E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
⚠️😳😢 Jamaa huyo wa Nigeria kwa jina la Jay Boogie ambaye alijibadili jinsi kuwa mwanamke , kwasasa anapigania uhai wake baada ya sajari zilizofanywa ndivyo sivyo kumletea shida ikiwemo figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi na hivyo kutakiwa kupandikizwa figo nyingine ili kuokoa maisha yake
Ambapo, kwa huzuni Jay Boogie ameachia video akiwa hospitalini kitandani kuomba wasamaria wema wamsaidie matibabu
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
"Sawa nimekubali nyumba yangu ninayoishi ni sawa na banda la wafanyakazi wa Wolper, sawa lakini je! ushawahi kuiona nyumba ya Wolper? Labda nimwambie tu Wolper kwamba mimi ni mwanamke na ni mwanamke haswaa niliyekamilika, nimeweza kujenga kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, umenielewa?"
"Hizo hizo gari zangu unazoona hazifai mimi nimenunua kwa jasho langu sijadanga, naomba utambue kwamba mimi sio mdangaji, sijadanga nimenunua kwa pesa yangu, kwa jasho langu na nyumba yangu nimejenga kwa kazi yangu. Sasa basi, ujue kabisa mimi ni mwanamke mpambanaji na mtafutaji haujawahi kunikuta hata siku moja mimi nadanga, mimi najivunia kwasababu nimepambana mwenyewe sina mapedeshee"
"Wolper una stress nakujua hali yako ya kimaisha kwa sasa sio nzuri, hata huko kuuza sabuni na mafuta sio kupenda kwako ni ukugumu wa maisha umekufanya upande juu ya meza kama mnenguaji. Kwa kinywa chako mwenyewe umekubali kwamba umehongwa sana mamilioni na mapedeshee ukazichezea pesa umekuja kushtuka ukubwani, umri ushaenda huwezi tena kupata pedeshee wa kukupa mamilioni ndio maana una stress, maisha magumu huelewi"
"Mimi nimekuzidi mbali mdogo wangu, nimekuzidi mbali mnoo, ni kwa vile tu ukishazoea kuhongwa huwezi kuthamini kitu cha mwanamke mwenzako mpambanaji unamuonea wivu, juzi tu hapa nimekupa mchongo wa mamilioni na nikakwambia usinipe hata mia hiyo pesa unayotaka kunipa wanunulie wanao chakula wapishane chooni maana tunajua uko mwenyewe, nimeshangaa kuona unanisema tena kwa mkazo, mimi sio levo zako, nimekuzidi mbali mnoo, tafuta pesa angalau utoke kwenye hiyo hali uliyonayo sasa"- Dida Shaibu, Mtangazaji wa Wasafi FM akimshambulia Jacqueline Wolper.
Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥
Toa maoni yako
1 307
#Tanzia
Msanii wa muziki kutoka Nchini Burundi, Miss Erica amefariki Dunia muda mfupi uliopita. Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Bumerec uliopo Jijini Bujumbura huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijawekwa wazi.
Ikumbukwe Msanii huyo ambaye aliwahi kutamba nyimbo nyingi ikiwemo wimbo wa "Mon Amour".
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi, amini.
1 307
WABONGO WAMKALIA KOONI MUME WA MAREHEMU HAITHAM KIM BAADA YA KUENDELEA KUPOSTI NYIMBO ZAKE KWENYE UKURASA WAKE WA IG.
Watanzania wameonyesha kuchukizwa na kitendo kinachofanywa na mume wa Marehemu Haitham Kim, Boshen, ambapo licha ya mke wake kufariki wiki kadhaa zilizopita, yeye ameendelea kuweka posti kwenye ukurasa wa Haitham wa Instagram akiwasisitiza watu waendelee kusikiliza nyimbo za Marehemu Haitham Kim kwenye Digital platforms zake zote.
Wabongo hao wanadai kwamba Haitham amefariki akiwa bado anaendelea na mziki wa kidunia, mziki ambao kiuhalisia unatambulika kama chukizo kwa Mwenyezi Mungu kutokana na namna unavyowasilishwa na wahusika. Ni vyema mume wake angetumia wakati huu kumuombea dua mke wake asamehewe madhambi na siyo kuendelea kuposti nyimbo zake jambo ambalo ni kama anazidi kumukosesha nafasi ya kusamehewa na Mungu huko aliko.
Wabongo hao wameenda mbali zaidi wakisema kama ingewezekana ni vyema hata hizo account za Haitham zingefutwa kabisa, picha zake zingeondolewa ukutani kutokana na sheria za dini ya Kiislamu. Wamesema kitendo hicho hakipendezi na kitamfanya aonekane ni mwenye kujali pesa kuliko kuipambania pepo ya mkewe huko aliko.
1 307
"Wanasema ukipania sana kukipata kitu ndio haukipati, hasa sisi tunaohitaji watoto ukiwa na uhitaji sana wa kupata mtoto ni ngumu sana kupata ndio maana mimi kuna wakati huwa nasahau kabisa najifanya kama sihitaji mtoto ili nipate mimba lakini Mwenyezi Mungu kama hajakupangia hajakupangia tu kwa wakati huo hata ufanye nini"- Wema Sepetu
1 307
𝗢𝗙𝗙𝗜𝗖𝗜𝗔𝗟: Timu 13 kati ya 24 tayari zimefuzu EURO 2024:
🇩🇪 Germany (hosts)
🇵🇹 Portugal
🇫🇷 France
🇧🇪 Belgium
🇹🇷 Turkey
🇪🇸 Spain
🏴 Scotland
🇦🇹 Austria
🏴 England
🇭🇺 Hungary
🇸🇰 Slovakia
🇦🇱 Albania
🇩🇰 Denmark
1 307
𝐖𝐀𝐍𝐃𝐄𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐈𝐍𝐆𝐈𝐀
Tayari timu ya Taifa ya Morocco ‘The Atlas’ imewasili Dar es Salaam, Tanzania kucheza dhidi ya Tanzania mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe la Dunia 2026 mchezo ambao utachezwa Jumanne Novemba 21, 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
1 307
FISTON MAYELE, Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Yanga ameingia kwenye orodha wa Wachezaji 10 wanaowania tuzo ya Mchezaji bora Afrika.
1 307
EVERTON YAPOKWA POINTI 10
Klabu ya Everton ya pale Liverpool England imepokwa alama 10 kwa kuvunja kanuni za ligi Kuu. Everton imekuwa klabu ya kwanza katika historia ya Epl kupokwa alama nyingi baada ya kuvunja kanuni.
Baada ya kupokwa alama hizo kwa sasa Everton imeshuka kutoka nafasi ya 14 mpaka ya 19 ikiwa na pointi 4.
1 307
TFF KUVIFILISI VILABU MILIONI 15 KISA FAINI.
Bodi ya Ligi itaingiza kiasi cha Tsh. 15 milioni kupitia faini mbalimbali ambazo imetoza kwa klabu, wachezaji pamoja na wataalam wa mabenchi ya ufundi kutokana na makosa waliyokutwa waliyotiwanayo hatiani.
Jumla ya klabu sita (6) zimetozwa faini [Yanga, Simba, KMC, Coastal Union, Stand United na Lipuli] kutokana na makosa mbalimbali.
• Yanga - 5,000,000
• Simba- 1,000,000
• KMC - 1,000,000
• Coastal - 1,000,000
• Stand - 500,000
• Lipuli - 3,000,000
Wachezaji wanne (4) [Kibu Denis, Henock Inonga, Djigui Diarra na Khalid Aucho] pia wametozwa faini baada ya kukutwa na hatia kwenye makosa mbalimbali.
• Kibu Denis - 500,000
• Henock Inonga - 500,000
• Djigui Diarra - 500,000
• Khalid Aucho - 500,000
Wataalam watatu (3) kutoka klabu tatu tofauti nao pia wamechezea rungu la faini [Kocha Msaidizi wa Yanga, Moussa Ndao, Kocha wa Mbeya City, Salum Mayanga na Kocha wa Viongo wa Mbeya City, Paul Nonga.
• Moussa Ndao - 500,000
• Salum Mayanga - 500,000
• Paul Nonga - 500,000
Endapo faini hizo zitalipwa, Bodi ya Ligi (TPLB) itavuta kiasi kisichopungua shilingi milioni 15 za Tanzania.
@dickson_masanja
1 307
Story kubwa kwenye upande wa Michezo Na burudani duniani siku ha leo ni kuhusu Mchezaji wa klabu ya Manchester City, Kevin De Bruyne, ambaye ameonekana katika orodha ya Waandishi wa wa nyimbo wa Drake kwenye albamu yake mpya ya FO ALL THE DOG,
De Bruyne, ametokea kwenye wimbo namba 27 unaoitwa Wick Man, kutoka kwenye albamu hiyo mpya ya Drake ya ‘For All The Dogs, ikiwa na watunzi watatu waliotajwa katika utayarishaji wa wimbo huo.
Waandishi hao waliopo kwenye ngoma hiyo ni pamoja na Drake mwenyewe, A.Mamam pamoja na K. De Bruyne.
Kupitia mtandao wa Twitter Mashabiki walijaribu kumchokonoa KDB na kujibu kuwa Drake alihitaji Assist ingawa wengi wanahisi amefanya utani tu huenda kuna mwandishi anaiywa Kevin De Bruyne.
Wewe unahisi ni KDB huyu huyu au yupo mwingine??
#fu
