E-PLUS MEDIA
Open in Telegram
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
1 307
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema nchi yake itawajibika kwa masuala yote ya usalama kwenye eneo la Gaza baada ya vita kumalizika, kauli ambayo huenda ikafanya mzozo wake na kundi la Hamas kuchukua muda.
Netanyahu, amesema wajibu huo wa usalama utachukuliwa kwa muda usiojulikana hadi pale kundi la Hamas litakapomalizwa.
1 307
Idadi ya watu waliouawa katika mapigano yanayoendelea katika ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia takriban watu 10,022, wakiwemo watoto wasiopungua 4,104, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya katika eneo la Palestina linaloendeshwa na Hamas.
#rfikiswahili
#UN
#Gaza
1 307
#MBONA HAWAELEWEKI HAWA
"Leo nimeenda katika ripoti ya CAG na kuanza kusoma, Haki ya Mungu kuna vitu vinatia kichefu chefu, angekuwa Hayati Magufuli hawa watu (waliotajwa kwenye ripoti ya CAG) wasingekuwepo, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Magufuli angeshawachomoa muda mrefu sana" Ezekiel Wenje, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Viktoria
1 307
NILITUMIA MILIONI 50 KUCHOMA
SINDANO 10 HIYO SINDANO TU
BADO KUSAFISHA FIGO - PROF JAY
Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva Profesa Jay amefanya mahojiano na Clouds FM na amefunguka haya
"Kuna sindano nilikuwa nachona kwa siku Mil. Tano asubuhi na Jioni. Ile sindano ndio iliyoniamsha. Nilikuwa nachoma mara Tano kwa wiki. Kwa wiki Mil. 25. Nilichoma kwa wiki moja kila siku mara Mbili. Nilichoma sindano 10 ni mil 50. Hiyo ni sindano tu, bado kusafisha figo, (dialysis) ukianzia pale Muhimbili ni Laki na Themanini kwa mgonjwa anayetoka nje ni Laki Tatu na Nusu. Hiyo ni mara moja na unatakiwa ufanyiwe hadi mara Nne kwa wiki kutokana na tatizo lako"
"Kwa kuanzia nimeanza na @professorjayfoundation kwa sababu nimeona watu wanapata tabu sana na hizi hela ni nyingi sana. Na wote hawawezi kufikiwa na Rais na watu wanataabika sana. Kwangu ilikuwa kawaida lakini kuna watu figo zilikuwa zimefeli. Nilikuwa nachomwa hivyo sindano lakini figo zangu zilikuwa hazijafeli na ni kwamba figo moja likuwa na na mchanga na moja ilikuwa inasuasua ilikuwa na sumu nyingi" @professorjaytz, Chairman of @professorjayfoundation
"Ingawa magonjwa ni mawaidha watu wanasema, lakini watu wanakufa sana, kwa mimi niliyekaa ICU siku 127, unajua kule ICU watu hali zao mbaya sana, kujikuta ICU na una- survive siku 127 sio mchezo" @professorjaytz
"Watu wanaumwa sana, na wanakufa mno, ndio maana nikasema foundation yangu nianze na suala la figo" @professorjaytz
"Kutokana na nilipopitia kwa sasa nipo vizuri kila siku naimarika namshukuru sana Mhe Rais @samia_suluhu_hassan yeye amenipigania kwenda India nilitamanii kukutana naye, kitendo alichokifanya alikifanya kama Mama. Kwahiyo nina sababu ya kushukuru na kumpa maua yake" @professorjaytz
1 307
"Kabla sijaokoka ndio nilichora hizi tattoo na nimetoka mbali sana, nimepitia THT (Tanzania House of Talent), nimepita Mchozi Band nimefanya kazi na Lady Jaydee, kwahiyo hizi tattoo wanazoniona ni kama alama tu kama Yesu alivyobaki kuwa na alama, kwangu ni kama ushuhuda na kila nikiziangalia nakumbuka mahali Mungu aliponitoa"
"Nilipitia kwenye mambo ya Madawa ya kulevya ambayo yalinipelekea kufikia sehemu mbaya sana na naweza kusema kwamba hiyo ndio ilikuwa njia yangu ya kunirudisha kwa Mungu, watumishi wa Mungu wengi ni wagumu kutoa sapoti, kwa mfano mimi siwezi kualikwa kwenye badhi ya makanisa kwasababu ya hizi tattoo nilizo nazo na hata sapoti yao kwangu ni ndogo"-Bella Kombo, Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania.
1 307
Baada ya Diamond na Harmonize kwa nyakati tofauti tofauti mwezi huu kueleza kuhusu kutapeliwa, sasa ni zamu ya aliyekuwa mpiga picha wa msanii Diamond Platnumz, @lukambaofficial amabaye kupitia Insta-story yake ameeleza kuhusu kutapeliwa kiasi cha Shilingi milioni 200.
Nini maoni yako kuhusiana na hili?
Au ni Wasanii wameamua kutembea tu na upepo huu kwa mwezi Novemba.
1 307
#HABARI KIONGOZI wa Kundi la Hamas, Mousa Abu Marzouk amesema kuwa ilikuwa ni vigumu kuachiliwa mateka wanaowashikiria wakati Israel ikiishambulia Gaza kwa mabomu.
Kiongozi huyo wa Hamas ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalumu na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), huku akiahidi kwamba kundi lake litawaachia mateka hao.
"Tutawaachilia, lakini tunahitaji kusitisha mapigano," amesema kiongozi huyo wa juu wa Hamas.
Wakati takribani watu 249 wanashikiliwa kama mateka na wananmgambo wa Hamas, Wizara ya afya inayoongozwa na kundi hilo Imesema kuwa watu 10,000 wameuawa tangu Israel ianze operesheni mwezi uliopita.
1 307
#HABARI KUFUATIA taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, imesema kuwa mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Israel huko Ukanda wa Gaza yamesababisha athari kubwa kwa watoto ambapo kila baada ya dakika 10 mtoto mmoja anauawa.
Guterres amesema hadi kufikia sasa takriban watoa Huduma 89 wa UN wamepoteza maisha wakati wa#NipasheHabari oezi la kutoa misaada kwa waathirika wa mapigano kati ya Israel na Hamas.
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Euro-Med Monitor, limesema karibu watoto 52,500 wako hatarini kukumbwa na njaa, magonjwa na vifo na wajawazito 55,000 hawana uhakika wa Usalama wakiwemo 5,500 wanaokaribia kujifungua mwezi Novemba mwaka huu.
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheHabari
1 307
MISIBA 9 ILIYOISIMAMISHA TANZANIA🇹🇿
Tanzania kama taifa tumepata misiba mingi sana ya viongozi wa serikali, dini, siasa, wasanii, wanahabari na watu wa kawaida lakini miongoni mwao kuna vifo ambavyo kwa namna yake vilipotokea Tanzania ilizizima na kuacha majonzi makubwa sana baadhi yao walikufa na watu pia (waombolezaji).
1) Edward Moringe Sokoine - 12 April 1984.
2) Mwl Julius Kambarage Nyerere - 14 October 1999.
3) Dr Omar Ally Juma - 4 July 2001.
4) Amina Chifupa - 26 June 2007.
5) Steven Charles Kanumba - 7 April 2012.
6) Rugemalilah Mutahaba - 26 February 2019.
7) Reginald Abraham Mengi - 2 May 2019.
8) Benjamin William Mkapa - 23 July 2020.
9) Dr John Pombe Joseph Magufuli - 17 March 2021.
Nafsi zao ziendelee kupumnzika mahala pema peponi🙏🕯️🕯️🕯️🤲
Mdau kifo cha nani hapo kilikugusa zaidi ikiwa leo tunaadhimisha kifo cha baba wa taifa mwalimu Nyerere?
1 307
PICHANI NI WASANII MARIOO NA NANDY
KABLA HAWAJAWA MASTAA.
ILA KUMBE WATU WANATOKA MBALI SANA.
1 307
RUBBY AWAPA POLE WAFUNGWA WHOZU, BILLNAS NA MBOSSO.
"Sema lile futa plus mkongo. Wote tunakosea na hata kwa funzo moja halitoshi kumfanya mtu kuwa mkamilifu tukiwa kama binadamu bado tutakuwa na mapungufu mengine kwa kujua na mengine kwa kutokujua. Tunatakiwa kurekebishana ila siyo kunyimana Rizki, wote tunatafuta kwa ajili ya familia zetu, leo Mbosso, Billnas na Whozu kesho huenda ni mimi na wewe lakini siyo kutiana umasikini kunyimana Rizki"
"Raiti kama Wazazi wetu wangekuwa na haki ya kuua watoto kisa makosa sijui kama mimi na wewe tungekuwa hapa. Teach them but don't destroy them, poleni kaka zangu ila pia tusiache kujifunza na kujua nini watu tunaowaimbia wanataka"
"Ila na wewe kaka yangu Mbosso tumefanya kazi yako vizuri ila kazi yangu umeshindwa kusapoti URIDHIKE, ona sasa umeyatimba, sasa mi nataka nitoe video ya uridhike ila sielewi my wangu"- Rubby ameandika.
1 307
SAKATA LA KUWAVUA UKUU WA SHULE WALIMU WAWILI KISA HONEY YA ZUCHU WANANCHI WAMVAA WAZIRI GWAJIMA, TULIA APONGEZWA.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya video moja kuvuja ikiwaonyesha watoto wakicheza wimbo wa msanii Zuchu "Honey" huku wakinengua viuno kwenye mjumuiko na walimu wao. Kitendo hicho kilionekana si kitendo cha kiungwana kwa watoto kwasababu wimbo huo haufai kusikilizwa na watoto kutokana na ujumbe wake, ambapo waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akishirikiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda waliamua kuwavua Ukuu wa Shule walimu wawili ambao wanafunzi wao ndio waliungana na kuchezeshwa Honey.
Mjadala huo ulifika Bungeni na kujadiliwa na Wabunge, ambapo hadi kufikia siku ya leo Novemba 6, 2023, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ametoa maelekezo walimu hao warudishwe mara moja kwenye vitengo vyao kwasababu maamuzi ya kuwashusha vyeo yalifanyika bila uchunguzi, kwa madai kwamba wakati mziki unapigwa shuleni hapo walimu hao hawakuwepo shuleni.
Baada ya uamuzi huo Watanzania wameenda kwenye ukurasa wa Instagram wa Dorothy Gwajima na kushambulia wakidai awali hakutenda haki alikurupuka, huku wengi wao wakimpongeza Dkt. Tulia kwa uamuzi huo uliotukuka na wenye utu.
1 307
ZIWA LANGU LIMELALA NA SINA MPANGO WA SURGERY; WEMA SEPETU
"Kwa nilivyopungua mlikuwa mnategemea nitakuwa na ziwa saa sita? Nyie kumbe wehu eeh🤣🤣🤣 ndio yamelala haswaa!! ndio maumbile kwani kuna tatizo gani?! na sina mpango wa surgery"- Wema Sepetu
1 307
ROSE MUHANDO AUBARIKI WIMBO MPYA WA PROFESSOR JAY.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rose Muhando ameposti wimbo mpya wa Professor Jay kisha kuandika
"Mungu ni Daktari wa Madaktari, ni Mungu wa Miungu na ni kamanda wa vitu, anatupigania daima watoto wake, pole sana kaka yangu Professor Jay, uliyoyapitia ni ushuhuda wa kukujenga zaidi ki imani, Mungu wetu hashindwi na jambo"
"Nakuomba wewe Mtanzania, Mkenya au kutoka popote pale pita kwenye platforms zote kusikiliza huu wimbo (Siku 462) kuna sehemu utakutoa na kukupa tumaini jipya"- Rose Muhando
