fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
"Ni kweli Paula amekuwa kimya kwenye mitandao tofauti na watu walivyomzoea awali, mimi ndio nimemsimamisha tulikaa chini tuka
"Ni kweli Paula amekuwa kimya kwenye mitandao tofauti na watu walivyomzoea awali, mimi ndio nimemsimamisha tulikaa chini tukakubaliana kwa pamoja tukaona inawezekana. Unajua hawa wasichana wanapenda kukaa huko kwenye mitandao lakini wanaumizwa sana na comment za mashabiki" "Mimi niliongea nae nikamwambia kama komenti zinakuumiza basi inabidi uache kuitumia sana, kwahiyo na yeye alisikiliza maneno yangu na sasa hivi anaishi maisha yake bora zaidi. Sasa hivi nimemuacha anafanya mambo yake anayoyapenda zaidi naamini akirudi atakuwa na sura tofauti"- Marioo, Msanii wa muziki Tanzania. Toa maoni yako

Kutoka kwa Haji Manara “Leo nakuja na ombi kwa Artists wetu wa kibongo, nataka nitengenezewe wimbo maalum kwa ajili ya Zaiyli
Kutoka kwa Haji Manara “Leo nakuja na ombi kwa Artists wetu wa kibongo, nataka nitengenezewe wimbo maalum kwa ajili ya Zaiylissa , Nataka wimbo unaomzungumzia Zay wa Bugaa, wimbo wa kumsifu yeye, wimbo wenye lahaja za kimahaba!! Songi la kufungulia Mwaka.Haijalishi ni Hip hop, Bongo flavor,Taarab,Mchiriku,Rap au Singeli, nnachotaka wimbo uwe tayari kabla ya tarehe kumi January 2024 Ofa yangu ni Shilingi Milioni Hamsini, Studio na Video juu yangu ila haki zote za wimbo ni zangu Nb: Jina la Wimbo ni Zai Wa Buga,Msije na Majina yenu ya kibiringanya.Zaiylissa ❤️Save the date 18/01/2024” - Haji Manara

ni kumbukizi ya kuzaliwa Msanii wa muziki Tanzania na Mbunge wa zamani, Professor Jay. "Nakushukuru sana Mungu Baba Mwenyezi
ni kumbukizi ya kuzaliwa Msanii wa muziki Tanzania na Mbunge wa zamani, Professor Jay. "Nakushukuru sana Mungu Baba Mwenyezi , Muumba wa mbingu na ardhi na vitu vyote vilivyomo kwa zawadi hii ya Uhai kwa mara nyingine tena, HAPPY BIRTHDAY TO ME, Sina Cha kukulipa baba zaidi ya kutangaza Sifa zako na Utukufu wako siku zote za maisha yangu🙏🏻🙏🏻 NB: Kwa Mashabiki wangu nina zawadi ya kipekee ya VIDEO ya SIKU 462 leo kuanzia saa tatu usiku kupitia FRIDAY NIGHT LIVE ya EATV Kisha nitakuwekea YouTube yangu PROFESSOR JAY subsdribe sasa hivi ili uwe wa mwanzo kuiona, LETS GO🦾🦾🦾 NUSU PEPONI NUSU KUZIMU is Out in all digital platforms LINK on BIO👆👆👆 " ameandika Professor Jay, Msanii wa muziki Tanzania. Kheri ya kuzaliwa kwake na hongera kwa kuongeza mwaka mwingine au kutimiza miaka kadhaa.

⚠️😳🥰 Tajiri huyo namba moja wa kike duniani afikisha ukwasi wa dola bilioni $U100 wiki hii kupitia kampuni yake ya vipodozi ya L'Oreal ambyo ndio kampuninkubwa zaidi ya bidhaa za urembo duniani, ashika nafasi ya 12 kwa utajiri akichanganywa na wanaume Francoise Bettencourt Meyers(70) pichani aliurithi utajiri toka kwa mama yake mzazi aliyefariki mwaka 2017 kisha akauendeleza, yeye ndie alikuwa mtoto pekee kwa mama yake mzazi, mama yake nae aliurithi utajiri huo kutoka kwa baba yake mzazi nae akauendeleza yaani babu wa mrembo huyo pichani, Babu yake alikuwa mtaalamu wa kemia ambapo mwaka 1909 ndio alianzisha kampuni hiyo nchini Ufaransa baada ya kutengeneza dye ya nywele kwa lengo la kuuza Baadaye kampuni hiyo ya bidhaa ghari za kifahari ikakua na kukua na kuongeza bidhaa za urembo zikiwemo za ngozi nywele, perfyumu na nyinginezo Kampuni kwa miongo(decades) mbalimbali ishakuwa na executives ambao sio wanafamilia kabisa ingawa Familia imekuwa ikisimamia biashara kwa ukaribu Tajiri huyo wa kike ndie mwenyekiti wa L'Oreal na pia yupo katika bodi ya directors ya kampuni hiyo, yeye ameolewa na amezaa watoto wawili wa kiume ambao pia ni sehemu ya directos wa kampuni hiyo L'Oreal ndio kampuni kubwa zaidi ya bidhaa za urembo duniani na inamiliki kampuni tanzu zaidi ya 40 maarufu duniani katika bidhaa za urembo zikiwemo Maybelline na Lancome. Mabalozi wa makampuni hayo ni mastaa maarufu duniani wakiwemo wanamitindo, wanamuziki na waigizaji wa filamu, Marekani, India, Ufaransa na kwingineko ambao nao hulipwa.mkwanja mrembo kwenye mikataba yao Ukiacha hiyo, tajiri huyo wa kike pia ni mwenyekiti wa kampuni nyingine kubwa ya familia yake inayoitwa Tethys huku CEO akiwa mmoja wa watoto wake wa kiume Licha ya utajiri mkubwa alionao na kushika nafasi ya 12 kiduni akichanganywa na wanaume, lakini yeye sio mtu wa maisha ya kujioneshaonesha, kila siku hupenda kupiga piano kwa masaa kadhaaz pia ni muandishi wa vitabu, ameandika vitabu viwili hadi sasa, A five-volume study of the Bible and a genealogy of the Greek gods

photo content

Anne Rwigara (41), aliyekuwa mkosoaji wa Serikali ya Rwanda na mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa zamani nchini Rwanda, Assin
Anne Rwigara (41), aliyekuwa mkosoaji wa Serikali ya Rwanda na mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa zamani nchini Rwanda, Assinapol Rwigara amefariki dunia nchini Marekani saa chache baada ya kueleza kupatwa na maumivu makali ya tumbo. Rwigara alifahamika zaidi baada ya kukamatwa yeye na familia yake na kukaa gerezani kwa siku kadhaa mwaka 2017 baada ya uchaguzi wa urais wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukwepaji kodi na kupelekea mali za familia, kikiwemo kiwanda cha tumbaku na akaunti za benki kushikiliwa. Anne alishtakiwa kwa kosa la kukusudia kusababisha machafuko, kufanya uhalifu alioshirikiana na kaka yake na mama yake na mashtaka mengine na baadaye Anne aliachiliwa na mahakama, lakini dada yake mkubwa Diane, ambaye alitaka kuwania urais, na mama yake Adeline walikaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kwa mujibu wa Reuters, chanzo cha kifo cha mwanamke huyo bado kinatiwa mashaka hadi sasa na watu wa familia yake.

Urusi imefungua tena ubalozi nchini Burkina Faso baada ya kufungwa zaidi ya miaka 30 iliyopita, ishara ya kuendelea kuimarika
Urusi imefungua tena ubalozi nchini Burkina Faso baada ya kufungwa zaidi ya miaka 30 iliyopita, ishara ya kuendelea kuimarika kwa uhusiano baina ya nchi hizo tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso mwaka 2022. Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulianzishwa mwaka 1967, lakini Urusi ilifunga ubalozi wake mwaka 1992 na Burkina Faso ikafuata mkondo huo mwaka 1996.

HALIMA MDEE NA WENZAKE WANAKARIBISHWA ACT WAZALENDO Kauli ya Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu kwenye mahojiano maalum ya kufungia mwaka yaliyofanya na Mwanahalisi jana tarehe 29 Desemba 2023. “Ninatamka kwa kujiamini kabisa kwamba Halima Mdee na wenzake tunawakaribisha kwa mikono miwili ndani ya Chama cha ACT Wazalendo. Nafasi ipo kwa wao kuendeleza mapambano ya kuwatetea na kuwapigania Watanzania” “Mwanasiasa makini ni lazima upime kwenye mzani makosa ya mtu na mazuri yake. Mimi ninaweza kusema Halima Mdee na wenzake wana mazuri mengi kutokana na rekodi zao za nyuma. Makosa ninayoyasikia, yanasameheka” “Kwa maoni yangu, Mdee na wenzake ni kielelezo cha mapambano ya wanawake kwenye siasa. Wengi wao walifanya vizuri sana majimboni 2020 na hatuwezi kuliangamiza jeshi lote lile. Ni hasara kwa Taifa, ni hasara kwa harakati za ukombozi wa wanawake” “Kila mwanasiasa, na kila binadamu hukosea, muhimu ni kupima makosa na thamani ya mtu. Hilo ni jambo muhimu zaidi” “Hivyobasi, ninatamka kuwa wakati wowote, Mdee na wenzake wakihitaji kujiunga na Chama hiki, milango ipo wazi”- Ado Shaibu.

photo content

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Twitter👇 https://twitter.com/EplusMediaTv?t=OOCtdqDd1L27Uq8rLZ1UJg&s=09

photo content
+2

FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medi
+9
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/

photo content
+8

KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://yo
+9
KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK

Bila ushabiki wala uchawa tueleze vitu kwa "facts", kati ya "Show" ya Alikiba kwenye uzinduzi wa michuano ya African Football
Bila ushabiki wala uchawa tueleze vitu kwa "facts", kati ya "Show" ya Alikiba kwenye uzinduzi wa michuano ya African Football League Uwanja wa Benjamin William Mkapa Jijini Dar es Salaam na "Show" ya jana ya Diamond Platnumz kwenye uzinduzi wa Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar ipi ni "Show" kali zaidi? Zingatia "Set", "Light", "Performance ya Msanii", "Performance ya Dancers", "Sound", "Production ya Video" pamoja na mapokezi ya "Audience". Toa maoni yako

Hii picha ya Zari mbona "ina-trend" 🤔
Hii picha ya Zari mbona "ina-trend" 🤔

Dulla Makabila 😂 "List Yangu No 2 Ni Hii Hawa Watu Hawanaga Kabisa Mazoea Na Kiumbe Chochote Kile Zaidi Ya Wale Waliowazungu
Dulla Makabila 😂 "List Yangu No 2 Ni Hii Hawa Watu Hawanaga Kabisa Mazoea Na Kiumbe Chochote Kile Zaidi Ya Wale Waliowazunguka Aidha Familia Au Team Ambayo Wanafanya Nayo Kazi Na Ata ikitokea Umekutana Na Mmoja Wao Kati Yao Mkishamaliza Kitu Kilichowakutanisha Basi Kesho Yake Yupo Busy Na Mambo Yake Nafikili Life Style Yao Ni Nzuri Pia Sababu inawahepusha Na Vitu Vingi Kama Unafiki Unafiki Na Vitu Vingine Na Pengine Kufanya Ata Thamani Zao Ziendelee Kupanda Sio Kwa Mashabiki tu Mpaka Kwa Mastar Wenzao Binafsi Nawapenda Sana Kwa Namna Wameamua Kuishi Maisha Yao 👍 KESHO NAWAPA LIST NYINGINE MUWE KARIBU NA INSTAGRAM YANGU. - Dulla Makabila, Msanii wa muziki wa Singeli Tanzania Toa maoni yako

Licha ya nyimbo zake kuwa ndefu wastani wa dakika (7) hadi (13), Muimbaji wa muziki wa Injili Tanzania Bahati Bukuku amesema hajawahi kuandika nyimbo kwenye daftari kisha kwenda kurekodi studio kama wanavyofanya waimbaji wengi. Amesema yeye huwa anaenda studio na kichwa cha habari pekee kisha linapigwa beat anaanza kurekodi hapohapo. Bukuku amesema ni vigumu mtu kuamini lakini tangu anaanza kuimba huwa anafanya hivyo na hajawahi kuandikiwa wimbo na mtu. Album yake ya kwanza Yashinde Mapito aliirekodi kwa siku tatu pekee licha ya Albumu hiyo kuwa na nyimbo nyingi na zenye dakika nyingi. Toa maoni yako

photo content

Oscar Oscar ✍️ "Simba ndiyo Msanii mwenye Mafanikio zaidi katika historia ya Muziki wa Tanzania, kumchukia ni kujiiumiza bila
Oscar Oscar ✍️ "Simba ndiyo Msanii mwenye Mafanikio zaidi katika historia ya Muziki wa Tanzania, kumchukia ni kujiiumiza bila Sababu yoyote ya msingi. Watu kama Mbwana Samatta, Hasheem Thabit na Diamond Platinumz kwenye Sanaa na Michezo, walistahili hata kusomwa na Watoto wetu kwenye Mtaala Mpya wa Elimu. Jana pale Zanzibar kulikuwa na Legendary performance kutoka kwa 🦁. NB: kama unadhani namtetea Bosi wangu, ruksa na wewe kumposti Bosi wako" - Oscar Oscar, Mtangazaji wa Wasafi FM. Toa maoni yako