E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
DODOMA; Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuvunja Baraza la Mawaziri kwa kile anachodai kuwa wameshindwa kuchukua hatua kwa wale walio chini yao waliotajwa waliotajwa kufanya ubadhilifu wa mali za umma katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
-
Mbunge huyo ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa mjadala wa kuchangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu ripoti ya CAG ulioanza jana Novemba 2.
-
"Toka jana na leo kila Mbunge akisimama anazungumzia ubadhilifu uliofanyika, yamefanyika madudu makubwa sana mpaka nasikia moyo wangu unavuja damu. Taarifa ya CAG Rais amesomewa mwezi wa Tatu. Leo nimiezi Sita mmefanya nini katika wizara zenu kwa ubadhilifu ulioanishwa? Tunamshauri Mhemiwa Rais avunje Baraza la Mawaziri kuanzia kesho. Tulipofikia ni pabaya." amesema Mbunge huyo.
1 307
DODOMA; Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasam amesema ifikie mahala wabadhilifu wa mali za umma wachukuliwe hatua kali badala ya kufuata mifumo ya utawala bora na badala yake watumie udikteta ili kukomesha tabia hiyo kwa wanaofanya ubadhilifu.
-
Mbunge Tabasam ameyasema hayo leo Novemba 3 Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Bunge akichangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
-
"Ifikie mahali tuanze kudikteti mambo mengine. Habari ya Utawala Bora kwenye wizi hapana! Utawala Bora majambazi yanazidi tuu. Mtu anaiba kuku anauwawa hawa wanaiba pesa za kutosha," amesema Mbunge huyo.
1 307
ESTER BULAYA: BALOZI SIRRO ARUDISHWE NCHINI AJIELEZE KUHUSU FEDHA ZA MFUKO WA POLISI
Akichangia mjadala wa uchambuzi wa Ripoti ya #CAG, Mbunge huyo wa Viti Maalum amesema kwa mujibu wa Kifungu cha 66(3) cha Sheria ya Jeshi la Polisi Sura Na. 333 kimeainisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ndiye mwenye mamlaka ya matumizi ya Fedha za Mfuko huo ambapo hadi Ukaguzi unafanywa Balozi Simon Sirro alikuwa IGP
Amesema ukaguzi umeonesha kulikuwa na ubadhirifu wa takriban Tsh. Bilioni 1, hivyo Serikali imrudishe Balozi Sirro aje aeleze kilichotokea kwasababu Mfuko huo ulianzishwa kwa lengo la kuwasaidia Askari wanapopatwa na matatizo kazini
1 307
Akichangia mjadala wa uchambuzi wa Ripoti ya #CAG, Mbunge wa Geita Vijiji, Joseph Kasheku Musukuma amesema “Katika kipindi ambacho Wabunge wanataka kulieleza Taifa ni kipindi hiki cha Ripoti ya CAG, wapo 1, 2, 3 wengine wapo huko ‘Kantini’, hakuna ‘Usiriasi’. Kaeni hapa msikilize mjue tunachokisema, nimuombe Rais na Waziri Mkuu wafute safari zote hadi taarifa hii ikamilike.”
1 307
Christopher Olonyokie Ole Sendeka mbunge wa jimbo la Simanjiro amechafukwa na wizi uliotajwa na CAG na kuahidi kuwa ataenda kuwataja waliohusika na upotevu wa pesa za Standard Gauge Railway (SGR).
Aidha Mbunge Ole Sendeka ameendelea kueleza kwa maumivu kuwa kama angekuwa Waziri hakuna ambaye angebaki ofisini endapo tu alitajwa na ripoti ya CAG.
1 307
Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara amependekeza wanaobainika kula fedha za Serikali wanyongwe ili wabaki watu wema katika Taifa na wanaoonekana ni wazembe katika kazi wafukuzwe.
Waitara amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).
"Kwanza Mwenyekiti kuwanyonga hawa tutakuwa hatujawaonea, ni haki yao kwa sababu katika utumishi wa umma ukiacha sisi Wabunge na Waheshimiwa Mawaziri, Watumishi wa umma wengi wamesoma na wanaiba kitaalamu, uzembe ulipo ni sisi Wabunge kwamba mtu ameshaiba, ripoti ipo, taarifa ziko mezani, vyombo vipo hawawajibishwi. Hivi niye Waheshimiwa mnawafundisha nini watoto wetu?, kwamba wao wanajua wakikua wakiiba watahamishwa kutoka kwenye tasisisi hii kwenda nyingine na hakuna uwajibikaji". amesema Waitara.
Amewaomba Wabunge wenzake kusimamia weledi na wasisubiri kuja kuambiwa wachukue hatua na kuongeza endapo hatua hazitachukuliwa kwa waliotajwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2021/2022, mwaka 2024 hatachangia.
1 307
Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya amesema kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mashine za kukusanyia mapato katika baadhi ya Halmashauri nchini zilizimwa bila sababu za msingi.
"Chamwino walizima mashine ya POS kwa muda wa siku 1,905, Uvinza walizima mashine ya POS kwa siku 1,133, Ushetu walizima mashine ya POS kwa siku 397, Sengerema walizima mashine ya POS kwa siku 185. Mnajua kwa nini wanafanya hivi? Kwa sababu tunawalea". amesema Bulaya
Amesema hao Wakurugenzi wa hizo halmashauri bado wapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) wanasema watawachukulia hatua ila hakuna matokeo.
"Wengine bado wapo kwenye vituo vya kazi halafu mnataka tuyanyamazie, mnakumbuka wakati Rais anapokea ripoti alivyozungumzia mikopo ya 10% fedha ambazo hazijakusanywa zimeongezeka kutoka Bilioni 47 mpaka Bilioni 88". ameongeza Bulaya.
1 307
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko amesema wao kama wabunge wamesema sana kuhusu kuchukuliwa hatua kwa wanaofanya ubadhirifu hivyo ni wakati wa wanaohusika kuwekwa hadharani na hatua nyingine zifuate.
"Watanzania pia ni maskini wanalipa kodi ili tufanye maendeleo, leo unakuta Mtanzania kule kijijini anakamatiwa kuku ili achangie kujenga darasa au zahanati halafu tunapoteza matrilioni ya fedha kwa uzembe,"amesema Matiko.
Amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) waliendesha mnada kwa mfumo wa kielektroniki wa kuuza vitalu vya utalii ambapo kampuni ya MS Game Hunters Limited ilichukua vitalu saba na wakagoma kulipa takribani dola laki 5.9 na walipoulizwa kwenye kamati walisema hawakuwa na mamlaka ya kuwazuia.
1 307
"Binafsi kama Mwalimu nina furaha kucheza hii derby kubwa, kwa ujumla tumejiandaa vizuri sana na tulikuwa na wiki nzuri ya kujindaa kipi bora cha kufanya leo, najiamini na nina amini wachezaji wangu kwakuwa watacheza mchezo vizuri sana, kesho tutacheza tofauti na tulivyokuwa tunacheza huko nyuma, tutacheza kwa ubora mzuri tofauti na derby iliyopita".- Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga SC.
Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥
Toa maoni yako
1 307
Ubashiri uliotolewa na Chombo cha habari cha 90MINS kuhusu Washindi wa Ballon D'Or miaka kumi (10) ijayo. Utabiri huo umemtaja Kylian Mbappe kushinda Tuzo sita (6) kati ya kumi (10).
NB : Darubini ya hawa jamaa haijamuona Erling Haaland 🇳🇴 🤔
Toa maoni yako
1 307
Msanii wa Bongofleva ZUCHU kutoka WCB WASAFI Ameshangazwa na kitendo Cha TAMKO lililotolewa na Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda Kuwashusha VYEO waalimu ambao wameonekana wakiwa kati kati ya Watoto Huku wakicheza na wanafunzi hao Wimbo wake wa "Honey"
Akiongea Kupitia katika kipindi Cha Jana na Leo Cha Wasafifm Zuchu Amesema kuwa:
"kwanza imeniumiza mno Kwa sababu kitu kilichotokea pale hakikuwa KIBAYA wala Cha kudhuru Mtoto Kwa namna nyingine Yeyote, ni vitu ambavyo Sisi kama wasanii tukienda mashuleni Huwa tunatambulishwa Kwa Kazi zetu za kisanaa na wanazifurahia"
"Ni kitu ambacho kimeniuma sana sikutegemea WALIMU Kushushwa Vyeo Kushushwa mishahara Yao Kwa sababu ya Wimbo wangu!!"
"Wimbo wa Honey una Miezi Mitatu tangu utoke, maudhui yake yanajulikana na Mashairi yake yanajulikana Hata kama mnayataka Mashairi yake niwaforwadie muyasome SIDHANI kama Kuna sehemu Ambayo Haina maadili"
"Tukubali tukatae Mtoto anavyocheza Wimbo wowote Huwa anaikariri Kwa Haraka sana, hakuna Nyimbo Ambayo inafundishwa shuleni! Nyimbo Yeyote Mtoto Lazima aisikilize Nyumbani kwao Kwa Mzazi wake, maudhui ya Nyimbo zinazochezwa na watoto tunazijua hatuna haja ya kufafanua sana"
"Wimbo kama wa Honey maudhui yake ni ya kawaida Hauna Mashairi ya kutusi hivyo kama Msanii sikuona sehemu yeyote kwenye Mashairi Mtoto akiisikiliza na kuiimba kutakuwa na Lugha ya matusi ndani yake" Amefunguka Zuchu Kupitia Wasafifm 🗣️
Follow ukurasa wetu wa Instagram 👇
https://instagram.com/e_plus_media?igshid=MzNlNGNkZWQ4Mg==
1 307
"Wazazi tusiwalazimishe watoto wetu kusoma Udaktari, tuwaache watoto wenyewe wapende maana udaktari ni kazi ambayo mtu anatakiwa apende mwenyewe"- Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
1 307
Pichani ni Salama Salmini, Staa mkongwe alitetemesha kwenye Tentemente ya Dudubaya ambaye kwasasa ameamua kuigeukia stara na amekuwa mtu wa dini zaidi.
1 307
"Kila chenye mwanzo hakikosi mwisho, siamini kama huu ni mwisho, ila naziona dakika za mwisho. Tulianza pamoja! tulifurahi, tulishinda sana, ila acha tumalize dakika za mwisho pamoja kesho"- Rayvanny
1 307
MIMI NA CHIBABA HATUNYONYANI; WEMA SEPETU
"Mimi najitaftia na mwenzangu anajitaftia tuko 50 kwa 50 hakuna ambaye ananyonyeka, nilichonacho naweka mazeni tunagawana na yeye akipata anaweka mezani tunagawana. Hakuna ile kwamba mimi changu usiguse! hapana, tunasapotiana na kuna muda nakosa kabisa ananisaidia au yeye akikosa kabisa namsaidia, tunaenjoy mapenzi yetu kwa aina hiyo"- Wema Sepetu
1 307
MPINA HAJUI HESABU, ACHA NIMREJESHE DARASANI; MWIGULU NCHEMBA
1. Katika Bajeti 44 trilion zinapigwaje 30 trillion? Alafu na mishahara ya Trilion 20 ikaendelea kulipwa? Huku mtaani miradi ya Matrilion ikaendelea kutekelezwa? Hata hili umeshindwa kuling'amua?
2. FIU kwa sehemu kubwa inachambua miamala ya secta binafsi, hicho unachoona kwenye hiyo ripoti yao ni namna Wafanyabiashara wamepata ahueni wanafanya manunuzi makubwa nje ya nchi kwa pesa nyingi wanakuja kuuza kwa faida kubwa, hiyo ndiyo faida ya uchumi wa watu na siyo vitu, awamu yenu mlifunga nchi biashara zikafa ndio maana hili linakuwa suprise kwenu. Uchumi halisi unapokuwa lazima miamala mingi ifanyike nje na ndani ya nchi kwasababu biashara haina vikwazo wala kufungiwa. Mama karejesha imani ya Wafanyabiashara nchini, wawekezaji wengi wamepata uhakika wa mitaji yao wameamua kuleta mapesa mengi kwa njia ya miamala maana dunia sasa ni cashless economy.
3. Hakuna mkopo uliovunja sheria, hakuna mkopo ambao haukupitishwa kwenye bajeti. Bajeti ambayo wewe uliiunga mkono kwa kinywa chako binafsi ukatamka "Ndiooo". Kwa taarifa yako tu awamu hii kila kitu kimewekwa wazi wananchi wanaona kila jambo na wanapata muda wa kukosoa, wanajibiwa kwa hoja bila kutekana na kuuana. Awamu yenu mmeliingiza Taifa hili kwenye mikopo umiza (Nyonyadamu) mliyokuwa mnachukua mikopo kimyakimya huku mkidanganya watu kuwa mnajenga kwa pesa za makusanyo ya ndani kumbe ni uongo mkubwa. Tena mlikopa kwa masharti mabovu ya kihuni mkitoa pesa kwa single source kwa makampuni yaliyowapa rushwa na ushahidi upo hadharani CAG kausema. Mlikopa kwenye mabank ya kibiashara yenye riba za kutisha, leo hii unapata wapi uhalali wa kushuku mambo ambayo yako wazi kila mahali? Mama anatafuta hela kwenye taasisi zenye riba ya chini ya 1%, kila mkopo unawekwa hadharani, unakoelekea panajulikana na kazi inaonekana, hakuna tena blah blah.
4.SGR inaendelea hakuna kilichosimama, natambua wewe na wenzio hao mnaokesha kupiga majungu mlitarajia mradi huu ukwame ili sukuma gang mjigambe kwamba nyinyi ndio mabingwa na miamba ya nchi hii, hilo mmekwama endeleeni kumeza panadol maana mama hana shughuli ndogo kila kona anapeleka maendeleo. Mama alikuta lot 2 tena zikiwa asilimia za chini sana, kwa muda mfupi kapiga asilimia zaidi ya 90 na kaanzisha nyingine 5, hapa ndio panawafanya mchanganyikiwe kabisa.
5. Kuhusu uhujumu uchumi, as we speak ulitakiwa uwe gereza la butimba kwa uhalamia na ukatili mkubwa uliowafanyia wavuvi wa nchi hii, umewatia umasikini wa kutisha, ulichoma nyavu zao ukawafunga, wengine wakatoroka nchi, uliwafanyia hivi kwasababu hawakukupa rushwa, hili liko wazi na ushahidi upo.
6. Nawapa taarifa tu na hao wenzio, nchi imetejea kwenye mstari sahihi, wananchi wana furaha, hawatekwi, hawatishwi, hawabambikiwi kesi, wapinzani wamepewa kila wanachotaka lakini hawana ajenda, uchumi wa watu umeimarika, fedha zinaonekana mtaani, hakuna kilichosimama na miradi mipya ya kutosha.
Mwisho, number hazidanganyi, ni muda mwafaka urejee darasani, weka tunguli zako likizo, weka ulozi wako pembeni ingia kibwetani, ukitoka huko ndio uje tuzungumzie haya mambo lakini kwa sasa huna unachokifahamu yamekuzidi kimo.
