E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
"Mumama jua ni wakati gani sahihi wa kuzungumza na mume wako masuala ya maendeleo, na sio kila wakati umpigie makelele baba wa watu. Kaamua kukutoa kukupeleka dina, dina tena inakuwa siyo dina inakuwa ni makelele, ooh hizi hela tulizomaliza hapa si bora tungenunua kiwanja, si bora tungedunduliza tununue paso"
"Acha kishaufu mwanamke mwenye kichwa kirefu kama mradi wa Mwendokasi, kula chipsi zako rudi nyumbani kamfanyie mahaba mume wako na siyo makelele"- Blandina Lukindo, Mtangazaji wa TV na Radio
1 307
Inaelezwa kuwa muamuzi Ahmed Arajiga ndiye atakayekabiziwa filimbi kuichezesha kariakoo Derby leo November, 5 kama mwamuzi mkuu.
Hii hapa Safu nzima ya Waamuzi wanne watakao kuwa na haki ya kusimamia mchezo huo.
Ahmed Arajiga: Muamuzi wa kati
Mohamed Mkono: Line 1
Kassim Mpanga : Line 2
Ramadhan Kayoko : Fourth official
1 307
CCM itanunua kila goli kwa ng’ombe mmoja kwa timu itakayoshinda kati ya Simba au Yanga Jumapili kwenye mchezo wa ‘derby’ - Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Paul Makonda (@baba_keagan) akizungumza kwenye usiku wa tuzo za #WISACAwards2023
1 307
“Wapinzani wangu wana wachezaji wazuri sana eneo la Kiungo, nami nataka niwazuie wasicheze kutoka eneo hilo, nitachagua wachezaji sahihi wa kazi hiyo, leo watacheza wachezaji wangu bora eneo hilo” Coach Robertinho, Simba SC.
1 307
Sudan Kusini ni nchi inayoongoza Afrika kwa kuwa na watu warefu
Tanzania ni mkoa gan unaongoza kwa watu warefu?
1 307
🎙️ Heung-Min Son:
"Nataka kuhakikisha kila mtu katika nchi yangu anafurahi kuniona nikicheza mpira kwa kiwango cha juu zaidi.
Nina furaha sana kuona bendera za Korea Kusini kwenye uwanja wetu wa Tottenham. Nataka kucheza kwa kiwango cha juu kadiri niwezavyo, Nawashukuru Wakorea Kusini kwa sapoti yao kubwa wanayonipa.
"Najihisi kama ni balozi wa nchi yangu, tunapocheza saa 3 usiku. (Saa za Kiingereza), ni saa sita usiku nchini Korea. Tunapocheza Ligi ya Mabingwa, ni saa kumi na moja asubuhi nchini Korea na kuna watu huwa wanaamka kuniona kwenye TV.
"Lazima nitoe kila kitu kwa ajili yao ili wapate burudani."
1 307
Kwa sasa mvua zinanyesha kwenye maeneo mengi ya nchi yetu, tunaamini Mabwawa ya kuzalisha Umeme yatajaa na tutapumzika na huu Mgao unaoendelea. - MDAU
1 307
Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limefikia makubaliano na Group Amaury (wamiliki wa vyombo vya habari vya France Football na L'Equipe ) ili kuboresha hadhi ya tuzo za Ballon d’Or duniani.
Chini ya ushirikiano huo mpya, UEFA imesema tuzo zote za Ballon d’Or zitasalia pamoja na kuongezwa kwa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa wanaume na wanawake.
Groupe Amaury inaendelea kuwa na haki juu ya chapa ya Ballon d’Or na mfumo wa upigaji kura hautabadilika kazi ya UEFA itakuwa ni kuzitangaza kibiashara na kuandaa event hiyo kila mwaka
Kumbuka Mwaka 2010 FIFA nao waliingia kwenye Ballon d'Or lakini baadaye wakatoka na kuanzisha tuzo ya 'The Best'.
1 307
IRINGA: WAKAMATWA WAKIANDAA NYAMA YA MBWA ILI WAKAWAUZIE WATU
Wananchi wanne wa Kijiji cha Ugwachanya Kilichopo Kata ya Mseke Mkoani Iringa wamekutwa wakimchuna Mbwa kwa ajili ya maandalizi ya nyama.
Akizungumzia kuhusu Mkasa huo Mmiliki wa Mbwa huyo Bi. Veronica amesema kuwa alipata taarifa ya mbwa wake kupotea ambapo alifanya jitihada za kumtafuta na kuwakuta watuhumiwa wanne ambao ni Nicholaus lunyungu, Kalista Mhenzi, Jane Kihaga na Charles Kihaga wakiwa wanamchuna mbwa wake.
Amesema kuwa aliwakuta watu hao wakimchuna mbwa huyo huku wakimwita mmiliki huyo kwa ajili ya kuzungumza faragha jambo ambalo alilipinga na kuwaita majirani kwani tukio la kupotea mbwa mtaani hapo limekuwa likijirudia.
Kwa upande wao wao wanaotuhumiwa kumchuna mbwa huyo wamesema kuwa walimkuta mwenzao Kalista Mhenzi akimchuna mbwa mara baada ya kusikia vishindo ndani kwake.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Igavilo Kijiji cha Ugwachanya Bi Ester Mkini amekiri kuwepo kwa tukio la mbwa kuchunwa kwa ajili ya nyama ambapo watuhumiwa hao wanaitumia kwa ajili ya kula wao wenyewe.
Amewaonya wananchi wa eneo lake kuacha tabia hiyo kwani haikubaliki huku watuhumiwa wa tukio hilo wakishurutishwa kununua mbwa mwingine na kumkabidhi mmiliki wake.
Chanzo: Nuru FM
1 307
"Halafu waheshimiwa wabunge mimi najiuliza, ukienda sehemu nyingi sasa hivi ukiingia kwenye maduka tusuti tumepanda kweli bei, ukigusa ni milioni 1.2 lakini anakuja mwingine ananunua hata tano na kamoka kazuri na kingereza kingi kumbe wezi, ukimkuta ofisini mtu ameulamba vizuri kachomekea kumbe ni mwizi,"- Mbunge Musukuma
1 307
Messi au Maradona
Papa Francis:
“Nachagua 🇧🇷 Pele. Maradona akiwa kama mchezaji alikuwa mtu mzuri sana, lakini kama mtu wa kawaida alishindwa kuishi kibinadamu na watu.
"Messi, kwa upande wake, ni sahihi sana, muungwana. Lakini, Kwangu mimi, kati ya hawa watatu, bwana mkubwa ni Pele. Mtu mwenye moyo na ubinadamu mkubwa sana."
1 307
SONIA MONALISA AREJEA NCHINI TANGU ALIPOONDOKA NA PAULA KWENDA KUSOMA UKRAINE.
Ni takribani miaka miwili na miezi kadhaa tangu mtoto wa Mwigizaji mkongwe nchini Monalisa, Sonia alipoondoka kwenda masomoni yeye na Paula Kajala ambapo wote walienda kwa ajili ya masomo. Baadae yalitokea machafuko nchini humo ambayo yalipelekea kuhamishwa na kupelekwa nchini Netherlands kuendeleza masomo yake, na juzi alitua nchini Tanzania kwa mwaliko maalumu wa WASIC akiwa kama host namba mbili kwenye tuzo hizo zilizoonyeshwa kupitia chanel ya Sinemazetu ya Azam TV.
Kupitia ukurasa wa Monalissa wa Instagram ameandika.
"Baada ya miaka miwili na siku zake kadhaa, my daughter is coming back home for the WISAC Awards 2023. Mabibi na mabwana, host wetu namba mbili ni Sonia, karibu nyumbani baby girl"- ameandika
1 307
Pichani ni Sonia Monalisa baada ya kutua kwenye ardhi ya Tanzania hapo jana akitokea nchini Netherlands ambako anasoma masomo ya levo ya juu (Chuo Kikuu).
