E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
SAD NEWS
Taarifa Rasmi zilizotolewa na kituo cha Radio cha B&B Kigali F.M wamethibitisha kuwa,Aliyewahi kuwa Kocha Simba na Baadae APR FC, raia wa Tunisia Dkt Adel Zrane, amefariki dunia hii leo, Aprili 2, 2024.😭
Aidha mchezaji wa zamani wa Simba ambaye alinolewa na kocha huyo, Taddeo Lwanga amethibitisha taarifa hizo.
Hadi umauti unamkuta Adel alikuwa ni kocha wa viungo wa Klabu ya APR ya Rwanda iliyoshiriki Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar Januari mwaka huu.
1 307
Aliyewahi kuwa Kocha wa Viungo wa Kikosi cha Simba Sc, Adel Zrane kutoka Tunisia 🇹🇳 amekutwa akiwa amefariki ndani ya Apartment aliyokuwa akiishi huko nchini Rwanda ambako alikuwa akihudumu na kikosi cha APR.
Aidha mchezaji wa zamani wa Simba ambaye alinolewa na kocha huyo, Taddeo Lwanga amethibitisha taarifa hizo
1 307
Mamia ya waumini wa Dini ya Kiislamu wanaojihusisha na mitandao ya kijamii wamelaani/kuchukizwa na kitendo cha muumini mwenzao na msanii nguli wa Muziki wa kidunia Duniani Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz baada ya kushiriki tamasha la mtoko wa PASAKA linalotafsiriliwa kama ( kusherehekea ufufuo wa mwana wa Mungu Bwana Yesu Kristo).
Akiwa kwenye tamasha hilo siku ya jana Diamond Platnumz alipanda jukwaani na kusoma moja ya mstari kwenye biblia, kitendo ambacho kimewafanya waumini wenzake wa dini ya Kiislamu wamuone ni mtu anayetapatapa na asiye na msimamo. Yote tisa, kumi Diamond Platnumz alinyanyuka kitini alipokuwa ameketi kisha kwenda kucheza mapambio na Christina Shusho baada ya wimbo wa Shusha nyavu kumnogea.
Wengi wamedai hawamtambui kama ni Muislam aliyethabiti kwasababu hana mwelekeo na hii sio mara yake ya kwanza kusherehekea ufufuo wa Yesu Kristo. hata hivyo Diamond Platnumz mwenyewe ameonekana kutokujali kwasababu yeye ndiye mkurugenzi mkuu wa Wasafi Media kivyovyote vile asingeweza kuacha kutoa sapoti kwa dini zingine ili kudumisha umoja na mshikamano wa Watanzania.
Mtoko wa PASAKA ni tamasha kubwa ambalo lilianza mwaka jana na liliandaliwa na Rose Muhando, Christina Shusho na Diamond Platnumz, lakini mwaka huu Rose Muhando amekaa pembeni na kuwaachia maandalizi Christina Shusho na Diamond Platnumz.
