ru
Feedback

Не попадитесь на канал ботавода! Telemetrio находит и помечает такие каналы 👉 Хотите видеть метку — оформите подписку

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Открыть в Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

Больше
1 307
Подписчики
+124 часа
-27 дней
-1330 дней
Архив постов
photo content

⚠️🥰 Davina Halima Yahaya mwigizaji maarufu Bongo ameolewa kwa mara nyingine Mwigizaji huyo ambaye tayari ana watoto, mbali n
⚠️🥰 Davina Halima Yahaya mwigizaji maarufu Bongo ameolewa kwa mara nyingine Mwigizaji huyo ambaye tayari ana watoto, mbali na uigizaji pia ni mwanasiasa

⚠️😢 Mdada aliyemuua pacha wake kwa kumchoma visu mfululizo kisha kuukata mwili wake vipande vipande kwa shoka ahakumiwa miak
⚠️😢 Mdada aliyemuua pacha wake kwa kumchoma visu mfululizo kisha kuukata mwili wake vipande vipande kwa shoka ahakumiwa miaka 15 jela Tshepho Mogoshadi Mphahlele(35) alifanya ukatili husika huko Limpopo, S.Afrika tarehe 18 Januari 2023 na hukumu imetoka sasa Siku ya tukio yeye na pacha wake waliingia katika majibizano makali yaliyozaa ugomvi ambapo akachukua kisu kumchomachoma pacha wake hadi akafariki, kisha akachukoa shoka kuukatakata mwili wake Alikimbia ila siku mbili baada alijisalimisha mwenyewe polisi

⚠️ Amanda Poshy mwigizaji wa Tanzania ambaye kwasasa anaishi nchini Uingereza na familia yake ameandika yafuatayo "Wazazi wafundisheni watoto kuwa na mioyo mizuri ila msisahau kuwafundisha moyo mzuri una kikomo,wafundisheni watoto wawe na mioyo mizuri ya kusamehe ila msisahau kuwafundisha wasikubali kulazimishwa wasamehe mabaya yatakayowaumiza na kuwatafuna ndani kwa ndani mpaka kusababisha vifo, Wafundisheni watoto wamtendee binadamu yoyote mazuri ila msisahau kuwafundisha kama anayemtendea atamrudishia mabaya basi hata iwe ndugu yake asiogope kumtoa kwenye maisha yake na kwenye hili kazia zaidi kuwa yeye siyo Malaika kiasi akimuweka pembeni aliyemfanyia ubaya atalaumiwa kwa maana hata yeye ni binaadamu Mwisho msisahau kuwafundisha kuwa kwenye dunia hii asitokee mtu akaichukulia roho yake nzuri kuwa sababu ya yeye kupokea lolote iwe kwa kubembelezwa au kulazimishwa,nikimaanisha asitokee mtu yeyote akamlazimisha akubali lolote lile ambalo litamsababisha ayaishi maumivu ili tu athibitishe ana roho nzuri Hata wewe mzazi wake uliyemleta duniani huna ruhusa ya kumlazimisha yeye akubali kitu kitakachompa maumivu maisha yake yote na hata kusababisha kifo cha mapema kwa msongo wa mawazo Mfundishe kama kuna mtu atamsema kwa roho mbaya kwa kusimamia msimamo wake basi kuna mwingine atamsifia kwa roho yake kwa yale mazuri atakayoyaona kupitia yeye Mungu abariki vizazi vyetu vilivyopo na vijavyo"

photo content

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wananchi mkoani humo, limefanikiwa kumnasa mtu mmoja Alex Msigwa (34) amba
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wananchi mkoani humo, limefanikiwa kumnasa mtu mmoja Alex Msigwa (34) ambaye ni dereva Bajaji Mjini Iringa, kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio 15 ya ubakaji ambapo zaidi ya watoto 20 wenye umri wa kati ya miaka 6 mpaka 14 walibakwa kwenye matukio hayo. Alex alikuwa akiwakamata watoto hao majira ya usiku na wengine mchana kwa kuwatishia kuwa yeye ni Polisi au Ustawi wa Jamii akidai kuwa anakamata watoto wazururaji kisha kwenda kuwabaka.

"Mlima Hanang una miamba laini sana. Ulifanya mlima ushindwe kubeba ule mzigo na ndipo ukatokea utelezi. Na ule utelezi kwa k
+1
"Mlima Hanang una miamba laini sana. Ulifanya mlima ushindwe kubeba ule mzigo na ndipo ukatokea utelezi. Na ule utelezi kwa kuwa kuna maji na udongo unaotokana na volcano na miamba laini ukazalisha tope na likaanza kushuka chini kwa kasi likazoa mawe Mlimani yale mawe yakakumbana na miti ikiyokuwa Mlimani yakazoa ile miti. Kwahiyo kukawa kuna matope maji, mawe na miti yanashuka kwenye makazi ya watu" "Yakawa yanagonga nyumba zikawa zinatengeneza mzigo mwingine zinagonga nyumba zingine" Mobhare Matinyi, Msemaji Mkuu Wa Serikali. Millard Ayo presenter.

Baada ya kiungo wa Real Madrid Aurelien Tchouameni, sasa ni zamu ya kiungo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana na kla
Baada ya kiungo wa Real Madrid Aurelien Tchouameni, sasa ni zamu ya kiungo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana na klabu ya Chelsea Michael Essien kuingia kwenye 18 za Ticha Konde @harmonize_tz Michael Essien amemsifia msanii @harmonize_tz kwa njia ya kipekee katika kile alichokitaja kuwa yeye na muziki wake anafanya mambo ya kustaajabisha!. Essien alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ali-post picha yake kwenye ukurasa wa Instagram huku akiunganisha na wimbo wa Harmonize ‘Sijalewa’ ambao umetoka hivi karibuni. Baada ya kuonesha heshima hiyo kubwa, Harmonize alifika kwenye ukurasa wa Essien na kumuandikia ujumbe mrefu akimshukuru huku pia akifichua kwamba kitambo akiwa Chelsea, yeye alikuwa akisafiri hadi kijiji cha pili ili tu akamshuhudie Essien katika vibanda umiza. Essien alishuka kwenye comment na kuandika; “Unachokifanya na muziki ni cha ajabu sana, endelea hivyo kaka Harmonize, upendo mkubwa.” Nini maoni yako kuhusu haya mashavu anayo-win Harmonize? #millardayopresenter

Poleni sana wana Hanang' , Mungu awatie nguvu wakati huu mgumu mnaopitia.
Poleni sana wana Hanang' , Mungu awatie nguvu wakati huu mgumu mnaopitia.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupungua kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano December 06, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi December 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3158 kwa lita, dizeli Tsh. 3226 na mafuta ya taa 3423. EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi December 2023 yaliyoonesha kupungua kwa bei yanatokana na bei za mafuta (FOB) kwenye soko la dunia kupungua mwezi huu kwa wastani wa 0.86% kwa mafuta ya petroli na 9.11% kwa mafuta ya dizeli. EWURA imesema pia gharama za kuagiza mafuta (premium) kwa Bandari ya DSM zimepungua kwa wastani 24% kwa mafuta ya petroli na 30% kwa mafuta ya dizeli na kwa Bandari ya Tanga gharama za kuagiza mafuta (premium) zimepungua kwa 30% kwa mafuta ya petroli na 17% kwa mafuta ya dizeli, Bandari ya Mtwara haikupokea shehena ya mafuta. EWURA pia imesema mabadiliko haya yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 8.72% na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 27 kwa petroli a asilimia 23 kwa dizeli. Itakumbukwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano November 01, 2023 saa 6:01, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ilikuwa ni Tsh. 3274 kwa lita, dizeli Tsh. 3374 na mafuta ya taa 3423. #MillardAyopresenter

***Binti wa Zambia🇿🇲 'Chikondi Jemima Chitala' mwenye Ndoto ya kuwa Afisa Polisi akiwa katika pozi tofauti za ndoto zake***
+3
***Binti wa Zambia🇿🇲 'Chikondi Jemima Chitala' mwenye Ndoto ya kuwa Afisa Polisi akiwa katika pozi tofauti za ndoto zake***

photo content

EHISPANIA WAWEKA REKODI KWENYE MANUNUZI YA GESI YA URUSI🇷🇺🛢🇪🇸 Unaweza kujiuliza maswali mengi kuhusu vile vikwazo ambavy
EHISPANIA WAWEKA REKODI KWENYE MANUNUZI YA GESI YA URUSI🇷🇺🛢🇪🇸 Unaweza kujiuliza maswali mengi kuhusu vile vikwazo ambavyo Bunge la Ulaya waliviweka dhidi ya Urusi kwa kuyakataza mataifa yake kutofanya biashara kabisa na taifa hilo, vimeishia wapi? Ni takribani miezi tisa sasa ndani ya mwaka huu, Serikali ya Hispania imefanikiwa kuagiza kiasi kikubwa cha gesi ya Urusi mara sita (6) zaidi ya ilivyofanya mwaka 2018. Kwa kifupi, kwa mwaka 2023 pekee, taifa la Hispania imenunua kiwango kikubwa cha gesi kutoka nchini Urusi na kuweka rekodi ya manunuzi kwa taifa hilo. Kupitia Gazeti la El Mundo la Uhispania, Ofisa mmoja wa Uhispania alisema, “Mwaka huu utaisha zaidi ya mwaka uliopita ambapo mfumo wa gesi wa taifa letu ulipokea gesi nyingi zaidi ya Urusi katika historia yake yote” Hii sasa ndo vita yenyewe kama mlikuwa hamjui. Lengo la Mmarekani ni kumng’oa Urusi katika umiliki wa uuzaji wa Gesi katika bara zima la Ulaya lakini wameshindwa.

"Nina miaka 11 Tanzania na nina miaka 9 sasa niko na mume wangu Masai, nilikuja hapa Tanzania kufanya volunteering ya utafiti
"Nina miaka 11 Tanzania na nina miaka 9 sasa niko na mume wangu Masai, nilikuja hapa Tanzania kufanya volunteering ya utafiti wa mambo ya uhifadhi, nilianza kufanya kazi Ifakara tulikuwa na 'camp' ya wanyama na nilijifunza Kiswahili kule kule" - Stephanie Fuchs "Siku ya kwanza kukanyaga kisiwa cha Mafia ndiyo nilikutana na mume wangu Sokoine, yaani hiyo siku nilitembelea tu kijijini kutaka kuona mazingira nikakutana na Masai watatu na nilivyomuona yeye nilimpenda tu"- Stephanie Fuch "Unajua unapokutana na mtu unaweza kuvutiwa na sura na mwili wake kabla hujajua tabia yake, lakini ukimwangalia sura, mwili na tabasamu unapenda na unavutiwa, lakini ile siku niliona kama vile wao walikuwa 'busy', walikuwa wanafanya kazi ya ulinzi"- Stephanie Fuchs

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, leo
+3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, leo December 06, 2023 amewatembela na kuwajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko ya matope na mawe yaliyotokea Wilaya ya Hanang ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara. Dkt. Tulia ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa uharaka na kazi nzuri ya kuhudumia majeruhi hao na ameipongeza timu ya Madaktari waliotoka Mikoa ya jirani kufika mapema katika Hospitali ya hiyo kuongeza nguvu kwa ajili ya kuhudumia majeruhi hao. #MillardAyoUPDATES

Bajaji ya Mwananchi wa Katesh iliyoharibiwa na Maporomoko ya tope,mawe na miti iliyotokea Jumapili Desemba 3 saa 11:30 asubuh
Bajaji ya Mwananchi wa Katesh iliyoharibiwa na Maporomoko ya tope,mawe na miti iliyotokea Jumapili Desemba 3 saa 11:30 asubuhi.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe , siku ya Alhamisi, tarehe 7 Desemba 2023, atafa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe , siku ya Alhamisi, tarehe 7 Desemba 2023, atafanya ziara mkoani Manyara, Wilaya ya Hanang kutembelea wahanga wa tukio la mafuriko ili kutoa pole na faraja kwa familia zilizokumbwa na janga hili.

"Wataalamu wetu wa Hali ya hewa na miamba wanajaribu kutabiri hali inakwenda vipi. Utabiri wa Leo asubuhi unaonyesha kwamba b
"Wataalamu wetu wa Hali ya hewa na miamba wanajaribu kutabiri hali inakwenda vipi. Utabiri wa Leo asubuhi unaonyesha kwamba bado picha za satellite zinaonyesha kuna wingu linaisogelea wilaya ya Hanang ikiwemo Mji mdogo wa Katesh. "Kuna kazi kubwa inayofanywa na Serikali kujaribu kuepuka tatizo hili hapa hapa Hanang kwanza iwapo kama hali itabadilika tena" Mobhare Matinyi, Msemaji Mkuu Wa Serikali Cc clouds tv

Kutoka Kwa Mange KIMAMBI Yuko hai. Yuko nje kwenye matibabu. Alifanyiwa operation. Sijui ana hali ya gani kwa sasa. İla Mungu
Kutoka Kwa Mange KIMAMBI Yuko hai. Yuko nje kwenye matibabu. Alifanyiwa operation. Sijui ana hali ya gani kwa sasa. İla Mungu bado hajampenda zaidi…. Yupo hai…….. Huyu jamaa toka akabwe na Covid kipindi kile afya imekuwa mgogoro sana. Huyu ndo mfano hai wa watu waliopata serious Covid alafu afya hazikurudi tena. . Nikipata habari zaidi nitawaletea….Tumuombee apone….. Hanaga shida huyu baba….

photo content
+9