uz
Feedback

Firibgarlarga uchmang! Telemetrio bunday kanallarni topadi va belgilaydi 👉 Belgini ko‘rmoqchi bo‘lsangiz, obuna bo‘ling

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Kanalga Telegram’da o‘tish

Get the latest news,videos,and more everyday.

Ko'proq ko'rsatish
1 307
Obunachilar
+124 soatlar
-27 kun
-1330 kun
Postlar arxiv
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema idadi ya waliofariki kwenye maporomoko wilayani Hanang mkoani Manyara imeongezeka na kuf
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema idadi ya waliofariki kwenye maporomoko wilayani Hanang mkoani Manyara imeongezeka na kufikia 87 huku idaidi ya majeruhi waliopo hospitalini ikipungua na kufikia 30.

SIJAFA NA SITAKUFA MPAKA NITAKAPOKAMILISHA KAZI YA MUNGU ILIYONILETA DUNIANI; PHILIP MPANGO "Yamesemwa mengi na wengine bado wanasema mimi ni mzuka, wale mnaopenda kusoma biblia Zaburi ya 100:18 aya ya 17 inasema sitakufa nitaishi...... kwahiyo mkae na amani niko salama nilikwenda nje kufanya shughuli maalumu kwa takribani mwezi mmoja sijapungua hata kidogo" "Mitandao ni mizuri lakini baadhi ya watu wanaitumia visivyo, mkiandika uongo mnawaumiza watu wengi, wapo watu wengi ambao wameumizwa na maneno yasio ya msingi, tujitahidi sana kutumia mitandao ipasavyo kwa kumuogopa Mungu, wale waliokuwa wanatuma picha yangu na mshumaa pembeni, wengine wakasema mzee amekata moto" "Mimi kufa bado kabisa, kazi ambayo Mungu alinituma kufanya sijaimaliza, wakati utakapofika nitarejea kwa muumba wangu, asanteni sana najua mmeniombea kweli"- Amesema Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango baada ya kushiriki ibada ya Jumapili katika kanisani katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska kiwanja cha ndege Dodoma leo Disemba 10, 2023.

photo content

Hamisa mobetto
Hamisa mobetto

"Mungu ni mwema tumehitimisha kazi ambayo mlitutuma kuifanya Hanang mkoani Manyara. Haikuwa rahisi kila siku unaamka asubuhi unakutana na kuzungumza na watu wanaolia, kulalamika, kuomboleza kutokana na maumivu wanayopitia, watu waliokata tamaa, waliopoteza matumaini baada ya kujikuta wamepoteza ndugu, jamaa na marafiki, kushuhudia masanduku ya watu waliopoteza maisha wengi kiasi kile, lakini pamoja na yote hayo unazungumza na watu ambao wamepoteza mali zao na kujikuta hawajui hata waanzie wapi" "Imagine ndani ya muda mfupi anajikuta hana Baba wala Mama, hana ndugu wala jamaa, amepoteza watoto wake wote na hajui walipo, hajui wako hai au wamepoteza maisha maana hata miili yao haijaonekana" "Hakika ilikuwa ni wiki ambayo imenipa funzo kubwa sana la maisha, wiki ambayo imenipa experience mpya katika kazi yangu, sikuwahi kufanya kazi kama hii hapo kabla, kama interview ya huyu Mama nilitamani nitupe mic 🎤 chini nipige kelele labda nitapata ahueni ya maumivu yaliyojaa kifuani kwangu, aiseeh ni kama movie lakini ndio uhalisia. Tunamshukuru Mungu sana kwa kibali cha kutimiza jukumu hili Alhamdulillah tumelitimiza vile lilivyopaswa kwa uwezo wake, Mungu awape nguvu waathirika wote hakika hawatabaki kama walivyo sasa na aziweke mahali pema roho za Marehemu wote"- Ameandika Kijah Yunus Mtangazaji wa Clouds TV

photo content

⚠️😢 Mwanafunzi wa masomo ya kiarabu ajiua kwa madai Mungu hajamjibu maombi yake Alfa Musa(22) toka nchini Nigeria alikuwa mw
⚠️😢 Mwanafunzi wa masomo ya kiarabu ajiua kwa madai Mungu hajamjibu maombi yake Alfa Musa(22) toka nchini Nigeria alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sheikh Kamaldeen ya masomo ya kiarabu Tarehe 7 December hii chumba chake kilikutwa mlango umefungwa kwa ndani na ulipovunjwa alikutwa amejiua mwili wake unaning'inia huku akiwa ameacha ujumbe wa kuwaomba msamaha wazazi wake kwa uamuzi aliochuukua, amedai amejiua sababu Mungu hajamjibu maombi yake Amedai ni bora kujiua kuliko kutenda dhambi. Ameomba akazikwe kwao Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kujaribu kufanya uchunguzi zaidi, hata hivyo tayari amezikwa na baadhi ya wanafunzi wenzie kushea picha za mazishi

"Mimi bado ni muumini hai wa Prophet Malisa na hata juzi nilienda kwenye Tamasha lake, ilikuwa ni lazima niende kwasababu hak
"Mimi bado ni muumini hai wa Prophet Malisa na hata juzi nilienda kwenye Tamasha lake, ilikuwa ni lazima niende kwasababu hakuna wakati ambao namhitaji Mungu kama wakati huu"- Gigy Money

"Maisha magumu hadi raha jamanii "- Kajala
"Maisha magumu hadi raha jamanii "- Kajala

photo content
+4

FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medi
+9
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media
+9
KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media

photo content

Haji Manara atangaza kumsaidia Chid Benz. Nimeona mitandaoni kuhusu lawama nyingi tunazopeana za kutomsaidia Msanii Chid Benz, kutokana na hali anayopitia ya Matumizi ya Uraibu anaoutumia. Kwanza niseme mimi ni mshabiki mkubwa sana wa Chidi ,na Style yake ya kurap ilinipa wakati mzuri wa kuenjoy maisha miaka ile, kisha ni Mtoto wa kiswahili kama nilivyo mimi, Tumetokana na Hasslers na tunastahili kusaidiana hata kama tumeteleza!! Najua Watu kadhaa washajaribu kumsaidia lakini bado hajakaa sawa, nipo tayari kumsaidia ,kuondokana kabisa na tatizo lake la kutumia Uraibu wake. Raha yangu ni kumuona anarejea kwenye hali yake kama zamani, ni mtu talented kweli kweli, Kisha Mwana wa kitaa, uwezo wangu mdogo unaniambia naweza kusaidia na am ready. Gharama zote za Rehab ikiwa ni pamoja na malazi, Chakula na matibabu ntazibeba, aje tu Wiki ijayo @manaratv__ Samora Avenue Salamander Tower. Kuna Clip nimeiona mchana huu mitandaoni ikitembea imenichona na nadhani kuna haja ya kumsaidia very serious. Sijui nampata wapi Shujaa wangu huyu lakini mpeni salaam zangu, Mwambieni kaka yako Haji amepata shauku kubwa ya kukusaidia, ningeweza kuifanya kimya kimya lakini nampatia wapi Chidi?" ameandika Haji Manara. Toa maoni yako

photo content

Najma Paul
Najma Paul

DR. MWIGULU NCHEMBA NAMBA MOJA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAONO YA RAIS SAMIA. Ameandika Mwalimu Zuberi Kimaro wa Kyeer, Machame Kwanza hongera sana kwako Mhe Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, kwako nimeridhika 100%, utendaji wako hauna mashaka kabisa, ni fact ambayo wanasheria huiita Undisputed one! Leo nataka niseme upande wa Mawaziri ambao technically ndo wasaidizi wako wa karibu zaidi ya Mhe Rais na ambao hutoa tafsiri ya vision ya Rais aliyepo kwa mujibu wa Ibara ya 54(3) ya Katiba ya Tanzania. Katika kutafsiri vision yako Mhe Rais ambayo iko centred katika dhana ya kimageuzi kwenye zile 4Rs zako wapo Mawaziri kadhaa wanaofanya vema kutafsiri hii vision ya MAMA ambao wanafiti kukaa kwenye hii tafakuri, ila mimi ninae mmoja tu Waziri wa Fedha MR CLEAN. Kwanza Waziri wa Fedha kitaalamu ndio Mchumi no.1, huyu Waziri ndio Architect wa mifumo ya kiuchumi ya nchi, ndiye mwenye mandates ya kuset shilingi iweje, GDP iweje, inflation rate iweje etc. Ni huyu ndiye anayetafsiri vision ya Mhe Rais katika mawanda ya kiuchumi. Kwa mujibu wa tafakuri yangu leo inaniambia, Waziri wa sasa wa Fedha amefanikiwa sana kutafsiri maono yako katika angle ya kiuchumi na honestly kwa upande wa Mawaziri wote kwangu mimi huyu Waziri wa Fedha Dr. Mwigulu Nchemba a.k.a "MR CLEAN" ndio Waziri namba (1), anayetekeleza kikamilifu maono yako, na hapa nitaenda kwa data kwa maeneo kadhaa ya mfano. 1. Maono ya Rais ni watoto wote masikini wapewe elimu bure bila ada na wapate mikopo, hili hata halikuwa gumu. Mr Clean ametoa Fedha za elimu bure shule zote msingi na Sekondari, na mikopo vyuo vyote vya kati, elimu na vikuu, tumeona shule mpya zikijengwa kikamilifu zaidi bila michango. 2. Maono ya Rais Samia ilikuwa ni kufungua barabara vijijini Mr. Clean akaanzisha tozo na matusi tukampa, sasa TARURA wana Fedha kutoka 200B nasikia sasa hivi zimefika 1.4 trillion, Mr. Clean alikuwa mbele ya muda sana, tozo zimekuwa muarobaini wa tatizo la barabara nchini. 3. Mhe Rais maono yako yamekuwa ni kuboresha afya, kijana wako Mr.Clean ametekeleza hilo, tumesikia MRI hospitali zote kanda CT scan mikoa yote, tayari Bajeti ya Wizara ya Afya imeongezeka sana. 4. Maono ya mama ni kuona umeme unafika katika kila kitongoji cha Taifa hili, Mr Clean amemwaga mapesa kila kitongoji sasa kina umeme na kazi zinaendelea kila pembe ya nchi kuhakikisha upatikanaji wa umeme sio kilio tena 5. Maono ya Rais Samia ni kuona udhibiti ubadhirifu wa Fedha za Umma Mr Clean amemwongeza bajeti Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG na kuimarisha ofisi ya Mkaguzi wa ndani, hongera Dr. Samia Haya mambo na mengine mengi yanayofanywa na Dr. Mwigulu Nchemba yanahitaji big minds za kiuchumi na wizara Vibrants za Fedha ili kuweka uwelekeo huu wa kisela sahihi Zaidi ya yote miaka 62 ya uhuru inatupa nafasi nzuri sana ya shukrani ya Mungu kwa ajili yako, lakini zaidi inatupa nafasi ya kufanya tafakuri ya harakati zetu za mipango kuelekea uhuru wa kiuchumi ambapo askari mithiri wa Dr. Mwigulu Nchemba Mr Clean ni watu muhimu sana kutufikisha huko🙏.

photo content

KAMA HAUNA UHAKIKA WA KUMUOA MTOTO WA WATU BORA UMUACHE MAPEMA SIO KUMCHEZEA; RAMMY "Kama humpendi mtoto wa watu usimfanye ku
KAMA HAUNA UHAKIKA WA KUMUOA MTOTO WA WATU BORA UMUACHE MAPEMA SIO KUMCHEZEA; RAMMY "Kama humpendi mtoto wa watu usimfanye kuwa ndio chombo cha starehe, unamtafuta pale unapomhitaji tu, kama hauna uhakika kama kuna siku utakuja kumuoa ni heri umuache sio kumpotezea muda. Unamtumia na unasema "wa kumuoa atakuwa yeye?" Ipo siku maneno yako yatakuhukumu"- Rammy Galis

SIJAMCHITI MPENZI WANGU KWA MIAKA 15; FREDY VINJABEI "Mimi nina mpenzi huu mwaka wa 15 sijawahi kubadilisha, nimeanzana nae t
SIJAMCHITI MPENZI WANGU KWA MIAKA 15; FREDY VINJABEI "Mimi nina mpenzi huu mwaka wa 15 sijawahi kubadilisha, nimeanzana nae tangu nikiwa mdogo, ndiye alikuwa msichana wangu wa kwanza kumuona kwenye macho yangu nikasema huyu nimempenda, sijawahi kubadilisha na sijawahi kumchiti"- Mfanyabiashara Fredy Vinjabei