en
Feedback
Elimu kwanza

Elimu kwanza

Open in Telegram

Elimu kama bahari,sote hilo twalijua Utamaliza dahari,elimu itabakia Yatosha kuwa fahari,fungu ukijipatia Japo hukosi dosari,hata wakikusifia

Show more
The country is not specifiedEducation72 159
1 070
Subscribers
-124 hours
-47 days
-1030 days

Data loading in progress...

Tags Cloud
No data
Any problems? Please refresh the page or contact our support manager.
Incoming and Outgoing Mentions
---
---
---
---
---
---
Attracting Subscribers
September '26
September '26
+4
in 0 channels
August '26
+11
in 0 channels
Get PRO
July '26
+40
in 0 channels
Get PRO
June '26
+34
in 0 channels
Get PRO
May '26
+22
in 0 channels
Get PRO
April '26
+25
in 0 channels
Get PRO
March '26
+9
in 0 channels
Get PRO
February '26
+7
in 0 channels
Get PRO
January '26
+18
in 0 channels
Get PRO
December '25
+35
in 0 channels
Get PRO
November '25
+21
in 0 channels
Get PRO
October '25
+25
in 0 channels
Get PRO
September '25
+109
in 2 channels
Get PRO
August '25
+14
in 0 channels
Get PRO
July '25
+19
in 0 channels
Get PRO
June '25
+33
in 0 channels
Get PRO
May '25
+27
in 0 channels
Get PRO
April '25
+71
in 0 channels
Get PRO
March '25
+36
in 0 channels
Get PRO
February '25
+36
in 0 channels
Get PRO
January '25
+54
in 0 channels
Get PRO
December '24
+21
in 0 channels
Get PRO
November '24
+35
in 0 channels
Get PRO
October '24
+41
in 0 channels
Get PRO
September '24
+25
in 0 channels
Get PRO
August '24
+29
in 0 channels
Get PRO
July '24
+47
in 0 channels
Get PRO
June '24
+20
in 0 channels
Get PRO
May '24
+43
in 0 channels
Get PRO
April '24
+142
in 0 channels
Get PRO
March '24
+29
in 1 channels
Get PRO
February '24
+13
in 0 channels
Get PRO
January '24
+37
in 0 channels
Get PRO
December '23
+36
in 0 channels
Get PRO
November '23
+18
in 0 channels
Get PRO
October '23
+23
in 0 channels
Get PRO
September '23
+39
in 0 channels
Get PRO
August '23
+26
in 0 channels
Get PRO
July '23
+4
in 0 channels
Get PRO
June '23
+5
in 0 channels
Get PRO
May '23
+5
in 0 channels
Get PRO
April '23
+9
in 0 channels
Get PRO
March '23
+6
in 0 channels
Get PRO
February '23
+6
in 0 channels
Get PRO
January '23
+9
in 0 channels
Get PRO
December '22
+7
in 0 channels
Get PRO
November '22
+9
in 0 channels
Get PRO
October '22
+4
in 0 channels
Get PRO
September '22
+12
in 0 channels
Get PRO
August '22
+8
in 0 channels
Get PRO
July '22
+209
in 0 channels
Date
Subscriber Growth
Mentions
Channels
08 September0
07 September+1
06 September0
05 September+1
04 September+1
03 September0
02 September0
01 September+1
Channel Posts
Habari njema" Elimu Kwanza Online Duruus Tunatoa fursa ya kipekee kwa wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu kujiunga Duruus zetu za Online" Badala ya kulipia Kiasi cha Tsh 30,000/= kama pesa ya usajili basi watalipia kiasi cha Tsh 10,000/= tu Offer hii ni kwa wanafunzi wa vyuo pekee,Walio Tanzania au nje ya Tanzania,Africa mashariki au nje ya Africa Mashariki" Ratiba yetu ya kusoma kwa njia ya mtandao ni rafiki kwa kila mtu haiwezi kuingiliana na ratiba zako za masomo au za kazi,Hivo usipitwe na fursa hii adhimu ya kujifunza dini yako tukufu" Bofya link ujaze form kisha fuata taratibu zingine za usajili https://forms.gle/ULyk2M7zcwE1BfuM9 Mwisho wa usajili ni Tar 10/09/2026-M Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi: +255745000324 Whatsapp/kawaida.

2
*🕌 DARSA: SEMINA MASJID MUNIRA - SINGIDA MJINI | رسالة واجبنا نحو ما أمرنا الله به لشيخ الإسلام محمد بن عبد الوهاب | MAJLISI YA 1️⃣* 📺 Karibu katika Majlisi hii ya kwanza, Sheikh Muhammad Sungi حفظه الله anaanza kusoma na kufafanua risala hii muhimu ya Sheikh Muhammad ibn Abdul Wahhab Rahimahullah inayohusu "Wajibu wetu katika kuyaelekea yale ambayo ametuamrisha Allah mtukufu." Sheikh anachambua maraatib (daraja) saba ambazo ni lazima kwa kila Muislamu kuzijua na kuzitekeleza anapopata amri yoyote kutoka kwa Allah, ikiwemo: - Elimu (Kulifahamu jambo). - Mahaba (Kukipenda kile ulichoamrishwa). - Azma (Kuwa na nia thabiti ya kutekeleza). - Kufanyia kazi kwa vitendo. - Ikhlaas na Mutaba'a (Kufanya kwa ajili ya Allah na kufuata Sunnah). - Tahadhari (Kuepuka mambo yanayoharibu amali). - Thabat (Kudumu katika haki). Ungana nasi katika darsa hili ili upate faida hizi za kielimu zitakazokusaidia kuboresha ibada zako. *🔗 Sikiliza hapa:* https://youtu.be/so8HkizuG2A _______ 📺 *Ungana nasi kupitia:* @Manhaj Online TV // @Manhaj Media Pro 📡 Instagram | YouTube | Facebook | TikTok | X
34
3
*_UKUMBUSHO_* Elimu kwanza Online Duruus tumefungua dirisha la usajili kwa dufua ya 07-Msimu wa 07" Tunatoa Elimu ya kisheria kwa ngazi ya Iptidai na Mutawasitwa,Online-kwa njia ya mtandao *KWA JINSIA ZOTE* Maelezo zaidi kuhusu program yetu yanapatikana kwenye form ya usajili Bofya link soma maelezo kisha jaza form ya kujiunga na masomo https://forms.gle/ULyk2M7zcwE1BfuM9 *⚠️BAKI SIKU 09 PEKEE KUFUNGWA KWA DIRISHA LA USAJILI* 📌Ikiwa umejaza form,umefanya malipo na haujapewa namba ya usajili wala kuungwa kwenye group basi tukumbushe tafadhali 📌Na ikiwa umejaza form na haujakamilisha usajili basi harakisha kukamilisha usajili kabla ya Tarehe ya mwisho ⚠️Mwisho wa usajili ni Tar 10/09/2026" Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi: Whatsapp https://wa.me/message/2DXZ6NZOD257G1 📲 +255745000324 Mudiru" Mohammadi Sungi #ELIMU_KWANZA_ONLINE_DURUUS"
44
4
Elimu kwanza Online Duruus tumefungua dirisha la usajili kwa dufua ya 07-Msimu wa 07" Tunatoa Elimu ya kisheria kwa ngazi ya Iptidai na Mutawasitwa,Online-kwa njia ya mtandao *KWA JINSIA ZOTE* Maelezo zaidi kuhusu program yetu yanapatikana kwenye form ya usajili Bofya link soma maelezo kisha jaza form ya kujiunga na masomo https://forms.gle/ULyk2M7zcwE1BfuM9 *⚠️BAKI SIKU 11 PEKEE KUFUNGWA KWA DIRISHA LA USAJILI* Mwisho wa usajili ni Tar 10/09/2026" Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi: Whatsapp https://wa.me/message/2DXZ6NZOD257G1 📲 +255745000324 Mudiru" Mohammadi Sungi #ELIMU_KWANZA_ONLINE_DURUUS"
61
5
+1
01-Kufunga Duruus.mp3
98
6
ELIMU KWANZA ONLINE DURUUS" JILSA YA KUFUNGA DURUUS" -Nasaha kutoka kwa Sheikh Said Isimbula -Nasaha kutoka kwa Sheikh Abdulwahab Twaha -Kalima kutoka Mudiru -Matokeo ya mitihani 📁Audio 1_2
88
7
Bishara njema" Elimu kwanza Online Duruus tumefungua dirisha la usajili kwa dufua ya 07-Msimu wa 07" Tunatoa Elimu ya kisheria kwa ngazi ya Iptidai na Mutawasitwa,Online-kwa njia ya mtandao Maelezo zaidi kuhusu program yetu yanapatikana kwenye form ya usajili Bofya link soma maelezo kisha jaza form ya kujiunga na masomo https://forms.gle/ULyk2M7zcwE1BfuM9 Mwisho wa usajili ni Tar 10/09/2026" Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi: Whatsapp https://wa.me/message/2DXZ6NZOD257G1 📲 +255745000324 Mudiru" Mohammadi Sungi #ELIMU_KWANZA_ONLINE_DURUUS"
103
8
*08-Fadhila,Ubora na Malipo ya kufunga A'ashuraa Hakika funga ya Ashuraa ina malipo makubwa kwa Allah mtukufu aliye juu,Hapaswi Muislamu kuacha kufunga" Imekuja katika Hadeeth:" {عن أبي قتادة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه سئل عن صوم يوم عاشوراء فقال يكفر السنة الماضية} أخرجه مسلم Maana ya Hadeeth: *{Kutoka kwa Abuu Qatada Allah amridhie hakika Mtume wa Allah Swala na amani ziwe juu yake aliulizwa kuhusu Funga ya Ashuraa,Akasema:" inafuta madhambi ya mwaka uliyopita}* Hadeeth Imepokelewa na Muslim" Hadeeth imebainisha ubora wa funga ya Ashuraa,Hivo basi inampasa kila muislam kufunga na awahimize watoto na mke wake kufunga" ●Ifanye funga yako iwe bora zaidi kwa kusoma Quran kufanya adhkari n.k ●Iliyokuwa Ssuna ni kufunga siku moja kabla ya A'shuraa na Siku ya A'shuraa yenyewe" Jumla zitakuwa siku mbili" Au kufunga siku ya A'shuraa na siku moja mbele" jumla siku 2" Mwenye kufunga Ashuraa peke yake-yan siku ya 10 pekee-pia inafaa" ●Utumie mchana wa funga yako na hata baada ya kufuturu kumuomba Allah-Mlilie Mola wako shida zako" kubwa zaid usisahau kuomba pepo" ●Ashuraa ya mwaka huu itakuwa Tar 25/06/2026 Alkhamisi" Allah atufanyie wepesi katika kuyaendea matendo mema na asitunyime ujira wake قد أحسن من انتهى إلى ما سمع Hakika amefanya vizurii mwenye kufanyia kazi kile alichojifunza Mohamed Sungi" 08 Muharram 1448 H 23 Jun 2026 M Temeke-Dar Es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
111
9
07-Funga ya Ashura-Chanzo na hekima ya kufunga Utakumbuka kuwa katika makala iliyopita tulitaja Historia ya Funga Ashuraa,Na kwamba ni funga hii ilikuwepo hata kabla ya ujio wa Mtume Swala na Amani ziwe juu yake" Katika makala utajifunza kwa ufupi chanzo cha Funga ya Ashuraa na hekima yake ni ipi haswaa? Muumini wa Kwanza kabisa kufunga Ashuraa alikuwa ni Nabii na Mtume wa Allah Musa Amani iwe juu yake,Alifunga katika hali ya kumshukuru Allah mtukufu aliye juu" Kwa Kumuokoa yeye na wana wa Israel dhidi ya Firaun" Mfalme na kiongozi katili mwenye kiburi na kufuru mbaya kuwahi kutokea katika historia ya Binadaam" Na katika hili imekuja Hadeeth" عن ابن عباس رضي الله عنهما قال (- قدِمَ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم المَدينةَ، فوجَدَ اليَهودَ يَصومونَ يَومَ عاشوراءَ فسُئِلوا عن ذلك؟ فقالوا: هذا اليَومُ الذي أظهَرَ اللهُ فيه موسى، وبَني إسرائيلَ على فِرعَونَ، فنَحنُ نَصومُه تَعظيمًا له، فقال النَّبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: نَحنُ أولى بموسى مِنكُم، فأمَرَ بصَيامه) أخرجه البخاري ومسلم Mtume wa Allah ﷺ alipofika Madina, aliwakuta Wayahudi wanafunga siku ya Ashura. Akauliza kuhusu jambo hilo. Wakasema: “Hii ni siku ambayo Allah alimnusuru Nabii Musa na Wana wa Israil dhidi ya Firauni, hivyo sisi tunaifunga kwa kuitukuza.” Mtume ﷺ akasema: “Sisi tuna haki zaidi kwa Musa kuliko nyinyi.” Kisha akaamrisha siku hiyo ifungwe.) Hadeeth Imepokelewa na Bukhary na Muslim" ●Hadeeth imebainisha hekima kubwa ya kuwekwa Sheria ya Funga ya Ashuraa" Nayo ni kuadhimisha siku hii na kumshukuru Allah mtukufu aliye juu kwa kumuokoa Musa amani iwe juu yake na wana wa Israel Dhidi ya Firaun" ambapo ilikuwa ni Tarehe 10 Muharram karne ya 13 kabla ya Yesu Amani iwe juu yake. .●Firaun ni jina la cheo cha kiongozi na mfalme katika misri ya kale,Aliye ishi miaka 1200KK Takribani-Yan karne 13 kabla ya kuzaliwa Iss bin Maryam Amani iwe juu yake" Wanachuoni wa Kiislamu na wasomi wa historia wametofautina juu ya jina lake halisi!? Baadhi wakasema jina lake ni Mus'abu bin waleed au Waleed bin Rayyan" Kama alivotaja Alfayruuz Ãbaad kwenye kitabu chake "Baswair dhawiy ttamyiyz" Baadh wanasema jina lake ni "Ramsess wa pili na mwanaye Merneptah" ●Firaun alikuwa ni mtu katili,jeuri,aliyejaa kufuru kupita kiasi" Mauaji ya kiholela na kuwafanya watumwa wana wa Israel" mbaya zaidi alidai kuwa yeye ndio Muumba mbingu na Ardhi" Allah mtukufu aliye juu alimtuma Mtume wake Mussa akamkanye na arudi kwenye njia ya sawa kufuata dini ya hakki na kuacha dhulma" " lakini akakataa kata kata na kufanya kiburi" kisa Chake ni maarufu kwenye Quran ●Kupitia kisa hiki tunajifunza kuwa Mtu hata akiwa na uwezo,majeshi na jeuri kiasi gani!! Hawezi kumshinda Allah mtukufu" ●Vile vile tunajifunza katika kisa hiki kuwa Hakki na waumini wa kweli ni wenye kushinda Japo baada ya muda mrefu" na kufru na makafiri ni wenye kushindwaa hata wakionekana kuwa na nguvu katika baadhi ya nyakati. ●Hadeeth yaonesha kuwa Baadhi ya Ibada za Umma zilizopita pia ibada zetu Muda wa kuwa Sheria haijakataza na kuleta kinyume chake" mfano wake ni Funga ya A'shuraa-Na hii yaonesha kuwa Uislam ni dini Hakki na ndio Dini ya Manabii na mitume yote. قد أحسن من انتهى إلى ما سمع Hakika amefanya vizurii mwenye kufanyia kazi kile alichojifunza Imeandaliwa na: Mohamed Sungi 07 Muharram 1448 H 22 Jun 2026 M Temeke_Dar Es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
107
10
06-Funga ya Ashuraa-Historia yake" Miongoni mwa Ibada za kipekee zinazopatikana kwenye mwezi wa Muharram ni Funga ya A'shuraa" Imekuja kwenye Hadeeth kadhaa miongoni mwazo ni:" عن عائشة رضي الله عنها قالتْ (كان يوم عاشوراء تصومه قريش في الجاهلية،وكان رسول الله صلى الله عليه وسلم يصومه في الجاهلية،فلما قدم المدينة صامه وأمر بصيامه،فلما فرض رمضان ترك يوم عاشوراء،فمن شاء صامه ومن شاء تركه) أخرجه البخاري ومسلم Kutoka kwa Aisha Allah amridhie amesema:" (Ilikuwa siku ya Ashuraa wanafunga Quraishi katika Jahliyah-Yan kabla ya Uislamu-Na alikuwa Mtume wa Allah Swala na Amani ziwe juu yake akifunga siku hii katika Jahliyah" Pindi alipohamia Madina alifunga na akaamrisha watu wafunge,Basi pindi ilipofaradhishwa Ramadhan akaacha kufunga Ashura,Basi ikawa mwenye kutaka anafunga na mwenye kutaka anaacha) Hadeeth ameipokea Bukhary na Muslim. ●Hadeeth inaonesha kuwa Funga ya A'shuraa ilikuwepo hata kabla ya Uislamu" ●A'shuraa ni Siku ya 10 katika Mwezi wa Muharram''-Ambapo kwa mwaka itakuwa Tarehe 25/06/2026 Alkhamiis ●Funga ya A'shura ilikuwa ni wajibu kabla ya funga ya Ramadhani-Jambo ambalo linaonesha umuhimu wa funga hii ●Baada ya kufaradhishwa Ramadhan Funga ya Ashuraa ikawa si Lazima-Na hii ndio maana ya kauli yake aliposema-Ilipofaradhishwa Ramadhan akaacha kufunga" yan si kama aliacha kufunga kabisa hapana' Maana yake aliacha kufunga katika sura ya ulazima akawa anafunga kwa Sura ya Ssuna" ●Katika Hadeeth tunajifunza kuwa,Kafiri anaweza akafanya baadhi ya matendo mema na yasimsaidie chochote kwa Allah mtukufu kwa sababu ya ukafiri wake" kama walivokuwa Quraish wakifunga Ashuraa pamoja na Shirk zao" na kwamba hilo halikuwafanya wawe wema ●Ni lipi chimbuko la funga hii ya A'shuraa mpaka makafiri nao wafunge siku hii............Fuatilia makala inayofuata Inshallah قَدْ أحسن من انتهى إلى ما سمع Hakika amefanya vizuri mwenye kufanyia kazi kile alichojifunza Imeandaliwa na: Mohamed Sungi 06 Muharram 1448 H 21 Jun 2026 M Temeke-Dar Es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
80
11
05-Ubora wa kufunga katika Mwezi wa Muharram Mwezi wa Muharram pamoja na kuwa ni moja katika mwezi mitukufu,Lakini pia imethibiti Kufunga swaumu ndani yake" Imekuja katika Hadeeth ambayo ameipokea Muslim katika sahihi yake" عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم {أفضل الصيام بعد رمضان شهر الله المحرم،وأفضل الصلاة بعد الفريضة صلاة الليل} وفي رواية: {الصلاة في جوف الليل} أخرجه مسلم" Maana ya hadeeth" _*(Kutoka kwa Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe naye amesema : Amesema Mtume wa Allah Swala na Amani ziwe juu yake "Funga iliyobora zaidi baada ya Ramadhan ni mwezi wa Allah Muharram,Na Swala bora zaidi baada ya Faradhi ni Swala ya usiku,Na katika Riwaya nyingine imekuja "Swala katikati ya Usiku") Hadeeth imepokelewa na Muslim Allah amrehemu" ●Hadeeth Inaonesha juu ya ubora wa kufunga katika mwezi wa Muharram,Na kwamba funga hii inachukua nafasi ya pili baada ya Ramadhan katika ubora" ●Swaumu iliyotajwa kwenye Hadeeth hii-imetafsiriwa na wanachuoni kuwa ni Funga ya Ssuna ya kujitolea-yan Funga isiyokuwa na wito maalumu katika kitabu na ssuna-kwa maana hiyo hapa zinatoka zile funga za ssuna zenye wito maalumu kwenye sheria na zimebainishwa ubora wake mahsusi kama funga ya Arafa,Sittat Shawwal,Ashuraa n.k hizi ni bora zaidi" ●Hadeeth inatuhimiza kufunga swaumu ya ssuna ya kujitolea katika Mwezi wa Muharram" hivo basi muislam usikose kufunga walau siku kadhaa katika mwezi huu" siku 2,10 au 15 N.k kadri ya uwezo wake" Ili kudiriki hizi fadhila, ●Kwa mwenye kutaka kufunga mwezi wa Muharram basi afunge baadhi ya siku tu,Asifunge mwezi mzima kwa sababu hilo halijathibiti" ●Kwa mwenye kuchuguza kwa umakini hali ya miezi mitukufu atagundua kuwa mwezi wa Muharram ni tofauti na miezi mingine kama Dhul-Qaada na Rajabu ambayo hakuna dalili iliyothibiti yenye kuhimiza kufunga katika miezi hiyo" قد أحسن من انتهى إلى ما سمع Hakika amefanya vizuri mwenye kufanyia kazi kile alichojifunza Imeandaliwa na: Mohamed Sungi 05 Muharram 1448 H 20 Jun 2026 M Kwa mama Kibonge-Dar Es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
76
12
04-Nafasi ya Mwezi wa Muharram kati ya miezi mingine Katika makala iliyopita nilibainisha kuwa mwezi wa Muharram ndio mwezi wa kwanza katika Kalenda ya kiislamu-kama yalivotimia makubaliano katika utawala wa Khalifah Omar bin khattab Allah amridhie, Aidha ifamike kuwa mwezi wa Muharram ni katika miezi mitukufu ambayo ameitaja Allah katika Quran tukufu, Amesema Allah mtukufu aliye juu: { إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ } سورة التوبة ٣٦ {Hakika idadi ya Miezi kwa Allah ni kumi na mbili katika kitabu cha Allah siku alipoumba Mbingu na Ardhi,Kati yake kuna minne mitukufu,Hiyo ndio dini ya sawa sawa,Basi msidhulumu humo nafsi zenu....}Suratul Tawbah 36 Na katika Hadeeth" عن أبي بكرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: {السنة اثنا عشر شهرًا منها أربعة حرم: ثلاثة متوالية،ذو القعدة وذو الحجة والمحرم ورجب مضر الذي بين جمادى وشعبان} متفق عليه _Kutoka kwa Abuu Bakrah Allah amridhie kutoka kwa Mtume Swala na Amani ziwe juu yake Amesema:_ {Mwaka una miezi 12,Kati yake kuna miezi minne mitukufu,Mitatu kati yake ni yenye kufuatana ambayo ni Dhulqaada,Dhulhijjah,Muharram na Rajabu ambao uko baina ya Jumada na Shaaban} Hadeeth Mutafaqun A'layhi ✨Ayah na Hadeeth Zimejulisha kuwa Mwezi wa Muharram ni katika miezi mitukufu" ●Miongoni mwa upekee wa miezi hii Minne mitukufu ni Kuwa Allah mtukufu aliyejuu Ametutahadharisha kufanya dhulma-yan madhambi ndani ya miezi ya hii-kwa sababu madhambi yake ni mabaya zaidi kuliko madhambi katika miezi mingine" {وقال قتادة: "إن الظلم في الأشهر الحرم أعظم خطيئة ووزرا منه في سواها} Amesema Qatada: {"Hakika dhulma katika miezi mitukufu ni kosa kubwa zaidi kuliko katika miezi mingine} ●Dhulma mbaya zaidi ni kumshirikisha Allah mtukufu aliye juu ambaye hana mshirika" ●Na wanachuoni wametaja sababu ya kuitwa miezi mitukufu kuwa" Ni kwa ajili ziada ya utukufu wa miezi hii na ubaya wa madhambi ndani yake" Pia kwa sababu Allah ameharamisha vita ndani ya miezi hii" وفي الختام وأسأل الله حسن الخاتمة Tumuogope Allah mtukufu na tuchunge mipaka yake hii ndio salama yetu Duniani na Akhera" Fuatilia makala inayofuata........Inshallah Imeandaliwa na: Mohamedi Sungi 04 Muharram 1448 H 19 Jun 2026 M Ilala-Dar Es Salaaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
72
13
03-Mwaka mpya wa kiislamu-Hatimaye wakati wetu utapita Tumeagana na mwaka uliopita,Tumeingia mwaka mwingine,Umri umeongezeka,Maisha yanasonga,Kila mmoja wetu anaenda mbio kupambania ndoto ya maisha yake" Katika kupita wakati-masiku,miezi na miaka-Kuna mazingatio makubwa kwa mwenye kutafakari,Kwa sababu kila dakika ipatayo basi hukuweka mbali na dunia na kukuweka karibu na akhera' Ikiwa umeandikiwa kuishi miaka 50 duniani basi kila mwaka unapokatika unapunguza umri wako-Kutoka 50 49 48 47 46 mpaka unaumaliza umri wako" Kupitia wakati "cha mbali huwa karibu,Kipya huchakaa,Mtoto huzeeka,Mzee ndio kabisaa hutoweka duniani" Anasema Allah mtukufu aliye juu" 《يقلب الله الليل والنهار إن في ذلك لعبرة لأولى الأبصار》 سورة النور ٤٤ Allah hugeuza usiku na mchana hakika katika hilo kuna mazingatio kwa wale wenye ufahamu Mwenye mafanikio na furaha ni yule anayetafakari jinsi gani anaumaliza umri wake,Jinsi gani anafaidika na wakati wake katika yale yenye faida katika Dini na Dunia yake, Na mwenye hasara ni yule atakayeghafilika akapitwa na wakati wake pasina faida yoyote,Basi hasara yake ni kubwa mnoo-Allah atuweke mbali" Hatimaye wakati wetu utapita tutakufa kwa furaha tuliyo nayo au kwa huzuni tulizo nazo,Na tutasahaulika kama vile hatukuwahi kuwepo kwenye dunia hii-Ispokuwa yule ambaye Allah atabakisha kumbukumbu yake baina ya walio hai" Ewe Allah tunakuomba utajo mwema kwa wale waliobakia" Kama ni hivo basi huna sababu ya kumuasi mola wako,wala kuwa na kibri kujiona au kuwadharau wengine, Inatajwa kuwa mtu mmoja aliandika kwenye ukuta wa jirani yake" "Maisha ya mwanadamu ni Hadeeth tu basi ewe ndugu yangu kuwa Hadeeth nzuri kwa hao watakaosimuliwa" Ewe ndugu muislamu fahamu kuwa" Maiti si yule aliyeveshwa sanda akawekwa kwenye kaburi-Huyu amepumzika" Maiti ni yule aliye hai" anaishi hana fadhila yoyote anakufa pasina athari yoyote,uhai wa mwili utaisha lakini matendo mema ni umri wa pili usio isha, Allah amrehemu mshairi mmoja aliposema" ما ماتَ من زرعَ الفضائلَ في الورى بل عاشَ عُمراً ثانياً تحتَ الثرى فالذِّكرُ يُحيي ميتاً ولربَّما ماتَ الذي ما زالَ يُسمعُ أو يُرى Hakufa yule aliyepanda mbegu za wema miongoni mwa watu, Bali ameendelea kuishi maisha ya pili hata akiwa chini ya udongo. Kwa kuwa kumbukumbu njema humfanya maiti aendelee kuwa hai,Na pengine akafa yule ambaye ingali bado anasikia na anaona-Yan atakapokuwa hana jema lolote" Natia nanga kwenye makala hii kwa kuiusia nafsi pamoja na nyinyi kumcha Allah kwenye hali zote" Tukipata katika yale tunayotamani tumshukuru Allah,Tukikosa Tufanye Subra Na tukifanya dhambi basi tufanye haraka kutubia-hakika hii ndio anuani Pekee ya Maisha yenye furaha" Tunamuomba Allah atupe mazurii katika Hii dunia na atupe mazuriii akhera" sisi pamoja na wazazi wetu Imeandaliwa na: Mohamedi Sungi 03 Muharram 1448 H 18 Jun 2026 M Temeke-Dar Es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
94
14
02-Mwaka Mpya wa kiislamu-Je yafaa kupongezana kwa munasaba wa kuingia mwaka mpya? Ndugu Muislamu ikiwa ulifatilia makala namba 01 Kuhusu mwaka mpya na kalenda ya Kiislamu basi bila shaka utakuwa umefahamu vema historia yake japo kwa ufupi! Lakini hapa kuna jambo muhimu unapaswa kujifunza ili usibaki katika tahayari juu mwaka mpya na kalenda ya Kiislamu". Jambo lenyewe ni hivi: Je inafaa kupongezana kwa munasaba wa kuingia mwaka mpya wa kiislamu?au kusherehekea? Jawabu ni kwamba: Jambo hili halina asili katika dini yetu-yan hakuna dalili si kwenye Quran wala si kwenye Hadeeth wala si kutoka kwa wema waliotangulia Inayoonesha kupongezana au kusherehekea kuingia mwaka mpya wa kiislamu" Hivo basi kufanya hivo ni Bidaa na uzushi unapaswa kujiweka nao mbali" Aliulizwa Sheikh Ibn Baaz Allah amrehemu kuhusu hukumu ya jambo hili!? Akasema" أما بعد: فالتهنئة بالعام الجديد لا أعلم لها أصلاً عن السلف الصالح، ولا أعلم شيئاً من السنة أو من الكتاب العزيز يدل على شرعيتها، لكن من بدأك بذلك فلا بأس أن تقول: وأنت كذلك، إذا قال لك: كل عام وأنت بخير، أو قال: كل عام وأن تكون بخير، فلا مانع أن تقول له: وأنت كذلك، نسأل الله لنا ولك كل خير أو ما أشبه ذلك. أما البداءة فلا أعلم لها أصلاً. نعم. Ama baada ya hayo: Kuhusiana na kupeana hongera kwa mwaka mpya, sijui kuwa jambo hilo lina asili yoyote kutoka kwa Salafu Wema (watangulizi wema wa Umma huu). Wala sijui chochote katika Sunnah au katika Kitabu Kitukufu cha Allah kinachoonyesha kuwa jambo hilo limewekwa kisheria. Lakini ikiwa mtu ndiye atakayekuanza kwa kukutakia hivyo, basi hakuna ubaya kumjibu kwa kusema: “Na wewe pia.” Akikwambia: “Kila mwaka uwe katika kheri,” au “Kila mwaka uwe mzima na katika mema,” hakuna ubaya kumwambia: “Na wewe pia; tunamuomba Allah atuletee sisi na wewe kila la kheri,” au maneno yanayofanana na hayo. Ama kuanzisha wewe mwenyewe kutoa pongezi hizo, basi sijui kuwa jambo hilo lina asili yoyote ya kisheria....Mwisho wa kunukuu _Rejea Majmuul fatawa ya sheikh Ibn Baaz_ Tunajifunza kupitia kwenye fatwa ya Sheikh Ibn Baaz Allah amrehemu Masuala yafuatayo" 01-Kupongezana kwa munasaba wa mwaka Hili jambo halipo kisheria 02-Ikitokea mtu ameanza kukupongeza kwa kukuombea dua basi yafaa kumuitikia kwa kumwambia-Nawe pia,Tunaomba Allah kwetu sisi na kwenu kila la khery na mfano wa maneno hayo" 03-Hakuna sherehe za Mwaka mpya wa kiislamu 04-Uislamu ni Dini ambayo inaegemea dalili kwenye ibada zake-Hivo basi ikiwa jambo halina dalili haifai kulifanya kuwa ni dini" 05-Maswahaba ambao ndio waasisi wa kalenda hii ya kiislamu hawakusherehekea wala kubadilishana pongezi juu ya kuingia mwaka mpya 06-Salama ya Dini ya muislamu ipo kwenye kufuata kitabu na Ssuna kwa ufahamu wa wema waliopita" قد أحسن من انتهى إلى ما سمع Hakika amefanya vizuri mwenye kufanyia kazi kile alichojifunza Imeandaliwa na: Mohamedi Sungi 01 Muharram 1448 H 16 Jun 2026 M Mnazi Mmoja-Dar Es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
95
15
*01-Mwaka mpya wa Kiislamu"* Leo ni Tarehe 29-Dhulhijjah-1447 H sawa na Tar 15/06/2026 M" Mwezi wa Dhulhijjah ndio mwezi wa 12 na wa mwisho katika Kalenda ya kiislamu,Na mwezi wa Muharram-Unaofuata baada ya huu-ndio mwezi wa kwanza katika kalenda ya kiislamu ijulikanayo kama kalenda ya hijiria" Punde si punde tutakuwa ndani ya mwaka mpya wa kiislamu" Kalenda ya kiislamu-Hijria Ilianzishwa katika Ukhalifa wa Umar Bin khattab radhi za Allah ziwe naye,Hivo basi Omar bin Khattab ndio muasisi wa kalenda ya kiislam-Hijiria" Ni ipi sababu ya kuanzishwa kwa kalenda ya kiislamu? قال ابن حجر في فتح الباري: "وذكروا في سبب عمل عمر التاريخ أشياء: منها ما أخرجه أبو نعيم في تاريخه ومن طريقه الحاكم من طريق الشعبي: "أن أبا موسى كتب إلى عمر: إنه يأتينا منك كتب ليس لها تاريخ، فجمع عمر الناس، فقال بعضهم: أرخ بالمبعث، وبعضهم: أرخ بالهجرة، فقال عمر: الهجرة فرقت بين الحق والباطل فأرخوا بها، وذلك سنة سبع عشرة. فلما اتفقوا قال بعضهم: ابدءوا برمضان، فقال عمر: بل بالمحرم فإنه منصرف الناس من حجهم، فاتفقوا عليه" Amesema Ibn Hajar al-Asqalani katika kitabu chake Fath al-Bari: "Wanazuoni wametaja sababu mbalimbali zilizomfanya Umar kuanzisha tarehe ya Kiislamu (Hijria). Miongoni mwa riwaya hizo ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Ash-Sha‘biy kwamba: Abu Musa alimwandikia Umar akisema: 'Barua zinatufikia kutoka kwako lakini hazina tarehe.' Umar akawakusanya watu kwa ajili ya mashauriano. Baadhi wakasema: 'Anzeni kuhesabu miaka tangu Mtume apewe Utume.' Wengine wakasema: 'Tangu Hijra-yan tangu mtume ﷺ alipohamia madina.' Umar akasema: 'Hijra ndiyo iliyotenganisha haki na batili, basi tuhesabu miaka kuanzia hapo.' Hilo likafanyika mwaka wa 17 Hijria. Walipokubaliana juu ya hilo, baadhi wakasema: 'Tuanze mwaka kwa Ramadhani.' Umar akasema: 'Bali kwa Muharram, kwa sababu ni mwezi ambao watu hurudi kutoka Hijja zao.' Wakakubaliana juu ya hilo." Riyawa hizi zinajulisha kuwa: 01-Kalenda ya kiislamu ilianzishwa kwa ajili ya kudhibiti matukio muhimu na muda wake-Baina ya waislamu 02-Kalenda ya kiislamu ilianzishwa mwaka wa 17 Hijiria 03-Inaitwa kalenda ya Hijria kwa sababu walikubaliana mwaka wake wa kwanza uwe ule mwaka alihama mtume ﷺ kwenda madina" 04-Walikubaliana kuwa mwezi wa kwanza katika kalenda ya kiislamu uwe mwezi wa muharram" kwa sababu ndio mwezi ambao watu hutoka kwenye ibada ya Hijjah" 05-Hivo basi tangu kuhama Mtume ﷺ kwenda Madina imepita miaka 1447-Yan Karne 15. Nataraji utakuwa umejifunza kitu kuhusu kalenda ya kiislamu-Allah akubariki, Anza kufatilia sasa kalenda hii tukufu ambayo inawaunganisha umma wa kiislamu" Imeandaliwa na Mohamedi Sungi Tar 29 Dhulhijjah 1447 H 15 Jun 2026 M-Tandika Dar Es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
99
16
06-HUKUMU ZA EID AL-ADHA KWA UFUPI" ●Inasisitizwa sana na Sheria yetu tukufu kuswali Eidil-Adha,Mpaka wanawake walio kwenye hedhi au nifasi wanasisitizwa kwenda kwenye viwanja vya Eid ●Mwanamke mwenye hedhi au nifasi akihudhuria kwenye muswala wa Eidi atatoa takbirah na kuitikia dua ya waislamu,Ispokuwa hatoswali ●Ni ssuna kwa mwenye kutoka kwenda kuswali eid kuvaa nguo nzuri na kujitia manukato kwa wanaume wa kiislamu-wanawake wavae nguo nzuri za stara pasina kuonesha mapambo wala kujitia manukato ●Ni ssuna kwa mwenye kutoka kwenda kuswali Eidil-Adha kutokula chochote toka inapoingia Alfajir mpaka atakaposwali Eid ●Ni ssuna kutembea kwa miguu ukiwa unaelekea kwenye muswala wa Eid ispokuwa kwa dharurah kama vile umbali n.k ●Swala ya Eid-haina Qabliyah wala Baadiyyah ●Ukifika kwenye muswala wa Eid uwanjani kaa chin-endelea kutoa tabkirah mpaka swala itakapo simama ●Kila mtu atoe takbira yeye mwenyewe-haifai kutamkishana yan akawa mmoja anaongoza tabkira wengine wanaitikia-hii haifai ●Baada ya Imamu kumaliza swala kwa kutoa salamu-Unakhiyar kati ya kusikiliza khutbah au kuondoka-yan si lazima kusikiliza khutbah ●Ni ssuna kubadili njia wakati wa kurejea kutoka kwenye muswala wa Eid-yan njia uliyoenda nayo si utakayorudi nayo ●Kisha ibada ya kuchinja Udh-hiyah ni baada ya kuswali Eid,Kuchinja ni ssuna iliyosisitizwa sana haipaswi kwa mwenye uwezo kuiacha,Baada ya Swala utachinja-kisha utanyoa na kukata kucha ●Eidil Adha ni sikukuu yenye siku 04 za kusherehekea-yan Siku ya 10,11,12 na 13 Dhulhijjah ●Unaweza kuchinja Udhhiyah ndani ya siku hizi 4 ●Kwa mwenye kuchinja atagawa nyama mafungu matatu,Moja lake,Pili la Jiran na tatu humpa maskini yeyote Muislam ●Haifai kuuza nyama au ngozi za Udh-hiyah-Mambo ni mawili ule au utoe zawadi/Sadaka basi ●Takbirah za Eidil-Adha huendelea mpaka alasiri ya siku 13 Dhulhijjah ●Eid ni katika alama kubwa za uislamu hivo tunapaswa kudhirihisha Alama hii majumbani,barabarani mpaka sokoni-kwenye mitandao ya kijamii N.k ●Hii ni sikukuu ya kula, na kunywa na kumtaja Allah-jiachie-pasina kufanya isirafu -wala kumuasi Allah ●Inapendeza kutembeleana sikukuu ya Eid na kubadilishana zawadi kati ya ndugu jamaa na marafiki" wazazi wawili hutangulizwa katika hili عيدكم مبارك،تقبل الله منا ومنكم صالح الأعمال،وأعاده الله علينا وعليكم أعواما عديدًا وزمنًا طويلا،وفي كل عام وأنتم بخيرٍ Mohamed Sungi 10 Dhulhijjah 1447 H 27/05/2026 Tandika Dar Es Salaam
148
17
05-Siku ya Arafa Nayo ni siku tukufu siku ya 09 kwenye mwezi wa dhul-hijjah, Siku ambayo mahujaji wageni wa Allah husimama kwenye viwanja vya Arafa kutekeleza nguzo muhimu katika ibada ya Hijjah, Hii ndio siku ambayo amesema Mtume Swala na amani ziwe juu yake" 《خير الدعاء دعاء يوم عرفة》أو كما قال عليه الصلاة والسلام {Dua iliyokuwa bora zaidi ni dua ya siku ya Arafa.... } Ni matumaini yangu,Tumeamka sote hali ya kuwa tumefunga Walhamdu lilah,Ispokuwa kwa wale wenye dharurah" Jioni ya Siku ya Arafa ndio kilipo kilele cha ubora wa siku hii tukufu, Ukiweza basi ukifika jioni ya leo jitenge peke yako mlilie mola wako haja na shida zako zote,Kubwa zaidi katika yale utakayoomba basi iwe kuomba mwisho mwema na pepo ,Na uepushwe na moto تقبل الله منا ومنكم صالح الأعمال Mohamedi Sungi 09 Dhul-Hijjah 1447 H 26/05/2026 M-Tandika Dar es salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
123
18
04-KHATIBU WA ARAFA MWAKA HUU 1447H/2026M ●Sauti yake si ngeni kwenye masikio ya wengi miongoni mwa waislamu ●Ni katika wanachuoni wakubwa wa zama zetu kwenye Elimu ya Quran na visomo vyake ●Huo msahafu ulio nao mikononi mwako umepitia mikononi mwake-ikiwa tu umechapwa Madina Saud Arabia Sheikh Alliy Bin Abdulrahmani Alhudhaifiy Allah amuhifadhi" Mwenye umri wa miaka 79 Alizaliwa Tar 22/05/1947 M ambayo sawa na Tarehe 01 Rajab 1366 H-katika kijiji cha Alqarnul Mustaqiym kilichopo kusini mwa makkah" Sheikh Alliy Bin Abdulrahman Alhudhaifiy amezaliwa na kukulia katika familia ya dini na elimu-ambapo baba yake alikuwa Imamu na khatibu katika jeshi la Saud Arabia, Elimu yake ya awali aliipata kwa masheikh wa kijiji chake,Akamaliza quran yote kwa kuangalia chini ya Sheikh Mohammad bin Ibrahim Alhudheifiy Allah amrehemu,Pamoja kuhifadhi baadhi ya mutuun za baadhi ya vitabu vya kisheria, Mwaka 1381H ambayo sawa na 1961M,Akiwa na umri wa miaka 14 alijiunga na Madrasatu Assalafiyah na kuhitimu hapo kwa kiwango cha mutawasitwa-Yan Secondar Mwaka 1383H sawa na 1964M akajiunga na Maahadil Ilmiy na kusoma kiwango cha Thanaawiy na kuhitimu mwaka 1388H_1969M akiwa na umri wa miaka 21 Mwaka huo huo alijiunga na chuo kikuu cha Alimam Mohammad bin Suud cha kiislamu kilichopo Riyadh,katika kitivo cha sheria na kuhitimu mwaka 1392H sawa na mwaka 1972H akiwa na umri wa miaka 25 Mwaka 1395H sawa na mwaka 1976M alipata masters katika chuo kikuu Al-azhari-Misri na badae akapata Ducturah-Yan Degree ya tatu katika chuo hicho cha Al-azhari kilicho Cairo Misri. Sheikh Alliy Bin Abdulrahmani Alhudheifiy aliteuliwa kuwa Imamu na khatibu wa Masjid anabawiy mwaka 1399H sawa na mwaka 1979' akiwa na umri wa miaka 32 Takriban, Badae mwaka 1401H Sawa na mwaka 1980M alihamishiwa makka akiwa imamu na khatibu hapo kwa muda wa mwaka mmoja na kurudishwa tena Madina mwaka 1402H sawa na mwaka 1981M akiwa ni Imamu na khattib katika Masjid alnabawiy mpaka leo hii-ambapo ni zaidi miaka 40 sasa" Pamoja na hayo Sheikh amekuwa muhadhir na profesa katika chuo kikuu cha kiislamu Madina kwa muda mrefu sasa Aidha amewahi kuwa imamu katika Masjid Qubaa kwa nyakati tofauti tofaut kabla ya kuteuliwa kuwa imamu msikiti wa Mtume Swala na Amani ziwe juu yake, Vile vile Sheikh ni Rais ya kamati ya kielimu ya kupitia masahafu chapa ya Madina" Hivo hivo ni mjumbe wa kamati ya kusimamia uchapishaji wa mas-hafu ya mfalme fahad Allah amrehemu Mwaka huu tarehe 18/05/2026 ambayo ni sawa na Tarehe 01 Dhul-hijjah 1447H aliteuliwa kuwa khatibu wa Arafa katika Masjid Alnamirah,akiwa ni khatibu wa 17 katika historia ya makhatibu wa Arafa katika Ufalme wa Saudi Arabia toka mwaka 1925" Sheikh Alliy Alhudhaifiy ni katika wasomi maarufu zaidi wa quran katika ulimwengu wa kiislamu,Toka miaka ya 80,akijulikana kwa sauti yake murua ya polepole mwenye kuchunga hukmu za Tajweed,matokeo na sifa za herufi" Sheikh Alliy Alhudhaifiy ametoa wanafunzi wengi na wasomi wengi wa quran, Miongoni mwao ni 01-Sheikh Abdullah Aljuhaniy Imam na khatibu Masjidil-haram Makkah 02-Sheikh Abdulmuhsin Alqasim Imam na khattibu Masjid Alnabawiy madina Na wengineo wengi Allah amuhifadhi Sheikh Alliy Alhudheifiy,Ampe afya njema na umri kwa manufaa ya uislamu na waislamu Imeandaliwa na: Mohamed Sungi 24/05/2026M 07 Dhul-hijjah 1447H Tandika-Dar Es Salaam
120
19
03-HALI YA WEMA WALIOTANGULIA PAMOJA NA QURAN KATIKA NYAKATI NA SEHEMU TUKUFU قال الحافظ ابن رجب الحنبلي رحمه الله تعالى Amesema Alhafidh Ibn Rajab Alhanbaliy Allah amrehemu {فأما الأوقات المفضلة كشهر رمضان،وخصوصا الأوقات التى تطلب فيها ليلة القدر،أو الأماكن المفضلة كمكة لمن دخلها من غير أهلها فيستحب فيها الإكثار من تلاوة القرآن،اغتنامًا لفضيلة الزمان والمكان} اهـ _ملخصًا-لطائف المعارف ٢٠١_ {Ama nyakati bora kama vile mwezi wa Ramadhani,Hasa hasa yale masiku ambayo hutafutwa ndani yake usiku wa laylatul qadr,Au sehemu bora-tukufu kama vile Makkah kwa mwenye kuingia humo katika wasiokuwa wakazi wake,Basi inapendeza kukithirisha sana kusoma Quran humo ili uchume ubora wa wakati na sehemu uliyopo} _Nimenukuu wa ufupi,Rejea kitabu Latwaiful maarifu ukurasa wa 201_ Maelezo ya ziada: 01-Wema waliopita walikuwa wakifika sehemu tukufu au nyakati bora wanasoma sana Quran kuliko kawaida 02-Hii ni kwa sababu kusoma Quran kuna malipo makubwa Kwa Allah-na kusoma hiyo Quran kwenye nyakati au sehemu bora malipo yake ni makubwa zaidi,hii ni kwa sababu malipo ya amali njema katika nyakati au sehemu bora huwa ni makubwa zaidi 03-Tunahimizana kusoma sana Quran ndani ya hizi siku 10 Dhulhijjah-Allah atuwafikishe 04-Ukiweza basi hitimisha Quran yote ndani ya kumi hili japo mara moja 05-Mwenye kupenda kusoma Quran yote ndani ya siku hizi basi afanye hivi: Siku ya 01 dhulhijjah soma Juzuu 4,hivo hivo siku ya pili soma juzuu 4,kuanzia siku ya 3 na kuendelea mpaka siku ya 8 soma juzuu 3 kila siku,Kisha siku ya 09 ambayo ni siku ya Arafa soma juzuu 4 Jumla zitakuwa juzuu 30" 06-Herufi moja kwa mwenye kusoma Quran hulipwa thawabu 10 kama ilivyothibiti kwenye hadeeth-hii ni nyakati za kawaida- Usiniambie kwenye miezi mitukufu malipo yake yapoje!!? Ikiwa mema hulipwa mara dufu kwa mara dufu?? قال تعالى {وفي ذلك فليتنافس المتنافسون...} الآية 07- {Na katika hilo basi washindane wenye kushindana} Ayah Imeandaliwa na Mohamed Sungi 29 Dhul-Qaadah 1447 H 17/05/2026 M Mbagala-Dar es Salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
146
20
02-YALE ANAYOPASWA KUYAEPUKA MWENYE NIA YA KUCHINJA UDH-HIYAH عن أم سلمة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: {إذا رأيتم هلال ذي الحجة وأراد أحدكم أن يضحي فليمسك عن شعره وأظفاره حتى يضحي}، وفي رواية { فلا يمس من شعره وبشرته شيئا } أخرجه مسلم Kutoka kwa Umm Salamah-Allah amridhie-amesema,Hakika Nabii Mohammad Swala na Amani ziwe juu yake amesema:Pindi mtakapo uona mwandamo wa mwezi wa Dhul-hijjah na akataka mmoja wenu kuchinja basi azuie nywele zake na kucha zake-asizikate mpaka atakapochinja} katika riwaya nyingine imekuja {Asiguse kitu katika nywele na mwili wake} Hadeeth ameipokea Imamu Muslim Faida tunazopata kwenye Hadeeth 01-Hadeeth inaonesha kuwa ukiandama mwezi dhul-hijjah na mtu akawa na nia ya kuchinja udh-hiya basi ni haramu kwake kukata nywele-zote na kucha zake 02-Mwenye nia anayekusudiwa hapa ni yule aliyeandaa mnyama tayari kwa ajili Udh-hiyyah" 03-Katazo linamuhusu mmiliki wa mnyama pekee yake,Hivo basi ikiwa mume ndio mmiliki wa mnyama wa kuchinjwa basi katazo halimuhusu mke na watoto linamuhusu yeye pekee,Na ikiwa mmiliki wa kichinjwa ni mke basi katazo halimuhusu mume na watoto" na mfano wake 04-Hivo hivo katazo halimuhusu wakala-yan yule aliyepewa jukumu la kuchinja pekee ambaye si mmiliki wa mnyama wa kuchinjwa" 05-Yule ambaye alikata nywele na kucha zake mwanzo kwa sababu hakuwa na nia ya kuchinja kisha akawa na nia ya kuchinja katikati ya kumi la kwanza la dhul-hijjah,basi ataanza kujizuia tokea pale alipoweka nia 06-Katazo linamuenea kila mwenye nia ya kuchinja awe mwanamke au mwanaume' 07-Ibada ya kuchinja ni katika ibada kubwa na tukufu hivo muislamu hupaswi kuacha kuchinja muda wa kuwa una uwezo,Ni uzurii uliyoje wa kauli ya Sheikh wetu Abuu Nufaida Sembe Allah amuhifadhi aliposema WAISLAMU TUSHINDANE KUCHINJA,TUNACHINJA KWA AJILI YA ALLAH MOLA WETU KWA NINI TURUDI NYUMA,TUNASHINDWA NA WASHIRIKINA AMBAO WANACHINJA KWA AJILI YA MIZIMU NA SHIRKI ZAO!! nimenukuu kwa ufupi maana ya yale aliyoyasema Sheikh. Imeandaliwa na: Mohamed Sungi 29/Dhul-qaadah/1447-H 17/05/2026-M Tandika-Dar es salaam وفق الله الجميع لما يحب ويرضاه
124