E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
"Nikipewa kazi niifanye naifanya katika kiwango kikubwa kuliko hata matarajio ya walionipa kazi yaani navuka target always na watu wanaona na makampuni yanaona" - @hajismanara
Cc Clouds TV
1 307
“Kuita timu ni mwalimu ndio anaita ,kuna chombo kimezungumza kwamba mimi ndio naletewa majina ,nikaletewa majina Samatta hayupo nikamuingiza ,hakuna mwalimu ambaye atasimama na kusema TFF inamuitia timu”
Majibu ya Rais wa TFF kuhusu uitwaji wa kikosi kinachoiwakilisha timu ya Taifa Taifa Stars , na kauli za baadhi ya watu kusema yeye ndiye aliyemuita Samatta na sio kocha .
Wallace Karia
1 307
Mahakama ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma imemhukumu Jeremia Ngendabanka, mkazi wa Kijiji cha Buhingu kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kupatikana na viungo mbalimbali vya Sokwe Mtu.
Ngendabanka ambaye ni mkulima alikamatwa Septemba 22 mwaka huu na nyara za Serikali ambazo ni mkono, kichwa na ngozi vya Sokwe Mtu vikiwa na thamani ya TZS milioni 12.
1 307
“Hatuwezi kwenda Mbinguni sababu tulisali sana, Tulifunga sana, Tulinena kwa lugha, Tulitoa Mapepo, Tulisali Novena na Litania nyingi. Hukumu ya Mwisho itahusu ni kwa Kiasi gani tuliwajali wengine” CDF Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo
1 307
HOTUBA YA MWISHO ALIYOIANDIKA QADAFFI
QADAFFI ANAANZA HIVI:
"Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu mpaji, na mwenye rehema...
Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule.
Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo. Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili.
Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia"
waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo. Walikua hawasikii wala hawaoni.
Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua. Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kuleta mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubapeari" Maana yake.
Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka. Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida. Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.
Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni.
Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.
NB: Hizo ni Nukuu zake sio Mimi.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.
1 307
"Kifo cha mke wangu kimenichukua sana akili na bado kimeendelea kunichukua kwasababu kile kitu sijawahi kukizoea, nashindwa hata kulala nyumbani kwangu, nimehama tulipokuwa tunaishi na Marehemu mke wangu, siwezi kulala kwenye kitanda changu kwasababu yule alikuwa ni mke wangu, tulikula viapo mimi nilishawahi kumwambia wewe ndio mwanamke wa maisha yangu na yeye aliwahi kuniambia mimi ndiye mwanaume wa maisha yake. Kwahiyo kile kitu hadi leo kinaniumiza na sidhani kama nitapata mwanamke atakayeziba pengo lake"
"Mtoto wetu hadi sasa bado hajui kama mama yake amefariki, bado tumemficha, ila mimi kama mzazi naona kuna umuhimu wa yeye kujua kwasababu anakua lazima alitambue hili mapema japokuwa ndugu zangu wanajitahidi sana kumficha. Watu wanasema nisiposti video za zamani za mke wangu eti nakosea, niwaambie tu kwamba yule alikuwa mke wangu, tumejuana kwa miaka 12 sio rahisi kumsahau kirahisi hivyo, mimi ndio najua maumivu ninayoyapitia, waniache"- Boshen mume wa Marehemu Haitham Kim
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
⚠️😳😢 Mwanamke wa nchini Kenya Leyla Abdikadir ameingia mikononi mwa vyombo vya sheria baada ya kuchukua kisu kutaka kumchoma house girl wake kwa jina la Zuhura Isale akimtuhumu kuwa na mahusiano na mume wake, ambapo katika kujiokoa house girl aliruka kutoka dirishani gorofa ya kwanza
Tukio limetokea tarehe 11 November hii huko Nairobi. Ugomvi ulianza baada ya Leyla kuona kwamba house girl wake alimuandalia kifungua kinywa mume wake wakati yeye kama mke alishaweka sheria ndani ya nyumba kuwa ni marufuku kumuandalia chakula mume wake, na hapo ndipo akamtuhumu house girl kuwa na mahusiano na mumewe na kuchukua kisu kutaka kumchoma nacho
Baada ya house girl kuruka dirishani na kuelezwa kuumia vibaya, Leyla alijaribu kumpelela house girl wake hospitali ya karibu lakini ilibidi ahamishiwe hospitali ya rufaa ya Kenyatta kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata ambapo bado anatibiwa
Leyla ametoka kwa dhamana ila kesi itatajwa tarehe 19 February 2024 na kuanza kusikilizwa tarehe 29 March 2024
1 307
"Maisha yanazidi kuwa magumu kila kunapokucha, au kuna sehemu tumekosea??. Nawaza tu sisi wenye vibarua viwili vitatu na bado kuipata hiyo pesa ni kasheshe, wasiokuwa na vibarua wala ishu wanayoisikilizia sijui wanaishije huko mtaani' au mwisho wa dunia nyie alafu hatuna taarifa"- Romyjons
1 307
.
▪️Oktoba 2021 Eric Tshimanga Katompa alikuja Tanzania akampiga Abdallah Pazzi kwa pointi
▪️Novemba 2023 Eric Tshimanga Katompa amerudi Tanzania na kumpiga tena Abdallah Pazzi kwa pointi
1 307
Derek Chauvin, aliyekuwa afisa wa polisi wa Minneapolis aliyepatikana na hatia ya kumuua George Floyd, alidungwa kisu na mfungwa mwingine na kujeruhiwa sana Ijumaa katika gereza la shirikisho huko Arizona, mtu anayeelewa kuhusu suala hilo alikiambia chombo cha habari cha The Associated Press.
Shambulio hilo lilitokea kwenye Taasisi ya Urekebishaji ya Shirikisho, Tucson, gereza la usalama wa wastani ambalo limekuwa likikumbwa na kasoro za usalama na upungufu wa wafanyakazi. Mtu huyo hakuwa na ruhusa ya kujadili hadharani maelezo ya shambulio na alizungumza na AP kwa sharti la kubaki bila kutajwa jina.
Idara ya Magereza ilithibitisha kuwa mfungwa huyo alishambuliwa katika FCI Tucson saa 12:30 jioni. Katika taarifa, shirika hilo lilisema wafanyakazi waliokuwepo walizuia tukio hilo na kutekeleza hatua za kuokoa maisha ya mfungwa huyo, ambaye hawakumtaja jina, kupelekwa hospitalini kwa matibabu na uchunguzi zaidi.
1 307
Cristiano Ronaldo - " katika historia ya mafanikio yangu lazima nimshkuru rafiki yangu Albert Fantrau . Tulicheza wote katika klabu moja wakati tulipokua vijana wadogo..
Nakumbuka wakati klabu ya Sporting ilivyowasili, walitwambia wanahitaji mchezaji mmoja ambaye atafunga mabao mengi ndio atachukuliwa na academy yao” tulishinda mechi hiyo bao 3-1 , mmoja alifunga bao la kwanza , alafu Albert alifunga nayeye bao akitumia kichwa na bao la tatu ndio lilivutia wengi. Albert alikua yeye na golikipa . Mimi nilikua nyuma yake , alimpiga chenga kipa kilichokua kinabaki niyeye kufunga bao tuu kwa sababu alikua ana uwezo huwo kutokana na jinsi golikipa alikua hayupo golini lakini chaajabu Ni kua alinipa pass kisha nikafunga bao
Kutokana na kiwango nilichokionyesha kwenye mechi , nilichaguliwa na Academy na kabla ya mechi nilimfuata rafiki yangu nikamuuliza: « kwanini hukufunga bao lile? Akajibu wewe ni bora kuliko mimi. Na wewe una ndoto kubwa ya kua mchezaji mkubwa duniani hii ndio bahati yako 😌😌
Maneno haya yalimfanya mtangazaji aliyemuhoji Cristiano Ronaldo kwenda kumuuliza Albert kama ni kweli na alihakikisha kama nikweli . Na alieleza kua career yake iliishia pale pale kwa vile hakuhitaji kucheza tena soka na kwa sasa hana kazi yeyote anayoifanya. Lakini wapi umepata pesa ya kujenga nyumba zuri hivi na gari lakifahari namna hii na inaonekana una pesa wewe : mtangazaji alimuuliza. Albert alimjibu hivi vyote unavyoviona hapa na kuna vingi tuu ambavyo huvioni vyote kabisa vinatoka kwa rafiki yangu Cristiano Ronaldo
Funzo: kamwe usimsahau mtu yeyote aliyewahi ku kusaidia ili ufikiye mafanikio yako .
SUBSCRIBE | Tazama Videos KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
NABII MKUU DKT.GEORDAVIE AKABIDHI GARI NA SHILINGI MIL 11.4 KWA MUANDAAJI YA MISS TANZANITE MANYARA.
Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie ametoa gari jipya aina ya Honda station wagon yenye namba za usajili T169 EEP kwa muandaaji wa mashindano ya Miss Tanzanite Manyara Bi. Aminata pamoja na shilingi milioni 11.4.
Nabii Mkuu amekabidhi gari hilo jana katika ibada ya chuo kikuu cha manabii baada ya Bi.Aminata kuelezea changamoto anazokutana nazo katika kazi yake ambapo Nabii Mkuu aliguswa na kuamua kumsapoti gari hilo na fedha hizo ili aweze kuendesha ofisi yake ikiwa ni pamoja na kuwalipa washindi na washiriki wa mashindano hayo.
Kwa upande wake Bi. Aminata amemshukuru Nabii Mkuu kwa moyo wa upendo wa kusaidia watu huku akimuombea Nabii Mkuu Aishi miaka mingi ili awasaidie watu wengine wanaokutana na changamoto mbalimbali maishani mwao.
