E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
Treni ya Umeme ya Kisasa ya (SGR) ikipita maeneo ya Pugu Jijini Dar es Salaam katika majaribio yake ya kawaida. Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza majaribio ya Treni hiyo ya SGR kutoka Mkoani Dar es Salaam hadi Mkoani Pwani na hivi karibuni itaendelea na majaribio hayo mpaka Mkoani Morogoro. Huduma rasmi za Usafiri huo zinatarajiwa kuanza Mwezi wa Julai, 2024.
1 307
Hakika mtu sie nyau, pichani ni Farida wa Eliud Samwel akiwa kwenye muonekano wa kistaa zaidi.
1 307
Baada ya Zari kumpwelepweta, kumchezea kisha kufungasha virago kwake na kurudi geto kwake Uganda, Shakib ajitosa na muonekano huo akiwa amevalia suti mpya walau imliwaze.
1 307
"Ilikiwa ni majira ya saa 11 jioni, imekuwa ni ajali mbaya kwangu kushuhudia, nimeshuhudia watu wamepondekapondeka, wengine unamtoa kiwiliwili unakuta hana miguu imekatika, watoto wengi wanafunzi wa kizungu waliokuwa kwenye bus school wamepoteza maisha, kuna mtoto mmoja tumeshindwa kumuokoa tumejaribu kumvuta tukatoka na mguu mwili umekandamizwa na vyuma"
"Watu waliofariki ni wengi na ambao wapo kwenye hali mbaya ni wengi vilevile, wapo pia wazungu watalii waliokuwa wanaenda uwanja wa ndege wamefariki, nimeshuhudia ajali mbaya nipo kwenye majonzi mazito"- Shuhuda wa ajali ya Arusha Ngaramtoni iliyotokea jioni na kuua watu 25.
1 307
⚠️ Mwanadada mmoja kutoka Medina ameibuka kusema kwamba miaka mingi iliyopita alinyanyaswa kingono na mmoja wa ndugu zake wa kiume(cousin). Baada ya kufanyiwa ukatili husika alimuomba Allah(Mungu) ili ndugu husika asije kupata watoto katika maisha yake
Na sasa ni miaka 15 imepita tangu mnyanyasaji wake afunge ndoa ila bado hajapata mtoto yeyote
Muhanga huyo ameweka wazi kuwa anafurahi sana anapomuona mwanaume husika anavyopata shida kuhangaika kwenda kwa daktari mpya kila mwaka
Mwanadada amemalizia kwa kueleza kwamba anampenda sana Allah
1 307
⚠️😳 Mwanajeshi huyo wa nchini Uingereza ambaye ana mke wa kikiristo, aingia hatiani kwenye mikono ya sheria baada ya kufunga ndoa nyingine ya kiislamu na mwanamke wa nchini Kenya huku akidai hakuwa akijua kinachoendelea sababu shughuli ilifanyika kwa Kiswahili 😳
Sajenti Dravikula pichani aliletwa nchini Kenya na wenzie kwa ajili ya mafunzo ya kambi ya kijeshi na wakati akiwa Kenya akaingia katika mahusiano na mwanamke wa Kenya anayeitwa Kuki Watson kisha wakafunga ndoa mwaka 2021
Lakini mambo yalibumburuka kwa mabosi wa mwanajeshi huyo baada ya kutaka kusafiri na mke wake mpya kwenda nae Uingereza ndipo akaambiwa sheria za Uingereza haziruhusu ulichofanya hiyo ndoa mpya ni batili kwasababu bado yeye na mkewe wa kwanza wametengana tu ila sio kuachana rasmi kwa talaka kwani bado kesi yao inaendelea mahakamani
Mke wa kwanza walifunga ndoa huko Fijji mwaka 2011, mke wa kwanza ndie alilimbilia mahakamani kudai talaka, mume huyo baada ya kufunga ndoa hii ya pili amedai alijua haihesabiki ingawa sheria za Uingereza zipo wazi kutoruhusu mtu kuoa tena ikiwa talaka rasmi bado
1 307
⚠️😳 Jamaa huyo ameibuka kusema kwamba kinadada wanaovaa vipini vya pua na kuvaa vikuu miguuni huishia kuvutia wanaume wapenda ngono na sio sio wanaume wenye maono ya ndoa
1 307
⚠️😳🥰 Minong'ono yaibuka na watu kubaki midomo wazi kila mtu anasema lake kufuatia gauni hilo la send off na viatu alivyovaa mwanadada Alice pichani kugharimu shilingi milioni 4.5 za Kitanzania
Alice ni mtoto wa bilionea wa Tanzania, Wilson Gabusha wa jijini Moshi, Kilimanjaro. Alice alipoulizwa gharama za gauni hilo na viatu alivyovaa ndio amesema ametoa shilingi milion 4.5 tu
Hiyo tisa, kumi sherehe nzima ya send off pekee imetajwa kugharimu shilingi milioni 300 za Kitanzania 😳
1 307
Mke wa marehemu bilionea Msuya aachiwa huru na mahakama
Mahakama kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam imemuacha huru mfanyabiashara Revocatus Everist na Miriam Mrita mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao
Wawili hao walifikishwa mahakamani February 23 mwaka 2017 wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 103 wakituhumiwa kumuua mdogo wa bilionea Msuya, Aneth Msuya kwa kumchinja huko Kigamboni, Dar es salaam mwezi May 26, 2016
“Baada ya kujiridhisha pasi na kuacha shaka, mahakama hii inawaachia huru wawili hawa kutokana na upande wa mashtaka kutothibitisha makosa dhidi yao"
Pichani aliyesuka ni mke wa marehemu bilionea Msuya na aliyevaa kilemba ndie aliyeuwawa
1 307
Naibu Waziri wa Mambo ya nje Mhe. Jumanne Sagini mapema ya leo alipotembelea majeruhi wa ajali iliotokea Arusha Februari 24, 2024 waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru wakiwemo majeruhi 11 ambapo 7 kati ya hao ni Raia wa Mataifa ya Nje ya Tanzania.
Majeruhi wote wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mount Meru na hali zao za Afya zimeendelea kutengamaa wakiwa chini ya uangalizi wa Madaktari wabobezi wa kada Mbalimbali za Afya.
1 307
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini, leo februari 25,2024, amewatembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali iliyotokea Pass ya Ngaramtoni siku ya jana, Februari 24,2024, iliyohusisha lori na magari madogo matatu.
Mhe. Sagini amewatembelea majeruhi hao katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Arusha Mount Meru, kwa taarifa za mpaka hivi sasa, ajali hio imepelekea vifo 25 na majeruhi 21.
#ZBCUpdates
1 307
SERIKALI KUTOA SHILINGI MILIONI 1 KWA WALIOPOTEZA MAISHA KWA AJALI ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe.John V.K Mongela ametoa salamu za pole kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Watanzania wote, kwa niaba ya Serikali kufuatia vifo vya watu 25, vilivyotokana na ajali ya gari iliyotokea jana jioni Februari 24, 2024 eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru.
Mhe. Mongella ametoa pole wa ndugu jamaa na marafiki waliokusanyika nje ya jengo la kuhifadhia maiti, kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, wakisubiri maelekezo ya Serikali kuhusu msiba huo mapema leo Februari 25, 2024.
Amesema kuwa, Serikali inatoa shilingi milioni moja kwa kila marehemu, ikiwa ni ubani kwa ajili ya kugharamia shughuli za mazishi pamoja na kutoa jeneza kwa familia zitakazohitaji kulingana na imani za dini zao.
Amewasilisha salamu za pole kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi, wakiongozwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye yupo safarini Namibia kushiriki mazishi ya kiongozi wa nchi hiyo.
“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kwa wafiwa wote, na ameagiza tushirikiane kwa pamoja kama wanaArusha na kama watanzania, kuwafariji wenzetu, na kwamba Serikali iko pamoja na wafiwa wote, na ameagiza Serikali kutoa ubani wa shilingi milioni moja kwa kila marehemu kwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi pamoja na kugharamia matibabu ya majeruhi wote” Amesema Mhe.Mongella.
Aidha, Mhe. Mongella ameweka wazi kuwa, msiba huo ni wa watanzania wote na Serikali imetoa kibali kwa ndugu na familia za merehemu kuanza kuchukua miili kwa ajili ya mazishi na tayari baadhi yao wameanza kuchukua miili hiyo.
#Mbeyacityfm
1 307
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kwamba majeruhi wote wa ajali iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, mkoani Arusha waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru kupatiwa matibabu bila kulipa gharama zozote.
Hayo yamesema na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel aliyefika hospitalini hapo leo Februari 25, 2024 kuwajulia hali majeruhi hao.
Dkt. Mollel amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri na mmoja amepewa rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC mjini Moshi.
"Rais Samia Suluhu Hassan ametuelekeza majeruhi wote wa ajali hii kupatiwa matibabu bila kulipa gharama zozote", amesema Dkt. Mollel
Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na Watanzania kwa ujumla kuwa watulivu wakati wakiendelea kuwatibia majeruhi na kwa wale waliopoteza ndugu zao utaratibu wakupatiwa miili unaandaliwa na wataalamu.
#AzamTVUpdates
Picha | Wizara ya Afya
Imeandaliwa na Claud Mshana
1 307
HUYU MTUMISHI ALIFARIKI NA MKE WAKE JANA KWENYE AJALI ILIYO UWA WATU 25 ARUSHA NGARAMTONI
PUMZIKA KWA AMANI
