fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
Shabiki wa Wolves Jamie Arnold, 32, kutoka Norton Bridge huko Staffordshire amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kutokana
Shabiki wa Wolves Jamie Arnold, 32, kutoka Norton Bridge huko Staffordshire amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kutokana na kumfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi beki wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand. Shabiki huyo pia amefungiwa kwa miaka saba kujihusisha na shughuli za mpira ndani na nje ya nchi Ferdinand alifanyiwa ishara hizo Mei 23, 2021 baada ya kushangilia bao la Manchester United dhidi ya Wolves akiwa kama mchambuzi wa zamu ndani ya BT Sport, huku mechi hiyo ikimalizika kwa Wolves kufungwa mabao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani. Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza kwa mashabiki kurejea uwanjani baada ya vikwazo vya coronavirus kuondolewa. Hukumu hii ndiyo hukumu kali zaidi kuwahi kutolewa kwa shabiki wa soka aliyepatikana na hatia ya unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi kwenye mechi za mpira wa miguu.

Mara yako ya mwisho kulia kwasababu ya Mpira ni lini?
Mara yako ya mwisho kulia kwasababu ya Mpira ni lini?

⚠️😳😢 Lawali mori(17) kijana toka Adamawa nchini Nigeria amedakwa na vyombo vya sheria kwa kumuingilia kingono jogoo Alidakw
⚠️😳😢 Lawali mori(17) kijana toka Adamawa nchini Nigeria amedakwa na vyombo vya sheria kwa kumuingilia kingono jogoo Alidakwa baada ya mkazi wa maeneo husika kwa jina la Estther Dimas kumuona akifanya kitendo husika na kuwataarifu polisi Lawali aposhikwa na kuhojiwa na polisi alikiri kumuingilia kingono jogoo ila hakueleza sababu ya kufanya hivyo

⚠️ Prophet Lovy, Prophet Malisa na Prophet Passion ambao waliongoza mkesha wa Usiku Wa Maajabu ambapo palikuwa na maombezi ya
⚠️ Prophet Lovy, Prophet Malisa na Prophet Passion ambao waliongoza mkesha wa Usiku Wa Maajabu ambapo palikuwa na maombezi ya kiroho na uponyaji katika viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi hadi kufikia Mchana wa Desemba 08, 2023 idadi ya vifo kutokana na Maafa ya Mafuriko ya Hanang imefikia 85 Watu wazima wakiwa 48 na Watoto 32 na kwamba Miili ya watu 79 imekwishatambuliwa. Idadi ya Majeruhi waliopokelewa katika Hospitali za Mkoani Manyara imefikia 133, Watu wazima 71 na Watoto 62 ambapo Waathirika wote wanatibiwa bure kama agizo la Rais Samia lilivyotaka na Serikali inagharamia mazishi ya waathirika wote. #hanang #manyara

photo content

Polisi nchini Kenya wanamshikilia msichana wa miaka 13 kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi kwa kutumia panga baada ya kutoke
Polisi nchini Kenya wanamshikilia msichana wa miaka 13 kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi kwa kutumia panga baada ya kutokea mvutano uliosababishwa na matumizi mengi ya simu. Kulingana na mkuu wa polisi wa kaunti ndogo ya Transmara Mashariki, Boniface Kavoo, mama wa binti huyo mwenye umri wa miaka 55 alitaka kumpokonya simu binti yake baada ya kutofurahishwa na tabia ya binti huyo kuchati na kuzungumza na simu muda mwingi. “Ni mazingira ambayo mama yake alitaka kumpokonya simu binti yake aliyokuwa akichati naye, inaonekana marehemu alikuwa mama mkali, na hakufurahishwa na msichana wake kufanya mawasiliano mengi bila yeye kujua,” ameeleza Kamanda Kavoo. Baada ya mvutano huo, katika hali ya kushanga mshukiwa aliokota panga na kumvamia mama yake kisha kumkata kichwani na ndipo alipofariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi.

MGANGA WA KIENYEJI ABAKWA Mwanaume mmoja huko Nigeria 🇳🇬 amembaka Mganga wa kienyeji mwenye umri wa miaka 26 (Mwanamke, pic
MGANGA WA KIENYEJI ABAKWA Mwanaume mmoja huko Nigeria 🇳🇬 amembaka Mganga wa kienyeji mwenye umri wa miaka 26 (Mwanamke, pichani) aliyeenda kumfanyia tiba asili nyumbani kwake.

Daktari Bingwa wa utambuzi wa magonjwa na sababu za vifo, Profesa James Shaba amefariki dunia Desemba 5, mwaka huu nchini Mar
Daktari Bingwa wa utambuzi wa magonjwa na sababu za vifo, Profesa James Shaba amefariki dunia Desemba 5, mwaka huu nchini Marekani alikokuwa akiishi. Profesa Shaba alihudumu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kustaafu, na moja ya rekodi zinazomtambulisha ni uchunguzi wa mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Sokoine aliyefariki kwa ajali Aprili 1984.

MIAKA 62 YA UHURU WA TANZANIA BARA TUNA PEPERUSHA BENDERA KILELENI . DIRA: “Ushiriki Madhubuti wa Kila Mwananchi na Mdau kati
+3
MIAKA 62 YA UHURU WA TANZANIA BARA TUNA PEPERUSHA BENDERA KILELENI . DIRA: “Ushiriki Madhubuti wa Kila Mwananchi na Mdau katika kujenga Tanzania Bora ya Kesho”

photo content

⚠️ Nabii Lovy Longomba Elias akiwa ndani ya viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar Ea Salaam ambapo ataungana na kina Prophet Ma
⚠️ Nabii Lovy Longomba Elias akiwa ndani ya viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar Ea Salaam ambapo ataungana na kina Prophet Malisa wa Tanzania, Prophet Passion Java wa Zimbabwe kwa ajili ya mkesha mkubwa wa kihistoria utakaoambatana na maombi maalumu na kupakwa mafuta yenye upako wa ajabu Dec 08/2023 Prophet Lovy ni mwanamuziki pia mjasiriamali, wakati Nabii Java pia ni socialite, promota wa muziki, mwandishi wa vitabu na mjasiriamali Prophet Java ambaye anatajwa kuwa na utajiri shilingi bilioni 125($50 million), alishakaririwa akisema kanisa ni biashara huku akidai sehemu kubwa ya utajiri wake ameupatia kwenye kanisa lake linalotajwa kuwa na matawi kadhaa nchi tofauti

Pichani ni Rais Samia Suluhu Hassan akiwatia faraja wananchi wa Hanang/Katesh
Pichani ni Rais Samia Suluhu Hassan akiwatia faraja wananchi wa Hanang/Katesh

UNAFANYA HIVI KWA MTOTO WAKO? Kama picha inavyojieleza, baba na mwanae wamezama kwenye maombi, unaweza kujiuliza kwa umri wa mtoto huyo anawezaje kusali? hana cha kuongea zaidi anaiga anachokifanya baba/babu yake. Kinachotendeka pichani ni kitu cha muhimu sana hasa kwa nyakati hizi, mzoeshe mtoto wako kusali, mfundishe ajue kuwa kusali ni lazima kama kwenda shule, kula, kulala, kuoga n.k mueleweshe umuhimu wa jambo hili katika maisha yake. Hii itamsaidia kuishi katika misingi ya dini yake, itamjengea njia nzuri ya kimaadili, itamfanya awe karibu na Mungu, itamuepusha kujiingiza kwenye ulevi, wizi, ukabaji, ubakaji n.k Wazazi wengi wa sasa hivi hawana muda na suala la kuwafundisha watoto juu ya umuhimu wa maombi, mzazi anakula bila kusali, analala bila kusali, anaamka bila kusali, anasafiri bila kusali, haendi kanisani wala msikitini kuswali, Instagram, Facebook na Tiktok zimetawala maisha yako na wakati wote huo mtoto wako anakuangalia na anakutazama wewe kama taa yake, unachokifanya anaona ni sahihi na yeye anaamua kufuata njia zako. Akiwa mtu mzima akaanza kukusumbua unaanza kumlaani, unatamani awe kama mtoto wa fulani, unasahau kama anaishi kwenye njia ulizomuandalia. Jamani hili jambo ni muhimu sana, mfundishe mtoto wako kumjua Mungu kuna faida nyingi, ipe mipaka mitandao, mtoto kwanza, jali kizazi chako ndio msingi wako wa baadae, kuna kuzeeka, kuumwa. Ikiwa haujamuandaa mtoto wako kuhusu umuhimu wa moyo wa huruma utasaidiwa na nani? inauma kuona kizazi chako kinaangukia kwenye ulevi. Akili kumkichwa

photo content

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambaye pia yeye na mama yake ni waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Que
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wakati wakiangalia athari za mafuriko yaliyotokea katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

Vannesa Mdee na Mtoto wake
Vannesa Mdee na Mtoto wake

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Pichani ni ngulii Wa Bongo movie Pastor Myamba Akiwa kwenye Picha ya Pamoja na Ubavu wake Wa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Pichani ni ngulii Wa Bongo movie Pastor Myamba Akiwa kwenye Picha ya Pamoja na Ubavu wake Wa Kushoto. Miaka Hiyo Pastor Myamba Alifanya vyema kwenye Movie mbalimbali Kama ((Dar to Logos ,She Is My Sister n.k)) Akiwa na Steven Kanumba. TOA MAONI YAKO HAPA

Baada ya msafara wa Mbowe kuzuiwa na jeshi la polisi kwenda wilayani Hanan'g kwenye eneo lililokumbwa na maafa, Mbowe alilaumu kitendo hicho kuwa si cha kiiungwana na kinawagawa watanzania kwani wahanga wa Hanan'g wanahitaji faraja ya watu wote. Mbowe alitaka kuahirisha ziara yake, lakini viongozi waandamizi wa Serikali, na viongozi waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama walimpigia na kumsihi asikatishe ziara hiyo. Viongozi hao walimjulisha RPC Manyara kuwa wamefuta maagizo yake na kwamba viongozi wa Chadema waruhusiwe kwenda Hanan'g. Baada ya kuondolewa kwa zuio hilo batili na la "kipumbavu" la Polisi, hatimaye Mbowe na msafara wake wamefika Hanan'g na kutembelea Kata ya Katesh, Ganana na Jorodom ambazo zimeathirika zaidi na maafa hayo. Viongozi hao wametembelea baadhi ya kaya na kutoa pole pamoja na kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu. Mhe.Mbowe amesema "Tulikusudia kusitisha ziara yetu lakini viongozi kadhaa waandamizi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wametusihi tusikatishe ziara na wametengua zuio la polisi. Tumetafakari na viongozi wenzangu. Hekima imetuelekeza kuwa wahanga wa maafa ya Hanan'g ni Watanzania wenzetu na wanahitaji faraja ya kila mmoja wetu. Nia yetu njema ya kuwapa faraja haiwezi kuzuiliwa na amri batili ya polisi. Tumekubali kuendelea na ziara kama ilivyopangwa awali" - MALISA GJ