E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
CHINO NA WENZAKE WAPATA AJALI MBAYA YA GARI, KADHAA WAVUNJIKA MIGUU.
Dansa Chinokid pamoja na wenzake wamepata ajali mbaya maeneo ya Tanga mapema leo asubuhi wakiwa wanatokea Dar es salaam kwenda Moshi kwa ajili ya show. Kwenye ajali hiyo mbaya ambayo wamegongana uso kwa uso na gari kubwa "Fuso" madansa watatu wamevunjika miguu huku Chino mwenyewe akiwa amekandamizwa na kitu kizito kifuani.
1 307
⚠️ Mama Diamond Platnumz amewaasa wazazi wawe na kawaida ya kuvitilia maanani vipaji vya watoto wao tangu wakiwa na umri mdogo na pia wasapoti vipaji vya watoto wao kwa ujumla
Amesema yeye alianza kuona kipaji cha Diamond akiwa na miaka 2 na akaamua kumsapoti mwanae kwa hali na mali katika harakati zake kimuziki
Kwasasa Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wakubwa Afrika wenye mafanikio kupitia vipaji vyao
1 307
IRANKUNDA ATAITUMIKIA TIMU YA TAIFA YA AUSTRALIA
Mchezaji Nestory Irankunda Ambae mwakani anatarajia Kutua Katika Klabu Kubwa Duniani ya Bayern Munich Ataitumikia Timu ya Taifa ya Australia
Licha ya Kuzaliwa Kasulu Mkoani Kigoma kwenye kambi ya Wakimbizi Nduta Camp kutoka katika familia Yenye asili ya Burundi na Baadae kutimkia Nchini Australia Mchezaji Huyo ameamua kuchagua Kuitumikia Timu ya Taifa ya Australia
Licha ya kuwa na Asili ya Burundi Nestory Irankunda Hajawahi kufika au kuishi Nchini Burundi
Watanzania na Warundi Ubishani Uishe Leo kuhusu Nestory Irankunda chaguo lake Ataitumikia Timu ya Taifa ya Australia
Ameandika Ahmad Mkunda
1 307
UENYEKITI WA MANGUNGU NI KAMA BOYA "KIGWANGALLA
Uenyekiti wa Mangungu umekuwa kama boya tu, kamwe usimtazame Mangungu kama Eng. Hersi. Eng. Hersi ana mamlaka kamili. Huwezi kumpima mtu mwenye mamlaka kamili na Mwenyekiti jina tu! Ni umbumbumbu.
Tatizo la Simba linaanzia kwenye ‘Nani ana mamlaka’ ya kufanya maamuzi kwa niaba ya timu?
Ilipaswa kuwa Bodi. Siyo Mangungu peke yake. Nani anateua hiyo bodi yetu? Bodi ina nguvu za kiutendaji kweli?
Kwa hiyo kama wanasimba tunataka UWAJIBIKAJI (accountability), basi tulipaswa kufukuza BODI nzima! Lkini je tuna hizo nguvu? Jibu tunazo, na hatuna 😀. Unarudi pale pale kwenye tatizo la msingi - MUUNDO wa utawala! Tuusuke huu kwanza.
Najua Mangungu alitoa ahadi nyingi za kisiasa wakati anagombea, asamehewe tu! Alikuwa anatafuta kura tu huyu Mheshimiwa 😀
Acha nimrudishe shule ya Business Studies bwana Glezabhai. Wakati tunasoma MBA kulikuwa na hii makala muhimu sana ya mwaka 1995 ya John Pound, ikiitwa The Promise of the governed corporation kwenye zile Harvard Business Reviews. Akasome kisha ajirekebishe. Link hii hapa hbr.org/1995/03/the-pr….
Ameandika mwanachama wa Simba SC Dr Hamisi Kigwangalla ✍️
1 307
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ghana, Black Stars, Raphael Dwamena (28) amefariki dunia baada ya kuanguka uwanjani leo Baada ya kupata mshtuko Wa moyo Dakika ya 23 ya Mchezo wakati wa mechi kati ya timu yake ya Egnatia Rrogozhine ya nchini Albania dhidi ya Partizani.
Dwamena aligundulika kuwa na tatizo la moyo mwaka 2017 ambapo alifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa cha kurekebisha mapigo ya moyo mwaka 2020.
Licha ya hatua hiyo ya matibabu, Dwamena alipata tena shida mwezi Oktoba 2021 alipoanguka uwanjani katika mchezo kati ya Blau-Weiss na Harterg katika Ligi ya Austria.
R.I P Raphael Dwamena 🕊️
1 307
MASAKA ON 🔥
NYOTA wa Kimataifa wa Tanzania Aisha Masaka, amefunga mabao mawili leo kwenye ushindi wa mabao 4-0 waliopata timu yake ya @bkhackenofcl dhidi ya PITEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Sweden.
Masaka alifunga mabao hayo akitokea Benchi dakika ya 49 na 59. Sasa Masaka anakuwa amefunga mabao 5 kwenye mechi tatu za hivi Karibuni akiwa na Manjano hao wa Sweden.
Hivyo basi, anakuwa amejipa zawadi nzuri ya Birthday yake.
Happy birthday @aishamagoal_10
1 307
WANANCHI SUPU DAY: Mashabiki na wanachama wa Yanga, wamejitokeza hapa Makao Makuu ya klabu yao kunywa supu ikiwa ni sehemu ya sherehe za ushindi walioupata Novemba 5, 2023 dhidi ya Simba.
#WananchiSupuDay #YangaSC #SupuDay
1 307
Dar aliingia na Bodaboda, Dodoma akaingia na Bajaji, Chato ameingia na Farasi. Safari ijayo sijui ataingia na nini.
1 307
"Nimeanza kucheza mpira toka nikiwa darasa la 5. Mwaka 1999 nikapata ajari ambayo ilipelekea kupoteza mguu wangu mmoja.
Sikukata tamaa, bado nilichagua kucheza mpira, na mwaka jana nilifanikiwa kuwa mfungaji bora wa Afrika na kufanikiwa kuipeleka Tanzania kwenye kombe la dunia la watu wenye ulemavu.
Nataka kuwa mfungaji bora pia kwenye kombe la dunia mwaka 2026 na matarajio yangu ni kucheza kwenye ligi kubwa kama ya Uturuki na Uingereza". Halfan Kiyanga.
1 307
#TBT: Mtangazaji maarufu Salama Jabiri(aliyeshika notebook) enzi hizo kabla hajawa maarufu
1 307
GEITA, Chato: MAMA Janeth Magufuli ambaye ni mjane wa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli amempokea Paul Makonda nyumbani kwake Chato mkoani Geita na kumfanyia maombi maalumu ya kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi.
-
Pia Mama Janeth Magufuli alimsihi Makonda kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa bidii ili kufanikisha malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutimiza ilani ya chama.
-
Makonda anaendelea na ziara yake katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo Novemba 10, 2023 aliingia Chato mkoani Geita akitokea Bukoba na kutembelea kaburi la Hayati Magufuli pamoja na kuzungumza na wakazi wa Wilaya Chato.
1 307
GEITA: Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amefika kumsalimia Suzana Magufuli ambaye ni Mama mzazi wa Hayati John Pombe Magufuli, nyumbani kwake Chato mkoani Geita.
-
Makonda anaendelea na ziara yake katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo Novemba 10, 2023 aliingia Chato mkoani Geita akitokea Bukoba na kutembelea kaburi la Hayati Magufuli pamoja na kuzungumza na wakazi wa Wilaya Chato.
1 307
Watoto waliojeruhiwa wanaonekana katika hospitali iliyoko kusini mwa mji wa Ukanda wa Gaza wa Khan Younis. Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas ilisema jana (Ijumaa) kuwa zaidi ya Wapalestina 11,000 na Waisraeli 1,400 wameuawa tangu kuzuka kwa mzozo kati ya Israel na Hamas mnamo Oktoba 7.
1 307
Mapema leo hii huko Riyadh, Saudi Arabia kulikuwa na ugeni mzito sana ambapo raisi wa Iran Ibrahim Raisi, raisi wa Syria Bashar Al Asad, raisi wa Uturuki Tayyip Edorgan, raisi wa Palestine Mahmoud Abbas, pamoja na waziri mkuu wa Pakistan walikutana na mwenyeji wao mfalme Mohamed Ben Solmon kwajili ya kujadili mambo mengi kuhusu mzozo wa Palestine.
Baada ya kikao chao kufanyika na haya yalikuwa ni maneno ya raisi wa Iran Ibrahim Raisi 🇮🇷 na hotuba yake ililenga mambo makuu:
➡️Leo ni siku ya kihistoria katika kuutetea Msikiti wa Al-Aqsa. Tunalenga kufanya uamuzi madhubuti na wa kihistoria kuhusu kile kinachotokea katika maeneo ya Palestina.
➡️Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu lazima iwe na nafasi chanya na sahihi katika kubainisha maana za umoja na mshikamano.
➡️Leo kwa niaba ya Umma wa Kiislamu tumekusanyika ili kuwasaidia watu wa Palestina.
➡️Leo ni siku ya kihistoria kwa ulinzi wa Msikiti wa Al-Aqsa.
➡️Maandamano ya mamilioni ya watu duniani kote yanaonyesha kuwa ulinzi wa Palestina uko ndani ya kila taifa.
➡️Tunawajibika kwa Mungu kwa yale yanayotokea Gaza.
➡️Leo, kila mtu lazima atangaze msimamo wake.
➡️Marekani ni mshiriki katika uhalifu wa Israel.
NB: Ikumbukwe Saudi Arabia ni kibaraka wa USA na leo hii amempokea Iran na Syria ambao ni maswahiba wa Urusi. Uturuki tangu mwanzoni mwa mgogoro wa Israel dhidi ya Palestine imeamua kusimama upande wa Palestine licha ya kuwa yeye ni kibaraka wa NATO. Hapa kuna jambo mrusi analipika kwani ikumbukwe yeye ndiye msuluhishi mkuu wa migogoro mingi baina ya nchi za kiarabu.
Tunaishi kwenye zama za utandawazi na nidhahiri shahiri Kila kona ya dunia wengi wamesimama na Palestine kwani wanapinga uvamizi wa Israel kutaka kuwanyang'anya Palestine ardhi yao unaoungwa mkono na USA. Tayari Hezbollah wana silaha za mrusi, muungano wa nchi za kiislamu leo zimeazimia jambo moja tu kuwa wako kinyume na USA pamoja na Israeli kuhusu operation Yao pale Gaza.
Ndio kwanza kunakucha na hili nyuma yake Kuna Putin, na huyu mzee huwa haingii kifala kwenye vita ya aina yoyote ile. Sasa USA kamkimbia kule Ukraine soon wanakutana tena pale mashariki ya kati 😀🔥
1 307
⚠️ Mwanadada Loveness Tarimo amesema yeye ni mwanamke na ana jinsi ya kike hivyo wenye shaka na yeye waondoe
Loveness ni mwalimu wa mazoezi(gym trainer), aliwahi kushinda taji la Miss Fitness 2019. Pia aliwahi kuwa mshindi wa 2 wa Miss Figure East Africa
C&P
