E-PLUS MEDIA
Open in Telegram
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
1 307
Rais wa Urusi Vladmir Putin amelaani kampeni ya hivi sasa ya Israel ya mashambulizi ya mabomu huko Gaza, ambayo yameua maelfu ya Wapalestina.
Akizungumza siku ya Jumatatu kabla ya mkutano na wajumbe wa Baraza la Usalama la Urusi, Putin alisema kwamba hakuna uhalali unaowezekana kwa kampeni hiyo.
."Matukio ya kutisha yanayoendelea hivi sasa katika Ukanda wa Gaza, wakati mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia wanaangamizwa bila kubaguliwa, hawana pa kukimbilia, hakuna mahali pa kujificha kutokana na mashambulizi ya mabomu, hayawezi kuhesabiwa haki na chochote," alisema Putin. .'Unapotazama watoto waliomwaga damu, watoto waliokufa, wazee wanaoteseka, vifo vya matabibu - ngumi zinakunjwa na machozi yanatoka. .hata hivyo hatupaswi, hatuwezi kujiruhusu kuongozwa na mihemko,’ aliongeza, akisema kwamba majibu ya ngazi ya juu yanahitajika ili kushughulikia ipasavyo hali katika kanda..
1 307
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken walifika mbele ya Kamati ya Ugavi ya Seneti kuomba ufadhili wa ziada wa dola bilioni 68.3.
Huduma ya vyombo vya habari ya Pentagon inaandika kuhusu hili. Kati ya kiasi hiki, bilioni 10.6 zinapaswa kwenda kusaidia Israeli, na bilioni 44.4 kusaidia Ukraine. Maafisa pia waliomba bilioni 3.3 kwa mahitaji ya kijeshi ya Marekani.
Wamarekani lazima waelewe kwamba kile kinachotokea Ukraine na Israel kinaathiri usalama wa taifa wa Marekani, Austin alisema.
1 307
VITA YA TATU(3) YA DUNIA ILISHAANZA TOKA MRUSI ALIPOIVAMIA UKRAINE; Kumbuka Daniel Alikaa Uhamishoni Babeli Tangu Mwaka 606 B.K Hadi 538... Ukichukua 606-538=68...!!😭🤔
#Neno Linasema; Basi Hapo Mtakapoliona Chukizo La Uharibifu, Lililonenwa Na Nabii Daniel Limesimama Katika Patakatifu [ Asomaye Na Afahamu ]... Math 24;15.
#>ZINGATIA HILI; Kumbuka Daniel Aliambiwa Muda Wa MAJUMA 70 Umeamriwa Juu Ya Watu Wako. Majuma 68 Yalishakwisha Tangu Daniel Alipokuwa Babeli, Na Sasa Hivi Tupo Juma La 70 Ukipiga Hesabu Vizuri Utaona, Ambapo Ukiwa Umekwisha Kukusudiwa👉 Daniel 9;24-27. [ Asomaye Na Afahamu ]. Over 🤸🏃🚴🏇🚁
_ By Askari Injili INNOMJESHI _
1 307
WAZIRI GWAJIMA ALIA NA WIMBO WA ZUCHU (HONEY) ADAI UNAHARIBU WATOTO.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima ameonyesha kuchukizwa na wimbo wa Zuchu (Honey) akidai kwamba wimbo huo umetokea kupendwa sana na watoto wa shule ya msingi huku tatizo kubwa likiwa ni maneno ya kihuni yaliyotumika ndani yake ambayo kimsingi hayapaswi kusikika kwenye masikio ya watoto.
"Honey wangu akinuna namkatia viuno...."- huu ni moja ya mstari kwenye wimbo huo ambao unawafanya watoto waimbe kwa hisia huku wakinengua viuno jambo ambalo halikubaliki kabisa kwasababu linachangia mmomonyoko wa maadili.
Waziri Gwajima amewaonya Washereheshaji, Ma-Dj na Walimu waache kuupiga wimbo huo mashuleni na hata kwenye sehemu ambazo zina mkusanyiko wa watoto ili kuuepuka mkono wa sheria. Aidha Dkt. Gwajima amemtaka Zuchu apunguze ukakasi kwenye nyimbo zake anazotunga na ikiwezekana aimbe wimbo maalumu kwa ajili ya kuwaelimisha watoto kwani nyimbo zake zinapendwa sana na watoto.
1 307
HARMONIZE SIO MTU MBAYA ILA HANA SHUKRANI; BABA LEVO
"Mimi sioni kama Harmonize ni mtu mbaya ila ni mshikaji ambaye hanaga shukrani, na hicho ni kitu cha kawaida watu kukosa shukrani kwa watu waliowasaidia. Ndio maana tunaambiwa tenda wema uende zako, lakini kwa mimi sioni ubaya wowote wa Harmonize, hatujawahi kusikia kampiga mtu na mimi nakutana na Harmonize mara nyingi mbona hajawahi kunipiga?!"
"Tukikutana na Harmonize tunasalimiana vizuri tu na sometime anakuwa na mahela anatuonyesha kwamba ana pesa na hizo pesa akiziweka vibaya nazikwapuaga mara mojamoja"- Baba Levo
1 307
DYLAN SIYO MWANANGU NI MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ; BILLNAS
"Habari za mimi kufananishwa na Dylan nazisikia kama watu wengine wanavyozisikia mtandaoni, lakini siyo mtoto wangu na haiwezekani. Yanayoendelea ni kama mtu umeona ndege inapaa juu alafu mtu akwambie ile ni ndege yako wakati hata hujui ni ya nani na ni kina nani wamo ndani"
"Mimi sijawahi kuwa kwenye mahusiano na Hamissa Mobetto, sio mama mtoto wangu na ni kitu ambacho hakiwezekani ingawa kweli tuliwahi kuwa washkaji lakini sasa hivi hatuna ushikaji tena. Zamani nilikuwa na namba yake na yeye alikuwa na namba yangu lakini baada ya haya maneno kuja tuliblockiana"
"Nandy haumizwi na hizi taarifa kwasababu anajua mimi sijawahi kuwa kwenye mahusiano na Hamissa, mke wangu ni muelewa hawezi kuwaza lolote kwasababu anajua ukweli na isitoshe wale ni marafiki kwahiyo kama kungekuwa na ukweli wasingekuwa na ukaribu na hata nikikutana na Diamond huwa namwambia yule mtoto ni wake"- Billnas
1 307
CHANZO CHA VITA KUU YA TATU YA DUNIA.
Picha unayoiona hapo chini Ni msikiti wa dhahabu maarufu Sana duniani kwa jina la AQSA, ambao uko katika viunga vya mji wa Jerusalemu.
Msikiti huo ulijengwa baada ya Vita ya jihadi iliyopiganwa Kati ya uislam na uyahudi na kupelekea kubomolewa kwa hekalu la Sulemani na kujengwa msikiti huo. Vita hii ilifanya mji wa Jerusalem kuangukia mikononi mwa utawala wa kiislamu (islamc empire).
Waislamu duniani wanaheshimu na kuthamini eneo hili na kila Mwaka wanaenda kuhiji au kulitembelea eneo Hilo wanaloamini Ni takatifu katika dini yao.
Wayahudi na Wakristo wanaliheshimu na kulithamini eneo hili na kuamini ndipo lilipokuwepo hekalu lililojengwa na mfalme Sulemani.
Vita na migogoro mingi unayoishuhudia mashariki ya Kati chanzo Chake Ni msikiti huu wa dhahabu. Kila dini linadai Ni mahali pake patakatifu.
Vita ya tatu ya kidunia ambayo itahusisha slaha za nyuklia , chanzo Chake kinaaminika kusababishwa na mgogoro wa msikiti huu wa AQSA.
Wayahudi wanampango wa kuubomoa msikiti huu ili kujenga hekalu jipya, na hapa ndipo chanzo Cha Vita ya kidini Kati ya mataifa ya kiislamu na mataifa yanayounga mkono Israel.
Vita hivi vitaitwa Vita vya AMAGEDON.
Mataifa ya GUGO yatapigana na mataifa ya MAGUGO. Mamilioni ya watu watakufa na dunia itakuwa katika eneo isiyo salama kuishi.
Nchi nyingi duniani zitakumbwa na mtikisiko wa kiuchumi, njaa, mafuriko na matetemeko ya ardhi.
Vita hivi vitaisha kwa makubaliano ya mkataba wa amani, ambao utaunganisha dini tatu za ukristo, uislam na uyahudi kuwa dini moja ya kishetani ambayo Ni ya mpinga Kristo, na dunia itaanza rasm matumizi ya no 666.
Dunia itakuwa na dini moja, serikali moja na fedha moja.
Kwa hiyo hakuna mtu kuuza Wala kununua, Wala kutibiwa asipokuwa na chapa ya kishetani ya no 666.
Myaonapo Mambo hayo yakitokea tambueni ya kwamba Siku za mwisho zimekaribia.
Mwenye kudhurumu azidi kudhurumu.
Mwenye uchafu azidi kuwa mchafu.
Mtakatifu azidi kujitakasa.
Mwana wa Adamu yupo mlangoni kulichukua kanisa lake.
Mungu akubariki
Kuhani wa kifalme
Mwl/mtume
David mahala.
0785788393 (whasap)
Maombi
Ushauri.
1 307
"Hivi wanawake wenzangu mnawezaje kucheat jamani? Mbona mimi siwezi na nikijaribu tu nitafumwa, alafu nikisema nicheat huwa najisikia vibaya kwenda kumvulia mtu mwingine, napenda kuwa na mmoja tusumbuane weeee tukiachana ndio nianze moja"- Husna Sajenti
1 307
"Mara yangu ya kwanza kumuona Nandy tulikutana chuoni kwasababu tulikuwa tunasoma chuo kimoja, baada ya hapo nilikuwa namuona kwenye mitandao nikampenda sana. Kwa mara ya kwanza niliongea nae kupita simu ya rafiki yangu ambaye alikuwa anaongea nae nikachukua simu yake nikaongea nae hapo nikazidi kumpenda zaidi"
"Kwa mara nyingine tulikutana kwenye Fiesta nikaanza kumsumbua kumtongoza, alichukua muda mrefu sana kunikubali kwasababu mimi mwenyewe kutongoza kidogo kunanisumbua. Nina mdomo mzito sana mpaka nimwambie mtu nimempenda ujue nimempenda kweli. Nandy kwa sasa siyo mjamzito kama watu wanavyosema ila ikitokea tutashukuru Mungu kwasababu sisi ni wanandoa na mambo kama hayo ndo baraka zenyewe"- Billnas
