E-PLUS MEDIA
Kanalga Telegram’da o‘tish
Get the latest news,videos,and more everyday.
Ko'proq ko'rsatish1 307
Obunachilar
+124 soatlar
-27 kun
-1330 kun
Postlar arxiv
1 307
***Mbali na Gari kuvuka kwa mapozi kwenye kidaraja cha kamba pamoja na kupaa kama chopper ni uongo gani mwingine wakina Vin Diesel (Van Diesel) wametufunga Kamba?***
1 307
Katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki usiku wa jana Jumatatu (Ankaragucu vs Rizespor) kulizuka fujo na mwamuzi wa mechi hiyo alipigwa ngumi na Rais wa timu moja kabla ya kupigwa teke la uso akiwa amelala chini.
Rais wa Ankaragucu, Faruk Koca, alimpiga mwamuzi, Halil Umut Meler, ngumi ya uso baada ya klabu ya Rizespor kufunga bao la kusawazisha dakika ya 90+7'.
Koca aliingia uwanjani na kumpiga ngumi hiyo wakati mwamuzi akipuliza filimbi ya mwisho, kuashiria mchezo huo umemalizika kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Eryaman.
Ligi ya Uturuki imesimamishwa kufuatia tukio hilo. Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, Meler na Koca walipelekwa hospitalini, huku Koca akiwa chini ya ulinzi na anatarajiwa kuzuiliwa baada ya kufuatia matibabu.
Meler alionyesha kadi nyekundu Wachezaji wawili (mchezaji mmoja) kila upande kabla ya Adolfo Gaich kuisawazishia bao klabu ya Rizespor.
Tukio hilo lilifikia haraka hadi kwa rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, ambaye alinukuliwa akilaani shambulio hilo. "Ninalaani shambulio dhidi ya mwamuzi Halil Umut Meler baada ya mechi, namwombea na ninamtakia ahueni" Erdoğan alisema.
“Michezo ina maana ya amani na udugu. Michezo haiendani na vurugu. Kamwe hatutaruhusu vurugu kutokea katika michezo ya Uturuki.” Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF), Mehmet Buyukeksi, baadaye alithibitisha kwamba Ligi Kuu “iliahirishwa kwa muda usiojulikana” kufuatia tukio hilo la vurugu.
Meler mwenye umri wa miaka 37 yuko kwenye orodha ya waamuzi wa UEFA na amewahi kuchezesha Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, na pia aliwahi kuchezesha mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Conference League kati ya West Ham dhidi ya AZ Alkmaar msimu uliopita.
Rizespor ilionyesha kuunga mkono mwamuzi huyo katika taarifa yake, ikisema: “Tunalaani vikali matukio yasiyofaa yaliyotokea baada ya mechi ya Ankaragucu"
Kwa upande wa Ankaragucu imesema kuwa imehuzunishwa na tukio hilo na kuomba radhi "Tumehuzunishwa na tukio lililotokea. Tunaomba radhi".
1 307
Staa wa nyimbo ya All My Life Rapa #LilDurk anaendelea kuweka wazi juu ya Imani yake ya Kiislamu huku akisema kuwa kwa sasa yeye sio Mwanachama wa Genge lolote la kihuni.
Katika siku za hivi karibuni Rapa huyo ameonyesha mabadiliko makubwa katika maisha yake ya kila siku, katika profile yake ya Instagram ameandika "Almost healed it's scary when I heal🤲"
Kwa tafsiri ya kiswahili ikimaanisha "Karibu nipone na inatisha zaidi ninapopona🤲"
Nini maoni yako?
1 307
#BURUDANI Jada Pinkett ameibuka upya kusema kofi alilopigwa mchekeshaji Chris Rock na mume wake Will Smith siku ya tuzo za ‘Oscars’ mwaka jana liliokoa ndoa yake kwa sababu baada ya kofi hilo mambo mengi chanya yaliendelea.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ Jada Pinkett anasema “Sikuhudhuria tuzo za Oscar mwaka huo lakini ninafurahi. Naliita ‘kofi takatifu’ kwa sababu mambo mengi mazuri yalikuja baada yake.”
Jada Pinkett ameongeza kusema alikuwa anafikiria kuondoka upande wa Will Smith lakini baada ya kofi hilo likamfanya asiwaze kuachana naye kamwe.
Tukio gani limewahi kuokoa mahusiano yako?
1 307
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limetoa ufafanuzi juu ya taarifa za Mwanamke mmoja wa miaka 40 Mkazi wa Kazegunga ambaye anadaiwa kuonekana November mwaka huu baada ya kufariki October 17,2018 wakati akijifungua Mtoto katika Hospitali ya Baptist iliyopo Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji na kuzikwa Kazegunga alipokua kaiishi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Filemon Makungu amesema kuna matukio mawili ya Watu ambao wameonekana wakiwa hai ingawa Familia wamesema walifariki “Matukio haya tumeyafatilia yote na inatakiwa kuthibitisha kisayansi tumeshapeleka vipimo kwa Mkemia Mkuu bado hatujaletewa majibu tukiletewa tutatoa maelezo yaliyokamilika lakini kwa matukio haya mawili bado upelelezi tunaendelea nao kujua kwa kina zaidi ili kujua ukweli wa yule aliyefariki na huyu aliyeokotwa akiwa hai”
Mwezi November mwaka huu Familia ilisema Mpendwa wao huyo alionekana katika eneo la Ilagala Wilayani Uvinza ambapo miezi 11 iliyopita tukio kama hili la Mtu kufariki kisha kuzikwa na kuonekana tena lilitokea Kijiji cha Kandaga Wilayani UVinza Mkoani Kigoma ambapo pia mazingira yake yanahusishwa na imani za kishirikina kutumika kupoteza Watu na kuonekana tena baada ya muda mrefu kupita.
AyoTV mpaka sasa imeshawahi kuripoti matukio matano kama haya ya kusemekana Mtu amefariki na kuzikwa na baadaye Ndugu kudai wamemuona tena Ndugu yako akiwa hai, matukio hayo yametokwa mwaka 2018 Kasulu, mwaka 2020 Kasulu, mwaka 2021 Kasulu, mwaka 2022 Uvinza na mwaka 2023 Kigoma DC. #MillardAyoUPDATES
1 307
MPENZI WANGU HATAKI NIMPE PESA, NIKIMPA ANAKASIRIKA KAMA AMENIFUMANIA.
"Kitu ambacho kinanishangaza kwa mpenzi wangu, yeye hataki nimpe pesa, kuna kipindi nilimpa laki mbili ili imsaidie kwenye shughuli zake alikasirika sana utadhani amenifumania nikichati na wanawake wengine. Alikasirika kiasi kwamba niliwaita ndugu zake wakaja kusuruhisha ugomvi wetu"- amesema mwanaume huyo pichani.
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/yÿbÿ
1 307
TANZIA:Mwanamuziki wa Afrika Kusini, Bulelwa Mkutukana maarufu kama Zahara, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 34.
Zahara amefia Hospitalini Jijini Johannesburg alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya ini yaliyoanza kumsumbua wiki mbili zilizopita.
Kabla ya kifo chake, amekua akizushiwa kifo mtandaoni hivi karibuni hadi kulazimu familia yake kukanusha mara kwa mara na kutaka Watu wamuombee mema.
Nyota huyo aliyewahi kutamba na vibao kadhaa kama 'Loliwe' na 'Destiny', na mshindi wa Tuzo kadhaa za Muziki nchini humo.
1 307
⚠️ Unakubaliana na polisi huyo kuhusu hili la malezi au ?
Anaitwa Bright ni polisi wa Nigeria, ameibuka mtandaoni kusema kwamba miongoni mwa makosa makubwa yanayofanywa na wazazi na jamii kwa ujumla katika malezi ni kuwapa sana uhuru watoto wa kiume huku wakiwabana sana watoto wa kike na matokeo yake watoto wa kiume ndio kugeuka kuwa tishio kwa watoto wa kike na kusababisha hata mafundisho ya wazazi na walezi wanayoyatoa mara kwa mara kwa watoto wa kike kwa muda mrefu kuishia kuwa kazi bure
Katika kukazia point yake ametolea mfano kwamba unakuta watoto wa kike wenye umri mdogo chini ya miaka 18 wapo kwenye mahoteli au nyumba za wageni lakini ukifuatilia kwa kina waliowaita huko ni vijana wa kiume ambao nao wengine unakuta hata bado kufikisha miaka 18, ila wanawaita ili wafanye "upumbavu"
Anasema mafundisho ya kimalezi na kiuhuru yasiwe ya kiubaguzi kwa watoto kuepuka wimbi kubwa la athari linalowakumba watoto wa kike ambalo husababishwa na uhuru mkubwa wanaopewa watoto wa kiume na kukua nao wakidhani kitu flani kukifanya ni sahihi hata kama sio sahihi sababu hawakumbushwi sana kimalezi kama watoto wa kike
1 307
⚠️ Kujifungua mtoto mwenye kilo 4 au zaidi sio afya ni tatizo hilo - Professor Janabi
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkurugenzi wa hospitali ya taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema wajawazito wanaojifungua watoto wanene wasidhani watoto wao wana afya njema
"Pale wodini unakuta mtu amejifungua mtoto ana Kilo 4, ndugu wanasema mashallah, hapo hakuna mashallah, mtoto ni over weight huyo, si jambo la kufurahia ni tatizo hilo. Si sahihi kwa mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mkubwa kupita kiasi"
Ameongeza kuwa unene uliopitiliza kwa mtoto unamuweka hatarini kuja kupata magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya figo, moyo, shinikizo la juu la damu pamoja na kisukari anachoweza kupata kutoka kwa mama
Aidha, ameshauri wajawazito kuzingatia ulaji mzuri wa vyakula kwasababu una athari za moja kwa moja kwa mtoto atakayezaliwa
1 307
⚠️😭 Nisher aliyekuwa director wa videos zikiwemo za Bongofleva afariki dunia. Inadaiwa alijijeruhi wiki kadhaa zilizopita akawa amelazwa hospitali na kifo kumchukua hatimaye
Nisher ameelezwa ni mtoto wa kwanza wa GeorDavie nabii maarufu jijini Arusha
1 307
⚠️😳 Makampuni 18 yaripotiwa kusitisha uhusiano wa kikazi/kibiashara na Diddy, ni baada ya wanawake 4 kujitokeza kufungua kesi za kueleza kudai kupitia unyanyasaji wa kingono mikononi mwa Diddy kwa miaka tofauti. Kufuatia tuhuma hizo Diddy pia imemlazimu kuachia ngazi kama mwenyekiti wa Revolt
Kati ya 4 waliojitokeza wawili wamesema walikuwa wanafunzi wakati walipokumbana na unyanyasaji husika, mmoja alisema alifanyiwa unyanyasaji wa kingono 1991 akiwa mwanafunzi wa chuo na na mwanamke mwingine amesema alifanyiwa 2003 akiwa na miaka 17 kwa wakati huo akiwa mwanafunzi wa high school alipandishwa ndege binafsi na watu karibu na Diddy baadaye wakaenda kuonana na Diddy yakatokea yaliyotokea
Wote wamesema kabla walilazimishwa madawa ya kulevya miilini mwao na Diddy na watu wake wa karibu na kudai vitendo husika vya kingono vilitokea katika nyumba yenye studios za Diddy na kudai kurekodiwa vikiendelea.
Mwanamke wa nne ametuma mahakamani picha zake akiwa studio kwa Diddy 2003 nyingine akionekana yupo mapajani mwa Diddy, mwanamke husika amezibwa sura kwa sababu maalum[za kiusalama]
Mmoja wa watu wa karibu na Diddy aliyetajwa na mwanamke wa 4 kuhusika na unyanyasaji yeye mwezi uliopita alitajwa katika kesi nyingine ya unyanyasaji kabla ya kuhusishwa na Diddy na mwanamke mwingine
Awali, mwanadada Cassie aliyekuwa mpenzi wa Diddy kwa miaka 10 alifungua kesi ya kudai kunyanyaswa kingono na Diddy na kueleza kulazimishwa kutumia madawa ya kulevya wakati akifanyiwa vitendo husika alivyodai kuambataba na vipigo na kunyimwa uhuru hata wa maisha yake binafsi
Diddy alitajwa kukimbilia kukaa meza moja na Cassie waliyamalize haraka, ambapo ilidaiwa awali Cassie alitaka $30 million akae kimya na asiendike kitabu kuhusu maisha yao ya kimapenzi. Mwanasheria wa Cassie alikana na kudai upande wa Didddy ndio walitaka kumpa Cassie pesa ili akae kimya. Lakini hata hivyo, ni kama haijasaidia kuyamaliza mapema na Cassie kwani wanawake wengine wamejitokeza kudai kupitia unyanysaji wa kingono
Diddy ambaye pia kwa miaka mingi anadaiwa kuhusika na kifo cha Tupac, amekana tuhuma hizo kwa kudai zina lengo la la kumchafua na kueleza kuwa wanawake husika wanataka kulipwa pesa, ingawa baadhi ya watu maarufu akiwemo ex wa Diddy walionekana kumuunga mkono Cassie kwamba kuna nyakati alikuwa anaonekana na majeraha kipindi alipokuwa katika mahusiano na Diddy
1 307
UNASUBIRI NINI CHAT NA MAFANS KIBAO WANAOSUPPORT MPIRA KUHUSU MPIRA KWA KUJIUNGA HAPA KWENYE LINK:-https://t.me/joinchat/QZcUBeMotA8wMmNk
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
