E-PLUS MEDIA
Open in Telegram
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
1 307
Tanzania imeshika nafasi ya pili Afrika na ya 10 duniani kwa idadi ya watalii wanaoingia nchini, huku idadi ya watalii wakiongezeka kwa asilimia 19 kufikia mwezi Septemba mwaka huu, ikitanguliwa na Ethiopia ambayo utalii wake umekua kwa asilimia 26.
Ripoti iliyotolewa Novemba 30 mwaka huu ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Utalii Duniani iitwayo "World Tourism Barometer" imebainisha kuwa idadi hiyo inalinganishwa na idadi ya juu iliyopata kufikiwa ambayo ni kabla ya janga la Uviko-19 mwaka 2019.
Aidha, katika kipengele cha mapato ya sekta ya Utalii, Tanzania imekuwa ya 10 duniani na ya tatu Afrika (ikiwa nyuma ya Mauritius na Morocco kwa Afrika) katika nchi ambazo zimeongeza kwa kiwango kikubwa mapato yake ikilinganishwa na mwaka 2019 ambapo ripoti hiyo inaonesha kwa Tanzania yameongezeka kwa asilimia 26.
1 307
AMEFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA
Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF) limemfungia maisha kujihusisha na masuala ya soka, aliyekuwa rais wa klabu ya Ankaragucu, Faruk Koca, baada ya kumpiga ngumi muamuzi.
TFF imefikia uamuzi huo wa kumfungia Koca baada ya kumpiga ngumi mwamuzi mwishoni mwa mechi ya Super Lig dhidi ya Caykur Rizespor ambapo mechi iliisha kwa sare ya 1-1.
Pia, TFF imeipa adhabu klabu yake ya Ankaragucu kulipa faini ya lira Milion mbili (£54, 000) sawa na zaidi ya Milion 149 za Kitanzania.
Ankaragucu imetakiwa kucheza michezo mitano (5) bila mashabiki kutokana na machafuko machafuko yaliohusisha mashabiki na viongozi wa klabu hiyo.
Mechi katika ligi zote za soka nchini Uturuki zilisitoshwa wa muda usiojulikana baada ya kiongozi huyo kufanya vurugu baada ya timu yake kukubali bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya wapinzani wao Rizespor.
1 307
Kwa mnaosafiri Kwa ajili ya Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka, ni jambo jema,uwe peke yako au na familia yako
Jiandae ki saikolojia
1.Hakikisha gari iko vizuri
2.Safiri mchana tu
3.Waza kufika salama na si saa ngapi
4.Epuka mafuta ya vichochoroni
5.Kama kwenu mbali yaani km 700 na zaidi basi safari yako unaweza kuikata vipande viwili
6.Ukiwa na wasi wasi na uwezo wako tafuta mtu ukifika mpe posho kidogo na nauli arudi
7.Kuwa makini sana unapoanza safari na unapokaribia kufika
8.Usipende kusimama porini usipopajua bila sababu au kuchimba dawa
9.Usiku ukipishana na gari punguza mwendo huku ukiibia kushoto kwako kidogo
10.Epuka kushindana na gari/mtu ambaye hata hujui anatoka na anakwenda wapi hata kama gari lake ni sawa na la kwako
11.Kama vipi andaa chakula toka kwako anayeendesha atumie vyakula vyepesi bites zaidi nyama kavu za kutafuna
12.Akili yako muda wote iwe barabarani na sio unakokwenda au unakotoka
13.Jitahidi njiani si kila mtu ajue unaenda wapi
14.Hakikisha upepo uko sahihi wakati wote
15.Hizi mvua kuwa makini ukiona inazidi tafuta mahali salama paki subiri ipungue kisha uendelee
16.Hakikisha hakuna gari lolote nyuma linakufuata kwa muda mrefu bila sababu,chukua namba kisha mpishe aende
ÑB.
sina shaka utaambulia japo moja kati ya hayo
1 307
Fahamu kuhusu Shoroba za wanyamapori 🐘🐃🦏🦒🦓
MAANA YA USHOROBA
Ushoroba ni eneo la asili ambalo wanyamapori wanalitumia kupita kutoka eneo moja kwenda jingine, au ni eneo linalounganisha maeneo mawili yaliyohifadhiwa.
FAIDA ZA USHOROBA
Ushoroba unasaidia wanyamapori kupita ili kujipatia mahitaji yao kama chakula na maji katika eneo jingine maana hakuna eneo ambalo lina mahitaji yao yote kwa muda wote.
FAIDA ZA USHOROBA
Ushoroba unapunguza migongano baina ya watu na wanyamapori, unasaidia wanyamapori kuhama eneo lao linapokuwa na changamoto ya majanga ya asili kama moto, mafuriko, ukame, nk.
FAIDA ZA USHOROBA
Ushoroba unasaidia wanyamapori wa eneo moja kwenda kuchanganya vinasaba wanapozaliana na wanyamapori wa eneo jingine na hivyo kupata kizazi imara kinachoweza kuhimili changamoto za magonjwa, ukame, nk.
#Tawa
1 307
⚠️😳 Jake mtangazaji wa BBC pia mwanasheria wa haki za binadamu, anasema akiwa kwenye ndege kwa safari ya saa sita toka Brussels, Ubelgiji kwenda Montreal, Canada, jirani katika siti yake alikuwa mwanamke
Na katika mazungumzo yao kama abiria, mwanamke husika akamueleza kwamba alikuwa kwenye ndoa ambayo kwa miaka minne aligundua mume wake anamsaliti kwa kuchepuka na wanawake wengine ila alijifanya kama hana anachojua kuhusu usaliti wa mumewe kwenye ndoa yao
Ambapo, mwanamke husika alianza kujipanga kimya kimya na safari yake ya Canada ndio amehamia huko moja kwa moja akaanze maisha yake mapya huku nyuma mume hajui kama mkewe kahamia moja kwa moja Canada kwani alimuaga tu kuwa anasafiri kuna vitu anaenda nunua
1 307
"Ni Professor Jay na Sugu wasanii ambao wamewahi kusimama na mimi katika kipindi cha kutengwa kwangu. Watabaki kwenye historia yangu milele." - Lady Jaydee, Msanii wa muziki Tanzania.
1 307
⚠️ Bunge la Ulaya lapinga serikali kuwaondoa wamasai Ngorongoro
Bunge la Ulaya limechukua hatua hiyo Desemba 14, 2023 ambapo kura 493 zimekubali Wamaasai waachwe maeneo yao
Kura 29 zimependekeza waondolewe huku kura 17 zikikosa maamuzi
Bunge hilo limelaani kuondolewa kwa wamaasai kwa kisingizio cha uhifadhi, pia limesisitiza haki za wenyeji ni sharti lisiloweza kujadiliwa kwa mpango wowote wa uhifadhi
Serikali ya Tanzania imekuwa ikiendelea na mchakato wa kuwahamisha baadhi ya wakazi wa wilayani Ngorongoro kwa maelezo ongezeko lao linawaweka katika ushindani na wanyama pori
Aidha, wabunge wanaitaka serikali ya Tanzania kuruhusu ziara za uchunguzi wa taasisi za Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Ulaya (EU) katika maeneo husika
Credit: Jamiiforums
1 307
"Vijana wengi Wakike na Wakiume wanateshwa na roho ya kujichua na jini mahaba"- Mwl. Sialove Lukumay
1 307
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imezindua mtambo unaotumia hewa tiba yenye mgandamizo ya oksijeni (Hyperbaric Medicine Treatment) ambao unatibu magonjwa zaidi ya 10 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ya pili Kusini mwa Jangwa la Sahara kutumia mtambao huo uliogharimu TZS milioni 250.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mtambo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema kupitia matibabu hayo, mgonjwa huingizwa kwenye kifaa maalumu na kupatiwa tiba kupitia hewa tiba ya oksijeni iliyogandamizwa kwa asilimia 100.
Amesema wagonjwa watakaonufaika ni wale wenye vidonda sugu ambavyo matibabu mengine yameshindikana kama wagonjwa wa sukari, walioathirika na moshi baada ya kuungua na moto na waliopata changamoto za upungufu wa oksijeni mwilini kama waliozama kwenye maji baharini nakadhalika.
Wagonjwa wengine ni pamoja na walioungua na moto, wenye upungufu mkubwa wa damu ambao kwa njia moja au nyingine hawawezi kuongezewa damu, waliopata ajali na kupata majeraha mwilini yasiyopona na wagonjwa wenye maambukizi kwenye mifupa isiyopona.
1 307
Tuna uandishi wa kikasuku usiozingatia taaluma. Yani mtu anaokota habari bila kuilewa vizuri anaichapa. Ndio maana SAUT kitabaki kuwa chuo bora cha habari maana ukisoma uandishi lazima usome Media Law, Human Rights Law na Constitutional Law.
Pia kuna option za Criminal Procedure Law na Law of Evidence ili ukiripoti mambo ya kisheria usiwe tabula rasa (angalau uwe na uelewa kidogo).
Anyway; ngoja nitoe shule kidogo maana wengi wamepotoshwa eti akina Halima wamerudishiwa uanachama. SI KWELI. Kwanza ieleweke hawakufukuzwa uanachama na Baraza Kuu, bali Kamati kuu (angalia next slide utaona). Kamati Kuu ya Chadema iliwafurusha tar.27/11/2020 na uamuzi huo kutangazwa na Mwenyekiti Mbowe tar.28/11/2020.
Akina Halima wakakata rufaa Baraza kuu ambalo liliketi tar.12 May 2022 na kubariki maamuzi ya Kamati kuu. Akina Halima wakaenda Mahakamani kupinga maamuzi ya Baraza kuu.
Hoja zao zilikua;
1. Hawakupewa haki ya kusikilizwa.
2. Suala lao kushughulikiwa kwa dharura
3. Kuhofia usalama wao
4. Baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu kuwa pia wajumbe wa Baraza kuu na hivyo kuathiri maamuzi (law of impartiality).
Leo Jani Cyprian Mkekha ametoa maamuzi kama ifuatavyo;
1. Kuhusu haki ya kusikilizwa amesema waleta maombi (akina Halima) walipewa haki ya kusikilizwa lakini wakaamua kutokuitumia.
2. Kuhusu suala lao kushughulikiwa kwa dharura, amesema Chadema walikua na haki ya kushughulikia kwa dharura kwa mujibu wa Katiba yao ibara ya 6.5.1(d)
3. Kuhusu kuhofia usalama wao, Jaji Mkekha amesema hoja hiyo haina mashiko maana waleta maombi (akina Halima) hawakuripoti kwenye chombo chochote cha usalama.
4. Kuhusu "Law of Impartiality" hapa ndo pameleta shida. Jaji Mkekha amesema haikua sahihi wajumbe wa Kamati kuu (iliyowafukuza uanachama akina Halima), kushiriki kikao cha Baraza kuu ambacho kilisikiliza rufaa zao. Amebatilisha maamuzi ya Baraza kuu kwa sababu ya kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati kuu.
Kwa kifupi Jaji Mkekha amesema Baraza kuu la Chadema likae tena (bila uwepo wa wajumbe wa Kamati kuu) na lipitie upya rufaa za akina Halima. Kama hujaelewa muite MISSO MISONDO umuulize Malisa amepigaje hapo?
Imeandikwa na MALISA GJ
1 307
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtoza faini ya TZS milioni 3 mwanamuziki Madee pamoja na kumfungia kujishughulisha na kazi za sanaa mpaka hapo atakapolipa faini hiyo kwa kosa la kuchapisha wimbo unaokiuka maudhui ya BASATA.
Aidha, limemtoza faini ya TZS milioni 1 mtozi (producer) Mr. T Touch pamoja na kumwamuru msanii huyo kuutoa wimbo huo kwenye majukwaa ya kidijitali.
Vilevile, BASATA imemtoza faini ya milioni 1 mhusika aliyepandisha wimbo huo kwenye majukwaa ya kidijitali.
1 307
Maisha ni FUMBO.
Huyu mtoto picha zake zilisambaa Mitandaoni wiki moja nyuma akiwa kwenye Mashindano ya Fashion huko Nigeria 🇳🇬 katika Jimbo la Aba akiwa amevalia T-shirt yake nyekundu ya ADIDAS.
Kampuni ya ADIDAS imemuona na kumpa Ubalozi wa bidhaa zake bhana🥳
Wakati wako ukifika hakuna wa kuzuia.
SHARE NA WENGINE
1 307
SITAKI MKE WANGU AWE KWENYE MITANDAO, WATAMTONGOZA NIBAKI MPWEKE; HAMISI
"Mimi nikioa sitaoa mwanamke maarufu ambaye anatumia mitandao ya kijamii na nikikuta anatumia nitamkataza kwasababu nikimposti watu wakimuona watamtongoza mwisho tunaachana"
"Mke wangu mtamuona siku ya harusi tu hekaheka za harusi zikiisha hamtamuona tena, sitaki kabisa mke wangu awe kwenye mitandao, ila mimi nitaendelea kutumia mitandao kwasababu atakuwa amenikuta natumia kwa muda mrefu"- amesema Hamisi Actor
1 307
Kutoka Kwa Diva The Bawse
Nyie Director Nisher amefariki dunia😭 Chanzo Cha Kifo Chake Ni Majeraha baada Ya kujikata na panga kwa nyuma akalazwa hospital hajawah kutoka icu Mpaka Kifo Kilipomkuta
inasemekana walikuwa wamezinguana na mke wake ndio akafanya hivyo (kujipiga kisu mithili ya Panga kilicholeta majeraha yaliomlaza ICU Mpaka uhai wake kukatika )
inasemekana mtoto wake alikuwa anaumwa yule mtoto akaja kufa tangia hapo akawa hayuko sawa ndio yaliotokea yakatokea Maskini Nisher. Nafatilia zaid ntawaandikia , thanks nisher for a good contribution in our Music Industry!. Mungu akulaze Mahala Pema Amin.
