en
Feedback

Don't get caught by a cheater! Telemetrio finds and tags such channels 👉 If you want to see the tag, subscribe

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Open in Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

Show more
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
Rose Muhando kwenye hekaheka za kuieneza Injili Ulimwenguni.
Rose Muhando kwenye hekaheka za kuieneza Injili Ulimwenguni.

⚠️😢 Kuna wakati nilifikiria kutaka kujiua, mke alinizunguka nikapoteza sehemu kubwa ya mali zangu na nikakosa mwelekeo - Emeka Ike Wengi walikuwa wanajiuliza ukimya wa muda mrefu wa Emeka Ike(56) muigizaji wa Nigeria alijizoelea umaarufu miaka ya nyuma Akihojiwa katika interview mpya, Emeka kwa masikitiko ameeleza yaliyompata ndani ya ndoa kutoka kwa aliyekuwa mke wake(Suzanne) ambaye wana watoto 4 pamoja kuwa ndie aliyesababisha anguko lake Emeka amesema aliyekuwa mkewe alimtuhumu mambo ya uongo kuwa anamfanyia ukatili wa vipigo na akaja kushangaa mambo yapo mitandao na kwenye vyombo vya habari watu wanamuona Emeka mbaya. Emeka amesema alipomuuliza mke wake vipi kwani huwa nakupiga mke akajibu sio unajua wewe ni mtu maarufu mambo kama hayo ya kuongelewa hivi na vile hata kama si kweli hayaepukiki Emeka amesema kuna kipindi alisafiri kwenda Marekani na begi lake tu lakini kumbe huku nyuma mke wake akawa anafanya yake, Emeka aligundua hata habari za kumfanyia ukatili mkewe ni mpango uliosukwa na mke wake ili kumharibia Emeka Emeka amesema alivyoenda tu Marekani mke akaenda kwenye shule ya secondary inayomilikiwa na Emeka akatimua wanafunzi wote na kuifunga shule, mke akabeba kila kitu ndani ya nyumba akaacha nyumba tupu. Mke alihodhi na kuuza viwanja na mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na Emeka. Emeka amesema alipoteza karibia 80% ya ardhi aliyokuwa akimiliki anakuja kushangaa watu wanajenga kwenye ardhi aliyokuwa akiimiliki Emeka anasema hata elimu ya chuo kikuu yeye ndie alimlipia mke wake gharama ila hakujua kuwa alimpenda mwanamke ambaye yeye hakumpenda na hicho anasema kitendawili ambacho kinawakumba wengi kuwekeza kwa mtu na kumpenda mtu kumbe yeye hakupendi ila hujui mtu huyo anawaza nini kuhusu wewe Anasema mke wake alikuwa mjanja mjanja na ndie aliyevunja ndoa. Anasema aliyekuwa mkewe aliwahi kumwambia yeye si aina ya mwanamke wa kuwa kwenye ndoa ila Emeka hakumpatiliza sana. Mkewe alikimbilia mahakamani 2015 kutaka ndoa yao iliyodumu kwa miaka 14 ivunjwe kwa madai mume ni mkatili anampiga, 2017 ndoa ilivunjwa mahakamani baada ya mke kusisitiza hataki ndoa japo upande wa Emeka na familia yake hawakutaka ndoa ivunjwe Emeka amesema anasikitikia vijana wa sasa ambao pia wanakumbana na wanawake wengi tu ambao sio wa kuwa nao kwenye ndoa ila wanalazimisha kuoa wanawake hao huku wakiwapuuza wanawake sahihi waliotulia wenye sifa za kuwa kwenye ndoa kwa utulivu Emeka anaamini pia kulikuwa na wanaume waliokuwa wanamzuzua aliyekuwa mkewe hadi kumuona hafai

photo content

⚠️😳 Mke wa Stivo Simple Boy atajwa kupata mimba ya mwanaume mwingine nje ya ndoa yao Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kilicho karibu na wanandoa hao wawili wa nchini Kenya hali hiyo imemvuruga Stivo ambaye ni mwanamuziki mwenye jina kupitia ngoma kama Fresh Barida na Vijana Tuache Mihadarati Kuhusu suala hilo, Stivo ameonekana akijitetea kwamba walikuwa wametengana muda kidogo na mkewe kwa jina la Grace Atieno na waliporudiana ndio akahamaki mkewe ana mimba ya mwanaume mwingine Mkewe amekataa kuongelea suala hilo kwasasa akisema atakuja ongea ya upande wake baadaye Hata hivyo, katikati ya mwaka huu, mkewe huyo akihojiwa alisema ndoa yao ina hali mbaya sana kiuchumi na kuhitaji wasaidiwe na wasamaria wema , alisema hata kula yao ilikuwa shida kwa kipindi hicho kwani Stivo alikuwa amefulia sana ndio sababu akawa hatoi hata wimbo mpya, pia akaunts za Stivo za mitandao ya kijamii alisema hazipo mikononi mwa Stivo bali zipo chini ya meneja wake aliyedai anamkandamiza Stivo kimaslahi mumewe hajui hata akihitajika kikazi huwa analipwa kiasi gani

photo content

⚠️😳 "Harmonize hawezi kunisaidia alitaka tu kupita na upepo wa wimbo wangu wa "Tamaa Mbaya" - Twenty Percent
⚠️😳 "Harmonize hawezi kunisaidia alitaka tu kupita na upepo wa wimbo wangu wa "Tamaa Mbaya" - Twenty Percent

BADO NIPO AZAM TV Kutoka kwa mtangazaji kinara wa kandanda nchini Tanzania, Baraka Mpenja kutoka Azam Media amefunguka haya "MOJA YA Swali ambalo nimeulizwa sana na Mashabiki wangu, Mwamba uko wapi hatukusikii?, NI KWELI umefukuzwa kazi Azam TV?. Hahahahah!. Kwa sababu ni Swali linalojirudia sana, ngoja niwape majibu mridhike Watu wangu. Mimi bado ni Mfanyakazi wa Azam Media LTD, nina Mkataba na Kampuni hii kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati. Naendelea na majukumu yangu kama kawaida ya Kutangaza soka na kuzalisha Vipindi kama Mshikemshike Viwanjani. Guys! wengi mmenijua kupitia kutangaza kandanda, lakini hamjui kama mimi ni MTOZI (Producer) wa Vipindi, nina majukumu mengine ambayo nayatekeleza kila siku. Kwahiyo, ondoeni shaka ndugu zangu, mimi nipo na ninaendelea na kazi zangu na wakati wowote mtanisikia nikitangaza mechi mbalimbali kama kawaida. Watangazaji wa kandanda tupo wengi AZAM TV, lazima kuwe na Rotation kama timu ya Mpira wa Miguu, Viongozi wanamtumia kila Mtangazaji kwa mahitaji maalumu na kila Mtangazaji ni hodari mno, MashaAllah!. Hakuna FIGISU YOYOTE, Viongozi wangu ni Watu Waadilifu, sitamani wasingiziwe uongo, ni WATU maridadi ambao wamejaaliwa maono makubwa. Mitandaoni huwa kuna mengi bwana!..., lakini chukueni kutoka kwangu, KILA KITU KIPO SAWA!. Wasalaam!"

photo content

WATU wawili ambao ni mume na mke wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kuacha njia na kugonga gema katika M
WATU wawili ambao ni mume na mke wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kuacha njia na kugonga gema katika Mlima Kinombedo, uliopo kijiji cha Mkwiti, wilayani Newala mkoani Mtwara majira ya saa moja asubuhi. Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo, imesema pikipiki iliyopata ajali ilikuwa ni namba za usajili MC 828 BUT, na chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kumudu pikipiki hiyo. Kamanda Katembo amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Ismail Hajili Chitapwidi, na mkewe ni Aisha Bakari Chilambo ambapo ametoa rai kwa watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwasihi abiria kuvaa kofia ngumu. Cc: Nipashe

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Salome Nko (pichani kulia) ambaye ni Mkazi wa Seele Singisi Wilayani Arumeru Mkoani
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Salome Nko (pichani kulia) ambaye ni Mkazi wa Seele Singisi Wilayani Arumeru Mkoani Arusha ameuawa na kufukiwa kwenye kinyesi cha ng’ombe na Mtu anayedaiwa kuwa ni Mume wake baada ya kutengana kutokana na kugombana na kila mmoja kuishi sehemu yake. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda amethibisha kufariki kwa Salome na kusema Watu kadhaa akiwemo Mumewe wanashikiliwa kwa uchunguzi.

Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha watu kuwa na upara. Baadhi ya sababu hizo ni; 1. Kurithi: Ikiwa upara upo katika fa
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha watu kuwa na upara. Baadhi ya sababu hizo ni; 1. Kurithi: Ikiwa upara upo katika familia yako, kuna uwezekano mkubwa wa kuurithi. 2. Mabadiliko ya Homoni: Mabadiliko katika viwango vya homoni kama vile wakati wa ujauzito, au hata matatizo ya tezi yanaweza kuchangia. 3. Msongo wa Mawazo: Msongo wa Mawazo wa muda mrefu unaweza pia kuathiri afya ya nywele. 4. Magonjwa: Magonjwa kama alopecia areata na magonjwa mengine ya ngozi au kiafya, yanaweza kuchangia kupoteza nywele. 5. Matumizi ya Dawa: Baadhi ya dawa zinazotumika kwa matibabu kama vile chemotherapy, dawa za homoni, na dawa nyingine zinaweza kuwa sababu. 6. Mlo: Lishe duni au upungufu wa virutubisho muhimu katika mwili unaweza kusababisha udhaifu wa nywele na hivyo kusababisha upotevu wa nywele.

Mkoa [Dar es Salaam] uko salama sana. Na yeyote ambaye anaendelea kulalamika kwamba mkoa huu labda una mambo mengi, una folen
Mkoa [Dar es Salaam] uko salama sana. Na yeyote ambaye anaendelea kulalamika kwamba mkoa huu labda una mambo mengi, una foleni nyingi, tafadhali, kuna vijiji vingi bado havijajaa unaeweza ukahamia huko mkoa ukauacha.” – Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeonya matumizi mabaya ya pesa ikiwemo wale wanaotumia pesa hizo kutengeneza mashada na maua kwa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeonya matumizi mabaya ya pesa ikiwemo wale wanaotumia pesa hizo kutengeneza mashada na maua kwa ajili ya kuwatunuku wapendwa wao. Akizungumza na Swahili Times, Meneja Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano, Noves Moses amesema pesa inapotumika kufanya shughuli nyingine tofauti ni kukiuka utaratibu pamoja na kuipa gharama Serikali kutengeneza pesa mpya kutokana uchakavu wa pesa. “Tuligundua pia maeneo mengi tu ya nchi utakuta noti zinatengenezewa mashada, zinatengenezewa maua, watu wengine wanatupa chini pesa au labda mtu anatoa burudani ile noti inachukuliwa inaenda kubandikwa sehemu yenye jasho, kichwani, kwenye paji la uso. Kwahiyo matumizi ya namna hiyo ndiyo ambayo tunatolea ufafanuzi kwamba mnapofanya hivyo mnakiuka sheria, hizi ni pesa ambazo zinatumia gharama ambayo ingeweza kutumika kufanyia mambo mengine kwaajili ya ustawi wa jamii lakini sasa zinatumika kutengenezea noti mpya,” ameeleza.

"Kufanya kazi ya aina moja (Uigizaji) na watoto wangu kidogo inataka moyo lakini mimi najitahidi kusimama kama mama nikipata
"Kufanya kazi ya aina moja (Uigizaji) na watoto wangu kidogo inataka moyo lakini mimi najitahidi kusimama kama mama nikipata muda naongea na Mwanaheri lakini pia naongea na Patrick, nawashauri wawe na heshima, nidhamu na bidii kwenye kazi yao kwasababu hii ndio ajira yetu tuliyoichagua" "Kuhusu kufanya nao kazi ya pamoja nipo kwenye mchakato huo na ikimpendeza Mungu haitachukua muda mrefu mtaiona kazi sokoni"- Hidaya Njaidi, Mwigizaji wa filamu Tanzania na Mama Mzazi wa Waigizaji Patrick Kanumba na Mwanaheri. Toa maoni yako

"Nilisimamiia kesi ya Feitoto (@feisal194) si kwa sababu ni Mzanzibar mwenzangu kuna mtu alikuja kuniona akaniambia stori ya
"Nilisimamiia kesi ya Feitoto (@feisal194) si kwa sababu ni Mzanzibar mwenzangu kuna mtu alikuja kuniona akaniambia stori ya Feitoto. Kipindi hicho alikuwa ameshindwa. Nilitazama ile judgment waliyoiandika. "Ile hukumu walioitoa na maandishi yaliyoandikwa na Kamati ya nidhamu. Niliisoma na nilitazama na sheria ya FiFa na TFF nikaona haina maana 'it doesn't make sense' Nilizungumza na Wanasheria wa Feitoto. "Sijui kama uwepo wangu kwenye Ile kesi ulisaidia. Ila ninachojua nadhani Rais Samia Suluhu Hassan kulisemea hili jambo na kushauri hili jambo limalizike, ndio ilisaidia" Fatma Karume

"Mwalimu Julius Nyerere aliwaambia wasaidizi wake walete mpiga picha. Sijui nani alipiga picha ile kama alikuwa wa mpiga pich
+1
"Mwalimu Julius Nyerere aliwaambia wasaidizi wake walete mpiga picha. Sijui nani alipiga picha ile kama alikuwa wa mpiga picha wa Ikulu au wa gazeti la Daily News. Nilikuwa na miaka 15 au 16. Nilipozi lakini Mwalimu Nyerere hakupenda pozi langu la kwenye picha. Akasema tutembee. Kwenye ile picha tulikuwa tunatembea. Alisema picha ya kusimama haipendezi akasema tutembee kwa style" "Baada ya Ile picha niliondoka kurudi Uingereza. Nilivyorudi Tanzania, Bibi yangu aliniambia Mwalimu ameniletea picha zangu. Zilikuwa nyingi. Picha moja alitia saini . Akaandika “For Fatma. With love from Julius K. Nyerere”. 🗣️ Fatma Karume

HIVI NI NINI KILIMUUA RITA? Rita ni kibao cha mkongwe Marlow 2005 Kila nikisikiliza mashairi nabaki kujiuliza nini kilsababis
HIVI NI NINI KILIMUUA RITA? Rita ni kibao cha mkongwe Marlow 2005 Kila nikisikiliza mashairi nabaki kujiuliza nini kilsababisha Rita kufariki?

Rais wa Urusi amepuuzia madai ya Marekani kwamba Moscow inaweza kuishambulia NATO na kueleza kuwa Urusi haina nia hiyo na mzo
Rais wa Urusi amepuuzia madai ya Marekani kwamba Moscow inaweza kuishambulia NATO na kueleza kuwa Urusi haina nia hiyo na mzozo kama huo ungeenda kinyume na maslahi ya nchi yake. Kauli hiyo imefuata wiki chache baada ya Rais wa Marekani, Joe Biden kuonya kwamba ikiwa Putin atashinda vita dhidi ya Ukraine, anaweza kuwa na ujasiri wa kushambulia NATO na kusababisha vita kati ya wanajeshi wa Marekani na Urusi.

“Wazazi Watanzania acheni kuiachia mitandao kuwalea watoto wenu, mtakuwa mnawapeleka kwenye shimo ambalo mtakuwa mmewapoteza.
“Wazazi Watanzania acheni kuiachia mitandao kuwalea watoto wenu, mtakuwa mnawapeleka kwenye shimo ambalo mtakuwa mmewapoteza. Kwetu sisi ni sawasawa na kuwatoa kafara watoto wako. Hata huko kwenye mitandao ilipoanzia bado kwenye televisheni zao, vishikwambi wameweka parental control, sisi huku tumevamia wazima wazima, tutapoteza watoto wetu.” – Nape Nnauye, Waziri wa Habari

KUTOKA ILALAAAAAAA ILA SIDISI TEMEKE HATA KINONDONI PIA....KING KONG🙌 Ukiachana na kubezwa na baadhi ya madhabiki na media m
KUTOKA ILALAAAAAAA ILA SIDISI TEMEKE HATA KINONDONI PIA....KING KONG🙌 Ukiachana na kubezwa na baadhi ya madhabiki na media mbalimbali huyu mwba ana balaa lake najua baadhi hawatanielewa hasa vizaz vya akina lunya killer njoo umwone mwamba kwenye hizi kolabo 1 geez,jay Moe ft chid-mim 2.mchizi wng 3.like faza like San 4.kiba ft chid-far away 5.Diamond ft chidbenz-nalia 6. CHID ft mzee yusuph 7.spark ft chid-lait ungejua Achana na goma la Taifa la DSM STAND UP mwamba anasehem yake najua Wengi watauliza huyu ni Nan na wengine watamjua Kwa sehem moja tu (uteja) hawatambui mwamba amekua mtu WA namna gan tukumbushane wengine wanasahau Huyu ndo KING KONG💪💪