E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), kabla ya kufupisha safari hiyo na kurejea nchini ili kushughulikia kwa karibu janga la mafuriko Wilayani Hanang amesema akiwa Dubai Mashirika mbalimbali yamechangia Tsh. bilioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia Waathirika wa janga hilo.
Akiongea na Wananchi walioathirika na janga hilo katika Shule ya Msingi Katesh Wilayani Hanang leo December 07,2023, Rais Samia amesema “Nawashukuru Watanzania waliotoa msaada kwa njia moja au nyingine, huu ndio upendo tunaozungumza siku zote, janga lilipotokea nilikuwa safarini, taarifa zimetoka wenzetu kule wamesikia na kwahiyo wenzetu kule wengi tu Mashirika yaliyokuwepo kule wametuchangia kiasi cha Tsh. bilioni 2.5 na nimeelekeza waziingize benki”
“Mpango kamili ukitimia wa Waziri Mkuu basi fedha za matumizi zipo pale na tunategemea michango zaidi ili tutimize mpango wetu wa kukamilisha makazi kwa walioathirika, wito
wangu kwa Kamati ni kufanya matumizi mazuri ya fedha zinazokusanywa, fedha za majanga sio za kumnufaisha Mtu binafsi kwahiyo tuwe Waadilifu”
#MillardAyoPRESENTER
1 307
Anaandika mchekeshaji na msanii wa filamu nchini @idrissultan
"Wengi wanaojitafuta wanaiga wengi waliojipata sababu hakuna anayependa kuishi kwa shida. Tatizo ni wengi waliojipata hawana vingi vizuri vya kuigwa na wengi wenye vizuri vya kuigwa wanaficha uhalisia wa jinsi walivyojipata. Jitafute kivyako vyako."
Kwa mtazamo huo wa Idris kuhusu mafaniki unampa big YES au big NO?
1 307
Msanii wa Bongofleva, Dogo Janja amesema anajivunia uzuri wa mke wake kwa sababu mtoto wao amepata Mama mrembo sana.
"Mtoto wangu ana Mama mrembo sana," ameandika Dogo Janja katika Instagram yake.
1 307
TRANSFOMA 8 ZAKAMATWA DAMPO PUGU
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kinondoni ,Kusini na Pwani, limekamata transfoma 8 za kupokea na kupoza umeme zilizoibwa katika mikoa mbalimbali ya Kitanesco hapa nchini kwenye yadi inayofanya biashara ya chuma chakavu eneo la Pugu Dampo, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es salaam.
1 307
(𝐈𝐦𝐞𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐍𝐚 𝐖𝐚𝐚𝐧𝐝𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐖𝐞𝐭𝐮)
KADRI uokoaji unavyoendelea, sambamba na miili ya waliofariki dunia kuzidi kuongezeka, ripoti ya awali kutoka kwa timu maalum ya wanajiolojia imebaini sababu ni Mlima Hanang', mkoani Manyara 'kushiba' maji, ukaelemewa.
Vilevile, wataalamu hao wamebaini mlima huo una chembe za volcano, jambo ambalo kitaalamu limechochea kuibuka kwa maporoko hayo.
1 307
Anauliza @officialalikiba
"Wimbo wangu wa mwisho kumshirikisha muimbaji wa kike, ilikuwa #SingleBoy ft @JideJaydee …. Wimbo wangu ninaotoa leo nimeimba na Malkia mwingine. Unahisi nani??"
Dondosha comment
1 307
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hapo jana (Alhamisi) alisafiri kuelekea mkoani Manyara na kukagua uharibifu uliosababishwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Hanang mkoani humo Jumapili.
Akitoa taarifa kwa Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, alisema idadi ya waliofariki katika mafuriko hayo Desemba 3 imeongezeka hadi 76 kutoka kiwango cha Jumatano 69, na kuongeza kuwa mafuriko hayo yamesababisha zaidi ya watu 5,600 kukosa makazi, na mazao 750 ya shambani yameharibiwa na mifugo mingi kuuawa.
“Takriban watu 440 kati ya 5,600 waliokosa makazi wanakaa kwenye vibanda vitatu shuleni huku wengine wakikaa na jamii,” alisema Mhagama.
Timu ya maafisa 1,285 kutoka idara za ulinzi na usalama walikuwa wakiendelea kutafuta miili zaidi, aliongeza.
"Serikali itawatimizia gharama za matibabu, chakula, na mahitaji mengine katika safari yenu ya kupona," Rais Hassan aliwahakikishia baada ya kukagua eneo la uharibifu na kutembelea wagonjwa waliolazwa hospitalini, na wale wanaokaa kwenye makazi.
1 307
WAKRISTO UKWELI NI UPI? BIBLIA IMERUHUSU WATUMISHI KUTOBOA PUA? KUFUGA RASTA? KUCHORA TATTOO JE?
Kumekuwa na maswali mengi juu ya mionekano ya watu hao wanaojiita wao ni Manabii wa Mungu, kwamba huko nchini kwao wana makanisa yao na yanajaza waumini hiyo ikimaanisha kwamba wanakubalika. Lakini pia wamekuja Tanzania kwa lengo la kutenda miujiza, kukanyaga mafuta na kubariki mamilioni ya watu.
Lakini Manabii hao wapo tofauti kidogo, wametoboa pua na kuweka vipini, wamefuga rasta, wamechora tattoo na hata lifestyle yao ni ya kidunia zaidi, kwa muonekano hawana utofauti na wasanii wa Muziki wa kidunia kama kina Diamond Platnumz, Burna Boy, Davido n.k. walipoulizwa kuhusu muonekano wao walisema ni kawaida ni sehemu ya kujipamba na biblia haijakataza mtu kujipamba.
Kwenye upande wa rasta zao wanasema hata Samson wa Delila alikuwa na rasta na zilimsaidia kupambana na maadui zake. Kama una uelewa kiasi kuhusu uhusiano wa biblia na kufuga rasta, kutoboa pua na tattoo je ni kweli haya matendo yameruhusiwa kwa mwanaume? wape elimu wasioelewa.
1 307
"Wanayoongea kuhusu mimi hayanishtui kwasababu hawana uthibitisho kama ni kweli. Mimi nimewahi kuoa na nilidumu kwenye ndoa kwa miaka 9 na tukafanikiwa kupata mtoto mmoja, nina mtoto mwingine Zanzibar ana miezi 8"-- Juma Lokole, Mtangazaji wa Wasafi FM.
Toa maoni yako
1 307
"Kwenye shughuli ya kumcheza mtoto wangu niliyoifanya hivi karibuni nilitumia milioni 34 za Kitanzania. Nimetunzwa mamilioni ya pesa na kila niliyewahi kumtunza kwenye shughuli yake ilikuwa ni lazima aje anirudishie pesa zangu na riba juu"- Kungwi na Mganga wa kienyeji Lulu White.
1 307
Mtangazaji na Mchungaji Harris Kapiga na mkewe washerehekea kutimiza miaka 20 ya ndoa yao tangu walipooana.
1 307
ROSE MUHANDO KUJA NA POMBE
Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando ametangaza kuachia wimbo wake mpya ambao ameupa jina la Pombe. Siku za hivi karibuni Rose Muhando alitangaza kuwa wimbo wake huo mpya utakuwa ni zaidi ya Secret Agenda ambao aliuachia mwaka jana na ukafanikiwa kupasua anga kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Kaa mkao wa kula kuisikiliza POMBE ya Rose Muhando.
1 307
⚠️ Manabii hao watua Tanzania kuungana na Prophet Malisa kushusha uponyaji kuelekea usiku wa mkesha wa maajabu yasiyo na hesabu
Watumishi hao wa Mungu wanatarajia kuungana na mtumishi wa Mungu Prophet Malisa kutoka Tanzania katika mkesha utakaofanyika tarehe 8/12/2023 katika viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar kuanzia 11:00 mpaka asubuhi
ZAIDI KUWAHUSU
Nabii Passion Java(36) ni mhubiri kutokea nchini Zimbabwe, anatajwa kuishi Marekani, pia ni socialite, promota wa muziki, mjasiriamali na mwandishi wa vitabu. Kanisa lake mwanzo aliliita Kingdom Embassy lakini baadaye akalibadili jina kuitwa Passion Java Ministries
Nabii Java anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola $50 millioni ambazo takribani shilingi bilioni 125 za Tanzania. Katika mahojiani kipindi cha nyuma alipoulizwa kuhusu chanzo cha utajiri wake alisema kuwa kanisa ni biashara na ndicho chanzo chake kikuu cha mapato, kanisa lake lina matawi nchi kadhaa. Alipoulizwa kuhusu mtindo wa rasta wa nywele zake alisema ni mambo ya Kimarekani
Nabii Java ana mke anayeitwa Lily ambaye wana watoto 2, lakini kabla aliwahi kuoa mwanamke mwingine anayeitwa Yasmin ambaye walizaa mtoto 1, alimpa talaka Yasmin baada ya kukutana na Lily mkewe wa sasa
Kwa upande wa nabii Lovy Elias(37) ni mwanamuziki pia mjasiriamali, ana asili ya Congo na aliwahi kuwa mmoja wa wanamuziki wa kundi la Longombas ingawa alizaliwa Kenya na kuanza shule akiwa Kenya, baadaye alihamia Marekani kuendelea na elimu yake kisha kuanzisha kanisa lake la Revelation Church of Jesus Christ lililopo Marekani anakoishi. Anatajwa kuwa ukwasi pia ana mke
1 307
⚠️Kufuatia matukio ya watu wanaojiua na wengine wakifa na siri za maumivu yao mioyoni mwao, Amanda Poshy mwigizaji wa Kibongo anayeishi Uingereza kwasasa na familia yake, afunguka ikiwemo kisa chake yeye
"Wapendwa kila siku naandika mnaweza kuona mimi sina kazi lakini kwenye kuelekezana naokoa maisha ya watu wengi bila kujua na pia siwezi kushangaa Waafrika asilimia 90% tumejaa chuki, kudhalilishana, dharau, ushenzi hata mtu ana jambo lake anaogopa kukuambia na yote hii inafikia mtu anabeba mazito mpaka kifua kinajaa kinakaribia kupasuka anaona suluhisho bora kujitoa uhai
Ukiangalia matukio ya baadhi wanaojiua kuna wapuuzi wasio na akili wanatukana wanaojiua wanawasema vibaya lakini narudia tena unaloweza kulibeba wewe kuna mwenzio hawezi na analoweza kulibeba mwi ngine wewe huliwezi
Nawapeni mfano wangu mimi kidogo tu, kwenye maisha yangu nimepitia maumivu makali mno kiasi kuna mambo nimeyapitia ambayo hata bibi na babu zangu hawajayapitia kuna kipindi nilikata tamaa na ukiangalia unaweza ukamueleza mtu akachukulia kama vile ni kitu cha kawaida ila mtu huyo huyo angesikia nimejiondoa uhai angesema khee kumbe alikuwa na mazito
Lakini huwezi amini nilikutana na mkaka kwenye park alinikuta nalia yule kaka aliniomba nimuambie nini tatizo hamuwezi amini maneno aliyoniambia nilisimama nikajifuta machozi tokea siku ile nilijiona mpya
So hii ndio maana ya kila wakati kuwaambia kama una tatizo nitumie Dm nieleze angalau ushauri tutakaopeana huwezi jua utakusaidia kiasi gani au pia ni bora usimamishe mtu barabarani mweleze kinachokuumiza usiogope
Halafu niwape siri hakuna watu wazuri wa kuongea nao kama watu msiofahamiana na wengine inakuwa ni malaika waliokujia kwa njia tofauti" ameandika
