E-PLUS MEDIA
Open in Telegram
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
1 307
Pichani ni Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Thailand Nualphan Lampham Kwenye Picha ya Pamoja na Bintiye
Rais Huyo Ameingia Kwenye Vitabu kuwa Rais wa Soka Mwanamke Duniani
Lini Bongo Tutampata Rais wa (TFF) Mwanamke? Au Karia Akimaliza Muda wake Tumchague?
1 307
Dubai Mwaka 2005 na Ilivyo Sasa 2024
Unadhani Kipi kimepelekea Hawa jamaa kuwa na Maendeleo ya Haraka ndani ya Miaka Michache tu ??
1 307
Anaitwa Hamida, ni Mtoto wa pili wa Msemaji Mstaafu wa Yanga #Bugatti Haji Manara 📸
1 307
Tumeona kazi kubwa aliyoifanya Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa (CCM) Paul Makonda kwenye Ziara zake na Tumeona akirudisha Imani za Watu kwenye Chama Cha Mapinduzi na Serikali.
Muda Mchache tu Baada ya kuteuliwa Katika Nafasi hiyo Miezi 6 iliyopita Rais anamtoa Katika Nafasi hiyo na Kumpeleka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Unadhani Kipi kimepelekea Rais Kumpeleka makonda Arusha?
1 307
NIWAHAKIKISHIE NCHI IPO SALAMA
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda amewahakikishia Watanzania kuwa nchi iko salama na kuwataka kuendelea kudumisha amani iliyopo.
Jenerali Mkunda ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akitoa salamu katika Ibada ya Pasaka Kitaifa ambayo imefanyika katika Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Central Tanganyika, Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.
Amesema yapo baadhi ya mataifa watu wake wanashindwa kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kutokana na kukosekana kwa amani na hivyo akisisitiza umuhimu wa kulinda amani kwani "maendeleo yoyote ya nchi msingi wake ni amani."
Follow ukurasa wetu wa Instagram 👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
“Nahisi ningebaki Bongo, ningeweza kufa kwa stress maana mtu anajifanya amesahau hata nyimbo zako wakati nchi ya jirani wanazipenda na hata kukupa shoo.Wabongo wengi kazi yao kubwa ni uzushi tu na si kitu kingine chochote,”
“Haya mafanikio nimeyapata kutokana na kazi yangu ya muziki, siyo kitu kingine chochote.
“Ndiyo maana natamani sana kuendelea kuishi hapa Kenya kwa sababu ndipo ninapopata heshima na kazi yangu ya muziki niliyoifanya kwa zaidi ya miaka 20 naona inaniweka pazuri,” - Mr Nice, Msanii wa muda mrefu kutoka Nchini Tanzania 🇹🇿 via GP.
Mkongwe huyo ameongeza kuwa amepata mafanikio makubwa akiwa Nchini Kenya 🇰🇪 kiasi kwamba ameanzisha mradi wake wa maji ya kunywa uitwao Nice water.
Toa maoni yako
1 307
Wananchi wa mtaa wa mkoani kata ya Kalangalala halmshauri ya mji wa Geita mkoani Geita wameshtushwa na tukio la kufariki kwa kijana Paschal Simon anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 20-26 wakati akichimba kaburi eneo la makaburi ya Lukirini
Kaburi hilo lilikuwa kwajili ya kumhifadhi bi. Ezilabeth Kalamu (80) ambaye amefariki kwenye mtaa huo
Baadhi ya wananchi wa mtaa huo wamesema wakati wakiendelea na zoezi la kuchimba kaburi , kijana huyo ameomba jembe ili asaidiane na wenzake na baada ya kutoka kwenye shimo hilo la kaburi amekuwa kama ameshikwa na kifafa kisha akaanguka
Baada ya kijana huyo kuanguka wenzake wamembeba na kumweka pembeni wakati zoezi la kuchimba kaburi likiendelea ndiyo wamegundua kuwa mwenzao tayari amepoteza maisha
Afisa mtendaji wa mtaa wa mkoani bw. Elisha Alex amesema baada ya kufika kwenye eneo la tukio amekuta mwili wa kijana huyo ukiwa umelazwa taratibu za kumepeka hospitali kwaajili ya uchunguzi zikaanza
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Geita Dkt. Thomas Mafulu amekiri kuupokea mwili wa kijana huyo hospitali hapo
Dkt. Mafulu amesema kutokana na kijana huyo kutokuwa na ndugu wanaomfahamu hisitori ya afya yake , huenda chanzo cha kifo chake kikawaa kimetokana na Shambulio la moyo au kifafa na hiyo huweza kutokea kutokana na mgonjwa kukosa huduma ya haraka kutoka kwa wataalamu wa afya
Na Mwandishi wetu Samwel Masunzu kutoka Mkoani Geita.
Toa maoni yako
1 307
WATU 12 WAKAMATWA KWA KULA MCHANA- ZANZIBAR
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu kumi na mbili kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao wanaifanya kuwa idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali kufikia sitini na mbili
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonyesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar kula hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na mbili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani
Aidha ameyataja makosa mengine ni pamoja na unyang’nyi, Madawa ya kulevya na makosa mengine ambapo watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi na wengine tayari wameshahukumiwa Mahakamani
1 307
"Nawashangaa sana Wanaume wachafu wasiojua kuoga Sifa ya mwanaume ni usafi mwanaume unatakiwa kuwa Romantic muda wote Mimi binafsi Sina ushikaji na wanaume wachafu."Mwanamuziki na Mtayarishaji wa Muziki, Bob junior
Follow Ukurasa Wetu wa Instagram 👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
Leo mwigizaji wa filamu Tanzania, @aqwelinaa_mwali na timu yake alienda kutoa misaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Mugabe iliyopo Sinza jijini Dar es salaam
Misaada iliyotolewa ni pamoja na madaftari, kalamu, sabuni za kufulia na kuogea, biskuti, pipi, juice, taulo za kike na n.k
Aidha, @aqwelinaa_mwali ambaye ameigiza kazi mbalimbali zikiwemo series za Haikufuma, Mwali na Juba amewashukuru wote waliojumuika nae kutoa misaada pia kuwashukuru walimu wa shule ya msingi Mugabe kwa kutoa ushirikiano mzuri na hii sio mara ya kwanza mwigizaji huyo kwenda kutoa misaada katika shule hiyo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
1 307
Baada Ya msanii Abby chams kusema kuwa yeye Amfahamu Tid na kumuita kibabu Cha kipara sasa Tid kaja juu.
NANUKUU.
Unajua saizi vitoto vidogo vina mashauzi me nashindwa kuelewa Kanasema Hakanijui me najulikana na ma Rais wote wa Tanzania Kenya Uganda wananifahamu Afu katoto kadogo kanakuja kusema hakajui kupika ugali saa nawaza kama kupika tu ugali hajui je chupi yake kataweza kufua kweli au Katavaa Inanukaa.
1 307
MICHAEL JACKSON ALITAKA KUISHI MIAKA 150......
Kama ulikuwa hujui basi ni hivi aliyekuwa muimbaji na mfalme wa pop duniani Michael Jackson alipanga mipango ili aweze kuishi miaka 150 hapa duniani
Baadhi ya mipango hiyo ni
- Aliajiri madaktari 12 ambao walikuwa wanampima kila siku kuanzia nywele hadi kucha za vidole vya miguu
- Chakula chake kila siku kilikuwa kinaenda fanyiwa majaribio na kupimwa kabla ya kula
- Aliajiri watu 15 ambao walikuwa wanampangia ratiba ya mazoezi na kumsimamia namna bora ya kufanya mazoezi
- Kitanda alichokuwa analalia kilikuwa na teknolojia ya kuthibiti oxygen
- Waliandaliwa watu maalum kwa ajili ya kumtolea vitu ndani ya miili yao kama vikiitajika kwa mfano figo .....na watu hao walikuwa wakilindwa na kuhifadhiwa na yeye
- Hizo zote zilikuwa jitihada na mipango ya kuishi miaka 150
-Mwaka 2009 tar 25 mwezi wa 6 ...moyo wake ulisimama ghafla kufanya kazi .....madaktari wake 12 walishindwa kumtibu
-Wakaongezwa madaktari wengine mabinhwa kutoka California na Los Angels lakini pia walishindwa
-Mtu ambaye kila hatua aliyokuwa anaipiga iliongozana na jopo la madaktari bingwa 12 Kwa miaka 25 mfululizo .....lengo lake ni kutaka kuishi miaka 150 lakini alishindwa licha ya jitihada zake
-Tar hiyi 25 mwezi wa 6 mwaka 2009 Michael Jackson alifariki dunia akiwa na miaka 50 TU
TUNAISHI KWA MIAKA TULIYOKADIRIWA NA MUNGU....HATA TUKIFANYA VIPI MUNGU AKIPENDA KUMCHUKUA MJA WAKE HAKUNA KITAKACHOSAIDIA.....
- Tafadhali mtag rafiki yako unaempenda
-Tafadhali share ili wengine wajifunze
Credit BWANA FACT
1 307
SABABU 5 KWANINI TUNAMPENDA MONALISA
Jina lake halisi anaitwa Yvonne Cherrie, alizaliwa 19 Agosti 1981, ni mshindi wa tuzo ya ZIFF kama Mwigizaji bora wa Filamu na mifululizo ya vipindi vya televisheni kutoka nchini Tanzania. Pia ni mtunzi wa muswada, Mwandishi, Mtayarishaji na Mwongozaji wa Filamu, anafahamika zaidi kwa jina lake la uhusika alioupata kama Monalisa.
Monalisa alianza kuonyesha mapenzi ya kuigiza tangu akiwa mtoto mdogo, alianza kuigiza akiwa na miaka 8 tu shuleni kwao na baadae kanisani. Mwaka 2001 mwezi wa nane aliolewa na Mtayarishaji/ Mwongozaji wa Filamu kutoka nchini Kenya George Otieno Okumu (Tyson) na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kwanza aitwaye Sonia mwaka 2002. Mwaka 2005 walitengana na mwaka 2012 akapewa talaka rasmi na Mahakama.
Mwaka 2007 alibahatika tena kupata mtoto mwingine wa kiume aitwaye Sean Abdulwahid Jr kutoka kwa mwanaume mwingine aitwaye Abdulkarim Abdulwahid. Monalisa amekuwa kipenzi cha watu wengi kutokana na karma yake aliyojaaliwa na Mungu, hizi hapa ni sababu chache kati ya nyingi kwanini watu wanampenda sana.
1. Ni mlezi mzuri wa watoto; ukilinganisha na mastaa wengine maarufu wenye watoto, Monalisa amekuwa wa tofauti kwenye upande wa malezi, haruhusu watoto wake wazagae mitandaoni mpaka watakapojitambua wenyewe, amewajengea hofu ya Mungu kwani mara nyingi amekuwa akionekana nao kanisani kwenye nyumba za ibada, watu wengi wamekuwa wakifurahishwa na mwenendo wa malezi kwa watoto wake.
2. Ni msiri haweki mambo yake wazi; kila kukicha tumekuwa tukishuhudia tambo za mastaa wetu wakijigamba kwa kumiliki magari ya gharama, kupanga nyumba zenye kodi kubwa, kujenga majumba makubwa, lakini kwa Monalisa ni tofauti sana, asilimia kubwa ya watu wa mtandaoni hawana taarifa zake, hawajui anaishi wapi, anamiliki nini wala anatembelea gari gani japokuwa sio mnyonge kiasi hicho pesa anayo.
3. Amekataa kujichubua, Miaka ya nyuma wakati bongo movie ndio inachangamka asilimia kubwa walikuwa wanachukuliwa wadada weupe, ambao wataonekana kwenye Tv vizuri, hicho ndicho kipindi ambacho wanawake walijichubua kwelikweli, ilikuwa fashion ya kipindi hicho, kipindi hicho kama hauna kopo la kipodozi ndani ulikuwa unaonekana wa kuja mjini, lakini yeye aliamini katika ngozi yake na mpaka sasa hajaigusa kwa kipodozi chochote na sura yake inawavutia watu wengi hakika.
4. Ni mfano mzuri wa kuigwa, ni nani asiyetaka kufuata nyayo za Monalisa? bila shaka hakuna kwasababu hana baya, mambo yake yamenyooka na ya kiheshima zaidi, kwenye account yake ya Instagram ukitembelea utagundua huyu ni mtu wa aina gani, heshima yake inajieleza yenyewe bila kujitangaza, ni wanawake wengi wanatamani kuishi maisha yenye utulivu, heshima, malezi mazuri bila kuwakwaza wengine.
5. Sio mtu wa kiki. Ni kawaida kwa mastaa ili uendelee kuvuma lazima utumie kiki, leo upo kwenye mahusiano na huyu kesho na yule, leo upo Dubai lazima uposti upo na mbaba anakulea huko kumbe ni mhudumu wa hotel, ndio maisha ya mastaa wetu, lakini kwa Monalisa imekuwa tofauti, amekuwa sio mtu wa kiki lakini bado anawika na jina lake linajumuishwa kwenye majina machache ya waigizaji wa heshima Tanzania.
Naam!! huyu ndiye Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa mama wa watoto watatu, Mwenyezi Mungu ampe maisha marefu, amjazie baraka, amuongoze kwenye misingi iliyosafi nyota yake izidi kung'aaa. Aendelee kupendwa zaidi, neema na baraka zimfae Amin🙏.
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
TAARIFA KUTOKA TBC.
Shirika la Utangazaji Tanzania TBC litaonyesha Michezo ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Simba SC Dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Kesho Ijumaa na Mchezo wa Yanga SC Dhidi ya Mamelodi Sundown siku ya Jumamosi
Michezo yote Hiyo Itaruka Mubashara Kupitia TBC1 Bure kwa Muonekano wa Picha ang'avu yaani FULL HD
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
