SHAIRI:
NASAHA KWA JABIRI MWALIMU.
MTUNZI:
ABUU DARDAA' AMRI BIN HASAN
MARKAZ UTHMAAN BIN AFFAAN' BOMANG'OMBE- KILIMANJARO- TANZANIA
بسم الله الرحمن الرحيم
1-Kuyarudi matapishi, Ni dalili ya kufeli,
Hajuri sio mzushi, Anakwenda na dalili,
Jabiri bila ubishi, Hulijui jambo hili,
Kidonda nzi haweshi, Unanuka kwelikweli.
2-Umeivua sunna, umekimbilia rai,
Mashekhe kuwatukana, Kwa hili sikushangai,
Umeyazusha mchana, Wajinga kuwalaghai,
Hajuri hakutukana, Usemayo hutambui.
3-Huyu Jabiri kapinda, Vipi mnamuamini!,
Maneno anayounda, Hayanasi akilini,
Kama njiwa yeye kinda, Hivi atakua lini!,
Mwili mzima vidonda, Ameshavunda yaqini.
4-Mtume kujitahidi, Hili mbona lipo wazi,
Wahyi huja sipidi, Kosa haliendelezi,
Kukuonya inabidi, Kwetu nasaha si kazi,
Tatizo u mkaidi, Nasaha husikilizi.
5-Hoja zake ni dhaifu, Akae chini asome,
Tena amekosa khofu, Hili wacha tuliseme,
Hajuri si mkosefu, Amtukane Mtume,
Huyu Jabiri ni mfu, Kwanini msimuhame?
6-Uongo mwingi kazua, Kuidhihirisha chuki,
Hajuri kumchafua, Hapa hajatenda haki,
Ni lini atatambua, Amuongoze Razaki,
Jabiri ulipotea, Mwalimu wa kudhihaki.
7-Hajuri hana adabu! Uko wapi ushahidi,
Wala hamna aibu, Kila siku mnanadi,
Tena bila ya sababu, Mnafanya makusudi,
Kiama kipo karibu, Kurejea inabidi.
8-Jabiri elimu hana, Kiburi kimemjaa,
Kurudia yaso mana, Kwa hili namshangaa,
Ukweli anaukana, Dalili kuzikataa,
Akuongoze Rabana, Nasaha zitakufaa.
9- Nasaha kwako Jabiri, Mwalimu nikuhusie,
Haki iliyodhihiri, Yanini uizuie,
Dini sio mashairi, Mizani ututungie,
Jabiri acha kiburi, Hilo ulizingatie.
10- Ubora sio kunena, Kuzonga wasikizaji,
Kuwavurugia tena, Uongo kuvaa taji,
Nakukanya ewe mwana, Karima mola mpaji,
Wakunyanyua Rabana, Mbora wetu mchaji.
JUMAANNE, 16 Dhul-Qaadah 1441 H
TAREHE: 07-07-2020.
https://t.me/duruuszakiswahiliTZ
جزاكم الله خيرا