ru
Feedback

Не попадитесь на канал ботавода! Telemetrio находит и помечает такие каналы 👉 Хотите видеть метку — оформите подписку

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Открыть в Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

Больше
1 307
Подписчики
+124 часа
-27 дней
-1330 дней
Архив постов
Jokate na Totoo
Jokate na Totoo

TAARIFA YA SERIKALI YA MAENDELEO YA HALI BAADA YA MAAFA YALIYOTOKEA WILAYANI HANANG MKOANI MANYARA. Na John Walter-Manyara Hadi kufikia sasa misaada mbalimbali inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali wilaya ya Hanang' mkoa wa Manyara palipotokea maafa ya maporomoko ya tope, mawe na magogo ina thamani ya shilingi bilioni 2,583,306,997.00 na fedha taslimu shilingi 5,208,729,711.00. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi katika taarifa yake ya desemba 24, 2023, Fedha taslimu zinajumuisha shilingi bilioni 2.5 zilizoletwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na shilingi 2,708,729,711.00 zilizomo kwenye akaunti ya Mfuko wa Taifa wa Misaada ya Maafa inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kati ya fedha hizo, kiasi cha sh. 2,289,260,025.00 zimechangwa na taasisi na mashirika ya umma kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na kiasi kilichobaki cha sh. 419,469,152.00 kimechangwa na wahisani mbalimbali. Serikali inaeendelea kuwashukuru Watanzania kwa utu, upendo, uzalendo na moyo wa kujitolea ambao umesaidia kupatikana kwa chakula cha kutosha na mahitaji muhimu ili kuwasaidia waathirika kuendelea na maisha yao na kusisitiza wanaoendelea kuleta misaada kujikita zaidi katika vifaa vya ujenzi. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Kambi tatu zilizokuwa zinatoa huduma zimefungwa baada ya waathiriwa wote 690 kutoka kaya 140 kurejea makwao na kwa ndugu zao. Ikumbukwe kuwa Waathirika 534 walikuwa wakilala kambini na 156 walikuwa wakija asubuhi na kuondoka jioni. Utaratibu wa kugawa misaada hiyo unaoratibiwa na Idara ya Maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na uongozi wa mkoa wa Manyara na wilaya ya Hanang pamoja na kamati zao za usalama, unatumia watalaam kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Kuhusu Mgawo wa misaada , taarifa imeeleza kuwa unalenga kwanza waathirika 1,292 waliothibitika kupoteza nyumba zao ama kuharibika au kuingia tope. Idadi hii ilipatikana baada ya tathmini ya kina ya picha za satelaiti, rekodi za sensa, ukaguzi halisi wa nyumba hadi nyumba na rekodi za serikali za mitaa katika ngazi ya vitongoji, vijiji na kata. Utaratibu wa ugawaji misaada umewekwa kwa kubandika majina ya waathirika kwenye ofisi za kata baada ya kukamilika kwa tathmini ambapo mhusika akifika huelekezwa kituo chake cha kupokelea misaada. Tangu wiki iliyopita wananchi wamekuwa na ratiba za kwenda kupokea misaada kila siku kutokana na wingi wa misaada hiyo. Kwa wastani kila kaya inapata chakula cha kutosha miezi sita au zaidi ambapo kwa baadhi ya bidhaa kama sukari wananchi hao wanapewa ya kutosha kutumia kwa zaidi ya miaka miwili kwa mujibu wa vipimo vya lishe. Misaada inayotolewa ni chakula cha mahindi, ngano, mchele, unga wa mahindi, unga wa ngano, maharage, mafuta ya kula, maziwa, unga wa lishe kwa watoto, mayai, sabuni, magodoro, mablanketi, mashuka, mikeka, ndoo, majiko ya kupikia ya gesi na mitungi yake, masufuria, nguo, viatu, kandambili na vingine vingi. Idadi ya watu waliopoteza maisha imebakia kuwa 89 tangu tarehe 11 Desemba na mwili mmoja wa mtoto wa kike bado haujatambuliwa. Maafa haya yalitokea alfajiri ya tarehe 3 Desemba, 2023, baada ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na maji kutoka mlima Hanang kuvamia vijiji vinne vilivyokuwa kando ya mlima Hanang na kata nne za mji mdogo wa Katesh wilayani Hanang. Hadi sasa majeruhi wanne bado wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara iliyopo mjini Babati na mmoja amepelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma. Serikali imegharamia matibabu, mazishi na kutoa mkono wa pole kwa wafiwa. Majeruhi wote walifikia jumla ya 139. Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa akaunti ya kielektronikia kuchangia fedha za misaada yenye nambari 9921159801 iliyopo Benki Kuu ya Tanzania na inayopokea fedha kupitia benki yoyote nchini na pia kutoka nje ya nchi kwa kutumia swift code ya TANZTZTX. Miamala yote inatakiwa kuwa na maelezo MAAFA HANANG.

photo content

⚠️Shamsa Ford ajifungua mwanae wa pili ambaye ni wa kike Miezi michache iliyopita msanii huyo maarufu aliolewa na Mlilo(Husse
⚠️Shamsa Ford ajifungua mwanae wa pili ambaye ni wa kike Miezi michache iliyopita msanii huyo maarufu aliolewa na Mlilo(Hussein Lugendo) ambaye ni mwigizaji anayechipukia Shamsa tayari ana mtoto mkubwa wa kiume kwa jina la Terry toka mahusiano yake ya mwanzo ingawa kipindi cha nyuma hakusita kueleza kuwa baba mtoto hajishughulishi katika malezi ya kuhudumia mwanae

⚠️🥰 Lucy Komba na mwanae wa 2 katika muonekano wa kusherehekea X-mas Msanii huyo wa filamu kwasasa anaishi nchinii Denmark a
⚠️🥰 Lucy Komba na mwanae wa 2 katika muonekano wa kusherehekea X-mas Msanii huyo wa filamu kwasasa anaishi nchinii Denmark alikoolewa

Beki wa kati wa Sevilla 🇪🇸 Sergio Ramos (37) anazidi kutanua kipaji chake cha muziki baada ya kushirikiana na kundi la muzi
Beki wa kati wa Sevilla 🇪🇸 Sergio Ramos (37) anazidi kutanua kipaji chake cha muziki baada ya kushirikiana na kundi la muziki la Los Yakis kwenye wimbo wao mpya wa "No Me Contradigas". 🎶 Wimbo huo umetazamwa na laki tisa huko YouTube ndani ya siku mbili.

"Tumeanza juma la mwisho kuufunga mwaka 2023 lenye sikukuu mbili za Krismasi na Mwaka Mpya. Namuomba Mwenyezi Mungu ili sote
"Tumeanza juma la mwisho kuufunga mwaka 2023 lenye sikukuu mbili za Krismasi na Mwaka Mpya. Namuomba Mwenyezi Mungu ili sote tuweze kufikia siku hizi tukiwa wazima wa afya, kusherehekea kwa pamoja, kwa upendo, amani, furaha na usalama. Katika sherehe hizi, baadhi yenu mnasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kujiunga na familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawasihi kuzingatia sheria ya usalama barabarani na kuchukua tahadhari na umakini mkubwa ili juma hili likawe lenye furaha, mkawe na muda mzuri na ndugu, jamaa na marafiki, na baadaye nyote mrejee mkiwa wazima wa afya kuendelea kufanya kazi ya kuliletea taifa letu maendeleo." @ikulumawasliano @ikulu_mawasiliano @samia_suluhu_hassan @Ikulu Mawasiliano #KaziIendelee #SisiTumekuelewa #TanzaniaYaSamia #TZS

Umemkumbuka ni Nani ?
Umemkumbuka ni Nani ?

VP MDAU NA WEWE USHAALIKWA AU BADO BADO..😀
VP MDAU NA WEWE USHAALIKWA AU BADO BADO..😀

Ya Lulu na Xmas
Ya Lulu na Xmas

Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Flavian Kassala amesema hayuko tayari kubariki ndoa ya jinsia moja kwani ni kinyume na maagano ya Mungu ya kutaka binadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi ulimwenguni. Askofu Kassala amesema bora abariki jiwe ukajengee nyumba na sio kubariki watu wa jinsia moja wanaotaka kufunga ndoa ndani ya kanisa hilo. Akihubiri katika misa ya kitaifa ya Krisimasi, amesema kubariki mapenzi ya jinsia moja ni kwenda kinyume na maandiko ya Mungu yanayotaka wanadamu wakazaliane na kuendeleza vizazi. Amesema binadamu anakataa uumbaji wa Mungu na kufanya mambo yaliyokatazwa huku wakitaka na kanisa liyabariki jambo ambalo amelipinga vikali.

photo content

KUWA MKWELI Ulianza lini kuacha kumfatilia Mrisho mpoto?
KUWA MKWELI Ulianza lini kuacha kumfatilia Mrisho mpoto?

Anaandika mtangazaji na mwanamitandao @Mwijaku ⬇️ "Yes yes Bao la kisiginoo ..! Nimefurahi sana nafasi ya K imekua covered na
Anaandika mtangazaji na mwanamitandao @Mwijaku ⬇️ "Yes yes Bao la kisiginoo ..! Nimefurahi sana nafasi ya K imekua covered na mwanamke ambaye hawezi kukusaliti hata ukiwa na hali gani au ukiwa na changamoto gani she will be there foe you . Am so proud of you "

Nimenenepa tena leo baada ya kuona taarifa kutoka FIFA kuwa Sisi Simba Sports Club tunavigezo vya kushiriki kombe la dunia ng
Nimenenepa tena leo baada ya kuona taarifa kutoka FIFA kuwa Sisi Simba Sports Club tunavigezo vya kushiriki kombe la dunia ngazi ya klabu Naitwa SEMAJI LA FIFA CLUB WORLD CUP -Ahmed Ally

"Nilikuwa nafanya biashara kwa sababu nilisoma kwenye biblia kwamba wanaume waliokuwa wanafanya kazi ya MUNGU hawakuwa watu w
"Nilikuwa nafanya biashara kwa sababu nilisoma kwenye biblia kwamba wanaume waliokuwa wanafanya kazi ya MUNGU hawakuwa watu wanaohubiri peke yake, na hata nilipokuwa nikiwahubiria wenzangu shule niliwaambia asilimia 75 ya watu kwenye biblia hawakuwa wahubiri ila walikuwa wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, viongozi hivyo MUNGU aliwatumia watu wa kawaida (secular world) zaidi kuliko wahubiri. Na nilikuwa natamani nikihubiri nisiwaambie tu nadharia ila niwaonyeshe pia kwa vitendo" - Mchungaji @pastortonyosborn

Leo Katika Historia Kwa mara ya kwanza tarehe hii ilihusishwa na siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika karne ya nne na kwa
Leo Katika Historia Kwa mara ya kwanza tarehe hii ilihusishwa na siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika karne ya nne na kwa mara ya kwanza iliidhinishwa mwaka 336 wakati wa utawala wa kifalme wa Kirumi chini ya Mfalme Constantine.

WANGAPI WANAMKUMBUKA HUYU POLISI..😀
WANGAPI WANAMKUMBUKA HUYU POLISI..😀

Krismas hii unasherehekea ukiwa wapi?umepata mwaliko tayari au mishe zinaendelea kama kawaida
Krismas hii unasherehekea ukiwa wapi?umepata mwaliko tayari au mishe zinaendelea kama kawaida

UMEJIFUNZA NINI HAPA
UMEJIFUNZA NINI HAPA