fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
Winga wa Al Nassr 🇸🇦 Sadio Mane (31) amefunga ndoa hii leo Januari 7, 2024 huko Keur Massar, Senegal 🇸🇳 na mrembo ambaye
Winga wa Al Nassr 🇸🇦 Sadio Mane (31) amefunga ndoa hii leo Januari 7, 2024 huko Keur Massar, Senegal 🇸🇳 na mrembo ambaye jina lake halijawekwa hadharani. Kila la heri fundi wa Mpira Sadio ❤️

"Natamani Mungu anijaalie nikifikisha miaka 40 niwe nimemaliza kuzaa, niwe nimemaliza majukumu yote ya mihangaiko nibaki na k
"Natamani Mungu anijaalie nikifikisha miaka 40 niwe nimemaliza kuzaa, niwe nimemaliza majukumu yote ya mihangaiko nibaki na kazi ya kulea, kula bata la uhakika. Mungu nipe uhai na Afya njema"- Wolper

"Jifunze kukaa mbali na vita ya familia, hiyo vita inayoendelea kwenye familia yako haikusaidii inakuua, vita za familia zina
"Jifunze kukaa mbali na vita ya familia, hiyo vita inayoendelea kwenye familia yako haikusaidii inakuua, vita za familia zinaleta vitu vinne kwenye maisha yako ambavyo hutaviona. Kwanza vinakuletea depression ya maana ambayo haina kichwa wala miguu, pili vinakuweka mbali sana na Mungu, kwasababu muda mwingi utautumia kugombana na kutukanana na ndugu zako hauwezi kuwa na muda wa kumkumbuka Mungu" "Tatu vita vya familia vinabeba laana ambayo itakutafuna wewe, ndoa yako na kizazi chako, hiyo ni laana ambayo shetani anaitengeneza juu yako kwasababu kwenye vita vya familia lazima utataka kumtakia mtu mabaya, utaenda kwa mganga ili kumteketeza fulani. Nne ni kwamba vita ya familia itakufanya usipige hatua ya maisha, achaneni na vita vya familia ni mbaya, inatesa moyo, siyo nzuri kwako jitenge na vita hii ambayo kusudi lake ni kukuteketeza"- Fiona

NISHA NA MUME WAKE - Actress @nishabebee akiwa vacation na Mume wake 🙌🙌😂😂😂huo mguu Wa mjomba etu Sasa nimeishiwa Nguvu😅
NISHA NA MUME WAKE - Actress @nishabebee akiwa vacation na Mume wake 🙌🙌😂😂😂huo mguu Wa mjomba etu Sasa nimeishiwa Nguvu😅😅😅😅Ila wamependeza sana Jamaniii si eeet..???

Watakuwa wenyeji wa wapi hawa?
Watakuwa wenyeji wa wapi hawa?

#HABARI Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijaweza kufahamika amefariki dunia na mwili wake kukutwa uvunguni mwa kitanda huku
#HABARI Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijaweza kufahamika amefariki dunia na mwili wake kukutwa uvunguni mwa kitanda huku akiwa na jeraha usoni katika Hotel ya Lunch Time iliyopo mtaa wa Mnazi Mmoja Manzese jijini Dar es Salaam Mwili wa mwanamke huyo umeonekana hii leo Januari 7, 2024, na taarifa za awali zimeeleza kuwa alifika hotelini hapo na mwanaume ambaye jina lake halijafahamika na kuchukua chumba na asubuhi ilipofika muda wa usafi waligonga bila mafanikio na mlango ulikuwa umefungwa na walipochukua fungua za ziada walikuta mwili uvunguni huku mwanaume huyo akitokomea kusikojulikana. Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wanaume kutofikia hatua kama hizo kwani na kudai kuwa inaonekana mwanamke huyo ameuawa na mwanaume aliyefika naye katika eneo hilo. Maafisa wa Polisi waliofika eneo la tukio na kuuchukua mwili wamesema kwamba taarifa zaidi zitatolewa uchunguzi utakapokamilika.

"Mtu yupo kwenye husiano lakini kiwiliwili na moyo kwa Rushaynah, nipumnzisheni jamani. Nipewe maua yangu wamegoma kumove on"
"Mtu yupo kwenye husiano lakini kiwiliwili na moyo kwa Rushaynah, nipumnzisheni jamani. Nipewe maua yangu wamegoma kumove on"- Rushaynah

"Alafu sijali lolote bwana ninae na ninatamba nae🫶"-Zaiylissa kwa Rushaynah
"Alafu sijali lolote bwana ninae na ninatamba nae🫶"-Zaiylissa kwa Rushaynah

NILIMUUA MWANANGU KWA BAHATI MBAYA NA SASA NIKO JELA. "Ilikuwa ni majaribu tu mtoto wangu msichana ambaye alikuwa na miaka 13 alianza tabia ya kutoroka shuleni akawa ananisumbua nikawa nampeleka shule na kumrudisha, sasa ikafika wakati nikaona kwamba amezidisha tabia ya kutoroka anaacha masomo na ni mtoto mdogo. Sasa mzazi nilivyoona anazidi kuharibika siku moja nikachukua fimbo nikaanza kumchapa" "Nilimchapa lakini sijui ni nini akafariki tu hivyo, ndio nikashikwa nikashtakiwa na kesi ya mauaji. Nimekaa lumande miaka miwili na nusu na nimefungwa miaka mitatu, nilikubali kosa kwasababu ni kweli ni mimi mwenyewe ndio nilitenda. Nina uchungu katika roho yangu na sio rahisi kuikubali hii hali lakini kupitia nguvu za Mwenyezi Mungu unaona nikama uko huru" "Ukweli Mungu ni mwema, kwasababu mimi nilipokuwa nyumbani nilikuwa najishughulisha na maisha yangu kwasababu nilikuwa nataka watoto wangu wasihangaike, wasikose chakula, mavazi na malazi lakini kwa ile kujidanganya kwa binadamu sikuwa namuweka Mungu mbele kwamba yeye ndiye muweza wa yote. Lakini tangu nimefika hapa nimemjua Mungu na nimejua kila kitu kinawezekana kupitia nguvu zake Mungu" "Alikuwa ni mtoto wangu lakini nilikuwa nimepewa na Mungu, kwasababu hata alivyoniponyoka kutoka kwenye mikono yangu haukuwa mpango wangu lakini hiyo naona ni njia moja Mungu aliitumia ili niweze kutambua mapenzi yake. Sasa hivi mimi ni mfungwa kimwili lakini kiroho mimi nimefunguliwa kwasababu nimekuja hapa nimemjua na namtumikia Mungu na ninajua amenisamehe na ameniweka huru sasa mimi sio mfungwa tena, natumikia muda wangu hapa nasubiri ukiisha niende kumtumikia Mungu"- amesema mwanamke huyo pichani ambaye ni mfungwa huko nchini Kenya

photo content

Mfahamu Kocha anayechukua Mshahara Mrefu kuliko wote kwenye mashindano ya Afcon Msimu huu, Djamel Belmadi wa Algeria analipwa mshahara wa Euro 208,000/= kwa mwezi sawa na milioni 570 za Kitanzania kwa Rate ya Leo ya kutoka bureau de change ya uhakika Kadoo @kadoobdc Pesa kama zote Orodha ya makocha 15 wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko wengine Afcon. 1 – Djamel Belmadi (Algeria) – 208,000 euros 2 – Rui Vitoria (Egypt) – 200,000 euros per month 3 – Jean-Louis Gasset (Ivory Coast) – 108,000 euros 4 – Walid Regragui (Morocco) – 60,000 euros 5 – Hugo Broos (South Africa) – 50,000 euros 6 – José Peseiro (Nigeria) – 46,500 euros per month 7 – Chris Hughton (Ghana) – 46,000 euros per month 8 – Aliou Cissé (Senegal) – 46,000 euros per month 9 – Sebastien Desabre (DRC) – 41,373 euros per month 10 – Kaba Diawara (Guinea-Conakry) – 30,000 euros 11 – Rigobert Song (Cameroon) – 29,000 euros per 12 – Tom Saintfiet (Gambia) – 22,982 euros per month 13 – Pedro Gonçalves (Angola) – 18,382 euros per 14 – Jalel Kadri (Tunisia) – 11,000 euros per month 15 – Baciro Candé (Guinea-Bissau) – 9,000 per month

photo content

Unapenda Nini kuhusu huyu jamaa😅😅🙌🙌🙌🙌🙌🙌?
Unapenda Nini kuhusu huyu jamaa😅😅🙌🙌🙌🙌🙌🙌?

Imekuwa huzuni sana katika Majeshi ya Israeli IDF kumpoteza binti wa vikosi maalu vinavofanya kazi ya kupambana na Hamas baad
Imekuwa huzuni sana katika Majeshi ya Israeli IDF kumpoteza binti wa vikosi maalu vinavofanya kazi ya kupambana na Hamas baada ya Sgt Shai Garmai wa Eneo la Samaria na Yudea. Alikuwa akiwafukuza Wapiganaji wa Hamas gari lake likapigwa na Bomu akapoteza Maisha. Abarikiwe Yeye Ahukumuye kwa Haki.

***Mdau anauliza; "hivi hii Rangi ya NJANO katika School Bus(Mabasi ya shule) uwa inamaanisha nin??***
***Mdau anauliza; "hivi hii Rangi ya NJANO katika School Bus(Mabasi ya shule) uwa inamaanisha nin??***

"Kocha anavyolalamika kuwa Kuna baadhi ya wachezaji hafurahishwi na viwango vyao, hii inatuaminisha pengine nyuma ya pazia ki
"Kocha anavyolalamika kuwa Kuna baadhi ya wachezaji hafurahishwi na viwango vyao, hii inatuaminisha pengine nyuma ya pazia kikosi hajakiita yeye, na kama amekiita yeye anaitaje wachezaji ambao anajua hawaingii kwenye mfumo wake?". 🎙️Juma Mwambusi Kocha wa zamani wa Ihefu,Yanga

Bondia Hassan Mwakinyo ametoa ombi kwa Promota wa pambano lake la January 27,2024 kati yake na Bondia Miya NKanku kutoka Cong
Bondia Hassan Mwakinyo ametoa ombi kwa Promota wa pambano lake la January 27,2024 kati yake na Bondia Miya NKanku kutoka Congo kwamba hataki Wachambuzi wa pambano hilo wawe Mabondia wenzake kutoka Tanzania wanaotumika kwenye mapambano mengine. Pambano hilo litapigwa New Amaan Complex Zanzibar na tayari Shirikisho la Ngumi Duniani (WBO) limeridhia liwe la kuwania ubingwa wa WBO Africa likiwa ni pambano la round 10 uzito wa kilo 72. Mwakinyo amenukuliwa akisema “Ombi la wazi kwa Promota Semunyu kutoka Familia ya Mogadishu pamoja na Mimi C.E.O wao, hatutaki Wachambuzi Mabondia mnaowatumia kwenye mapambano mengine, ikiwa itawaridhia Azam TV wakupe Kamati yao ya Wachambuzi yani Patrick Nyembela na Team yake ni Watu wamekuwa na utashi wa juu zaidi na ikiwa hakuna budi awepo Bondia basi kura zangu Naseeb Ramadhani, namba moja na ukikosa kabisa majibu, nitakuletea Wachambuzi wa ngumi kutoka Tanga”

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema hakuna fedha yoyote iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema hakuna fedha yoyote iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ajili ya maandalizi ya timu zitakazoshiriki fainali za mataifa Afrika (AFCON) hivyo wananchi wapuze taarifa hizo. Kauli hiyo imekuja baada ya michango mbalimbali inayoendelea kwa ajili ya kuziunga mkono timu za taifa hususani zilizofuzu michuano hiyo, ambapo baadhi ya wadau wa michezo wamedai timu zote 24 zilizofuzu zimekwishapewa fedha za maandalizi na CAF. “CAF hutoa zawadi za fedha kwa washindi kuanzia hatua ya 16 bora hadi bingwa wa michuano hiyo mikubwa kuliko yote barani Afrika. Tayari TFF na wachezaji wa Taifa Stars wameshafanya kikao na kukubaliana kuhusu mgao wa fedha hizo za zawadi kwa kila hatua ambayo timu itafika,” imesema TFF.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeujulisha Umma kuwa ndege yake aina ya Q300 (Bombardier) iliyopo kwenye matengenezo nchini Malta sio miongoni mwa ndege mpya zilizonunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha Mpango wa Ufufuaji wa ATCL ulioanza kutekelezwa mnamo mwaka 2016. Taarifa ya Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha ATCL kwa Umma imebainisha kuwa ndege hiyo haikununuliwa na Serikali bali ni miongoni mwa ndege mbili zilizopatikana kupitia mbia aliefanya uwekezaji kwa kuleta ndege mbili za aina ya Dash 8-Q300 mwaka 2008 na kupewa usajili wa namba 5H-MWG na 5H-MWF kwa kufuatana. ATCL imeongeza kuwa Ndege hizo za Q300 ziliundwa mnamo mwezi Mei 1997 na kabla ya kuwasili nchini zilikuwa zimetumika kwa takribani miaka 11. Hata hivyo, Kampuni ya Bombardier (Manufacturer) ilisitisha uundwaji wake tangu Mei 2009. “Ndege zilizonunuliwa na Serikali kuanzia mwaka 2016 ni ndege kumi na tatu (13) ambazo ni Q400 - Bombardier (5), Airbus A220-300 (4), Boeing 787-8 (2), Boeing 767-300F (1) na Boeing 737 MAX-9 (1).” imesema taarifa hiyo. “ATCL ilibakiwa na ndege ya Q300 moja yenye usajili wa namba 5H-MWF baada ya ndege yenye usajili wa namba 5H-MWG kupata ajali mwaka 2012 na kushindikana kutengenezeka kutokana na ukubwa wa uharibifu wa ndege hiyo.” “Ndege iliyobakia iliendelea na safari zake hadi mnamo Mei 2017 baada ya waundaji (Manufacturer) wa ndege hizi kuagiza kuwa ndege zote za aina hii duniani zisiendelee na safari hadi zitakapofanyiwa matengenezo ya lazima ya matenki ya mafuta kwa ajili ya usalama.” “Sanjari na agizo hilo, Ndege hii pia ilihitaji kufanyiwa matengenezo makubwa yanayojulikana kitaalamu kama "6C-Check" ambapo ilifika nchini Malta mwezi Novemba 2020 kwa ajili ya matengenezo hayo.” imesema ATCL. Aidha, kutokana na changamoto ya upatikanaji wa vipuri iliyosababishwa na athari za UVIKO 19 ambapo wazalishaji wa vipuri walipunguza na wengine kuacha utengenezaji wa vipuri kumesababisha matengenezo hayo kutokamilika kwa muda uliotarajiwa. Ndege hii inatarajiwa kurejea nchini baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo. Follow

photo content