fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید 👈

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
Lowassa kipenz cha wanyonge
Lowassa kipenz cha wanyonge

ALIYEVUNJA REKODI YA ELIUD KIPCHOGE AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI KENYA Mwanariadha namba moja duniani kwenye mbio ndefu za mara
ALIYEVUNJA REKODI YA ELIUD KIPCHOGE AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI KENYA Mwanariadha namba moja duniani kwenye mbio ndefu za marathoni duniani Kelvin Kiptum pichani amefariki dunia kwenye ajali ya gari nchini Kenya usiku wa kuamkia leo. Kiptum alivunja rekodi ya dunia mwaka jana kwenye marathoni rekodi ambayo ilikua ikishikiliwa kwa muda mrefu na mkongwe Eliud Kipchoge R. I. P legend

Ulemavu haupaswi kukuzuia kufanya kazi ya ndoto zako. #AfCON2023
Ulemavu haupaswi kukuzuia kufanya kazi ya ndoto zako. #AfCON2023

Bilionea kutoka Nigeria 🇳🇬 na mmiliki wa Access Bank, Herbert Wigwe amefariki Dunia katika ajali ya ndege. Helikopta iliyok
Bilionea kutoka Nigeria 🇳🇬 na mmiliki wa Access Bank, Herbert Wigwe amefariki Dunia katika ajali ya ndege. Helikopta iliyokuwa imembeba Herbert Wigwe na abiria wengine watano akiwemo mkewe na mwanawe, imeanguka Ijumaa jioni mpakani mwa Nevada na California, nchini Marekani

Unampa asilimia ngapi Mke wa Aristote kwa kutengeneza keki hiyo yenye mfanano na sura yake?
Unampa asilimia ngapi Mke wa Aristote kwa kutengeneza keki hiyo yenye mfanano na sura yake?

LOWASSA AWAKUTANISHA CHRISTINA SHUSHO NA BAHATI BUKUKU. Kwa mara ya kwanza tangu waingie kwenye ulimwengu wa Ustaa, waimbaji
LOWASSA AWAKUTANISHA CHRISTINA SHUSHO NA BAHATI BUKUKU. Kwa mara ya kwanza tangu waingie kwenye ulimwengu wa Ustaa, waimbaji manguli wa nyimbo za Injili Christina Shusho na Bahati Bukuku wameingia studio na kurekodi wimbo wao wa pamoja ambao ni wimbo maalumu kwa ajili ya kumuomboleza Edward Lowassa. Wimbo huo unaitwa Shujaa umelala, lakini pia ndani ya wimbo huo wamo waimbaji wengine kama Dayna Nyange, Nay Wamitego na wengine wengi.

KIKWETE: LOWASSA ALIPOPATA CHANGAMOTO NA KUKAA PEMBENI, TULIENDELEA KUWA MARAFIKI Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwet
KIKWETE: LOWASSA ALIPOPATA CHANGAMOTO NA KUKAA PEMBENI, TULIENDELEA KUWA MARAFIKI Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ametoa kauli hiyo baada ya kufika kutoa pole ya Msiba nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, 2024 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Moyo (JKCI). Akizungumzia kiongozi huyo, Kikwete amesema Mwaka 2005 tulipoteuliwa kugombea Urais, mwenzangu akaja kuwa Waziri Mkuu tukapata changamoto katikati mwenzangu ikabidi akae pembeni, tukaendelea kuwa pamoja kuwa marafiki na kushirikiana kwa kila linalowezekana" Kikwete ameongeza kuwa Lowassa ametoa mchango mkubwa katika taifa na yaliyotokea ni changamoto katika maisha lakini hayafuti mema na mazuri aliyofanya kwaajili ya nchi.

#TANZIA Aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Nkenge na Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Diodorus Kamala, amefariki dunia Februari
#TANZIA Aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Nkenge na Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Diodorus Kamala, amefariki dunia Februari 12, 2024 katika Hospital ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Mwaka 2011 Dk. Kamala aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji na Uholanzi ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 na kurejea nchini kuwa Mbunge hadi mwaka 2020.

"Mwaka 1995 siku moja asubuhi nikapokea ugeni mtoto akaja chumbani kuniambia baba kuna ugeni nikawakuta marafiki zangu watatu
"Mwaka 1995 siku moja asubuhi nikapokea ugeni mtoto akaja chumbani kuniambia baba kuna ugeni nikawakuta marafiki zangu watatu, Samwel Sitta, Edward Lowassa na Rostam Aziz, wakaja kuniambia kwamba tunataka muende na Edward Dodoma mkachukue fomu ya kugombea urais mimi nikasema jambo hilo halipo kwenye mawazo yangu, kama yeye lipo kwenye mawazo basi aende, naye akasema siendi bila ya wewe,"- @jakayakikwete "Basi tukabishana mpaka tukakubaliana kwamba wacha twende, tukaenda kuchukua fomu zile tukazijaza zikarudishwa, michakato ndani ya chama mwenzangu hakubahatika mimi nikabahatika kuwemo kati ya wale watano na baadaye tukapiga kura kwenye NEC nikawemo katika wale watatu, tukaenda mkutano mkuu nikawemo katika wawili, lakini kura zangu hazikutosha akapata Mzee Mkapa nikaja kuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje na mwenzangu akaja kuwa Waziri," - Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu #RIPLowassa

Edward lowassa hii ilikuwa Ruandwa - Nzovwe ,Mbeya mjini hii ilikuwa tarehe 19 October 2015 Pumzika Champion 🏆 Mwamba kabisa
Edward lowassa hii ilikuwa Ruandwa - Nzovwe ,Mbeya mjini hii ilikuwa tarehe 19 October 2015 Pumzika Champion 🏆 Mwamba kabisa 🙏

Tayali msanii peter msechu ameshatoa wimbo Maalum Kwaajili ya hayati Edward lowassa Follow us:-https://www.instagram.com/e_pl
Tayali msanii peter msechu ameshatoa wimbo Maalum Kwaajili ya hayati Edward lowassa Follow us:-https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media
+9
KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media

⚠️Tarehe 10 February Katalin Novak Rais wa nchini Hungary amejiuzulu baada ya kuibua taharuki kubwa kwa kumpa msamaha mwanaume aliyehusishwa katika kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto wa kiume. Msamaha aliutoa April mwaka jana kwa wafungwa kadhaa akiwemo mhusika ambaye alikuwa naibu mkurugenzi wa nyumba ya watoto. Lakini siku chache zilizopita ndipo mtandao mmoja wa habari nchini humo uliibua taarifa hiyo ya msamaha wa Rais, ambapo raia walipandwa na hasira na kuanza maandamano hadi ofisi ya Rais kumtaka awajibike aachie madaraka huku pia upinzani wa kisiasa nchini humo nao ukimshinikiza Rais ajiuzulu Ameitikia wito wa kujiuzulu, Rais huyo amesema alikosea kutoa msamaha kwa mfungwa husika kwani alifikiri hakutenda kosa husika. Rais pia ameomba radhi ikiwemo kwa wahanga wa unyanyasaji wa kingono ambao kwa msamaha huo waliona Rais wao hayupo pamoja nao katika mapambano dhidi ya janga hilo, Rais amesema anajali familia pia yeye ni mkiristo mwenye hofu ya Mungu Aidha, aliyekuwa waziri wa wizara husika ambaye aliidhinisha msamaha huo mwaka jana , na yeye amejiuzulu wadhifa wake wa sasa baada ya vuguvugu la wananchi kupamba moto na maandamano kuongezeka nchini humo Awali, mkurugenzi wa nyumba ya watoto nchini humo ndie alielezwa kuhusika na unyanyasaji huo wa kingono kwa watoto wa kiume kati ya mwaka 2004 hadi 2016 ambapo naibu mkurugenzi alielezwa kujaribu kufunika skendo hiyo iliyoripotiwa na Reuters. Mkurugenzi alihukumiwa miaka 8 jela na naibu wake alihukumiwa miaka 3 jela kabla ya msamaha wa Rais Rais Novak aliingia madarakani 2022, ni mwanasiasa wa kike maarufu nchini humo katika nchi hiyo ambayo siasa zimetawaliwa na wanaume

photo content

⚠️😳 Mchungaji Jimmy Odukoya awalipua wanawake wanaoamini hawapaswi kuwasapoti waume zao Akiongea kanisani kwake, mchungaji h
⚠️😳 Mchungaji Jimmy Odukoya awalipua wanawake wanaoamini hawapaswi kuwasapoti waume zao Akiongea kanisani kwake, mchungaji huyo wa Nigeria amesema wanawake wengi wanapenda kuwa bibi harusi ila hawapendi kuwa mke Ameeleza zaidi kwamba biblia imeweka wazi mwanamke anapaswa kuwa msaidizi kwa mume na sio kuwa tegemezi kwa mume "Mwanamke aliumbwa kuwa msaidizi na sio kuwa tegemezi, na huwezi kumsaidia mtu yeyote ikiwa wewe mwenyewe hujanolewa. Kama mumeo analeta meza wewe lete kiti, kama mumeo analeta mbegu wewe mwambie wapi aipande aridhini, wanawake wengi wanapenda kuwa mabibi harusi hawapendi kuwa mke" - amesema Mchungaji Jimmy licha ya kuwa na kanisa lakini pia ni mwigizaji, moja ya kazi alizoigiza ni pamoja na filamu ya The Woman King(2022) akiwa na mastaa wakubwa Hollywood Viola Davis na John Boyega ’

⚠️😳 Jamaa huyo kwa jina Aliyu ameibuka kusema kwamba kama unataka kuyaharibu maisha yako wewe kama mtu basi fanya kuingia katika ndoa na mtu ambaye anashabikia sana dini kuliko kawaida na ambaye ana uwezo wa kufikia hatua yoyote ile kumkingia kifua kumtetea anayeitwa mtumishi wa Mungu ambaye hata hayajui vizuri kiundani maisha yake binafsi ya siri Aliyu anadai kwamba wapo pia watu wengi ambao maisha yao yaliharibiwa na wazazi wao waliokuwa mashabiki wakubwa wa mambo ya kidini kupitikiliza na bado kuna wanaopitia hayo karne hii ya 21 Aliyu anasisitiza kwamba haelewi ni kwanini baadhi ya watu hupandwa na hasira pale mazungumzo yanapoibuka kuhusu mtumishi flani wa Mungu wanayemshabikia. Anashangazwa na baadhi ya watu kutokuwa na uwezo wa kuwatetea hata wazazi wao wanaofahamu kama ambavyo hufikia hatua yoyote ile kuwatetea wanaoitwa watumishi wa Mungu pasipo kuyajua maisha yao binafsi kwa kiundani Ameingia ndani kwa kusema unakuta watu wengine wana afya njema na hata shuleni walikuwa vizuri katika mijadala/malumbano ya hoja(debate) ila bado wana radhi hata wajitusi wao wenyewe ili tu kumtetea anayeitwa mtumishi wa Mungu ambaye bado hawamjui vizuri maisha yake binafsi ya siri. Anasema na hawajali hata gharama za maisha kupanda kama wanavyojali mtumisi flani wa Mungu akizungumziwa Kwa ufupi Aliyu anamaanisha ushabiki wa kidini au kiimaani ukizidi sana humuondolea mtu uwezo wa kufikiri

photo content

"Mimi na Diamond Platnumz tuko vizuri, bado ni mwanangu yeye anaitwa Naseeb Abdul mimi naitwa mzee Abdul, tuko vizuri hadi fa
"Mimi na Diamond Platnumz tuko vizuri, bado ni mwanangu yeye anaitwa Naseeb Abdul mimi naitwa mzee Abdul, tuko vizuri hadi familia yake ingawa kuna kipindi nilikasirika baada ya mama yake kuleta mambo ambayo hayakuwa ya kweli" "Diamond na Queen Darleen wote ni watoto wangu, sina shida nao na hata nikiwa na shida hawawezi kunitupa"- Mzee Abdul. Aidha Mzee Abdul amesema ameacha kuimba muziki kwasababu umri wake haumruhusu, ameshachelewa hata akisema aimbe vipi hataeleweka, lakini moja ya vipaji alivyojaliwa na Mungu ni kuimba na kuigiza na hata watu wa Tamthilia za Juakali, Huba, Pazia na nyinginezo wakimuita yupo tayari na atafanya vizuri.

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media
+4
KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media

EDWARD NGOYAI LOWASSA AFARIKI DUNIA Aliyewahi kugombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mtoto wake Fredrick Lowassa amethibitisha Pia, Lowassa aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2008 na kuweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza kujiuzulu. Rest in peace