قال الإمام السعدي رحمه الله تعالى ؛
يقول تعالى لنبيه صلى الله عليه وسلم: ﴿وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا﴾؛ أي: علمناه كتاب الله، فصار العالم الكبير والحبر النحرير، ﴿فَانْسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ﴾؛ أي: انسلخ من الاتصاف الحقيقي بالعلم بآيات الله، فإن العلم بذلك يصير صاحبه متصفًا بمكارم الأخلاق ومحاسن الأعمال، ويرقى إلى أعلى الدرجات وأرفع المقامات، فترك هذا كتاب الله وراء ظهره، ونبذ الأخلاق التي يأمر بها الكتاب، وخلعها كما يخلع اللباس. فلما انسلخ منها أتبعه الشيطان، أي: تسلط عليه حين خرج من الحصن الحصين، وصار إلى أسفل سافلين، فأزه إلى المعاصي أزًّا، ﴿فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ﴾ بعد أن كان من الراشدين المرشدين.
Allàh Mtukufu anawambia Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Na wasomee kisa cha yule tuliye mpa Aya zetu. Yaani: Tulimfundisha Kitabu cha Allāh, akawa mwanachuoni mkubwa na mtaalamu bora, “Basi akajitenga nazo, na Shetani akamfuata. Yaani: Alijivua kutokana na sifa ya kweli ya elimu ya Ayah za Allāh, kwani kwa elimu hiyo, mwenye kuwa nayo anakuwa na sifa ya tabia njema na matendo mema, na ananyanyuliwa kwenye daraja za juu na vyeo vya juu zaidi. Hivyo mtu huyu akakiwacha Kitabu cha Allàh nyuma yake, na akakataa (kusifika na )tabia ambazo Kitabu kiliamuru, na akajalia kama vile mtu anavyovua nguo. Alipojitenga nacho, Shet'ani akamfuata, yaani, akamdhibiti, alipotoka kwenye ngome mathubuti, na akawa chini ya walio chini, (shetani)akamwingiza kwenye madhambi moja kwa moja, "basi akawa miongoni mwa wapotovu." baada ya kuwa miongoni mwa walioongoka.
: ﴿وَلَوۡ شِئۡنَا لَرَفَعۡنَـٰهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُۥۤ أَخۡلَدَ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُۚ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلۡكَلۡبِ إِن تَحۡمِلۡ عَلَیۡهِ یَلۡهَثۡ أَوۡ تَتۡرُكۡهُ یَلۡهَثۚ ذَّ ٰلِكَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِینَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔایَـٰتِنَاۚ فَٱقۡصُصِ ٱلۡقَصَصَ لَعَلَّهُمۡ یَتَفَكَّرُونَ ﴾
Na tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Aayat, lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata matamanio yake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimfukuza hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua na kutoa ulimi. Huo ni mfano wa watu wanao zikanusha aayah zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.
[Surah Al-Aʿrāf: 176]
: قال الإمام السعدي رحمه الله عند تفسير هذه الآية
﴿وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا﴾ بأن نوفقه للعمل بها، فيرتفع في الدنيا والآخرة، فيتحصن من أعدائه؛ ﴿وَلَكِنَّهُ﴾ فعل ما يقتضي الخذلان، فـ﴿أَخْلَدَ إِلَى الأرْضِ﴾؛ أي: إلى الشهوات السفلية والمقاصد الدنيوية، ﴿وَاتَّبَعَ هَوَاهُ﴾ وترك طاعة مولاه،
“Na lau tungeli penda tungelimuinua kwa hio(elimu)” kwa kumjaalia taufiq kufanyia kazi elimu hiyo, ili apate kunyanyuliwa duniani na akhera, na alindwe kutokana na maadui zake. “Lakini yeye” alifanya kile kilichompelekea kufedheheshwa, “akakwamia kwenye ulimwengu”; Yaani: akachagua matamanio ya chini na malengo yalio duni, “Na akafuata matamanio yake” na akaacha kumtii Mola wake.
https://whatsapp.com/channel/0029VaXcb2HDDmFLw8VTxn1Q