E-PLUS MEDIA
Open in Telegram
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
1 307
INAWEZEKANAJE BINTI ALIYEBAKWA NA KULAWITIWA NA WANAUME WATANO AKAWA ‘SALAMA SALIMINI’ !!?
Kaka yangu Misime, unajua vile nakuheshimu, lakini hii taarifa yako hujamtendea haki yule binti wala watanzania. Kwanza mtu aliyebakwa na kulawitiwa na watu watano hawezi kuwa salama salmini. Neno "salama salmini" hapa limetumika kimakosa. Halikupaswa kuwepo.
Pili; umesema wanaosambaza taarifa za uzushi wamekosa utu na ubinadamu. Hivi kweli wasambaza uzushi wanaweza kukosa utu na ubinadamu kuliko wale vijana waliobaka na kulawiti? Sasa mbona mnawalaani zaidi wasambaza taarifa za uzushi kuliko mnavyowalaani wale wabakaji? Mbona sijaona press ya polisi ikiwataja wale wabakaji kuwa wamekosa utu na ubinadamu?
Hivi kweli mnaumizwa na uzushi kuliko mnavyoumizwa na ubakaji? Tafadhali shughulikeni na suala la msingi ambalo ni ubakaji, achaneni na haya mengine ambayo hayana public interest. Watanzania wanataka kuwajua vijana waliofanya unyama ule ni akina nani? huyo afande aliyewatuma ni nani? Na wamechukuliwa hatua gani za kisheria. Haya mengine yapotezeeni tu.!
(Via Malisa GJ Facebook
1 307
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kitendo alichofanyiwa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo, ni kinyume cha sheria na maadili ya Mtanzania.
Amesema binti huyo kwa sasa yupo kwenye mikono salama ndani ya moja ya vituo vya mkoa wake, akipata elimu ya unasihi itakayomsaidia kujikuza katika maisha yake ya kila siku.
Chalamila amesema hayo jana Agosti 8, 2024 akizungumza na Mwananchi ikiwa ni siku nne zimepita tangu Agosti 4, ziliposambaa picha jongefu kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huyo, huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na mume wa mtu wakimtaka kumuomba radhi mtu waliyemwita kwa jina la ‘afande’.
Wakati Chalamila akieleza hayo, watetezi mbalimbali wa haki za binadamu wametaka hatua za haraka zichuliwe dhidi ya waliohusika katika tukio hilo, huku wakitoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume kuchunguza matukio yote yaliyofanywa na watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Chalamila amesema kitendo alichofanyiwa binti huyo, kinalaaniwa na Serikali kwa nguvu zote, kwani ni kinyume cha sheria za nchi na utamaduni wa Mtanzania.
“Binti yupo mikono salama hajafa, mimi mkuu wa mkoa nafahamu kabisa yupo salama, yupo kwenye moja ya vituo vyetu na lazima binti huyo awe salama apone kisaikolojia, aweze kutulizwa vizuri na kupewa elimu ya unasihi itakayomsaidia kujikuza katika maisha yake ya kila siku,” amesema Chalamila.
1 307
JESHI LA POLISI LISIPAMBANE NA UVUMI, ILA LITOE TAARIFA ZINAZOTAKIWA JUU YA BINTI.
Jeshi la Polisi linasema binti aliyebakwa 'yuko salama salimini'! Hatupingani na kauli ya Jeshi la Polisi. Lakini pia tunapenda kupata ufafanuzi kutoka Jeshi la Polisi juu ya mambo yafuatayo:
1. Jeshi la Polisi lilimpeleka binti kupimwa afya yake katika Hospitali gani na lini hadi linatoka hadharani kusema kuwa 'yuko salama salama salimini'?
2. Je, ni daktari gani aliyempima binti huyo? Je, cheti hicho alikikabidhi kwa Jeshi la Polisi?
3. Je, Jeshi la Polisi wanaweza kuwa wasemaji juu ya afya ya mtu ambaye sio mtuhumiwa?
4. Je, familia ya binti huyo iko wapi, imepokeaje suala la binti yao, inasemaje juu ya afya yake?
5. Je, Ustawi wa Jamii wanahusikaje na suala la afya ya binti huyo kimwili na kisaikolojia?
6. Lakini ni kwa nini taarifa za watuhumiwa pia ziwe siri sana? Mbona Jeshi la Polisi linapiga picha watuhumiwa mbalimbali na kuongea na vyombo vya habari? Inakuwaje hili ni tofauti?
Jeshi la Polisi lilitakiwa kujiepusha kutoa kauli za mara kwa mara zisizojibu maswali ya jamii. Badala yake lingejikita kutoa taarifa sahihi juu ya jambo hilo. Usiri, ukimya na kutaoaminika kwa taarifa za Jeshi la Polisi ndiko kunafanya kuenea kwa uvumi. Uvumi hauwezi kupuuziwa kama hakuna taarifa mbadala na za kuaminika!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo! Askofu Emmaus Bandekile
Dar es Salaam, 9 Agosti 2024; saa 10:58 asubuhi
1 307
#HABARI Jeshi la Polisi nchini limewakata watu wanne kati ya sita wanaotuhumiwa kumbaka na kumlawiti binti mkazi wa Yombo Dovya Dar es Salaam ambaye video yake ilisambaa mitandaoni hivi karibuni akifanyiwa ukatili huo na wanaume watano.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime, imeeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mkoani Dodoma na Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu la Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nikson Idala Jakson.
"Uchunguzi uliofanyika hadi sasa umefanikisha kumpata binti aliyefanyiwa ukatili huo na amehifadhiwa eneo salama na anaendelea kupata huduma zinazostahili kupewa mtu aliyefanyiwa ukatili wa aina hiyo, aidha uchunguzi umebaini tukio hilo lilifanyikia eneo la Swaswa katika Jiji la Dodoma mwezi Mei 2024," imeeleza taarifa hiyo.
Aidha DCP Misime amesema kuwa, "Jeshi la Polisi lingependa kueleza pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne huko Dar es Salaam waliokiuka sheria na kusambaza picha mjongeo wa tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii ambao ni Frora Mlombola, Aghatha Mchome, Madatha Jeremiah Budodi na James Nyanda Paulo,".
1 307
UCHUNGUZI WA TUKIO LA BINTI WA YOMBO DOVYA
1. Hadi Agosti 9 Jeshi la Polisi limewatia mbaroni watuhumiwa 4 kati ya 6.
2. Binti yuko sehemu salama akipatiwa msaada wa kisaikolojia kutokana na tukio hilo.
3. Majina ya waliokamatwa mpaka sasa ni Clinton Honest Damas (Nyundo), Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jackon.
4. Jeshi la Polisi linatoa ilani yeyote anayewahifadhi wawili waliosalia anatenda kosa na wakikamatwa kwake na yeye atawajibika.
5. Tukio lilitokea Mei 2024 Saswa Dodoma.
6. Msako unaendelea na wahusika watafikishwa Mahakamani hivi punde.
1 307
#HABARI Jeshi la Polisi nchini limewakata watu wanne kati ya sita wanaotuhumiwa kumbaka na kumlawiti binti mkazi wa Yombo Dovya Dar es Salaam ambaye video yake ilisambaa mitandaoni hivi karibuni akifanyiwa ukatili huo na wanaume watano.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime, imeeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mkoani Dodoma na Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu la Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nikson Idala Jakson.
"Uchunguzi uliofanyika hadi sasa umefanikisha kumpata binti aliyefanyiwa ukatili huo na amehifadhiwa eneo salama na anaendelea kupata huduma zinazostahili kupewa mtu aliyefanyiwa ukatili wa aina hiyo, aidha uchunguzi umebaini tukio hilo lilifanyikia eneo la Swaswa katika Jiji la Dodoma mwezi Mei 2024," imeeleza taarifa hiyo.
Aidha DCP Misime amesema kuwa, "Jeshi la Polisi lingependa kueleza pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne huko Dar es Salaam waliokiuka sheria na kusambaza picha mjongeo wa tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii ambao ni Frora Mlombola, Aghatha Mchome, Madatha Jeremiah Budodi na James Nyanda Paulo,".
#EastAfricaRadio
1 307
+9
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2

MAKALA HURU:-TOP 10: KAULI ZA JPM ZILIZOTIKISA, TAZAMA UNIAMBIE IPI ILIKUKOSHA ZAIDI!
1 307
MAKALA HURU:-TOP 10: KAULI ZA JPM ZILIZOTIKISA, TAZAMA UNIAMBIE IPI ILIKUKOSHA ZAIDI!
1 307
+2
SAULI AZIKWA, ALILIWA NA WENGI,
MAZISHI YAKE YAFANYIKA GODIMA CHUNYA AACHA WAKE WATATU WATOTO KUMI NA SITA.
Na, PETER KAPOLA.
Marehemu Saul Solomon Mwalabhila ambaye alikuwa anajishughulisha na biashara ya usafirishaji pamoja na shughuli za uchimbaji madini ameacha wake watatu na watoto 16.
Mmiliki wa mabasi ya saul Solomon Mwalabhila aliyefariki Agosti 4,2024 umezikwa leo katika Kijiji cha Godima wilayani Chunya Mkoani Mbeya na kuhudhuriliwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwepo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarack Alhaji Batenga na Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka.
Akizungumza katika mazishi hayo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Batenga amewataka wanafamilia kuya enzi mazuri yote yalikuwa yakifanywa na marehemu Sauli Mwalabhila ili watoto walioachwa na marehemu waweze kunufaika.
1 307
+4
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2