E-PLUS MEDIA
Kanalga Telegram’da o‘tish
Get the latest news,videos,and more everyday.
Ko'proq ko'rsatish1 307
Obunachilar
+124 soatlar
-27 kun
-1330 kun
Postlar arxiv
1 307
Tumepokea taarifa ya Bus la kampuni ya Ester Luxury T763DKC linalofanya safari zake Dar - Rombo Mkuu kuanguka eneo la tambarare ya Makanya kuelekea Hedaru asubuhi ya leo.
Baadhi ya majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Same na wengine wameruhusiwa.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde
1 307
#SOMO: VITA YA ISRAEL NA PALESTINA.
(1). ARDHI YA ISRAELI NI URITHI KUTOKA KWA MUNGU.
Ukweli ni kuwa ardhi au nchi ya Israeli ni urithi kutoka kwa Mungu kwenda kwa Waisraeli, ambao ni watoto halali wa ndoa kupitia Sara. Biblia inayo maandiko mengi sana yanayoonyesha kuwa Mungu aliahidi kumpa Ibrahimu nchi yote ya Israeli, ili iwe urithi kwake na uzao wake. Lakini uzao huo ni kupitia kwa Isaka, Yakobo na hatimaye wanawe kumi na wawili. Sio nje ya mpangilio huu.
Ndio kusema kuwa Wapalestina hawatafanikiwa katika juhudi zao za kuimega Israeli katika mataifa mawili. Yaani kati ya Waisraeli na Wapalestina. Hata wakisaidiwa na ndugu zao Waarabu, au Waislamu wenzao, bado hawatafanikiwa. Hata Umoja wa Mataifa ukitaka kulazimisha mambo, ni kazi bure. Kwanini? Kwa sababu andiko la Biblia lasema ‘mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa Mwungwana’. Huu ndio msimamo wa Mungu; na kusudi lake ndilo litakalosimama.
(2). WAPALESTINA HAWAWEZI KUKALIA NCHI YA ISRAELI.
Ili kuonyesha kuwa kufuatana na Biblia, mtoto wa kambo hawezi kurithi, nitazungumzia taifa la Israeli lilivyo kwa sasa. Wachunguzi wa mambo wanasema kwamba Wapalestina, ambao kimsingi ni Waarabu, wanatokana na uzao wa Ishmaeli. Tayari nimeshaonyesha kwamba Ishmaeli ni mtoto wa kambo, na hakuruhusiwa kurithi pamoja na Isaka, mwana wa ahadi.
Kinachoendelea sasa ni watoto wa kambo (Wapalestina) wanadai kwamba nao wapewe ardhi au nchi yao ndani ya mipaka ya Israeli. Kwa maneno mengine wanadai haki ya kurithi pamoja na watoto halali wa ndoa (Waisraeli). Hili haliwezekani kamwe. Wala mikakati yote ya kuigawa nchi ya Israeli kati ya Waisraeli na Wapalestina haitafanikiwa kamwe.
Nimetumwa kuwafungua watu ufahamu na kukupa maarifa ya Neno la Mungu.
PROPHET WAMBURA MAGESA.
1 307
Baba mzazi wa Ibrahim Hamad ‘Bacca’ Amesema kabla ya mkataba mpya ambao Ibrahim Bacca amesaini ambao juzi Rais wa Klabu alitangaza beki Huyo ataendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2027 na maslahi yake yameboreshwa kwa Sasa japo babayake haligoma kuweka wazi yameongezeka kwa kiwango gani.\n\nLakini akiweka wazi kiwango Cha nyuma mtoto wake alikuwa analipwa million 1 beki Huyo wa timu ya taifa kutoka Zanzibar
1 307
MJUE DARASSA
Shariff Thabit Ramadhan anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Darassa ni msanii wa hip hop kutoka Tanzania, anayetambulika kwa wimbo wake wa 2016 'Muziki', akimshirikisha Ben Pol.
Kazi ya muziki wa Darassa ilianza mwaka wa 2012 alipotoa wimbo ‘Sikati Tamaa’. Kisha akapumzika. Alirejea mwaka wa 2016 na 'Utanipenda' akimshirikisha Rich Mavoko na pia akatoa wimbo wa 'Muziki' akimshirikisha Ben Pol, ambao ulipokelewa vyema na mashabiki ukapigwa kote Afrika Mashariki. Kwa mara nyingine, Darassa alitulia kabla ya kuibuka tena mwaka wa 2018.
Jina la kuzaliwa: Shariff Thabit Ramadhan
Tarehe ya kuzaliwa : 3 Septemba 1988 (umri 35)
Aina ya mziki : Hip hopAfro pop
Kazi : Rapper
Alipo Anza Mziki : 2014
Lebo : Usimamizi wa Kikundi cha Muziki wa Kawaida (CMG).
kwa style ya DARASSA kuzima kwa mwaka bila kutoa kazi wala ku post chochote kwenye social network zake na kurudi na ngoma zikasikika upya na kushika chats mbali mbali ivi kuna staa mwengine anaweza iyo style ama tutawasau mazima?
1 307
WANYAMA WALIOTAKASWA KWA NENO
1 Timotheo 4:1-5
[1]Basi ROHO ANENA WAZIWAZI ya kwamba NYAKATI ZA MWISHO wengine WATAJITENGA NA IMANI, WAKISIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO, na MAFUNDISHO YA MASHETANI;
[2]kwa unafiki wa WATU WASEMAO UONGO, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
[3]WAKIWAZUIA WATU wasioe, NA KUWAAMURU WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo MUNGU ALIVIUMBA VIPOKEWE KWA SHUKRANI na WALIO NA IMANI WENYE KUIJUA HIYO KWELI.
[4]Kwa maana KILA KIUMBE CHA MUNGU NI KIZURI, WALA HAKUNA CHA KUKATALIWA, KAMA KIKIPOKEWA KWA SHUKRANI;
[5]kwa kuwa KIMETAKASWA KWA NENO LA MUNGU NA KWA KUOMBA.
Katika waraka huu wa ndugu Paulo kwa Timotheo, Paulo akiongozwa na roho mtakatifu, aliona ya kuwa katika siku za mwisho, kuna watu ambao watakuja na mafundisho ya uongo, ya kishetani na wengi wataachana na imani ya kweli na kuuamini uongo huo. Ulaji wa nyama haujakatazwa mahali popote na biblia, ni mafundisho ya uongo yaliyotabiriwa yatakuweko siku za mwisho.
Hata hivyo, SIO WANYAMA WOTE WALIO SAFI KWA CHAKULA. Katika mstari wa tano, ni wazi kwamba nyama ya mnyama yeyote ALIYETAKASWA KWA NENO na kwa MAOMBI inafaa kukuliwa. Kwa hivyo ni vizuri kurudi kwenye NENO ili litufahamishe ni wanyama wepi ambao limetakasa ama kuwatenga. Pia ni wanyama wepi ambao MUNGU aliwaumba ili wapokelewe kwa shukrani na wale ambao wanaijua hiyo KWELI ama NENO. Mnyama ambaye hajatakaswa kwa NENO hata ukiomba hawezi akatakasika. NENO la MUNGU linasemaje? Je ni wanyama wepi WALIOTAKASWA kwa neno?
Mambo ya walawi 11:3-4,6-7,9-10
[3]Kila mnyama MWENYE KWATO katika miguu yake, MWENYE MIGUU YA KUPASUKA KATI, MWENYE KUCHEUA, katika hayawani, HAO NDIO MTAKAOWALA.
[4]Pamoja na hayo, WANYAMA HAWA HAMTAWALA katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; NGAMIA, KWA SABABU YUACHEUA LAKINI HANA KWATO, yeye ni najisi kwenu.
[6]Na SUNGURA, kwa SABABU HUCHEUA, LAKINI HANA KWATO, yeye ni najisi kwenu.
[7]Na NGURUWE, kwa SABABU YEYE ANAZO KWATO, ni MWENYE MIGUU ILIYOPASUKA KATI, LAKINI HACHEUI, yeye ni chukizo kwenu.
[9]Katika hao wote walio NDANI YA MAJI MTAKULA HAWA; KILA ALIYE NA MAPEZI NA MAGAMBA, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, MTAKULA HAO.
[10]Na hao wote WASIO NA MAPEZI NA MAGAMBA, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, HAO NI MACHUKIZO KWENU,
Isaiya 66:15-17
[15]Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ILI ATOE MALIPO YA GHADHABU YAKE KWA MOTO UWAKAO, na maonyo yake kwa miali ya moto.
[16]Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.
[17]Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; WAKILA NYAMA YA NGURUWE, NA MACHUKIZO, NA PANYA; WATAKOMA PAMOJA, ASEMA BWANA.
1 307
CHUMA KIMEKAA KITAKO.
Hii ndiyo ilikuwa mara ya mwisho Mike Tyson anapanda ulingoni kama bondia wa ngumi za kulipwa. Hakuwa Tyson yule ambaye alikuwa akiwalaza wapinzani wake kwa KO za roho mbaya.
Alionekana bondia wa kawaida kwenye hili pambano, hakuwa yule ambaye Dunia ilikuwa ikimfahamu kama 'The baddest man on the planet'.
Alipoteza kwa underdog Kelvin McBride, ulikuwa ni mwisho wa enzi...🥊
Kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho mwezi Juni mwaka 2005, apoteze pambano lake dhidi ya Kevin McBride,bondia bingwa wa zamani aliyewahi kushikilia mataji manne kwa pamoja ya WBC,WBO,IBF na WBA (Undisputed) kwa uzito wa juu MIKE TYSON alitangaza kupanda ulingoni tena kuvaana na Roy Jones JR Novemba 28 mwaka 2020.
Roy Jones JR alikuwa ni bingwa wa zamani wa dunia katika mizania minne, pambano ambalo lilichezwa kwenye ukumbi wa Staples Center, Los Angeles Marekani
Pambano hilo la maonyesho la raundi nane, lilibeba jina la ‘FRONTLINE BATTLE’,likiwa ni onyesho la kwanza la mfululizo wa ligi ya malejendari wa masumbwi, kwa ajili ya kuwania mkanda mpya ulioanzishwa wakati huo kwa jina la WBC (WBC Frontline Battle Belt).
Novemba 28 iliwadia na ndondi zikaanza kuchapwa Pambano likiwa la mgawanyiko na majaji watatu wa zamani wa Mabingwa wa WBC ambao walifunga pambano kama ifuatavyo:
Chad Dawson (sare 76-76), Christy Martin (79-73 kwa Tyson), na Vinny Pazienza (76-80 kwa Jones).
Kutoka kwenye KO za roho mbaya hadi kwenye ushindi wa points kwa bondia Mike Tyson,hii ndo tafsiri halisi ya kila lenye mwanzo lina mwisho.
Picha linaanza Tyson alikua mtoto mtukutu akijihusisha na matukio ya uporaji mitaani,hali iliyopelekea kupelekwa katika shule ya kurekebisha tabia (Jela ya watoto) huko New York.
Je unakumbuka tukio la mwaka 1997 Tyson kumng’ata sikio bondia mwenzake, Evander Holyfield😂😂😂?
1 307
"MIAKA MITATU ILIYO PITA NILIKUWA FUNDI SIMU"~MSANII RUGER KUTOKA NCHINI NIGERIA.
Msanii ruger kutoka nchini Nigeria,amefunguka kuwa miaka mitatu iliyo pita alikuwa fundi simu na kwa sasa amekuwa msanii Maarufu kitu ambacho hakuwai kutegemea kipindi hicho.
Ruger awashauri mashabiki kuwa wasikatishwe tamaa waendelee Kufanya kazi walizo nazo maana kazi hiyo inaweza kukupa mafanikio Makubwa.
1 307
"Mwanamke anayeacha paja lake kuonekana ni kahaba sugu,ukiwa unatembea na mwanamke kama huyo wewe ni chizi fresh."~ Pastor Ezekiel Odero asema.
1 307
ACHENI KUMTONGOZA MUME WANGU MTAMUUA NA PRESHA NIBAKI MJANE; KHADIJA
"Jamani naomba niwakumbushe msije mkamuua mume wangu na presha nikabaki mjane, maana huko DM meseji zenu ni tamu sana ila ni chungu kwa mume wangu, punguzeni kasi kidogo mimi ndiye mke wa Harmorapa"- Khadija Ziota
1 307
Orodha ya Timu za Taifa bora kwa mujibu wa Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) (FIFA World Rankings).
- Afrika
1. 🇲🇦 Morocco (13)
2. 🇸🇳 Senegal (20)
3. 🇹🇳 Tunisia (28)
4. 🇩🇿 Algeria (30)
5. 🇪🇬 Misri (33)
6. 🇳🇬 Nigeria (42)
7. 🇨🇲 Cameroon (46)
8. 🇨🇮 Coté d'Ivoire (50)
9. 🇲🇱 Mali (51)
10. 🇧🇫 Burkina Faso (57)
11. 🇬🇭 Ghana (61)
12. 🇿🇦 Afrika Kusini (66)
13. 🇨🇩 DR Congo (67)
14. 🇨🇻 Cape Verde (73)
15. 🇬🇳 Guinea (80)
16. 🇬🇦 Gabon (82)
17. 🇿🇲 Zambia (84)
18. 🇬🇶 Equatorial Guinea (88)
19. 🇺🇬 Uganda (92)
20. 🇧🇯 Benin (97)
21. 🇬🇼 G. Bissau (103)
22. 🇲🇷 Mauritania (105)
23. 🇲🇬 Madagascar (109)
24. 🇰🇪 Kenya (110)
25. 🇲🇿 Mozambique (111)
26. 🇨🇬 Congo (112)
27. 🇳🇦 Namibia (115)
28. 🇦🇴 Angola (117)
29. 🇹🇬 Togo (118)
30. 🇰🇲 Comoros (119)
31. 🇱🇾 Libya (120)
32. 🇹🇿 Tanzania (121)
33. 🇲🇼 Malawi (123)
34. 🇿🇼 Zimbabwe (124)
35. 🇬🇲 Gambia (126)
36. 🇸🇱 Sierra Leone (127)
37. 🇸🇩 Sudan (128)
38. 🇳🇪 Niger (129)
39. 🇨🇫 Central Africa (131)
40. 🇷🇼 Rwanda (133)
41. 🇧🇮 Burundi (139)
42. 🇪🇹 Ethiopia (144)
43. 🇧🇼 Botswana (145)
44. 🇱🇸 Lesotho (148)
45. 🇸🇿 Eswatini (149)
46. 🇱🇷 Liberia (153)
47. 🇸🇸 Sudan Kusini (166)
48. 🇲🇺 Mauritius (177)
49. 🇹🇩 Chad (181)
50. 🇸🇹 Sao Tome and Principe (191)
51. 🇩🇯 Djibouti (192)
52. 🇸🇴 Somalia (198)
53. 🇸🇨 Seychelles (199)
Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥
