E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Follow ukurasa wetu wa Twitter👇
https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09
1 307
Ni sehemu ya ibada ya maziko ya Mtayarishaji wa video mbalimbali za wanamuziki na filamu,muimbaji na mtunzi wa nyimbo Nic Davie maarufu NISHER,
Baadhi ya wasanii na waimbaji wa nyimbo mbalimbali akiwemo Fiq Q,Joh makini, Ben Paul wamejumuika na waombolezaji wengine katika ibada ya maziko ya mdau huyo wa Muziki na filamu nchini Tanzania.
#KutokaArusha
#tutaonanabaadae🙏
1 307
ALHAMDULILLAH KWA KILA KITU MPAKA KUFIKA HAPA NILIPO; FAIZA ALLY
Akiwa anasherehekea kutimiza umri wa miaka 40, Faiza Ally amemshukuru Mungu kwa kumjaalia kufika hapa alipo akiwa ni mwenye afya tele, nguvu, pesa na halali njaa. Faiza amewashukuru wazazi wake hao pichani Marehemu baba yake na mama yake ambaye yupo hai.
Pia amewashukuru ndugu, jamaa na marafiki zake lakini pia mashabiki zake ambao wamekuwa wakimsapoti siku hadi siku. Amewashukuru watoto wake ambao ndio sehemu kubwa ya maisha yake na amewaahidi kupambana usiku na mchana ili wasitaabike na umasikini wa duniani.
Happy 40 Faiza Ally 🙏
1 307
ZARI NA TANASHA SASA NI FAMILIA
Pichani ni Wazazi wenza na Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady na Tanasha Donah wakiteta jambo walipokutana huko Uganda kwenye show.
Wawili hao wote wamezaa na Mwanamuziki Diamond Platnumz kwa nyakati tofauti.
1 307
"Ni kweli nimefilisika lakini sikosi pesa ya kula, nimefilisika zaidi kwenye muziki na hii inatokana na watu walivyoubadilisha muziki. Tofauti na taarifa zinazosambaa huko mitaani kwamba nakosa pakulala na wala sina pesa ya kula, sio kweli"
"Nina mashamba Mwanza na Morogoro, nina kibanda changu nyumbani kwetu na mimi kuishi kwenye nyumba ya kupanga sijaanza leo, tangu enzi hizo nimekuwa nikiishi kwenye nyumba ya kupanga"
"Nikiamua kuwa kichaa kama walivyo wao naweza nikawa staa mkubwa zaidi yao, ila mimi sipendi njia za mkato"
"Freemason walishanifuata mara tatu wakitaka nijiunge na chama chao nifanikiwe haraka, lakini nilikataa kufanikiwa kwa kutumia njia hizo"
"Baada ya shetani kutuma wapambe wake kuja kunishawishi sasa ameamua kuja mwenyewe, matatizo hayaishi kwenye familia yangu na nakumbuka waliwahi kuniambia ukichoka kuteseka utasema" - 20% (Twenty Percent), Msanii wa muda mrefu wa Bongo Flava via MiliardAyo.
Toa maoni yako
1 307
"Mimi maisha yangu hayaendeshwi na kiki kwasababu kipaji changu kinajitosheleza, mambo yangu hayaendi kwa kiki kwasababu mashabiki zangu walinipokea vizuri wakanihakikishia kuwa uwezo wa kipaji changu ni zaidi ya kiki"- Irene Paul
1 307
MKUU WA WILAYA YA MPANDA ATOA ONYO KWA UONGOZI WA MANISPAA.
Onyo hilo limekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko ya Mwananchi mmoja wa kata ya Mpanda hoteli Manispaa ya Mpanda aliyefyekewa mimea ya Mahindi shambani kwake kwa kile kilichodaiwa kuwa amepanda mazao marefu kinyume na utaratibu wa sheria za Manispaa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusu wakati wa zoezi la kufanya usafi kama ilivyoada kila juma mosi kuna kuwa na zoezi hilo Mkuu huyo wa Wilaya ametumia nafasi hiyo kutoa angalizo kwa uongozi wa Manispaa Mpanda kusubiri Mahindi yakue ndipo wachukue hatua ya kuyafyeka hii inaleta taswira mbaya ambayo inaweza kuingombanisha serikali na Wananchi kwa kosa la watu wachache kushindwa kusimamia sheria zilizowekwa.
Aidha ametoa rai kwa Wananchi kufata taratibu na sheria ambazo zimekuwa ambazo zinawakataza kulima ndani ya Manispaa ili kuepusha migogoro kama hii ya kufyekewa mazao ambapo hakuna anayefurahia kuona kilichofanyika isipokuwa kila mmoja atimize wajibu wake pande zote wananchi pamoja na wasimamizi wa sheria.
Katika hatua nyingi baadhi ya Wakazi wa Mpanda hoteli Manispaa ya Mpanda wameupongeza uongozi wa Manispaa ya Mpanda kwa hatua ilizozichukua wakisema wanahitaji mji uwe safi na wakulima wakafanye shughuli za kilimo Mashambani vijijini na sio katikati ya mji huku wakienda mbali zaidi kuwa kuna haja ya Uongozi wa Manispaa kulisimamia zoezi hili pande zote za katikati ya Mjini ili kuondoa uchafu huku wakiyataja maeneo ya Ilembo, Uwanja wa ndege, Kashaulili, Kawajense na kwingineko wametaka hatua zichukuliwa ili kuwa fundisho hata kwa miaka mingine watu wasiendelee kulima maeneo ya mjini.
1 307
"Sio kwenye mitihani tu kwenye maeneo yote lawama zipo tu na ukiona unalaumiwa unafanya vizuri, usipo fanya vizuri watu wanasema chini chini hufanyi vizuri kwahiyo ukiona watu wanasimama na kukulaumu ujue mambo yako supa endelea"
"Lakini hakikisheni majukumu yenu yanaendana na shabaha ya sera ya elimu kama nilivyosema uratibu hususani katika upimaji na umahiri, tungependa kuwa na sera zinazosomana na kukamilishana" - Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1 307
ZIFAHAMU SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI USINYANYASWE FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI
IMEANDALIWA NA MAWAKILI
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAMU HAKI ZAO
JIFUNZE ZAIDI👇👇👇
https://youtube.com/channel/UCA9gimZo8zkeiXxpo8nZu7A
1 307
#Wajuakuwa: Kwa mtazamo, mtu angeweza kudhani kuwa Chinedu Ikedieze na Osita Iheme wanalingana kiumri. Walakini, kinyume chake ni kwamba Chinedu, ni mkubwa.
Chinedu Ikedieze ( Aki) ana umri wa miaka 43 na alizaliwa Bende, Jimbo la Abia, Nigeria, mnamo tarehe 12 Desemba, 1977, kwa familia ya Bwana na Bi. Michael Ikedieze Ogbonna. Alihitimu kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Usimamizi (IMT), ambapo alisoma Mawasiliano ya Misa.
Kwa upande mwingine, Osita Iheme (Ukwa) ana umri wa miaka 32 na alizaliwa mnamo 20 Februari, 1989, kwa familia ya Augustine Iheme na Herbert Iheme katika Jimbo la Abia, Nigeria.
Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jimbo la Enugu, ambapo pia alisoma Mawasiliano ya Misa.
Moja ya Kazi iliyowatambulisha, ni movie ya Aki na Ukwa miaka ya 2000. Marafiki Hawa KwA Sasa ni miongoni mwa matajiri wakubwa Nigeria .
Ni kazi Gani nyingine unayopenda toka kwa Hawa majamaa, dondosha comment yako hapa.
1 307
HAKEEM MWIGIZAJI BORA WA KIUME TUZO ZA FILAMU.
Kwa mujibu wa Tuzo za "Tanzania Film Festival Awards" Mwigizaji Hakeem Juma ndiye Mwigizaji bora wa kiume mwaka 2023.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Instagram story) Hakeem ameandika
"Alhamdulillah watu wangu, we did, nashukuru sana kwenu wote asanteni sana familia yangu, nawaahidi kufanya zaidi ili mzidi kufurahia kazi zangu, nawapenda sana Mungu anilindie nyie watu ili mpate mnachostahili kutoka kwenye kipaji changu, asanteni".
1 307
Baadhi ya mashabiki wa klabu ya Yanga wamemtaka raisi wa klabu hiyo, Eng Hersi anunue Uwanja wa Azam Complex uwe wao kwakua unawafaa sana na wanapata burudani na matokeo mazuri. Mashabiki hao wametoa kauli hiyo baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
