E-PLUS MEDIA
Open in Telegram
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
1 307
8️⃣. Sabato ilibatilishwa: Wakolosai 2:16, Wagalatia 4:10, Warumi 14:5
✍️Hapana, Sabato haijabatilishwa.
UFAFANUZI👇
📖Biblia ikisomwa kwa makini itafunua kwamba hizi ni sabato zinazohusiana na sikukuu. Kufuatana na Mambo ya Walawi sura ya 23: angalia hasa fungu la 37, 38 kwamba zilitolewa kama nyongeza na ndio maana Paulo alizipinga. Tofauti na Sabato ya siku ya Saba, hiyo ilikuwapo kabla ya dhambi (Mwa.2:1-3).
📖Mungu akaiweka kwenye sheria yake ya maadili yaani amri kumi (Kut.20:8-11).,
📖Ni alama ya Mungu kwa aliowaumba na kuwatakasa (Kut.31:17, 13;
📖Kutoka 31:17, 13 Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika. 13 Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.
📖Ezekieli 20:20,12 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 12 Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.
📖Yesu alipokuwako duniani aliiheshimu. (Luk.4:16, Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
📖Mathayo 24:20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
📖Waebrania 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.
📖itakuwa furaha yake watakatifu kuabudu mbele zake siku za sabato, kwenye mbingu mpya na nchi mpya. (Isa.66:22, 23).
9️⃣. Tuko chini ya neema hivyo hatulazimiki kutii sheria Rum. 6:14 – 15,
👇UFAFANUZI👇
📖Paulo anasema kwamba kwa kuwa chini ya neema, hatubatilishi sheria
Warumi 3: 31 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.
📖Warumi 3:20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
🔟. Tukiwa ndani ya Kristo, pumziko linatosha hivyo hatuihitaji Sabato.
📖Ni Mungu ndiye atoaye raha hata kwa kupitia sabato yake. “Iko raha ya sabato kwa watu wa Mungu” Ebr. 4:1-5, 9, 10
Jinsi wokovu ulivyo muhimu kwa mwanadamu, (Yoh. 3;16) ndivyo sabato ilivyo muhimu kwa wanadamu. (Mk.2:27)
1️⃣1️⃣. Watu wengi hawawezi kuwa wamekosea?
📖Wingi si hoja, bali ubora wa tabia ndio Mungu anaoutaka. (Mt. 7: 13, 14).
Mathayo 7: 13, 14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
📖Izingatiwe pia kwamba Biblia ilionya kuwa watazuka watu wenye kufundisha kwa kufuata tamaa zao.
2 Timotheo 4:3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
✍️Kwa hiyo hata kwa wingi wao, wanadamu wanaweza kukosea, hivyo tusifuate wingi bali tufuate Maandiko.
1 307
SABABU KUMI NA MOJA (11) ZA UWONGO ZINAZOTUMIWA NA WANADAMU KUHAFIFISHA SABATO YA MUNGU
1️⃣ Je, tuheshimu Jumapili kwa kuwa Yesu alifufuka siku hiyo?
✍️Hapana. Ni kweli baadhi ya wakristo wa awali kwenye miaka ya 90 hadi 100 BK walichagua kupumzika Jumapili kuepuka mateso makali yaliyowatofautisha na watu wengine. Hata hivyo Yesu anadai Je, tukatae amri ya Mungu kwa kuheshimu mapokeo?
📖 Wanafunzi waliokutana Jumapili hawakukutana kwa ajili ya ibada bali wengi hawakuamini kama Yesu amefufuka (Mk. 16:12-14)
📖Zaidi ya yote, mkutano wao wa Jumapili ulikuwa kwa hofu ya Wayahudi tu na sio ibada.
Yohana 20:19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
📖Biblia imetuamuru kuabudu siku ya Sabato na sio siku ya kwanza ya juma ambayo yesu alifufuka. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Kutoka 20:8
2️⃣. Je, si kalenda imebadilishwa?
✍️Ni kweli kalenda ilibadilishwa mwaka 1582 lakini haikuingilia mzunguko wa juma lenye siku saba. Kilichobadilishwa na Papa Gregory XIII kilikuwa kusahihisha kosa kwenye kalenda ya Julian (46 BC) iliyosema mwaka una siku 365¼. Kwa uhalisia kuna dakika 11 pungufu katika hesabu hiyo. Hadi mwaka 1582, kulikuwa na upungufu wa siku 10. Hivyo, mwaka 1582 kulikucha Alhamisi 4 Oktoba 1582 na kesho yake kukawa Ijumaa tarehe 15 Oktoba 1582.
📖Tunapoabudu siku ya sabato tunafanya kama Yesu alivyoabudu. (Luka 4:16.)
3️⃣. Ni vigumu kutambua ni siku ipi ndiyo ya saba katika wiki.
Ziko sababu mbili kuhusiana na jambo hili. Na siku inatambulika tu.
📖Kwanza ni siku aliyokufa Yesu Luka 23:52-56
Luka 23:52-56 mtu huyo alikwenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu. 53 Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake. 54 Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia. 55 Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa. 56 Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.
📖Yesu alikufa Ijumaa na alifufuka Jumapili. (Luka 24:1–2).
✍️ Pili ni majina ya siku ya Jumamosi katika lugha mbali mbali zaidi ya 100 bado ni sabato. Italia, siku ya Jumamosi ni Sabbato, Hispania ni Sabado, Ureno ni Sabbado, Urusi ni Subbota, Poland ni Sobota na Ugiriki ni Sabbatho. Maana ya majina yote hayo ni kwamba Jumamosi ndiyo sabato.
✍️Ikiwepo hoja ya tatu basi ni Kamusi. Ukisoma Kamusi, neno sabato, ni siku ya saba ya juma ambayo ni Jumamosi.
4️⃣. Je naweza kutunza siku yoyote katika juma na kuiita Sabato?
📖Hapana. Biblia imeeeleza kuwa Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Kutoka 20:8.
Biblia haijasema siku yoyote tu japo Ibada za familia, maombi ya faragha ni kila siku
📖M. Walawi 10:1-2
📖Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
5️⃣. Tutaitakasa siku ya Bwana, achana na Sabato
📖Hapana, siku ya Bwana ni Sabato na Yesu ndiye Bwana wa sabato
Ufunuo wa Yohana 1:10, Mk. 2:28., Kut.20:8
6️⃣ Sabato ilifanyika kwa ajili ya Wayahudi peke yao
📖Hapana, sabato ilifanyika kwa ajili ya wanadamu wote
Lakini sabato ni ya Bwana Kut. 20:10, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu.
Marko 2:27 Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.
📖Hivyo, kila aliye mwanadamu, sabato ni kwa ajili yake. Luka ambaye hakuwa myahudi alitakasa sabato (Mdo. 16:13.)
7️⃣. Amri 10 zilibatilishwa ikiwemo Sabato
✍️Hapana, amri za Mungu hazijabatilishwa.
📖watu wanaolisema jambo hili hawajaungwa mkono na Maandiko Matakatifu. Paulo anasema, kama isingekuwapo sheria, pasingekuwa na dhambi wala kusingekuwepo haja ya mwokozi. Rum. 4:15.
📖Sheria ya Mungu yote, pamoja na sabato ni ya haki, takatifu na njema Rum. 7:12.,
Sheria ya Mungu huwakilisha tabia ya Mungu
1 307
Kizaazaa kimeibuka huko!
Unakumbuka swala la shirikisho la soka la Ufaransa lilivyolalamika kwamba timu ya taifa ya Argentina imewasema vibaya wachezaji wake haswa jambo hilo likimkabili Enzo Fernandez? ambaye ndiye alikuwa Insta Live wakati nyimbo hiyo inaimbwa?
Sasa kuna taarifa mpya imetoka ambapo sasa kundi kubwa la waumini wa dini ya Kikristo wameijia juu nchi ya Ufaransa kwa kile kinachodaiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya Olimpiki inayoendelea nchini Ufaransa walimdhihaki Yesu Kristo kwa kutengeneza kundi la watu waliojifananisha na picha maarufu inayotambulika kwamba ni Yesu na wanafunzi wake wakila mkate wao wa mwisho kabla ya Yesu kusulubiwa ambapo igizo hilo walilifanya kwenye sherehe ya ufunguzi na limevuta hisia za watu wengi.
Kundi hilo la waumini wa imani ya Kikristo wamekosoa vikali tukio hilo wakidai ni dhihaka kubwa imefanywa dhidi ya Yesu Kristo na taifa la Ufaransa ambalo ndiyo muandaaji wa michezo hiyo ya Olimpiki wanatakiwa kuomba radhi.
#d1905_updates
1 307
ALIYEHUKUMIWA KUCHOMA PICHA YA RAIS ATEKWA NA KUPELEKWA KUSIKOJULIKANA!
Ndugu Watanzania!
Kuna taarifa Charles Chaula aliyehukumiwa kwa kuchoma picha [aliyoichora] ya Rais lakini aliachiwa kwa kuchangiwa faini na wananchi alitekwa jana katika Kijiji chao cha Ntokela cha Kata ya Ndato Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya.
Kwamba waliomteka walifika na gari jeusi na kumpakia kwa nguvu na kutoweka naye. Baba yake anaendelea kuhangaika kumtafuta bila ya mafanikio. Kwa mazingira yalivyo na historia ya Charles Chaula ya matukio ya hivi karibuni, sisi tunashawishika kuwa Chaula amechukuliwa na mamlaka kwa sababu maalum.
Kwa hiyo sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa waliomchukua Chaula kueleza ni wapi au mahali gani alipo na pia kueleza sababu za kumteka.
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mhe. Jaji Mwaimu amewanyoshea kidole Jeshi la Polisi kuwa watu wanakamatwa hawapelekwi moja kwa moja vituoni hupelekwa mahali kwingine kuteswa.
Kwa hiyo, kama Chaula atadhurika kwa namna ye yote ile au kama atapoteza maisha, basi ni wazi kuwa mamlaka zilimkomata hapo awali na kumfungulia mashtaka ndizo zitakalaumiwa kuhusika na hayo. Vinginevyo, tunatoa wito wa kumuachia au kumpeleka kesho mahakamani.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 2 Agosti 2024; saa 1:28 usiku
1 307
+9
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
+9
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
1 307
+7
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
UFAFANUZI KUHUSU (UNIT) UMEME
Wangi wamekuwa wanajuliza (UNIT) inakuwaje mpaka naambiwa nimetumia unit 10 basi leo nikupe maelezo kidogo ili ufumbuke macho pengine itakusaidia kujua mwenyewe hata bila kifaa kujua makadirio ya unit kwenye nyumba yako
Kwanza kabisa UNIT linatokana na kWh yaani Watt-hour yaani kwa kifupi ni tunapima kwa mda kiasi cha power ya umeme inyoflow yaani kupita kweye saketi
Hivyo basi UNIT1 ni sawa na watt 1000 kwa lisaa yaani power ya watt 1000 imeflow kwa lisaa limoja hivyo ukisikia UNIT 10 ni sawa na watt 10000 zimeflow kwa lisaa
Naukpa mfano kidogo ili tuelewane Pasi ina watt 1000 hivyo ukiiwasha kwa lisaa itakuwa imetumia unit 1 kama ina watt 2000 basi kwa lisaa itatumia unit 2
Mfano mwingine unataa za watt 20 tano ambazo jumla yake tuna pata watt 100 hivyo mpaka utumie UNIT 1 hizo taa basi zitapaswa kuwaka masaa 10
Kwa wenye motor au mashine za maji Mechanical horsepower Hp 1 ni sawa na watt 746
Jinsi sasa ya kupata makadilio ya matumizi yako yaani unaweza ukawa unatumia unit ngapi
Angalia vifaa vyako vinatumia watt ngapi yaani kama ni taa tv pasi friji na kadharika jumlisha kila kifaa watt zake kisha fanya mahesabu kwa kanuni ya kWh mfano taa = watt 20 Friji watt = watt 2000 pasi =watt 1000 tv=watt 80 labda redio watt 70 jumla hapo utapata jumla 3070 watt zigawe kwa 1000 ndani ya lisaa yaani maanayake ni kwamba ndani ya lisaa utakuwa umetumia UNIT 3.07
Bila shaka tumeelewana kwa maelezo sahii
LIKE kisha SHARE
1 307
+3
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
+9
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
