ru
Feedback

Не попадитесь на канал ботавода! Telemetrio находит и помечает такие каналы 👉 Хотите видеть метку — оформите подписку

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Открыть в Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

Больше
1 307
Подписчики
+124 часа
-27 дней
-1330 дней
Архив постов
Mamlaka za afya Palestina zimeituhumu Israel kwa shambulio la anga ambalo liliharibu wadi ya wagonjwa wa moyo katika hospital
Mamlaka za afya Palestina zimeituhumu Israel kwa shambulio la anga ambalo liliharibu wadi ya wagonjwa wa moyo katika hospital kubwa ya Gaza ya Al Shifa, katika mapigano yanayoendelea. Shirika la afya duniani limeonya kuwa hali ni tete katika hospitali hiyo ambayo kwa sasa haina, umeme,maji na hata chakula. Jeshi la Israel limekanusha kuhusika likisema lipo tayari kuwahamisha watoto wachanga ambao wameathirika katika hospitali hiyo.

Idadi ya wapalestina waliouawa katika mashambulio ya Israel katika Ukanda wa Gaza yafikia 11,180 Idadi ya wapalestina walioua
Idadi ya wapalestina waliouawa katika mashambulio ya Israel katika Ukanda wa Gaza yafikia 11,180 Idadi ya wapalestina waliouawa kutokana na mashambulio ya Israel katika Ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia 11,180 tangu mapigano yalipozuka Oktoba 7 mwaka huu. Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika katika Kituo cha Matibabu cha Shifa, mkurugenzi wa ofisi ya habari ya serikali ya Gaza Bw. Ismail Al-Thawabteh amesema, kati ya watu waliouawa, kuna watoto 4,609 na wanawake 3,100, wengine zaidi ya elfu 28 wamejeruhiwa. Ameongeza kuwa, kutokana na mashambulio ya Israel na ukosefu wa mafuta kwa mashine za kuzalisha umeme, hospitali 22 na vituo 49 vya afya katika Ukanda wa Gaza vimesitisha kutoa huduma. Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP liliripoti kuwa, ofisi zake zilizopo Gaza zimeshambuliwa katika shambulio la anga la Israel, na kusababisha vifo na majeruhi ya wakimbizi wa Palestina waliotafuta hifadhi katika ofisi hizo.

"Hapa tunafanya biashara ya kukusanya vyuma na mpaka sasa hapa tuna miaka mitatu na katika miaka hii tukio hili limetokea mar
"Hapa tunafanya biashara ya kukusanya vyuma na mpaka sasa hapa tuna miaka mitatu na katika miaka hii tukio hili limetokea mara mbili. Tumepata hasara kubwa kuna vyuma vimeenda na maji, kuna mabegi ya nguo ambayo pia yameenda, kipaza sauti (mic) pamoja na mizani yaani hapa ni kama tunaanza upya" - Juma Paulo - Mfanyabiashara wa vyuma Boko - Dar-es-Salaam

DAR KINARA KWA WANAWAKE WENYE UZITO ULIOPITILIZA Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya M
DAR KINARA KWA WANAWAKE WENYE UZITO ULIOPITILIZA Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria (TDHS) ya Mwaka 2022, Mkoa wa Dar es Salaam una 54% ya Wanawake wanaokabiliwa na Uzito mkubwa au Unene kupita kiasi ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya 53% huku Mikoa ya Rukwa na Mara ikiwa na kiwango cha chini kwa 18% Ripoti imeonesha kundi linaloathirika kwa kasi ni Wanawake wenye kati ya Miaka 20 hadi 29 wengi wao wakiwa ni wenye Elimu na kipato kikubwa kwenye Kaya zao kulinganisha na wenye Elimu ndogo na kipato kidogo Takwimu za jumla, Zanzibar ina 46%, Tanzania Bara 36% huku maeneo ya Mijini yakiwa na 50% na Vijijini 28% ya Wanawake wenye Uzito Uliopitiliza.

"Kuna begi lilikuwa na nguo sasa ndani ya hizo nguo ndio kulikuwa na hela kama 200,000 na tulishimdwa kuokoa maana maji yalik
"Kuna begi lilikuwa na nguo sasa ndani ya hizo nguo ndio kulikuwa na hela kama 200,000 na tulishimdwa kuokoa maana maji yalikuwa mengi. Vimeharibika vitu vingi ikiwepo mzani ambao ni 300,000, vipaza sauti vitatu, nguo zimechukuliwa na maji pamoja na magodoro. Tunalala hapahapa kwa sababu ndio ofisi na ndio sehemu ya kazi hatuna sehemu nyingine ya malazi zaidi ya hapa na mimi nimekuwa hapa kwa miaka 4" - Frank - Mfanyabiashara wa vyuma Boko - Dar-es-Salaam

NAMTAFUTA MWANANGU ALIYEPOTEA Pichani ni Mwanangu anaitwa MECTRIDA WILSON amemaliza elimu ya msingi katika shule ya Msingi NY
+1
NAMTAFUTA MWANANGU ALIYEPOTEA Pichani ni Mwanangu anaitwa MECTRIDA WILSON amemaliza elimu ya msingi katika shule ya Msingi NYAMIAGA iliyoko Ngara mkoani Kagera. Baada ya kuhitimu darasa la Saba nilimpeleka kusoma tuition "Pre form one" Katika kituo kiitwacho "MWALIMU EDWARD TUITION CENTER" Kinachopatikana maeneo ya kanisa la Anglicans Ngara Mjini. MECTRIDA WILSON alikuwa anaondoka nyumbani kwenda tuition kila siku lakini Alhamis nikaja kupata taarifa kutoka kwa rafiki yangu (jirani) kuwa Mectrida yupo kwake tangu asubuhi na hajaenda tuition anasema anaumwa tumbo.Aliondoka Alhamis jioni baada ya kumuuliza kwanini hataki kwenda Tuition akiwa amevaa gauni NYEUPE na mkoti wa jeans wenye rangi NYEUSI. Tumejaribu kumtafuta lakini hatujampata, kwa maombi yenu na Msaada wenu naomba mnisaidie kutamfuta na atakayempata atoe ripoti kituo cha polisi pia anaweza kunipigia simu kwa namba hii 0673850278 Asante Na Mungu awabariki

ABALIMBA NI TAPELI LA KUPINDUKIA Haya ndio maisha ya mwanasoka feki ambaye alijifanya kuwa ni mchezaji wa Ligi ya England hadi kufanikiwa kuwadanganya watu wengi hasa Wanawake akiwemo mke wa zamani wa Thierry Henry. Kupitia ulaghai huo alikuwa akijipatia maelfu ya pauni, aliishi maisha ya gharama ,akitumia magari, nguo na nyumba za kifahari. Medi Abalimba alizaliwa nchini Congo DRC ,akiwa na umri wa miaka mitano yeye pamoja na familia yake walihamia London wakati wa migororo ya miaka ya 1990. Abalimba alijaribu kuishi kifahari kama Wanasoka wa Kimataifa. Mhalifu huyo analaumu ”Uanasoka uliokwama” kama sababu iliyompelekea kuwa mdanganyifu. Aliwahi kujifanya ni Nyota wa zamani wa Chelsea Gael Kakuta, vilevile aliwahi kukodi helikopta akawachukua wasichana wanne kutokea Manchester akawazungusha jijini London na baadaye kuwafikishia kwenye nyumba ya Kifahari aliyodanganya kuwa ni ya kwake. Manunuzi yake ya vitu vya kifahari madukani ndiyo yaliyomfanya akamatwe kwani mpelelezi mmoja ndani ya dukani fulani alimshtukia na kuwaita Polisi. Uchunguzi ulifanyika na alifungwa kwa miaka minne baada ya kukiri mashtaka ikiwemo kuchukua gari aina ya Range Rover bila idhini. Akiwa jela, aliingia kwenye mahusiano na muuguzi mmoja ambaye alimletea simu kwa siri gerezani. Uhusiano wao uligundulika na mwanamama huyo alihukumiwa kifungo cha miezi 20 kwa utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma. Kwa kutumia simu aliyopewa na muuguzi huyo akiwa jela Abalimba alikuwa akiongea na mke wa zamani wa Thierry Henry (Bi.Claire Merry) kila siku kwa miezi minne na alijifanya yupo jeshini Kuwait. Abalimba aliachiwa mwaka 2018 na aliendelea na uhalifu. Aliingia kwenye uhusiano uliodumu kwa wiki sita na Mwanamke mmoja maarufu na kumuibia pauni 32,000. Baadaye alipanga akakutana na Bi.Claire Merry, ambaye alimlaghai na kumuibia pauni 50,000. Alikamatwa tena na baadae alikiri makosa 15 ya ulaghai ikiwemo kutumia leseni ya udereva ya kughushi na kadi feki ya benki. Mwaka 2021 alihukumiwa kifungo kipya cha miaka minne. Katika miaka kumi iliyopita, Abalimba alishadai kuwa ni mpelelezi, nyota wa Ligi ya England, wakala wa soka, mchezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Mwanamuziki na Mwanajeshi.

photo content
+1

Msanii wa Muziki kutoka Tanzania, Harmonize ambaye kwasasa yupo USA ameweka wazi kuwa atafanya paledi (Maandamano) kuanzia Ai
Msanii wa Muziki kutoka Tanzania, Harmonize ambaye kwasasa yupo USA ameweka wazi kuwa atafanya paledi (Maandamano) kuanzia Airport mpaka konde Village, "Tangu muziki wetu au niseme SANAA yetu ianze, SIKUMBUKI lini mara ya mwisho msanii kutoka Tanzania kulipatia hili Taifa la mama samia tuzo Tatu (3) za kimataifa ndani ya usiku mmoilja.! Moja au mbili, Nakumbuka ila Tatu sina kumbukumbu kwahiyo paledi litaanzia airport mpaka KONDE VILLAGE alafu tunakesha mpaka asubuhi, soon nawarudia na Tarehe pamoja na saa ninayotua ...! KONDE GANG MUDA WENU WA KUTAMBA.." ameandika Harmonize

"😂😂Watu wanauliza T-shirt zangu natoa wapi!! Jamani t-shirt zangu natoa oda special, zinatengenezwa kwa materials ya turuba
"😂😂Watu wanauliza T-shirt zangu natoa wapi!! Jamani t-shirt zangu natoa oda special, zinatengenezwa kwa materials ya turubai ama mifuko ya mashine za kusagia unga zile zinazoshusha unga ukishasagwa😂 hivi vitambaa huwa vinajaa upepo vinalizunguka puto kulilinda dhidi ya miba"- Peter Msechu

NINA HAKI YA KUWA NA MPENZI HATA KAMA NINA MIAKA 60 KWASABABU NIMEUMBWA NA HISIA; BIBI WA MIAKA 60 Lucy Iburu, mama na bibi w
NINA HAKI YA KUWA NA MPENZI HATA KAMA NINA MIAKA 60 KWASABABU NIMEUMBWA NA HISIA; BIBI WA MIAKA 60 Lucy Iburu, mama na bibi wa miaka 60 kutoka nchini Kenya, hachoki kutabasamu kwa mbwembwe na maringo baada ya kufunga ndoa takatifu mwezi uliopita wa Julai mwaka 2023. Lucy amewanyamazisha watu wenye mawazo potofu kwamba mama au bibi wa rika lake hana nafasi ya kuwa kwenye mapenzi. Na hapa anasema "Kila kiungo ambacho kimeumbwa na Mwenyezi Mungu kina umuhimu, kama hakina umuhimu ni kwanini niumbwe na hisia za kupenda?, hakuna kiungo cha binadamu ambacho kinaweza kuitwa cha kizee kisa kusonga kwa miaka" "Ni makosa kwa mtu kuwa na maoni kwamba mimi ni mzee sana kiasi kwamba haoni kama naweza kuwa kwenye mahusiano nikiwa na miaka 60"- amesema

FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medi
+9
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/

photo content

MIMI NI MWANAMKE, NINA KILA KITU ALICHONACHO MWANAMKE; LOVENESS "Mimi ni mwanamke nina jinsia ya kike haya ni mavazi tu kutokana na shughuli zangu ninazofanya, najikubali kama mwanamke. Nina sehemu za siri za mwanamke kila kitu ambacho mwanamke anacho na mimi ninacho. Nina miaka 37, sina mtoto, bado sijaolewa ila nina mchumba ambaye bado hatujafunga ndoa" "Mchumba wangu ni mwanaume wa mazoezi kama mimi kwasababu siwezi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye siyo mtu wa mazoezi, changamoto kubwa ninayoipata ni kutengwa na jamii kiaina, mfano, tunaweza tukatoka out na mpenzi wangu lakini watu wakawa wanatushanga wakijua sisi wote ni wanaume, nimeshazoea kwa kiasi chake ila bado hii hali ya kuonekana mwanaume inanisumbua sana"- amesema Mlimbwende Loveness Tarimo alipohojiwa na Imelda Mtema wa Global Online. Aidha Loveness ambaye ni mshindi wa mashindano ya Miss Fitness 2019 ameongeza kuwa kwa sasa hawezi kuvaa siketi, top wala gauni na hii ni kutokana na muonekano wake kutokuwa rafiki kwa mavazi hayo lakini pia kutokana na kwamba ni mtu wa gym muda mwingi hafiti kwenye mavazi ya kike.

photo content

Football Insider imeripoti kuwa klabu ya Manchester United inaweza kumsajili Kylian Mbappe mwezi Januari kabla ya mkataba wak
Football Insider imeripoti kuwa klabu ya Manchester United inaweza kumsajili Kylian Mbappe mwezi Januari kabla ya mkataba wake na PSG kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa 2024. Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥 Toa maoni yako

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lawapongeza Rayvanny na s2kizzy baada ya wimbo wa "Mama Tetema" wa Msanii Maluma ambao kamshirikisha Rayvanny kuingia kwenye kinyang'anyiro (Tuzo) kubwa zaidi za muziki Duniani za Grammy 2024 kupitia Albamu ya Maluma. Ikumbukwe kwamba wimbo wa "Mama Tetema" ni "RMX" ya wimbo wa "Tetema" wa Rayvanny uliotengenezwa na Mtayarishaji (Producer) wa muziki Tanzania, s2kizzy.. Wadau wengi wa muziki Nchini Tanzania walikuwa wakisubiri matokeo ya Wasanii wa Afrika watakaotajwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho akiwamo Diamond Platnumz na Rema (Nigeria) ila Wasanii hao hawakufanikiwa kuchaguliwa badala yake, wametajwa Davido (kwa mara ya kwanza katika historia na ametajwa katika vipengele 3) Burna Boy (vipengele 4), Asake, Olamide, Ayra Starr na Tyla. Pia Diamond Platnumz, Nandy , Rayvanny na S2kizzy ndio Watanzania pekee mpaka sasa waliokuwa "Recognized" kupitia kazi za Wasanii waliowashirikisha kwenye Tuzo za Grammy. . Mbali na hivyo DiamondPlatnumz ndio aliopata "Grammy Credit Certificate" baada ya Alicia Keys kushinda kwenye kipengele cha "Immersive Audio Album" 2022. Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥 Toa maoni yako

photo content

MWANAMKE USIZAE KABLA HUJAFIKISHA MIAKA 35; HUDDAH "Wanawake tafadhali usiwe na mtoto kabla ya miaka 35, nenda kafanye uzazi
MWANAMKE USIZAE KABLA HUJAFIKISHA MIAKA 35; HUDDAH "Wanawake tafadhali usiwe na mtoto kabla ya miaka 35, nenda kafanye uzazi wa mpango wa miaka 10, nitakupa Daktari wangu atakupa ushauri usikimbilie kuleta mtoto katika ulimwengu huu wa fujo, watu wanahitaji kujitafuta wenyewe na Mungu kabla ya kutafuta kizazi chako, 90% ya wanawake ni single parents, na sio sababu wanataka, na wengine ni single parents ndani ya ndoa, funga miguu yako mpaka ukiwa tayari"- Huddah