E-PLUS MEDIA
Відкрити в Telegram
1 307
Підписники
+124 години
-27 днів
-1330 днів
Архів дописів
1 307
⚠️😳 Mahakama yaamuru Asamoah Gyan(37) amlipe fidia aliyekuwa mke wake nyumba 2, moja ikiwa nchini Uingereza na nyingine ikiwa Accra, Ghana, pia ampe kituo kimoja cha biashara ya petrol na gari mbili. Ni baada ya vipimo vya DNA kubaini kweli yeye ndie baba halisi wa watoto 3 aliokuwa akiwatilia shaka kuwa sio wake kwa madai aliyekuwa mke wake alichepuka
Gyan ambaye kabla ya kustaafu soka mwaka huu aliwahi kuwa Captain wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya nchini Ghana kisha kuchezea klabu kadhaa ikiwemo Sunderland, yeye ndie alitaka ndoa yao waliofunga mwaka 2013 ivunjwe.
Nyumba ya Aacra, Ghana aliyopewa ex wake huyo imeelezwa ilinunuliwa kwa ajili yake kabla/walipokuwa wakielekea kufunga ndoa yao 2023
Pia mahakama imeamuru kila mwezi Asamoah atoe pesa za matumizi kwa ajili ya watoto wao watatu £1,729 ambazo sio chini ya shilingi milioni 5.2 za Kitanzania
Kwa mujibu wa taarifa, inadaiwa kwamba mahakama ilieleza kuwa mama watoto wake huyo kwa jina la Gifty hakuwa na mchango wa moja kwa moja wa kipesa katika mali za mume wake, isipokuwa ndie alikuwa muangalizi na mlezi wa watoto wao 3 na hivyo mwanasoka huyo kwa upande wake yeye kupata muda wa kutosha kuweza kujiimarisha na kutimiza ndoto zake katika ulimwengu wa soka na kuchanua kiuchumi wakati mkewe akiwa anakomaa kulea watoto wao
1 307
SAD NEWS!!
Klabu ya Wydad Casablanca 🇲🇦 imetangaza kufariki dunia kwa beki wake wa kushoto,Oussama Faloh ambapo kifo chake kilitokea hapo jana akiwa hospitalini akipatiwa matibabu.
Faloh aliyekuwa na Miaka 24 alisajiliwa na Wydad Casablanca 🇲🇦 dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea Klabu ya Angers inayoshiriki Ligi Kuu Nchini Ufaransa 🇨🇵 na wiki tatu zilizopita alipata ajari ya gari iliyompelekea kupararaizi kisha kupelekwa hospitali kabla ya mauti kumfika.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un 🙏🏿
1 307
YAANI KUNA AJALI NYINGINE HUWA ZINAFIKIRISHA SANA JINSI ZILIVYOTOKEA. Hii imetokwa leo katika kijiji cha Ihemi na kusababisha kifo cba Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Cc:
RSA Tanzania
1 307
“Ninaomba Msamaha kwa Mambo yote ambayo Wajerumani waliwatendea Mabibi na Mababu zenu hapa” Rais wa Ujerumani akiwa Kwenye Makumbusho ya Vita ya Majimaji.
1 307
Israel imeripotiwa kuendelea kutekeleza mashambulio ya anga katika ukanda wa Gaza, wakati huu idadi ya watu waliouawa katika eneo la Palestina ikiongezeka hadi 9,061.
Kwa upande mwengine, zaidi ya watu 1,400 wameuawa nchini Israel katika vita vinavyoendelea kati ya wapiganaji wa Hamas na jeshi la Israel.
1 307
Bolivia imekuwa nchi ya Kwanza kuvunja Uhusiano wa Kidiplomasia na Israel Ikifuatiwa na Colombia, sababu ni Matendo ya Israel huko Gaza. Chile nayo imemrudisha nyumbani balozi wake wa Israel. Mataifa haya yapo America ya Kusini na Idadi kubwa ya Raia wake ni Wakristu Wakatoliki.
1 307
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepinga vikali wazo la kusitisha mapigano Gaza, akilinganisha na kujisalimisha kwa Hamas.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa mapigano, alidai kuwa ustaarabu wenyewe uko hatarini. .‘Miito ya kusitishwa kwa mapigano ni wito kwa Israeli kujisalimisha kwa Hamas, kujisalimisha kwa ugaidi, kujisalimisha kwa unyama,’ Netanyahu alisema, na kuongeza ‘hilo halitafanyika.’ Pia alirejea ulinganisho kati ya mashambulizi ya Hamas na 9/11. ."Kama vile Marekani isingekubali kusitishwa kwa mapigano baada ya kulipuliwa kwa Bandari ya Pearl au baada ya shambulio la kigaidi la 9/11, Israel haitakubali kusitisha uhasama na Hamas baada ya mashambulizi ya kutisha ya Oktoba 7," alisema. .
.netanyahu alidai kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel lilikuwa likifanya jitihada za kuepusha maafa ya raia, licha ya waangalizi wa kimataifa kuikosoa Israel kwa kulenga miundombinu ya kiraia na kuwanyima vifaa muhimu. .alihalalisha hilo kwa kusema ‘hata vita vya haki zaidi vina vifo vya raia visivyokusudiwa.’ Pia alitoa uhalali wa jibu gumu la Israel kwa kusema, ‘ikiwa Hamas na mhimili wa uovu wa Iran utashinda, utakuwa shabaha yao ijayo.
1 307
Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier ameeleza kuona aibu kwa ukatili wa kikoloni ambao nchi yake iliifanya nchini Tanzania.
Majeshi ya Ujerumani yaliua takribani watu 300,000 wakati wa vita vya Majimaji, ambayo ni mojawapo ya vita kubwa dhidi ya ukoloni.
Rais Steinmeier ameyasema hayo wakati akizungumza mkoani Songea ilipotokea vita hiyo.
"Ninaomba msamaha kwa kile Wajerumani walichokifanya kwa mababu zenu mahali hapa"
"Kilichotokea hapa ni historia tunayoshea, historia ya mababu zenu na mababu zetu wa Ujerumani".
Vita ya majimaji ilitokana na sera ya Ujerumani iliyoundwa ili kuwalazimisha wazawa kulima pamba kwa ajili ya kuisafirisha kwenda nje.
Rais Steinmeier amesema atazipeleka hadithi hizi Ujerumani, ili watu wengi zaidi nchini mwake wazifahamu.
1 307
Hiki ni moja ya kikosi cha IDF ambacho kimefutwa leo baada ya kulipuliwa na bomu katika Daraja la Givati wakati wa operation ya uvamizi wa Gaza.
1 307
Yemen yatangaza vita dhidi ya Israel!!!!
‘Vikosi vyetu vilivyojihami vimerusha makombora ya balestiki na ya kusafiri, pamoja na idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani, dhidi ya shabaha mbalimbali nchini Israel. Tutaendelea kufanya mashambulizi hadi uvamizi wa Israel ukomeshwe, msemaji wa Jeshi la Yemen Yahya Sarie Anu.
1 307
HISTORIA YA MGOGORO KATI YA ISRAELI NA PALESTINA KATIKA MTAZAMO WA ASKOFU - I
Katika Kitabu chake kiitwacho 'Israel and the Nations' (1963), F. F. Bruce anaeleza kuwa rejea ya awali kabisa iliyo nje ya Biblia juu ya taifa la Israeli inapatikana katika maandishi yaliyoko katika mnara uliowekwa mwaka 1220 Kabla ya Kristo na Farao au Mfalme wa Misri, Merneptah alipokuwa akisherekea ushindi wa vita kadhaa baada ya kuziteka na kuzishinda nchi nyingi.
Baadhi ya majigambo yake ilikuwa ni kujivuna jinsi alivyozishinda nchi jirani ikiwemo Israeli: 'Israel is desolate; it has no seed left' (Israeli imekuwa mahame, hakuna uzao uliobakia). Ipo hoja kuwa wakati huo Israeli lilikuwa haijawa taifa rasmi, bali ilikuwa ni jamii isiyokuwa na jeshi rasmi na huenda hali hiyo ilitokea vizazi viwili baada ya wana wa Israeli kuondoka Misri chini ya uongozi wa Jemedari na Nabii Musa.
Miaka 400 baadaye, Mfalme wa Moab aliyeitwa Mesha naye aliweka mnara wa ushindi ikiwa ni kuashiria kuwa pia aliishinda Israeli katika vita. Na haya ndiyo maandishi yake: 'Israel utterly perished for ever" (Israeli imeangamizwa na kiteketezwa kabisa na milele). Majigambo ya wafalme hao yalionyesha furaha yao kuishinda nchi yenye nguvu na ilikuwa ni kawaida kwa majemadari wa nyakati zile kuongeza 'chumvi' katika kutoa taarifa kwani ukweli ni kuwa Israeli ilikuwa haijaangamizwa, wala haikuteketezwa kabisa ingawa ni kweli ilikuwa imepiteza vita.
Majigambo ya Farao Merneptah yanaungwa mkono na ushahidi wa Musa alipoandika kuwa Waameleki na Wakanani walioishi katika nchi ya mlimani walishuka chini, waliwashambulia na kuwafukuza hadi Hormah (Hesabu 14:45).
Uchunguzi wa Ki-Biblia na nje ya Biblia (extra Biblical sources) unaonyesha na pia kupatana kuwa Hormah ulikuwa ni mji mashuhuri wa nchi ya Wakanani ambayo kabla iliitwa Zephath ulioharibiwa na wana wa Yuda na wana wa Simioni (Waamuzi 1:17). Pia, Joshua anamtaja Mfalme wa Zephath kuwa miongoni mwa watu aliowashinda katika vita (Yoshua 12:14).
Baadhi ya wasomi wa Biblia na wataalamu wa elimu kale (archaeologists) wanasema kuwa Hormah ndiyo Tell es-Sheriah wakati wengine wanasema ndio Tell el-Milh (Tell Malhata) huku wengine wakisema ni el-Mesas (Tel-Masos).
Kwa kufuata ushahidi huo, tunaweza kusema kuwa Israel ilianza kutajwa kama taifa huru na mataifa ya jirani mwaka 1220 Kabla ya Kristo. Hii ni yapata miaka 3250 iliyopita. Hii ni zaidi ya miaka 3000 iliyopita, Israel kama taifa linatajwa nje ya Biblia kuwa lilikuwa katika nchi iliyoitwa Kanani ambayo pia imeitwa kwa majina tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti kama Kanani, Zephath, Hormah, Yuda, Palestina, Israel, nk. Nchi hiyo moja ilijulikana kwa majina tofauti tofauti kulingana na nani aliiteka na kutawala wakati huo.
Baadaye tutaleta historia ya kuundwa kwa taifa ambalo ndilo Jumuiya ya Madola ya Israel. Hii ni pamoja na kutekwa kutokwa kwa Wayebusi mji ambao baadaye ukaitwa Yerusalemu na Mfalme Daudi. Kwa ufupi, igomvi, mapigano na mgogoro wa kugombania Mji wa Yerusalemu na nchi ya Israel ni mapambano ya miaka zaidi ya 3250 iliyopita ikihusisha jamii kubwa mbili ambazo ni Waisraeli na Wapalestina. Hayo ni mapambano yaliyoanza miaka 1200 kabla ya Ukristo na miaka 1820 kabla ya Uislam kuanza.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 31 Oktoba 2023; 05:20 asubuhi
1 307
WAKILI MSOMI STELLA AMALIZA MWENDO!
Taarifa zimetufikia kuwa wakili msomi Stella Makali amefariki dunia kwa ajali 2 Novemba 2023 mkoani Iringa. Sisi Askofu tunatoa pole kwa familia, Tanganyika Law Society (TLS) na Kanisa Anglikana Tanzania ambako alitumika kama mwimbaji wa sauti ya kwanza (soprano)!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 2 Novemba 2023; 02:48 usiku
1 307
Israel ilituma boti za makombora kwenye Bahari Nyekundu, jeshi lilisema jana (Jumatano) baada ya vikosi vya Houthi nchini Yemen kurusha makombora na ndege zisizo na rubani kuelekea mji wa mapumziko wa Israeli wa Eilat.
"Boti za makombora za Jeshi la Wanamaji la Israeli ziliwasili katika eneo la Bahari Nyekundu," Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) lilisema katika taarifa, na kubainisha hatua hiyo ilifanywa kufuatia "tathmini ya hali na kama sehemu ya juhudi za kujihami katika eneo hilo."
Msemaji wa IDF Daniel Hagari aliambia mkutano na waandishi wa habari kwamba usiku wa Jumanne na Jumatano, "tishio lingine la angani" liligunduliwa katika eneo la Bahari Nyekundu, kusini mwa Eilat, baada ya vikosi vya Houthi kutuma ndege zisizo na rubani na kombora kuelekea mjini mapema Jumanne.
