda walipo waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuharibika kwa nyumba na miundombinu mingine kutokana kuporomoka kwa tope na mawe kutoka mlima Hanang, Katesh Mkoani Manyara. Waathirika hao walio katika kambi hiyo ya muda wanahudumiwa na serikali na wameishukuru serikali kwa jitihada zilizofanyika za kuhakikisha wanapata huduma hizo muda wote.

MAAFA HANANG | Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Disemba 05, 2023 amewajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha ku
+1
MAAFA HANANG | Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Disemba 05, 2023 amewajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuporomoka kwa tope na mawe kutoka Mlima Hanang, Katesh Mkoani Manyara. Majeruhi hao wanapatiwa matibabu bure na Serikali katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara. Imeandaliwa na PresenterWaMillardayo

#SikiaHii: Utafiti uliofanywa katika chuo kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani unaonyesha kuwa, kazi za ziada za nyumbani k
#SikiaHii: Utafiti uliofanywa katika chuo kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani unaonyesha kuwa, kazi za ziada za nyumbani kwa wanafunzi "Homework" huwafanya kuwa maskini. Utafiti huo umeongeza kwamba, hakuna mafungamano yoyote kwa mafanikio ya wanafunzi kimasomo na wao kupewa kazi za ziada za nyumbani. Hapo vipi, ulipokuwa shule ulikuwa unamaliza "Homework" yako kwa wakati? Millard Ayo presenter.

BASHUNGWA AAGIZA KAZI KUONDOA TOPE KATIKA MJI WA KATESH IFANYIKE USIKU NA MCHANA. Waziri wa Ujenzi, Innocent. Bashungwa amewaagiza wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini ( TARURA) kwa pamoja kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ya kuondoa tope kwenye makazi ya watu na kwenye miundombinu katika mji wa katesh Wilayani Hanang. Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati alipoambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama, Waziri wa Madini, Anton Mavunde kukagua hali ya miundombinu na kujionea jitiada za uokoazi unaoendelea, tarehe 4 Disemba 2023. “TANROADS shirikianeni kwa pamoja na TARURA kwa kuongeza mitambo na vifaa ili kazi ya kuondoa tope ifanyike usiku na mchana katika maeneo yote ya mji wa Katesh ikiwa ni pamoja na humu kwenye makazi ya watu, Sokoni na kwenye miundombinu ya barabara,” amesema Bashungwa Waziri Bashungwa amesema Serikali itahakikisha inafanya kila jitihada ambazo zitaruhusu shughuli za uzalishaji zinaendelea kama kawaida na maisha yarejee kama ilivyokuwa awali. Amemtaka Meneja wa TANROADS mkoa Manyara kuhakikisha mitambo na vifaa vyote vinakuwa na mafuta na kazi ifanyike usiku na mchana bila kuwepo na kikwazo wala sababu yoyote. Kwa Upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama amesema kazi ya uokozi inaendelea ikiwa ni pamoja na utafutaji wa miili inayosadikika bado haijapatikana. Amesema Serikali inaendelea kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanagharamia shughulia za mazishi, ikiwa na kutoa matibabu bure na huduma zote kwa waathirika wa maafa haya. Waziri Jenista amesema wanajipanga kuhakikisha wanarejesha huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na umeme, maji na huduma nyingine za kijamii zilizoathiriwa na maafa hayo.

photo content

Tulipata mvua za wastani jana majira saa 11 jioni ila tumepokea maji mengi kutoka milimani kupitia mto mkondoa na wami ambapo
Tulipata mvua za wastani jana majira saa 11 jioni ila tumepokea maji mengi kutoka milimani kupitia mto mkondoa na wami ambapo mto wami umepasua na maji kuingia mtaani nyumba zimeharibika na baadhi ya mali za wananchi katika kata Rudewa na Mvumi zaidi lakini tumepata kifo cha Mtu moja mtu mzima mwanume. Shaka Hamdu Shaka Mkuu wa Wilaya Kilosa 05 Disemba 2023

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa viongozi wengine kwenye helcopter iliyozunguka kukagua maeneo yaliyoathiriwa na Ma
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiwa viongozi wengine kwenye helcopter iliyozunguka kukagua maeneo yaliyoathiriwa na Maafa ya Maporomoko ya tope na mawe kutoka mlima wa Hanang' Mkoani Manyara 04 Disemba,2023

VIFO VYAONGEZEKA HANANG'. Idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya Maji na Matope kata nne za wilaya ya Hanang' mkoani Ma
+1
VIFO VYAONGEZEKA HANANG'. Idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya Maji na Matope kata nne za wilaya ya Hanang' mkoani Manyara imeongezeka na kufika 69 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema leo imepatikana miili Mingine miwili na kufanya idadi hiyo huku Majeruhi wakiwa ni 116. Akitoa pole kwa wakazi wa Hanang' leo Mjini Katesh waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema waathirika katika Maafa hayo wanapatiwa huduma zote stahiki na serikali ikiwemo malazi na chakula. Ameonya watakaotumia misaada hiyo tofauti na lengo, kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Ameelekeza misada yote itakayotolewa na wadau mbalimbali ipitie kwa wakuu wa mikoa kwenye maeneo yao.

TESA HAUMWI ATAREJEA KWENYE HALI YAKE YA KAWAIDA HIVI KARIBUNI; BOSS AZIZI Kufuatia mkanganyiko wa hali ya Mwigizaji mkongwe
TESA HAUMWI ATAREJEA KWENYE HALI YAKE YA KAWAIDA HIVI KARIBUNI; BOSS AZIZI Kufuatia mkanganyiko wa hali ya Mwigizaji mkongwe wa Filamu Tanzania, Bi Grace Mapunda maarufu kama Tesa kuonekana ikiwa amedhoofika ghafla, Muongozaji wa Tamthilia hiyo ya Huba Azizi Mohammed amewaondoa watu wasiwasi akisema kwamba Tesa yuko sawa haumwi na hivi karibuni atarejea kwenye hali yake ya kawaida kama watu walivyomzoea. Aidha Boss Azizi amesema Tamthilia ya Huba haina mpango wa kuisha leo wala kesho licha ya kuwa hewani kwa miaka saba sasa, amesema wameendelea nayo kwasababu ni Tamthilia pendwa na namba moja kuliko Tamthilia zote ndiyo maana hata DSTV wenyewe wanashindwa kuiondoa kwasababu inawalipa. Lakini pia wanawalipa wasanii wao vizuri ndiyo maana wasanii wengi walioanza na Tamthilia hiyo bado wapo.

MANABII WA MUNGU WATUA NCHINI KWA AJILI YA KUSHUSHA UPONYAJI Pichani ni Prophet Lovy Elias na Passion Java walipokuwa wanawas
MANABII WA MUNGU WATUA NCHINI KWA AJILI YA KUSHUSHA UPONYAJI Pichani ni Prophet Lovy Elias na Passion Java walipokuwa wanawasili nchini Tanzania kuelekea usiku wa Mkesha wa Maajabu yasiyo na hesabu. Watumishi hao wa Mungu wanatajia kuungana na mtumishi wa Mungu Baba Prophet Malisa katika mkesha utakaofanyika Disemba 8, 2023 katika viwanja vya Posta Kijitonyama kuanzia 11:00 mpaka asubuhi.

Mambo kadhaa najiuliza hadi sasa sipati majibu. Mheshimiwa Rais; Mama Samia amekatisha mkutano uliokuwa ukiendelea huko Dubai karejea kuomboleza pamoja katika msiba wa kitaifa uliotokea katika Wilaya ya Hanang, taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inasema Mama Samia ameondoka kurejea nchini na kuahirisha shughuli za mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (COP23) unaoshughulikia Mabadiliko ya tabia nchi uliokuwa ukiendelea Dubai. Mheshimiwa Waziri Mkuu amefika katika eneo la Hanang ambako kumetokea maafa ya mafuriko ya udongo yaliyopelekea vifo vya zaidi ya watu 63 Wakati Rais akiahirisha kuendelea na mkutano huko Dubai, huku Makamu wa Rais haonekani. Wananchi wanahoji alipo kiongozi wao wanatishwa kwamba Kiongozi yupo, amesafiri safari ya mbali ya nje ya nchi akiendelea na majukumu yake kama kawaida. Kuna mambo kama taifa tunaona kama hayapo sawa, hivi Rais anaihirisha shughuli yake, Makamu wake hata salamu za Rambirambi ameshindwa kutuma? Tuko serious kweli? Wananchi wanapaswa kupewa taarifa za safari za viongozi wao. Hapa katikati kuna kipindi Rais alisafiri safiri safari ambazo hazikutolewa taarifa na wananchi walipohoji ndipo safari zikaanza kutangazwa tena. Wananchi kujua alipo kiongozi wao ni haki yao. Ni Raia namba mbili katika nchi yetu, shughuli zake ni kwaniaba yetu, anapoenda mahali tunapaswa kujua maana anatuwakilisha huko. Akiwa na tatizo tunapaswa kujulishwa ili TUMUWEKE kwenye MAOMBI. Haya mambo ya kuambiana kiongozi yupo anachapa kazi kisha baadae tunapeana bahari mbaya tutazichoka; tukizichoka tutawachoka na watoa taarifa na hapo itakuwa mwisho wa ENZI. Tunaiomba serikali itupatie taarifa sahihi ni wapi yupo Makamu wa Rais wetu. Kama amesafiri tuambiwe ameenda nchi gani. Je taarifa ya maafa hajayasikia? Uko wapi ujumbe wake wa kutoa salamu za rambirambi kwa waliofariki? Abdoulquarim Malisa

photo content
+2

The Church of Christ Katesh unites with other Christians to give sorry to those who lost their loved ones due to the flooding
+1
The Church of Christ Katesh unites with other Christians to give sorry to those who lost their loved ones due to the flooding, this is due to the heavy rain that showed yesterday and caused the soil to fall into people’s homes in Hanang District more than 60 people have died, and we continue to pray for the families during this time. Kanisa la Kristo Katesh linaungana na wakristo wengine kutoa pole kwa waliopoteza wapendwa wao kutokana na mafuriko ya maji, hii ni kitokana na mvua kubwa iliyonyesha jana na kusababisha udongo kumomonyoka na kuingia katika makazi ya watu na kufukia nyuma pwmoja na magari, wilaya ya Hanang watu zaidi ya 60 wamekufa, tuendelee kuziombea familia zilizokubwa na janga hili

MAAFA HANANG : Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anaongoza zoezi la kuaga baadhi ya miili ya marehemu waliofariki katika maporomok
MAAFA HANANG : Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anaongoza zoezi la kuaga baadhi ya miili ya marehemu waliofariki katika maporomoko ya matope katika Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara. Zoezi hilo linafanyika Desemba 4, 2023 katika viwanja vya Shule ya Msingi Katesh. #AzamTVUpdates Imehaririwa na Onike Masayanyika na John Mbalamwezi

MAAFA HANANG | Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kufupisha safari yake ya kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko
MAAFA HANANG | Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kufupisha safari yake ya kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) huku Dubai na kurejea nchini, ili kushughulikia kwa karibu janga la mafuriko wilayani Hanang lililosababisha vifo vya watu 63 hadi sasa na wengine 116 kujeruhiwa. #AzamTVUpdates Imeandaliwa na Claud Mshana

MAAFA HANANG | Rais Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya watu wot
MAAFA HANANG | Rais Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya watu wote waliopoteza maisha kutokana na mafuriko katika Wilaya ya Hanang. Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa Disemba 4, 2023 imesema Rais Samia pia ametaka majeruhi wote waliopo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za serikali. Aidha, Rais Samia ameelekeza serikali ya Mkoa wa Manyara na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu, kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji, wapate makazi ya muda. Hadi sasa, idadi ya waliofariki kutokana na janga hilo la mafuriko imefikia watu 63 huku kaya zilizoathirika zikiwa ni zaidi ya 1,100 na kuathiri watu zaidi ya 5,000 huku ekari 750 za mashamba zikiwa zimeharibika. #AzamTVUpdates Imeandaliwa na Claud Mshana

MAAFA HANANG | Bohari ya Dawa nchini (MSD) imepeleka awamu ya kwanza ya vifaa tiba na dawa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika
MAAFA HANANG | Bohari ya Dawa nchini (MSD) imepeleka awamu ya kwanza ya vifaa tiba na dawa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko Hanang. Vifaa tiba na dawa hizo vimekabidhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini). Kwa mujiibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Instagram wa MSD, Meneja wa Kanda ya MSD Kilimanjaro, Rehema Shelukindo ameeleza kuwa, vifaa hivyo ni pamoja na maji ya dripu, dawa za kuponya magonjwa ambukizi na mengineyo(antibiotics), dawa za msumivu na mashuka. Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai ameeleza kuwa MSD itaendelea kupeleka bidhaa za afya katika eneo hilo kadri inavyoelekezwa na serikali. #AzamTVUpdate Imeandaliwa na Claud Mshana

MAAFA HANANG | Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu, Mganga Mkuu wa
+1
MAAFA HANANG | Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Afya, wamewasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kuona hali ya utoaji huduma na kutoa pole kwa majeruhi 11 wa maafa ya mafuriko yaliyotokea katika mji wa Katesh, Wilaya ya Hanang mkoani humo ambao wamelazwa katika Hospitali hiyo. Dkt. Mollel amesema kuwa Wizara ya Afya imejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za matibabu ili kuokoa maisha ya watu, amesema kuwa hadi sasa hospitali zote ndani ya Mkoa wa Manyara zimepokea na kuhudumia majeruhi 93 na wote wanaendelea vyema na matibabu. #AzamTVUpdates Imeandaliwa na Claud Mshana

MAAFA HANANG | Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, wilayani Hanang imeongezeka
+1
MAAFA HANANG | Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, wilayani Hanang imeongezeka na kufikia watu 63 baada ya kupatikana miili miwili wakati wa zoezi la uokoaji linaloendelea. Taarifa ya Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga aliyotoa asubuhi ya Disemba 4, 2023 inasema idadi ya majeruhi bado ni 85. Ameongeza kuwa shule za msingi Katesh, Hanang na Dumanang zitatumika katika kuhifadhi waathirika wa mafuriko hayo, na kuwataka wananchi kuhama mara moja maeneo ya hatari ili kujikinga na madhara mengine yanayoweza kutokea. #AzamTVUpdates Taarifa ya Hellen Kawiche imehaririwa na Claud Mshana

"Kwakweli mpaka sahivi na sisi hatuna uhakika ambacho tunachojua tumepata mvua, ambayo imeporomosha mawe na matope mazito kut
"Kwakweli mpaka sahivi na sisi hatuna uhakika ambacho tunachojua tumepata mvua, ambayo imeporomosha mawe na matope mazito kutoka mlimani, lakini serikali imeleta watafiti wa madini wameingia hapa jana jioni na sasa hivi navyoongea na ninyi wameshaanza kupanda kuelekea juu mlimani kuangalia lile tope ni tope la kawaida la mvua au kulikuwa na kitu kingine nadhani baada ya hapo tutajulishwa" - Queen Sendiga ,Mkuu wa mkoa wa Manyara