E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger 🇳🇪, Tanzania inashika nafasi ya pili kwenye Kundi E la Kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026.
#WCQ2026
1 307
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Clara Luvanga hapo jana alifunga Magoli mawili na kuisaidia Klabu yake ya Al Nassr Women kuibuka na Ushindi wa magoli 3-0 Dhidi ya Al Ahli Katika mchezo wa ligi kuu wanawake Nchini Saudi Arabia 🇸🇦.
Mpaka sasa Clara amefikisha Magoli 6 Msimu Huu kwenye Ligi hiyo lakini Hajaitwa kwenye Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania inayojiandaa kucheza na Togo
1 307
RAIS wa Liberia George Weah amekubali kushindwa katika uchaguzi na kiongozi wa upinzani Joseph Boakai baada ya ushindani mkali wa urais.
-
Boakai, makamu wa rais wa zamani ambaye alishindwa na Weah katika uchaguzi wa 2017, aliongoza kwa asilimia 50.9 ya kura dhidi ya Weah 49.1%, huku takriban kura zote zikiwa zimehesabiwa, tume ya uchaguzi nchini humo ilisema Ijumaa.
-
“Muda mfupi uliopita, nilizungumza na rais mteule Joseph Boakai kumpongeza kwa ushindi wake,” Weah alisema kwenye redio ya taifa. “Nawaomba muige mfano wangu na kukubali matokeo ya uchaguzi.
1 307
Wafuasi (followers) Instagram wa D Voice kabla na baada ya kujiunga na Wasafi.
Kabla hajajiunga nao alikuwa na 97.5k ila sai wameongezeka hadi kuwa 179k. Masaa 24 wameongezeka na 83k followers.
#king_kaizari
1 307
"Usione mtu yuko live anatukanana na mtu, analia, msishangae ile ni afya ya akili, msiwaone watu ni mastaa lakini mwenzako anatembea na mambo mengi kichwani, msongamano wa mawazo anawaza kodi ya nyumba milioni 12 ataipata wapi mwaka ujao ili asihame anapoishi. Anawaza kwanini mtu fulani anamiliki Range mimi sina"
"Kikubwa watu wanatakiwa wajue kwamba hatuwezi kulingana, hata kipaji ametupa Mungu na kila mmoja kampa kwa uwezo wake, ukikitumia kipaji vizuri kinakupa maisha ukikitumia vibaya kinakupa msongo wa mawazo ndiyo maana leo wakina Ronald wanaishi vizuri kwasababu walikitumia kipaji kuwa ajira, kwahiyo tuna changamoto kubwa ya wasanii wa Tanzania kuwa na afya ya akili"- Steven Nyerere
Wolper ni miongoni mwa wasanii wa Bongo ambaye siku kadhaa aliingia live katika account yake ya Instagram na kuanza kumporomoshea matusi Dida Shaibu pamoja na Juma Lokole huku akijinadi kwamba yeye ana maisha mazuri kuliko wao na amewazidi mbali. Hata hivyo watu wa karibu waliokuwa na Wolper siku hiyo wamesema wakati anaporomosha matusi alikuwa amelewa na isitoshe siku hizi hayuko sawa kutokana na kushuka kimaisha.
1 307
Zaiylissa na Hajji Manara wanadaiwa kuwa penzini ambapo kwa mujibu wa Juma Lokole ni kwamba Manara alimtuma Lokole apeleke ombi lake kwa Zaiylissa kwamba anampenda. Na mpaka sasa penzi lao lina wiki mbili, tayari Hajji ameanza jitihada za kujitambulisha nyumbani kwa kina Zaiylissa huko Mbagala ili aweze kumuoa Zai haraka.
Kwa mujibu wa Juma Lokole ni kwamba Manara yuko mbioni kumnunulia Zaiylissa gari kama zawadi ya asante kwa kumkubali. Hata hivyo sio siri tena wawili hao wameonekana pamoja usiku wa utambulisho wa D Voice wakiwa kimahaba zaidi.
1 307
WOLPER AMJIBU DIDA SHAIBU, VIGEZO VYA KUHONGWA UNAVYO?
Baada ya Dida Shaibu kujibu mashabulizi ya Wolper kwamba nyumba yake aliyojenga ni sawa na kibanda cha wafanyakazi wa Wolper, kisha Dida akamjibu kwamba ni kweli nyumba yake ni sawa na kibanda lakini yeye amejenga kwa pesa zake hajawahi kudanga kama Wolper. Na haya ndiyo majibu wa Wolper kwa Dida.
"Kupewa kipaji ujue alafu sina skendo ya kudanga na skendo ya kupendana, shida hamna kontenti mnaivua nguo Media ya Wasafi sana. Je vigezo vya kuhongwa unavyo? pesa ilivyo ya tabu"- amejibu Wolper alipokomenti kwenye page ya Lukamba huko Instagram.
1 307
KWENYE NDOA CHANGAMOTO HAZIISHI MKE WANGU, TUTAKUWA PAMOJA MPAKA MUNGU ATAKAPOMCHUKUA MMOJA WETU; RICH MITINDO
"Happy Anniversary my beautiful Gorgeous Pretty wife, I doing even want to imagine my life without you, my greatest gift from God. You blessed me watoto wazuri sana wewe ni sehemu yangu salama katika ulimwengu huu, nakupenda sana Mke wangu"
"Ila pamoja ya kukupenda kila siku kumbuka changamoto haziishi mke wangu hilo fahamu, maana wapo wanaosubiri kuona ndoa inavunjika si unajua maumivu yetu yanaweza kuwa sababu yao kufurahi kama ambavyo furaha yetu inafanya waumie, kwa uwezo wa Mungu tutaweza kusherehekea Anniversary nyingi hadi hapo mwenye mamlaka atakapomtaka mmoja wetu 🙏 I LOVE YOU"- Ameandika Rich Mitindo mume wa Wolper.
1 307
HAUNIKOMOI UNAJIDHALILISHA, KWANZA SIO TYPE YANGU; RUSHAYNAH
Baada ya hivi karibuni Hajji Manara kuhusushwa kimahaba na Zaiylissa mtalaka wa Dullah Makabila, Rushaynah ambaye pia ni mtalaka wa Hajji Manara amekuja na waraka huu.
"Mnalazimisha niongee, please put me out of yooo bulshts abeg, mnajua kabisa you guys are not my type to argue with. Unaweza ukahisi unaumiza watu roho kumbe unajitia aibu mtoto wa Kiislamu tena Maalim kabisa shame on you"
"Mtu mzima kisheti kama huna wazazi vile, Hajji unaenda kupiga picha badala ya kufanya toba ya kweli Astaghfillah mchafu hadi akili"- Rushynah
1 307
Anaandika Faiza Ally
"Ukiona huna imani na jambo zuri linalotokea kwa mwenzako jua kwamba una tatizo kubwa sana kwenye akili yako, nakumbuka miaka ya nyuma wakati naanza kujenga kuna rafiki yangu hakuamini kuwa hata mimi naweza kuwa na nyumba. Aliuliza kwa kila ninaemjua kama ni kweli na hata alipojua ninayo akasema iko kwenye bwawa inaweza kudondoka akaona bora aikashfu ajiaminishe kwamba hata kama ninacho ni kibaya"
"Matokeo yake alijenga haraka mpaka akasahau kuweka mlango nyuma pamoja na madirisha yakaenda upande yaani bad quality home kwasababu hakuamini alichokiona hivyo akakaza ili twende sawa. Sasa kuna watu wana ugonjwa huo yaani akiona unapendwa anasema unajing'ang'aniza, akiona unaishi vizuri atasema una fake, akiona una chochote kizuri hataamini na hata kama kipo atakitoa kasoro yoyote"
"Guys, Mwenyezi Mungu ana maana kubwa sana kutufanya tuwe wa tofauti na tusifanane na yeye na hata baraka zetu kazitofautisha sana, kabla ya kujaji au kumhusia mtu kwa ubaya kumbuka maisha yetu hayaji na muongozo, tunaongozwa kwa namna tusizozijua. Kama mimi mwenyewe maisha yangu siyajui nategemea kesho yangu itokane na mipango ya Mwenyezi Mungu, wewe unapata wapi uwezo wa kuyajua?"
"Tujifunze kuangalia baraka za wenzetu kwa wema kama ambavyo tunapokea baraka zetu kwa wema, ziwe ndogo ziwe kubwa ni mipango ya Mwenyezi Mungu kila mtu anajaaliwa kwa nafasi yake. Na kama anadanganya na uongo wake ndio unampa furaha basi muache furaha yake iendelee na uongo wake wewe unaumia wapi?"- ameandika Faiza Ally
1 307
⚠️😳 Mume wangu kuwa rika moja la umri na watoto wangu ilinipa hofu ikabidi nisubiri kwa miaka 10 ndio anioe - Mke wa Rais wa Ufarsansa kwenye mahojiano mapya
Brigitte Macron(70) ameolewa na Emmanuel Macron(45) ambaye ni Rais wa nchini Ufaransa kwasasa na ndoa yao ina miaka 16 sasa ingawa imeelezwa hawana mtoto waliyemzaa pamoja, Pia Rais huyo wa Ufaransa haijulikani bado kama ana mtoto kutoka kwa mwanamke mwingine au kama waliasili(adopt)
Ila mke wake huyo ana watoto watatu, wa kiume mwenye miaka 48, na wa kike wawili wenye miaka 46 na 39 toka kwenye ndoa yake ya kwanza
Brigitte akiwa na miaka 39 alikuwa mwalimu wa sanaa(drama) wa Emmanuel Macron ambaye kwa wakati huo alikuwa na miaka 15 na alikuwa darasa moja na mtoto wa kike wa mwalimu wake huyo. Na wakati huo ndipo mwalimu huyo na mwanafunzi wake huyo wakaanza kuoneshana ishara za kutakana kimahusiano wakati bado mwalimu huyo akiwa ameolewa
Wazazi wa Emmanuel hawakupendezwa na hali hiyo wakamhamishia mbali jijini Paris katika shule nyingine ajikite kwenye masomo. Brigitte alidhani Emmanuel kuhamishiwa mbali ingefanya avutiwe huko aliko na wasichana wa umri wake ila haikuwa hivyo
Emmanuel alipofikisha miaka 18 ndipo wakaanza rasmi mahusiano ya kimapenzi na mwalimu wake huyo, lakini alisita kuolewa mapema na Emmanuel kwa luhofia yupo rika moja na wanae aliona kama "angewaharibu" kwa namna moja au nyingine
Hivyo Brigitte akaamua kusubiri kwa miaka 10 ndipo 2007 akafunga ndoa na Emmanuel ambaye baadaye akaja kushinda Urais wa Ufaransa
Brigitte amesema tangu alipokuwa mwalimu Emmanuel alikuwa vizuri kwenye somo lake la sanaa
