uk
Feedback

Не попадись на ботовода! Telemetrio знаходить і позначає такі канали мітками 👉 Хочеш бачити мітку, оформляй підписку

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Відкрити в Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

Показати більше
1 307
Підписники
+124 години
-27 днів
-1330 днів
Архів дописів
"Watu wengi sana wananiuliza mbona hupost kazi zako za u-mc Instagram? Nimepelekwa polisi mara mbili kwa sababu ya kupost kazi nilizosherehesha. Moja tulienda kwenye send-off bibi harusi kwenye kunogesha katika kuonyesha pingu za maisha wakati anaenda kumchukua Bwana Harusi kwenye kiti alikuja na pingu kabisa katika hali ya kunogesha akamfunga mume wake akajifunga na yeye wanaenda kuchukua chakula wote sisi tukaona ni content tukachukua tukapandisha hewani. Comment zilikuwa mbaya na wenyewe wakaipata wakaniomba nishushe ila imeshaenda mbali wakashtaki tukapelekana polisi nikaonekana sina makosa sana. Nyingine tulienda kwenye harusi tukasherehesha nikapost kazi ya leo kama kawaida kumbe Bwana Harusi kimeo ana mke mwingine, mke kaamsha huko, picha umeona wapi kwa Samsasali na kumbe alishakubaliana na mpiga picha wake kuwa hakuna kutoa picha hata moja" - @dr.samsasali

photo content

"Mtoto huyu nimemuuguza kwa muda mrefu na katika maisha yangu sikutegemea nitakuwa na mtoto kama hivi anavuta unga na nini ma
"Mtoto huyu nimemuuguza kwa muda mrefu na katika maisha yangu sikutegemea nitakuwa na mtoto kama hivi anavuta unga na nini maana kama ni kusaidiwa amesaidiwa na watu kibao. Kusikia mwanao kabebwa huku, kabebwa kule mtu hutegemei unaipata tu. Kijana alikuwa mzuri, anaimba vizuri, anafanya kazi vizuri hata Mhe. Mwigulu Nchemba alikuja hapa tukakaa hapahapa kwa ajili ya Chid" - Mama wa Msanii wa Bongo Fleva Chid Benz. cc CloudsTv

"Mimi mwenyewe nilikuwa naumia, hii hali niliyonayo unayoiona ilikuwa si hali yangu mimi ni mnene nakupita wewe hapo lakini s
"Mimi mwenyewe nilikuwa naumia, hii hali niliyonayo unayoiona ilikuwa si hali yangu mimi ni mnene nakupita wewe hapo lakini sasa matatizo ambayo nimepitia kwa Chid yalikuwa mtihani mkubwa kwa kweli." - Mama wa Msanii wa Bongo Fleva Chid Benz. Cc CLOUDS MEDIA.

Mchezo wa Ligi Kuu Uhispania kati ya wenyeji Granada dhidi ya Athletic Bilbao umelazimika kuahirishwa baada ya kifo cha shabi
Mchezo wa Ligi Kuu Uhispania kati ya wenyeji Granada dhidi ya Athletic Bilbao umelazimika kuahirishwa baada ya kifo cha shabiki wa Granada katika dimba la Nuevo los Cármenes. Athletic walitangulia kupata bao la mapema kupitia kwa Inaki Williams, kabla ya mchezo kusimamishwa baada ya takriban dakika 15 pale Mwamuzi alipoarifiwa kuhusu tatizo jukwaani. Wakati shabiki huyo akiendelea kupatiwa matibabu wachezaji walitolewa nje ya uwanja lakini baadaye LaLiga ilithibitisha kuwa shabiki huyo amefariki na mechi itapangwa tena siku za usoni. Taarifa ya klabu ya Athletic Bilbao imesema “LaLiga na vilabu vyote viwili vimekubali kusitisha mechi kutokana na kifo cha shabiki dimbani Los Carmenes. “Klabu ya Athletic inatoa rambirambi zake za dhati. Mawazo yetu yapo kwa familia ya mtu huyo na wapendwa wake.”

Kutokana na kusambaa kwa taarifa za uzushi kumhusu Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango katika mitandao ya kijamii, Waziri wa H
Kutokana na kusambaa kwa taarifa za uzushi kumhusu Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango katika mitandao ya kijamii, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amevielekeza vyombo vinavyohusika kuchua hatua za kisheria kutokomeza matumizi mabaya ya mitandao. Waziri Nape amesema uhuru wowote unapoingilia uhuru wa mwingine ni uvunjaji wa sheria, hivyo Serikali haiwezi kulivumilia hilo.

"Wapo watu waliokuwa wanakuja kumchukua Chid kumpeleka sehemu za matibabu mimi nakuwa naenda kumtizama. Ila yeye anachotaka n
"Wapo watu waliokuwa wanakuja kumchukua Chid kumpeleka sehemu za matibabu mimi nakuwa naenda kumtizama. Ila yeye anachotaka ni kuwa na kazi akae mahali pazuri, aendeshe gari ndio hicho yeye anakihitaji ndio maana akifikishwa pale akakaa anaona mbona mimi ni mzima labda kuna kitu fulani tu hapati" - Mama wa Msanii wa Bongo Fleva Chid Benz. CC. CLOUDS MEDIA.

Msanii Chid Benz amesema ameona mitandaoni andiko la Haji Manara kuwa anataka kumsaidia kutokana na video iliyosambaa ikimuon
Msanii Chid Benz amesema ameona mitandaoni andiko la Haji Manara kuwa anataka kumsaidia kutokana na video iliyosambaa ikimuonesha anaomba omba pesa kwa marafiki zake kijiweni. Chid amesema kama kweli Manara alitaka kumsaidia na sio kutafuta kiki basi angetafuta namba zake kwanza awasiliane nae na kutimiza dhamira yake kwani uwezo wa kupata namba yake anao.

"Kutoa nyimbo maana yake pesa, huko wanakoweka nyimbo Mirabaha sijui boomplay yule Bwana analalamika hapati pesa sielewi kwan
"Kutoa nyimbo maana yake pesa, huko wanakoweka nyimbo Mirabaha sijui boomplay yule Bwana analalamika hapati pesa sielewi kwanini au nini kimetokea. Kwa sababu hiyo pesa ndiyo ingemsaidia kwenda kurekodi na ndio inakuwa hivyo hapati pesa." - Mama wa Msanii wa Bongo Fleva Chid Benz. Cc CloudsTV

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini kuhakikisha suala la kukatika kwa umeme linashughulikiwa kikamilifu na hakuna hujuma yoyote kama ambavyo inasemekana. Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo wakati akijibu swali ya Mwananchi wa Kijiji cha Masimba, Kata ya Tongwe Wilayani Muheza kuhusu kukatika kwa umeme huo Kijijini hapo “Ninakubaliana na yeye kuwa umeme unakatika kwa kuwa tunapitia kipindi cha mgao wa umeme lakini niwahakikishie Ndugu zangu Mheshimiwa Rais alitupa miezi sita kuhakikisha tunaondoa mgao wa umeme” “Tupo kazini na kwa mipango ambayo tunayo tunategemea ndani ya miezi sita hiyo tutakuwa tumeshaondoa mgao wa umeme, miezi sita inaisha mwezi wa tatu 2024, mpaka kufikia hapo na kwa mipango iliyopo miradi ambayo Mheshimiwa Rais ametupatia fedha tunatekeleza tunategemea tutaondoka kabisa kwenye mgao wa umeme” “Kwa kipindi hiki mvua zinanyesha, maeneo kwa maeneo, maeneo ambayo tunafanya uzalishaji wa umeme kule kwenye mabwawa yetu ya umeme Kidatu, Kihansu na Mtera ndio mvua zimeanza kwahiyo tunategemea kadiri mvua zinavyoendelea kunyesha, maji yanavyoendelea kujaa tutakuwa tumepunguza tatizo kwa kiasi kikubwa hivyo niwaondoe shaka, hakuna hujuma inayofanyika kama ambavyo inasemwa Watu wanauza majenereta, solar panel hapana, Serikali ipo kazini na tunaangaliza jicho kwelikweli

photo content

Bunge SC -Soka maarufu kama Tulia Boys wameendelea kung’ara katika Michezo ya 13 ya Mabunge ya Afrika Mashariki hapa Kigali Rwanda baada ya kuwalaza Sudan Kusini mabao 2-1 katika mchezo mkali na wenye matumizi makubwa ya nguvu. Haikuwa kazi rahis kwa Bunge SC -Soka hasa kutokana na kukabiliana na wachezaji warefu na wenye miili mikubwa na ambao kwao Matumizi ya nguvu ndo kila kitu . Pamoja na matumizi ya nguvu ya wapinzani, Bunge SC ilienda mapumziko ikiongoza kwa bao lililofungwa na Festo Sanga Senator (Makete) kufuatia pasi ya Nahodha Cosato Chumi (Mafinga Mjini). Mlinda mlango wa Bunge SC Abubakar Asenga (Ifakara) aliibuka shujaa kufuatia kucheza kwa uhodari mkubwa penati waliyopata Sudan Kusini. Kipindi Cha pili Sudan walisawazisha kufuatia mpira wa adhabu iliopigwa na Lomolo George. Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika Simai Hassan ( Nungwi) aliitendea haki pasi mpenyezo ya Jafary Chege ( Rorya) na kuipatia Bunge bao la pili na la Ushindi. Kwa Ushindi huo, Bunge inaendelea kukaa kileleni ikiwa na point sita, magoli sita ya kufunga na kufungwa magoli mawili.

photo content

"Chid tangu akiwa mdogo alikuwa anaimba imba. Hakuwa anasikiliza sana mziki ila akishika karatasi anaandika na anatoa wimbo.
"Chid tangu akiwa mdogo alikuwa anaimba imba. Hakuwa anasikiliza sana mziki ila akishika karatasi anaandika na anatoa wimbo. Na ameanza kuimba akiwa form one. Primary alisoma Boma, Sekondari nikampeleka Mgulani tukaona kama kuimbaimba kunazidi nikampeleka nyumbani Mafinga akaenda Mafinga Sekondari" - Mama wa Msanii wa Bongo Fleva Chid Benz. Cc CLOUDS MEDIA.

"Baba mzazi wa Chid alikuwa meneja wa Shirika la Nyumba pale Ilala. Sasa mimi nilikuwa naenda kuulizia nyumba katika kwenda p
"Baba mzazi wa Chid alikuwa meneja wa Shirika la Nyumba pale Ilala. Sasa mimi nilikuwa naenda kuulizia nyumba katika kwenda pale tukakutana, tukapendana akanioa" - Mama wa Msanii wa Bongo Fleva Chid Benz. Cc CloudsTv

"Rashid (ChidBenzi) alizaliwa tarehe 28.4.1985 akiwa na kilo 3.5 na wakati wa kujifungua nilienda nyumbani kwetu Iringa. Nili
"Rashid (ChidBenzi) alizaliwa tarehe 28.4.1985 akiwa na kilo 3.5 na wakati wa kujifungua nilienda nyumbani kwetu Iringa. Nilikuwa na furaha sana kupata mtoto wa kiume. Nilitaka asome mpaka amalize halafu baadae itajulikana nini MUNGU amemjalia kupata" - Mama wa Msanii wa Bongo Fleva Chid Benz. Cc CloudsTv

#BURUDANI: Msanii kutokea nchini Marekani Johnathan Jamall Porter anafahamika zaidi kama ''Blueface'' kupitia akaunti yake ya
#BURUDANI: Msanii kutokea nchini Marekani Johnathan Jamall Porter anafahamika zaidi kama ''Blueface'' kupitia akaunti yake ya mtandao ''X'' ameweka chapisho akieleza hisia zake mara baada ya kufanya vipimo vya damu kwa siri na kubaini mtoto aliyenaye siyo wake. Kwenye chapisho lingine Blueface alieleza hisia zake kwa kusema kwa sasa hana furaha, hawezi kujifanya kwa yuko sawa. Tunarudisha swali kwako, utafanyaje ukigundua mtoto uliyemlea siyo wako?

Dar Lux Waliishiaga Wapi Hawa Jamaa Walitamba Sana MIAKA Ya 2019
+2
Dar Lux Waliishiaga Wapi Hawa Jamaa Walitamba Sana MIAKA Ya 2019

SOMA KISHA UTUAMBIE NAULI YA KUTOKA DAR KWENDA MKOANI KWENU SHINGAPI?? DAR TO ARUSHA TSH 44000 DAR TO BUKOBA TSH 97000 DAR TO
SOMA KISHA UTUAMBIE NAULI YA KUTOKA DAR KWENDA MKOANI KWENU SHINGAPI?? DAR TO ARUSHA TSH 44000 DAR TO BUKOBA TSH 97000 DAR TO DODOMA TSH 31000 DAR TO IRINGA TSH 33000 DAR TO KIGOMA TSH 101000 DAR TO LINDI TSH 32000 DAR TO MBEYA TSH 56000 DAR TO MOROGORO TSH 13000 DAR TO MOSHI TSH 37000 DAR TO MTWARA TSH 39000 DAR TO MUSOMA TSH 92000 DAR TO MWANZA TSH 78000 DAR TO SHINYANGA TSH 67000 DAR TO SINGIDA TSH 46000 DAR TO SONGEA TSH 73000 DAR TO SUMBAWANGA TSH 95000 DAR TO TABORA TSH 68000 DAR TO TANGA TAH 23000 DAR TO MPANDA TSH 79000 DAR TO GEITA TSH 83000 DAR TO NJOMBE TSH 48000 DAR TO BABATI TSH 55000 DAR TO BARIAD TSH 67000 DAR TO KAHAMA TSH 68000

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Paul Clement siku ya leo akiwa katika kipindi cha #Gospeltraxx cha Clouds FM akijibu swa
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Paul Clement siku ya leo akiwa katika kipindi cha #Gospeltraxx cha Clouds FM akijibu swali la Mtangazaji lililomtaka aeleze ni lini na yeye atamua kuingia katika huduma ya uchungaji kama Waimbaji wengi wa nyimbo za injili wanavyofanya, Paul Clement alisema👇. "Mimi hapa nilipo ni Mchungaji tayari, na kanisa ninalo tayari. Kanisa ni Watu. Jengo ni issue nyingine, Lakini hapa tayari Mimi ni Mchungaji namtumikia Mungu, nina Washirika Dunia nzima ambao ninawahubiria injili" alieleza @ministerpaulclement