en
Feedback
E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Open in Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

Show more
1 307
Subscribers
+124 hours
-27 days
-1330 days
Posts Archive
MANDOJO; ROHO YA MAUTI NI KITENDAWILI KIGUMU BINADAMU ni nafsi, mwili ni kasha. Una sura nzuri, mwili laini, ukiwa na nafsi katili, wewe ni mtu mbaya. Umbile lake linaweza kukutisha au uso wake ukakuogofya, ila nafsi ni njema, huyo ni mwema. Unaweza ukaoga na kujitakasa, ukavaa nguo nadhifu na manukato ukajitwika, ukanukia uturi, ila nafsi ikiwa chafu, wewe ni mchafu. Yupo mhangaikaji wa dunia, jasho linabadili harufu ya mwili, lakini nafsi ni njema, huyo ni mtu msafi. Moyo huakisi nafsi. Matendo mema ya mtu huwakilisha moyo wake, vivyo hivyo nafsi yake. Katili, mwovu, mfitini, msaliti na jambazi, ni zao la moyo mbaya, ndivyo ilivyo nafsi ya mhusika. Mwili ni kasha, ubinadamu ni zao la moyo, ambao ni tunda la nafsi. Mfumo wa maisha ya mwanadamu ni kuishi na kukutana na watu. Ulimwengu ni walimwengu, jamii ni wanajamii. Hakuna jamii ya mtu mmoja. Ulimwengu utakukutanisha na walimwengu. Makutano hayo yatakuainishia watu wema, wenye ukakasi na waovu. Mitikasi ya kiulimwengu ilinikutanisha na Joseph Francis “Mandojo”. Nikafanya naye kazi. Kitu kimoja ambacho naweza kukithibitisha ni ubinadamu wake. Alikuwa mwema, muungwana na mwanajamii mzuri. Mandojo ni ana ya watu ambao wanaweza kukuumiza kichwa, kuwaza ni wakati gani alikuwa akikasirika. Muda mwingi ungemwona ametabasamu. Mchangamfu hasa. Ungependa kufanya naye kazi. He was an all-weather person. Septemba 29, 2023, Alliance Francaise, Upanga, Dar, zilifanyika sherehe za Bongo Flava Honors, kutambua mchango wa Mandojo na Domokaya, kwenye ukuaji wa Bongo Flava. Ilikuwa siku bora kupitiliza. Mimi kama mwanakamati ya uandaaji na msimamizi mkuu wa maudhui na promosheni, nili-enjoy mpaka mwisho. Mandojo na Domokaya ni professionals. Kuanzia nidhamu ya ratiba, muda hadi performance. Ni rahisi, vilevile ni burudani kufanya nao kazi. Nipo mbali na Dar. Saa 8 mchana jana (Jumapili), napokea simu ya Mwenyekiti wa Bongo Flava Honors, Sugu The Jongwe. Akanijulisha: “Kuna habari mbaya. Mandojo ameuawa.” Mazingira ya kifo yanaumiza zaidi. Dojo hanywi pombe kabisa, eti siku ya tukio alikunywa. Akahisiwa ni mwizi, akauawa. Roho ya mauti ni kitendawili kigumu ajabu. Usiku mwema, Brother. (c&c: Luqman MALOTO)

photo content

✍️ Ameandika hivi #Stevenyerere... " Mstafuuu,, Nawapa pole Family Nawapa pole Wasanii wote ,Hili ni pigo na Pengo pia, Masha
✍️ Ameandika hivi #Stevenyerere... " Mstafuuu,, Nawapa pole Family Nawapa pole Wasanii wote ,Hili ni pigo na Pengo pia, Mashabiki Wadau wa mziki poleni ,Huyu jamaaa Pamoja na mziki kumtambulisha lakini mimi binafsi namtambua kwa nidhamu yake ,upole wake Utu huwezi kumuona Mandojo kwenye Purukushani za Kitoto kamwe Au kugombana na mtu, Pumzika kaka Najaribu kuwaza hao wananchi walio jichukulia maamuzi yao binafsi wanajiskiaje kwa sasa ,Wanaona maumivu yetu,, Ni wasihi sana Ndugu zangu Hata tukikamata mwizi tuna vyombo vya usalama nadhani tuwafikishe huko kuliko kujichukulia maamuzi si sawa kabisa kabisaaa Pumzika kaka Tutaonana Baadaye"

TULIKUPENDA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI PUMZIKA KWA AMAN @mandojoofficial MBELE YAKO NYUMA YETU AMINA🙏
TULIKUPENDA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI PUMZIKA KWA AMAN @mandojoofficial MBELE YAKO NYUMA YETU AMINA🙏

DRC: Na Jerome Robert Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limetahadharisha kwamba maradhi ya homa ya nyani bado ni kitisho cha k
DRC: Na Jerome Robert Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limetahadharisha kwamba maradhi ya homa ya nyani bado ni kitisho cha kiafya kote ulimwenguni bila kujali mipaka. huku likielezea wasiwasi wake kwa kuangazia hasa mlipuko wa aina mpya na mbaya zaidi ya virusi vya homa hiyo, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. WHO limesema mwezi uliopita pekee, lilipokea ripoti za visa kutoka nchi 26 na Mkurugenzi wake, Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari kwamba kitisho bado ni dhahiri. Amesema, mlipuko huo hauonyeshi dalili ya kupungua, wakati kukiripotiwa visa 11,000 mwaka huu, pamoja na vifo 445, huku watoto wakiathirika zaidi. Rosamund Lewis, anayeongoza jopo la ufundi la WHO linaloshughulikia maradhi hayo, naye amesema wana wasiwasi sana na hali hiyo. Cc dwkiswahili Tuandukie maoni yako.... #radiokwizera #2024funguka

photo content

WHO yaonya kasi ya virusi vipya homa ya nyani Brazzaville, KUMEKUWEPO na ongezeko la kasi la virusi vipya vya homa ya nyani na kusababisha Shirika la Afya Duniani kutaka jamii kuwa na uanglifu mkubwa kutokana na kuzidi kusambaa barani Afrika. WHO imesema kwamba kumekuwepo na ongezeko kubwa la wagonjwa wa virusi hivyo vipya vya nyani tangu mwanzo wa mwaka 2024. Limesema nchi nyingi ambazo hazikuwa zimeathiriwa awali na ugonjwa huu zimeanza kuripoti wagonjwa wapya, dalili zikionesha kuenea kwa virusi hivyo kwa kasi zaidi. Kutokana na hali hiyo Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameitisha mkutano wa kamati ya wataalam wa dharura ili kubaini kama mlipuko huu unastahili kutangazwa kuwa Dharura ya Afya ya Kimataifa. Hadi sasa nchi kumi na tano za Afrika hivi sasa zina ripoti ya mlipuko huo na jumla ya wagonjwa 2,030 wamethibitishwa na vifo 13 vimeripotiwa mwaka huu ikilinganishwa na wagonjwa 1,145 na vifo saba mwaka 2023. Nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda ambazo hazikuwa zimeathiriwa na ugonjwa huo zimeanza kuripoti uwepo wa wagonjwa kuanzia katikati ya Julai 2024. Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambayo inachukua zaidi ya 90% ya idadi ya wagonjwa barani afrika imeeleza kuwa ugonjwa huo ulilipuka Septemba 2023 maeneo ya mashariki ya nchi hiyo. Nchi jirani za Rwanda na Uganda zimeripoti kuwapo kwa wagonjwa. Kenya pia imethibitisha. “Kipaumbele ni kuzuia kuenea kwa virusi haraka iwezekanavyo. Tunashirikiana na wadau katika kuunga mkono nchi kuimarisha hatua za kudhibiti mlipuko na kuhakikisha kuwa jamii inashiriki kikamilifu katika juhudi za kumaliza mlipuko huu kwa ufanisi,” alisema Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO wa Afrika. Ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu huenea na kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu kupitia mawasiliano na maji ya mwili, vidonda kwenye ngozi au kwenye nyuso za ndani za utando wa ngozi, kama vile mdomo au koo, matone ya kupumua na vitu vichafu. Dalili zake ni pamoja na kuvimba kwa tezi za limfu, homa, na upele ambao hubadilika kuwa malengelenge kisha ukakauka. Dalili zake nyingine ni uchovu,maumivu ya kichwa maumivu ya misuli na maumivu ya mgongo.

photo content

Homa ya nyani ni nini? Homa ya nyani ni kirusi ambacho wanasayansi walikibaini kwa nyani kwa mara ya kwanza mwaka 1958, na ji
Homa ya nyani ni nini? Homa ya nyani ni kirusi ambacho wanasayansi walikibaini kwa nyani kwa mara ya kwanza mwaka 1958, na jina hili la "Monkeypox" ndiyo lilitokana na ugunduzi huo Kirusi hiki kilibainika kwa binadamu kwa mara ya kwanza mwaka 1970 Ugonjwa wa homa ya nyani unatoka kwenye familia moja ya kirusi kinachofanana na kama kile cha ugonjwa wa ndui (smallpox), lakini hakisababishi ugonjwa hatari sana kama ilivyo kile kinachosababisha ugonjwa wa ndui Wakati tukiandika makala hii, WHO iko katika mchakato wa kufafanua majina mapya ya kirusi cha homa ya nyani na aina zake Kuna aina 2 za homa ya nyani: clade I (zamani ilifahamika kama aina ya Bonde la Kongo) na clade II (zamani ilifahamika kama aina ya Afrika Magharibi) Uchunguzi wa kipimo cha PCR unaonyesha kuwa mlipuko wa sasa umesababishwa na clade II, ambayo huwa na dalili zisizo kali zaidi kuliko clade I Dalili za homa ya nyani ni zipi? Kwa watu walio wengi, homa ya nyani sio ugonjwa wenye kuhatarisha maisha. Lakini unaweza kusababisha dalili kali, kuvuruga maisha ya kila siku, na unaweza kuhusishwa na unyanyapaa wa kijamii Homa ya nyani kwa kawaida husababisha homa na vipele venye muonekano usio wa kawaida, lakini dalili nyingine ni pamoja na Maumivu ya kichwa Maumivu ya mgongo Maumivu ya misuli Kuvimba kwa tezi za limfu Vipele vya homa ya nyani kwa kawaida hujitokeza usoni, mikononi, na miguuni, ingawa vinaweza pia kuathiri sehemu nyingine za mwili Hatimaye vipele hugeuka vigaga na kwisha Wanawake wajawazito, watoto, na watu wenye kingamwili dhaifu wanaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata dalili kali za ugonjwa huu

AFYA: Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitisha Mkutano wa Dharura kujadili hali ya usambaaji wa Homa ya Nyani (#Mpox), ambapo
AFYA: Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitisha Mkutano wa Dharura kujadili hali ya usambaaji wa Homa ya Nyani (#Mpox), ambapo Takwimu kutoka kwa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (CDC) zinaonesha ongezeko la 160% la Homa hiyo ikilinganishwa na Mwaka 2023 Takwimu zimeonesha tangu Januari hadi Julai 28, 2024, Visa 14,250 vimeripotiwa katika nchi kadhaa zikiwemo Burundi, Cameroon, Ghana, Liberia, Nigeria, #Rwanda, #DRCongo, na Afrika Kusini. Pia, katika kipindi cha Miezi 12 iliyopita, nchi 17 zimeripoti homa ya Mpox Aidha, #AfricaCDC imeripoti ongezeko la vifo 461, huku 450 vikitokea DR Congo ambako Ugonjwa huo umesambaa zaidi. Takwimu hizo ni nje ya maambukizi mapya yaliyoripotiwa katika nchi za #Kenya na #Uganda. Soma

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Twitter👇 https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
+8
KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Twitter👇 https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09

KUTOKA MITANDAONI Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇 https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW4
+9
KUTOKA MITANDAONI Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇 https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2

Kwani masoud ana maana gani hapa
Kwani masoud ana maana gani hapa

FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU TU FOLLOW HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_me
+9
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU TU FOLLOW HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/

KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://yo
+9
KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK

KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://yo
+8
KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Twitter👇 https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
+9
KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Twitter👇 https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09

…ni nadra sana kukutana na habari ya Tanzania 🇹🇿 kwenye magazeti yetu hapa Ufaransa 🇫🇷… Habari za Afrika zinazopewa kipau
…ni nadra sana kukutana na habari ya Tanzania 🇹🇿 kwenye magazeti yetu hapa Ufaransa 🇫🇷… Habari za Afrika zinazopewa kipaumbele hapa ni za huko West Africa, kwenye makoloni yetu ya zamani… Cha ajabu na kushangaza, leo habari ya mjukuu wangu wa Yombo Dovya imeongoza kwenye magazeti yote nchini hapa 🇫🇷… 😭 Yaani nchi inakuwa maarufu kwa habari ya kipuuzi! Kiukweli leo nimeumia sana hadi nikajivua koti la Ufaransa 🇫🇷 nikabaki na ngozi yangu nyeusi ya Tanzania 🇹🇿😭😭😭 Imagine, unapigiwa simu zaidi ya 10 kutoka kwa marafiki zako, sio kwa kukupongeza kupata treni ya SGR nchini kwako, bali kukuuliza «kipi kimetokea huko kwenu? Nasikia majeshi yenu yamebaka na kulawiti? » 😭

FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU TU FOLLOW HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_me
+9
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU TU FOLLOW HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media
+9
KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media