E-PLUS MEDIA
الذهاب إلى القناة على Telegram
1 307
المشتركون
+124 ساعات
-27 أيام
-1330 أيام
أرشيف المشاركات
1 307
TAKRIBAN MAHUJAJI 14 WA HAJJ SAFARIKI DUNIA KWA JOTO KALI
Takriban raia 14 wa Jordan wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia kutokana na joto kali, maafisa wamesema.
Wizara ya mambo ya nje ya Jordan ilisema raia wake 14 wamefariki "baada ya kupigwa na jua sana kutokana na wimbi la joto kali" na wengine 17 wameripotiwa kupotea.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Shirika la Red Crescent la Iran limethibitisha kuwa mahujaji watano wa Iran pia wamepoteza maisha, lakini haikueleza jinsi walivyofariki.
Maafisa wa Jordan walisema msako unaendelea kuwatafuta waliotoweka.
Katika taarifa yake wizara ya mambo ya nje ya Jordan ilisema kuwa inawasiliana na mamlaka ya Saudia kuhusu taratibu za kuzika au kusafirisha miili ya marehemu, kulingana na matakwa ya familia zao.
Hajj ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya watu duniani ambapo zaidi ya mahujaji milioni 1.8 wanashiriki hijja mwaka huu, kulingana na maafisa wa Saudi.
Lakini ina historia ya majanga makubwa ikiwa ni pamoja na mikanyagano na moto wa mahema. Lakini kwa miaka mingi, changamoto kuu hutokana na joto kali.
Halijoto wiki hii ilizidi 46C (114.8F) na kufanya tamaduni nyingi zinazofanywa nje na kwa miguu kuwa na changamoto hasa kwa wazee
Source BBC Swahili
1 307
+9
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
Rais wa maana kabisa huyu♥️ Hakika wananchi wa Senegal wanafurahia mema ya nchi yao.✍️
Amefuta ushuru kwenye bidhaa zote muhimu kwa wananchi wake ili tuu waishi vzr.✍️
Afutia ushuru bidhaa zifuatazo:
👉Mchele
👉Mafuta ya kupikia
👉Sukari
👉Mahindi
Na bidhaa nyingine nyingi ambazo zinakamilisha mahitaji ya mwananchi kwa siku nzima
1 307
Mwijaku atakiwa kulipa shilingi bilioni 5 kwa kumchafua Masoud Kipanya
Wakili wa Masoud Kipanya mtangazaji maarufu ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa kupitia vibonzo, Alloyce Komba kutoka kampuni ya Haki Kwanza Advocates amesema mteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa na kauli za Mwijaku juu yake mpaka kuna baadhi ya makampuni zimesitisha mikataba ya kufanya nae kazi
"Masoud anaona aibu hata kutembea mbele ya watu, tuhuma za kujihusisha na biashara haramu zimemuathiri”
Wakili huyo amemtaka Mwijaku kutoa ushahidi wa tuhuma hizo au kulipa faini ya shilingi bilioni 5 za Kitanzania
Awali, hivi juzi kati baada ya Mwijaku kuhama kutoka Clouds FM kwenda Crown FM, Masoud Kipanya alitoa maoni yake kuhusu hilo, lakini Mwijaku alionekana kutopendezwa
Mwijaku aliibuka kudai kwamba Masoud Kipanya anajihusisha na biashara haramu
Jana, Mwijaku aliitisha mkutano na waandishi wa habari kumuomba msamaha Masoud lakini leo Masoud Kipanya nae ameitisha mkutano na waandishi
1 307
+2
JIUNGE KWENYE GROUP LA E PLUS MEDIA UWEZE KUTOA MAONI NA KUCHAT...KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE LINK👉https://t.me/EplusMediaTz
1 307
+4
KUTOKA MITANDAONI
Zaidi follow ukurasa wetu wa instagram hapa kwenye link👇👇
https://www.instagram.com/e_plus_media?igsh=YW40cmNtdXV0OWZ2
1 307
"Uhusika wangu wa Kichawi una changamoto nyingi sana nakutana nazo, mara kadhaa nakutana na watu wenye uchawi wao huwaga wananipiga tu nakimbia wengine wananisaidia, niliwahi kupigwa pale Buguruni Malapa, nikapigwa Kariakoo pia nilipigwa Sabasaba, nilikuwa sina hili wala lile mama mmoja akatoka tu huko akanizabua kibao cha akili nilikisikilizia haswaaa kilikuwa kimeshiba"
"Watu wakamuuliza kwanini umempiga? akasema anaingilia kazi isiyomhusu huyu Mama mchawi. Navumilia kwasababu ndio kazi yangu nitafanyaje? lakini nafsi yangu huwa inaumia sana"- Bi Mwenda, Mwigizaji Mkongwe wa filamu Tanzania.
Toa maoni yako
1 307
"Mimi ndiye msanii wa kike tajiri namba moja Tanzania, kwa levo niliyofikia naweza kwenda kula China, kulala Afrika Kusini na nikarudi kuogelea Zanzibar kwa siku moja"- Shilole, Msanii wa muziki Tanzania.
Toa maoni yako
1 307
"Napenda sana kuwa na urafiki na watoto wa kiume kwasababu naamini ndio watu pekee ambao wanaweza wakakustiri na sio watoto wa kike. Nilikuwa na rafiki yangu mmoja anaitwa Said, huyo ndie alikuwa rafiki yangu wa shida na raha lakini alipata matatizo akawa hayuko uraiani alikutwa na hatia anatumikia kifungo jela"
"Sasa hivi kwakweli sina rafiki, mtu yeyote atakaejitokeza mbele yangu anakuwa mshikaji wangu pale inapobidi, lakini siwezi kusema kwamba ni rafiki yangu. Zamani nilikuwa na marafiki wa kike lakini ilifika muda nikagundua kwamba unakuwa na watu ambao hawako na wewe, uko na watu lakini hawafurahii kile unachokifanya, ili kuepusha matatizo zaidi nikaamua kujitoa, kwa sasa sina rafiki"- Aunty Ezekiel
1 307
"Kwa mzee Yusuph sitoki leo wala kesho, haniachi simuachi hatuachani mpaka kiamaaa"- Malkia Leyla Rashidi.
1 307
⚠️😭 Mchekeshaji wa Kenya, Fred Omondi afariki dunia baada ya kupata ajali
Fred ni mdogo wake Eric Omondi ambaye ni mchekeshaji maarufu nchini humo
1 307
DAR ES SALAAM - Balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Canada na Jamhuri ya Watu wa China na mhariri maarufu wa vyombo vya habari nchini, Ferdinand Kamuntu Ruhinda, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Ruhinda ambaye alipata kuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya CCM ya Uhuru na Mzalendo, na yale ya Serikali ya Daily News, Sunday News na HabariLEO kwa nyakati tofauti, atazikwa Jumatatu, Juni 17, 2024 kwenye makaburi ya Kondo, Kunduchi, mjini Dar es Salaam.
Ndugu Ruhinda ambaye pia alikuwa mwanzilishi wa magazeti ya Mwananchi na Redio Uhuru amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu akikakabiliwa na maradhi ya kisukari.
Msiba uko nyumbani kwake, Masaki mjini Dar Es Salaam na taarifa zaidi kuhusu msiba huo itatolewa baadaye leo Jumamosi, Juni 15, 2024.
1 307
Ni Pastor Irene Uwoya mwanzilishi wa huduma ya Friends Of God Ministry Free Jesus Gospel
