E-PLUS MEDIA
Відкрити в Telegram
1 307
Підписники
+124 години
-27 днів
-1330 днів
Архів дописів
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
1 307
"Sisi wanaume tupo tayari hata kulamba pasi ya umeme lakini sio kumchiti mwanamke tunayempenda"- Hajji Manara
1 307
⚠️😳😢 Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un aangua kilio na kujifuta machozi mbele ya maelfu ya kinamama akiwaomba waweke juhudi kwenye kuzaa kuongeza watoto ili kuikabili changamoto kubwa ya idadi ndogo mno ya watoto wanaozaliwa nchini humo miaka ya karibuni
Kilio hicho alikiangua tarehe 3 December hii katika mkutano wa taifa wa kinamama ikiwa ni miaka 11 imepita tangu ufanyike tena, ambapo akihutubia kwa kusema "dear mothers" amewaomba kinamama waongeze kasi ya kuzaa pia amewataka kinamama wawafundishe watoto wao itikadi za chama chake cha kikomunisti
Baadhi ya kinamama nao wameonekana wakiangua vilio katika mkutano huo
Kwa mujibu wa taarifa, sensa ya mwisho ya watu na makazi nchini Korea Kaskazini iliyofanyika mwaka 2008 inaonesha nchi hiyo ilikuwa na watu milioni 24 wanaoishi nchini humo lakini kwasasa inakadiriwa nchini hiyo ina watu milioni 25.7 wanaoishi nchini humo
1 307
⚠️ Baada ya Mange kuibua unyanyasaji wa kingono/kijinsia na utapeli unaofanywa na Kesha kwa wanawake kupitia saluni yake ya kuongeza shepu na kupunguza tumbo kisha wahanga kuibuka kutoa shuhuda mbalimbali za kunyanyaswa, Ebitoke anayedaiwa kuwa mama mtoto wa Kesha aibuka kufunguka
1 307
"Tumeongea na Mchungaji mmoja amesema kanisa lake limepotea eneo lilipokuwa halikuwepo alivyoamka siku ya Jumapili. Na tukio hili limetokea siku ya Jumapili iliyopita Saa 11 Alfajiri. Watu walikuwa wamelala
"Wananchi walisema walisikia kelele kubwa kama treni inapita ule mwanguko wa matope na mawe ulivyokuwa unaelekea kwenye makazi ya watu. Baadhi ya ndugu zetu siku hiyo hata hawakujua kilichowaua walikuwa bado wamelala" Mobhare Matinyi, Msemaji Mkuu Wa Serikali.
1 307
Fedha zikiwa zimeungua ndani ya duka baada ya moto ambao chanzo chake hakijafahamika kuteketeza maduka zaidi ya 20 eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Moto huo unatajwa kuunguza maduka hayo usiku wa kuamkia leo Desemba 5, 2023.
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi kwa taarifa zaidi.
1 307
KUNA WATU WANAZUSHIA WATU VIFO, WAMEMZUSHIA WAZIRI AMEWASAMEHE.
-
"Imefika wakati Watanzania wamekuwa wakisambaza Taarifa za uongo kuwazushia Watu vifo, Hii Ni mbaya Sana na Mungu hapendezwi na Tabia ya kusema Uongo" JPM
_
"Wapo Watanzania wametangaza kwamba Waziri wa Fedha Fillipe Mpango amefariki.. Watanzania ni kweli waziri Amelazwa Hospitali na hajafariki Kama Watu wanavyozusha yupo hai na kwa sasa anaendekea vizuri kiafya" JPM
_
"Alishtushwa Sana kuona Taarifa kwamba yeye amekufa na kuniandikia meseji niisome kwa Watanzania naomba Baba Askofu niruhusu... Amesema.. "Kweli ninaumwa Lakini kwa Sasa naendelea vizuri na Wote walionizushia kwamba Mimi nimekufa Tayari nimemuomba Yesu awasamehe" JPM MAGUFULI
1 307
Moto ambao chanzo chake inasemekana ni hitilafu ya umeme, umeteketeza kiwanda cha mbao pamoja na samani katika eneo la Tanki Bovu kwa komba mkoani Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mmiliki wa kiwanda hicho, moto huo umesababisha hasara ya shilingi milioni 30.
1 307
Sisi ni akina nani hata tushindwe kusema Asante Mungu kwa uhai huu usio na gharama hata ya sent tano?. Ama kwa hakika huu mwisho wa mwaka unatisha, haipiti siku bila vifo vya ajali na matukio mengine ya ajabu.
Mpaka sasa Takwimu zinaonyesha ni watu 63 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyotokea huko Hanang mkoani Manyara, ni mafuriko ya ajabu ambayo hayakutarajiwa kama yangetokea Tanzania tena kwenye mkoa wa Manyara. Tulipe uzito suala hili hata kwenye maombi yetu maana hatujui kesho kitatokea nini kipya. Kwani bado kuna kijana anaona aibu kumtukuza Mungu hata kwenye kipindi hiki cha msululu wa matukio ya kutisha?
Basi tusione haya kusema na Muumba wetu, watu 63 sio idadi ndogo ndugu zangu? Kipindi hiki kinahitaji maombi angalau mioyo yetu iliyojaa hofu ipate kupumua, kipindi hiki ni kipindi cha Mungu kwanza mambo mengine baadae. Angalia leo hii watu wanakufa kwa mafuriko ya matope, mafuriko ambayo yametokea kimuujiza-ujiza hata Serikali bado inahaha kusaka chanzo hasa cha maafa haya, hamuoni kama lipo jambo Mungu anatukumbusha?
Basi usiku wa leo kwa pamoja tuungane kujiombea sisi, taifa letu, ndugu zetu waliotangulia mbele za haki, wanaopambania uhai wao mahospitalini/majumbani na hata wale ambao wamenusurika kwenye janga hili lakini wamepoteza kila kitu chao, Mungu awatie nguvu na walivyopoteza vipatikane mara dufu🙏.
1 307
#SikiaHii: Utafiti uliofanywa katika chuo kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani unaonyesha kuwa, kazi za ziada za nyumbani kwa wanafunzi "Homework" huwafanya kuwa maskini.
Utafiti huo umeongeza kwamba, hakuna mafungamano yoyote kwa mafanikio ya wanafunzi kimasomo na wao kupewa kazi za ziada za nyumbani.
Hapo vipi, ulipokuwa shule ulikuwa unamaliza "Homework" yako kwa wakati?
Millard Ayo presenter.
1 307
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, yuko nje ya nchi kikazi na kuwataka Watanzania kupuuza taarifa zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii.
Mhe. Majaliwa alisema hayo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ulioko Mji wa Serikali, Mtumba, wakati akizungumza na washiriki na wadau mbalimbali kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
#kabaheza
1 307
Rais wa Club ya Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vilabu vya soka Barani Afrika ( ACA ) Injinia Hersi said leo ametembelea eneo la mafuriko katika kijiji cha Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kutoa pole kwa Waathirika na kuwasilisha misaada.
Taarifa rasmi kwa Waandishi wa Habari imeeleza yafuatayo “ Kwa kuunga mkono wito wa Rais Samia kuelekeza misaada ya haraka Wilayani Hanang, kwa kuunga mkono pia jitihada za Watanzania mbalimbali katika kuwasaidia Waathirika, Club ya Yanga kwa kushirikiana na GSM Foundation tumechangia vitu vyenye thamani ya Tshs. 40,000,000 pamoja na kutoa fedha taslim shilingi milioni kumi (10,000,000) kupitia akaunti ya mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa”.
Msaada huo umepokewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga pamoja na Viongozi mbalimbali walioweka kambi Katesh kusaidia zoezi zima la uokozi.
1 307
Rais wa Young Africans SC na mwenyekiti wa vilabu vya soka barani afrika ( ACA ) Mhandisi Hersi said leo ametembelea eneo la mafuriko katika kijiji cha Katesh wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kutoa pole kwa waathirika wote wa mafuriko hayo.
Akiunga mkono wito wa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na kwa kushirikiana na GSM Foundation klabu yetu ilichangia vitu vyenye thamani ya Tshs. 40,000,000 pamoja na fedha taslim Tshs. 10,000,000 kupitia Akaunti ya Mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa.
Msaada huo ulipokewa na Mh. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akiambata na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Sendiga pamoja na viongozi mbalimbali walioko hapa Katesh kusaidia zoezi zina la uokozi.
#timuyawananchi
#daimambelenyumamwiko
1 307
Klabu ya Simba leo imekabidhi msaada kwa ajili ya wahanga wa mafuriko na maporomoko yalitokea katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara mwishoni mwa juma lililopita.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' amemkabidhi msaada huo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dr. Damas Ndumbaro ambaye ataepeleka kwa wahusika huko Hanang.
"Kwa niaba ya Rais wa heshima Mohamed Dewji, Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti wapenzi na Wanachama wa Simba tunapenda kutoa pole nyingi kwa wahanga wa mafuriko na maporomoko huko Hanang.
"Wengi wa wahanga hawa ni wapenzi wa soka na sisi kama klabu tunaungana nao kwenye kipindi hiki kigumu," amesema Try Again.
Akipokea msaada huo, Waziri Dk. Ndumbaro ameushukuru Uongozi wa klabu ya Simba kwa kuona umuhimu wa kuwachangia wenzetu wa Hanang huku akiwaomba wadau wengine kuguswa na kutoa kwa ajili ya wahanga.
"Kwa niaba ya Serikali tunaushukuru Simba kwa mchango huu mkubwa kwa ajili ya ndugu zetu wa Hanang waliopata matatizo huko Hanang, watafarijika sana wakiona msaada huu kutoka kwetu," amesema Dk. Ndumbaro.
Msaada tuliotoa ni unga, mchele, mafuta ya kupikia, sabuni maji ya kunywa ambayo tumejaza gari mbili.
Katika zoezi hilo la kukabidhi msaada huo limehidhuriwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Neema Msitha.
- simbasctanzania
