E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
NUSRAT HANJE JIKO JIPYA LA MAULIDI KITENGE
Mtangazaji nguli wa Michezo Kutoka Wasafifm Maulid Kitenge
amefunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum Nusrat Hanje.
Harusi hiyo iliyofanyika kwa usiri mkubwa katikati ya wiki iliyopita imeibua mjadala mkubwa kwa kile kinachodaiwa mtangazaji huyo mkongwe kutowaalika marafiki zake wa karibu ambapo watu saba tu ndio walihudhuria tukio hilo.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram wa Mbunge Nusrat Hanje amethibitisha Hilo Kwa Kuweka Post "Happy birthday Mume Wangu" Huku akiambatanisha Picha ya Maulid Kitenge
1 307
Jamani vipara Hua vinawenyewe vipi Huyu msukuma kimemkubari au anazingua tu na fashion za watu😆😜🤸
1 307
Huyu ni Mwamuzi wa Pembeni aliyesimamia mchezo wa kirafiki kati ya Simba U17 na Serengeti Boys U17 katika dimba la Mo Simba Arena.
Katika mchezo huo Serengeti Boys walipoteza kwa goli 3 - 1.
Vipi Aruhusiwe Kuchezesha Ligi Kuu??
1 307
Tajiri Namba Moja Barani Afrika Aliko Dangote Ametoa magunia milioni moja ya mchele yenye thamani ya dola milioni 19.6 (49,917,868,000 Tsh) kusaidia kupunguza mapambano ya kiuchumi yanayowakabili Wanigeria.
Dangote wakati huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, anatoa chakula Bure kwa watu zaidi ya Elfu 10,000 kila siku katika jimbo alilozaliwa la Kano
1 307
SAFARI YA JENERALI MUHOOZI KAINERUGABA KUWA MKUU WA MAJESHI- UGANDA
Hii ndio Safari aliyoipita Jenerali MUHOOZI KAINERUGABA Mtoto wa Rais wa Uganda Yowery Kaguta Museven kuwa Mkuu wa Majeshi wa Nchi Hiyo
2000: Aliteuliwa kuwa Luteni wa pili, Kitengo cha Ulinzi wa Rais (PPU)
2001: Alipandishwa cheo kuwa Kapteni
2003: Alipandishwa cheo kuwa Meja na urekebishaji wa PPU katika Kikosi cha walinzi wa Rais (PGB)
2008: Alipandishwa cheo kuwa Luteni-Kanali na kuteuliwa kuwa Kamanda wa Vikosi Maalum katika UPDF
2010: Aliteuliwa kuwa kamanda wa Kwanza wa Kikundi Cha Vikosi Maalum (SFG)
2011: Alipandishwa cheo na kuwa Kanali
2012: Alipandishwa cheo na kuwa Brigedia Jenerali
2016: Alipandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali
2017: Ateuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa Rais wa Majukumu maalumu
2020: Aliteuliwa kuwa Kamanda wa vikosi maalumu
2023: Alipandishwa cheo na kuwa jenerali
Machi
2024: Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Uganda
NB: Rais Museven ALIEWAHI kusema kuwa Ikulu aliipata kupitia mapambano ya msituni Hivyo Basi Kama Kuna mtu anaye ona Yowery Museven anakosea Basi naye aende msituni 😊
1 307
Mshiriki kutoka Nchi ya Ivory Coast, Ibrahim Sow (14) ameibuka mshindi wa Mashindano Makubwa ya Kusoma Quran ya Afrika na kuzawadiwa kitita cha Dola za Marekani 10,000 (Tsh. milioni 27).
Akiwa kama mshiriki mdogo kuliko wote miongoni mwa washiriki 21 kutoka bara la Afrika na wengine waalikwa kutoka nje ya bara hilo. Mshiriki mwenye umri mkubwa alikuwa na miaka 25.
Mashindano hayo yamefanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Machi 24, 2024.
1 307
NILI INGILIWA NA NDUGU WA BABA "LAKISHA"
Rapa LakishaTz ambaye Staa wa Bongofleva DiamondPlatnumz alizama DM kumpongeza na wimbo wake "EX WANGU" Akiongea na Moja ya chombo Cha Habari Lakisha amefunguka mkasa mkubwa aliokutana nao kwenye maisha yake ambapo anasema kuwa ALIBAKWA NA NDUGU WA BABA YAKE kipindi akiwa Mdogo...
1 307
⚠️Dr.Modest Bafite afunguka kwa kirefu...
"Wanawake wajinga wachache walishindwa kuelewa busara za mababu, hao wanawake walishindwa kuelewa kuwa future ya dunia inawategemea, hao wanawake walishindwa kuelewa kuwa ustaarabu wa dunia unawategemea, hao wanawake walishindwa kuelewa kuwa tafsiri halisi ya maisha bila usimamizi wa mwanamke haiwezekani
busara za mababu ilikuwa mwanamke hatakiwi kupata elimu, hatakiwi kufanya kazi au biashara, walikua kazi walioyonayo ni kubwa mno na ngumu hivyo hawakutaka kuwaongezea mzigo, kazi kubwa ya mwanamke ilikuwa ni kulea FAMILIA,
na kazi ya mwanaume ilikuwa ni kutunza familia, wanawake hao wachache wajinga walionesha kuwa huu ni uonevu, udhalilishaji na ukandamizwaji, walichokisahau ni kwamba kulea ni kuandaa future na kuandaa future sio kazi rahisi, ( Tunaopambana kuandaa Kesho yetu tutakuwa tumeelewa, Kuiandaa kesho sio kazi rahisi ndio maana tunapambana usiku na mchana ili kesho yetu tusiyoijua iwe nzuri )
hao wanawake wachache wasio na akili wakaja na slogan ya haki sawa, Mwanamke anaweza bila kuwezeshwa, Mwanamke kazi yake sio kulea, Mwanamke hatakiwi kukaa nyumbani, Mwanamke na mwanaume wote ni sawa.
Wanawake wengi wenye akili wakanasa kwenye huo mtego wakashirikiana na wajinga and kupaza sauti, kwakuwa mwanamke ni wa thamani sana katika hii dunia, na yeye ndio muandaa future ya dunia, sauti yake ikasikika na ikaheshimika, Mwanamke akapelekwa shule, Mwanamke akapewa kazi, Mwanamke akaanza kufanya biashara, akasahau majukumu yake, akasahau mission yake duniani, Mwanamke akatumia nafasi aliyopewa kuwa Mtunzaji na sio Mleaji,
Mwanaume akakosa kazi ya kufanya, hawezi kulea, na akitunza huo utunzaji hauthaminiki, taratibu akaanza kuvunjika moyo, uwezo wa Mwanamke ukamfanya amuone mwanaume si kitu na hawezi kumwambia chochote,
Mwanamke akatumia nguvu aliyopewa vibaya, hizo nguvu zikamdhoofisha mwanaume, ndani ya nyumba mwanamke akawa ndio mwenye kauli, mtoto akakosa malezi bora, kwakuwa mleaji mzuri ni mwanamke na kasahau wajibu wake
matokeo yake sasa future imeharibika, malezi bora na upendo wa mama kwa mtoto vimepotea kwasababu mama yupo busy kujiimarisha kiuchumi, wameamua kuajiri wafanya kazi wa malezi, Wamesahau kazi ya kulea haihitaji mfanya kazi, kutokana na hilo tumepata kizazi cha Wasagaji na mashoga
, kizazi cha vijana wa kiume wasiotaka kufanya kazi maana mwanamke amechukua nafasi ya utunzaji, kizazi cha mwanamke asietaka kuwa chini ya mwanaume kwasababu ana uwezo kiuchumi, hii imepelekea mwanaume kupoteza nguvu yake ya asili ya uongozi na ya utunzaji, amepoteza confidence yake hivyo ameamua kuwa chini ya mwanamke,
kilichobaki kwasasa ni wanaume kufikiria kuimarisha nguvu za kiume kwasababu hawana kingine chaku offer tena katika hii dunia ya wanawake wenye nguvu, matokeo yake wanaume wamekuwa legelege, hawana maamzi, hawana chakufanya, Mwanamke akimchoka anamfukuza,
mwisho wa siku anaangukia kwenye pombe na umalaya, watoto wakiume ndio wanakuwa vulnerable kwasasa, na kupelekea future ya dunia kupoteza muelekeo kwasababu waliotakiwa kuiandaa wameacha jukumu hilo nakujitwisha kazi nyingine,
Kwasasa wamejitokeza wanawake wachache wenye akili timamu wanaotaka kuirudisha dunia kwenye mstari, wamegundua Dunia uliyo has wanaume legelege sio dunia now wameanza kampeni ya TUMLINDE MTOTO WA KIUME, wamegundua sasa kuwa DUNIA BILA NGUVU YA MWANAUME SIO DUNIA, wamegundua pia kuwa DUNIA BILA MALEZI BORA KUTOKA KWAO HAINA FUTURE,
N.B: haijawa too late, wanawake bado mnaweza kuikoa dunia na kubadili future yake mkitaka, tunawategemea katika hili, bila malezi yenu katika hii dunia tunakoelekea ni pabaya sana miaka 20 ijayo, msipo si duka mtajuta sana.
#Dr_Modest
1 307
⚠️😳 Baba alikuwa na kawaida ya kumnyanyasa mama kwa vipigo - mtoto wa Ngugi Wa Thiong'o(86)
Mukoma Wa Ngugi(53) ambaye ni mwandishi wa vitabu, mshairi pia profesa wa chuo kikuu amewashtua watu baada ya kuibuka kuweka wazi kuwa baba yake yaani Ngugi Wa Thiong'o ambaye ni mwandishi maarufu zaidi wa vitabu kutoka Kenya, na mwenye jina kubwa Afrika katika fasishi alikuwa na kawaida ya kumnyanyasa mama yake mzazi(Nyambura) mara kwa mara kwa vipigo na kuna kuna wakati mama yake alikimbilia kwao kupata hifadhi
Mukoma ameyasema hayo baada ya kuweka kipande cha habari katika gazeti kumhusu mama yake ambaye alifariki katikati ya miaka ya 1990s. Ameonesha upande huo mwingine wa baba yake kutoelezwa kwa kufunikwa na umaarufu katika kazi zake za uandishi wa vitabu
Nyambura alikuwa mke wa kwanza wa Ngugi Wa Thiong'o na walifanikiwa kupata watoto 6, na si chini ya watoto wake 4 kutoka mke wa kwanza walipata elimu zao za vyuo vikuu nchini Marekani
Kuvunjika kwa ndoa ya Ngugi Wa Thiong'o na Nyambura kumetajwa kuchochewa na mwandishi huyo maarufu mara kwa mara kuwekwa kizuizini na kukimbilia kuishi nje ya nchi uhamishoni(exiles) wakati wa utawala wa Jomo Kenyetta na hata Daniel Moi
Mkewe wa kwanza alipofariki Ngugi hakuweza kurudi kumzika sababu ya kukimbilia kuishi uhamishoni nje, nchini Marekani
Akiwa Marekani baadaye Ngugi Wa Thiong'o alimuoa Njeeri ambaye alimkuta na mtoto mmoja kutoka mahusiano yake ya awali kisha walifanikiwa kupata watoto wengine wawili kabla ya kuachana mwaka jana, sababu za kuachana kwao hazijulikani japo Njeeri nae anatajwa kuwa msomi anayeishi na kufanya kazi Marekani
Kwasasa Ngugi anaishi mwenyewe Marekani akiwa na changamoto za kiafya kwa figo zake kushindwa kufanya kazi vizuri ambapo anaangaliwa na wahudumu wa afya kwa ukaribu, anasafishwa figo mara tatu kwa wiki
Ngugi ambaye ana tuzo lukuki katika fasihi, kwa miaka mingi amekuwa ni profesa upande wa fasishi katika chuo kikuu cha California, Irvin nchini Marekani. Miongoni mwa vitabu vyake maarufu vinavyotumika shuleni na vyuoni katika kufundishia ni pamoja na Weep Not Child, The River Between, Petals Of Blood, Wizard Of The Crow, Decolonising The Mind, pia kitabu cha I Will Mary When I Want alichoshirikiana kukiandika akiwa na Ngugi Wa Mirii
1 307
⚠️😭 Mustafa Sabodo afariki dunia. Bilionea huyo ambaye pia ni mchumi kitaaluma, alizaliwa mkoani Lindi na wazazi wenye asili ya Kihindi na kupata sehemu ya elimu yake Tanzania na baadaye kuongeza elimu ya juu nje ya nchi na kufanya kazi huko
Katikati ya miaka ya 1990s alirudi Tanzania kufanya uwekezaji
Enzi za uhai wake alikuwa mchangiaji mkubwa wa kimaendeleo ikiwemo katika sekta ya elimu kwa kujenga shule, kutoa fedha kusaidia kujengwa chuo cha uwalimu, kusaidia sekta ya afya pia kusaidia kujenga visima zaidi ya 280 Tanzania
1 307
Sina ndoa wala mtoto sijisikii kwasasa, naogopa kuwa single mother - Flaviana Matata(36)
Mwanamitindo wa kimataifa toka Tanzania, Flaviana Matata amesema kwasasa hana ndoa pia hayupo kwenye mahusiano. Alipoulizwa na Rickmedia hata hivyo Flaviana amesema anawaheshimu wanawake wanaolea watoto peke yao ila kwake yeye anaona ni ngumu hatoweza kulea peke yake
Flaviana ambaye pia aliwahi kuwa mshindi wa Miss Universe Tanzania 2007 kisha kuingia top 6 katika shindano la dunia nchini Mexico, mwaka 2015 alifunga ndoa na mwanaume wa Kitanzania anayeitwa Deo Massawe mwaka 2019 ndoa yao ikavunjika na kupeana talaka. Miaka miwili baadaye yaani 2021 Flaviana kwa mara ya kwanza alifunguka kuhusu ndoa kwa kueleza yafuatayo...
“Hakuna anayefunga ndoa ili mwisho wa siku aishie kwenye kupewa talaka, nikiongea kwa kutumia uzoefu wangu, mwaka 2019 nilitalakiana lakini mitandao haikuniacha hata nipumue, ilikuwa ni kama nimefanya mauaji, kwa sasa nipo kwenye hali nzuri na nimepona, nawashukuru watu wangu wachache wa karibu kwa kuwa na mimi katika kipindi chote, ni kwa vile baadhi yetu tumechagua kuficha maumivu yetu kwenye hadhira”- Aliandika Flaviana kisha kuongeza
“Kwenye mitandao kunaweza kuwa na ukatili na hii inapelekea kutengeneza ugumu kwa watu kuongelea matatizo yao isipokuwa kwa watu wao wa karibu pekee, hatushiriki kumsaidia mtu yeyote kwa kumdhihaki pale ndoa yake inaposhindwa kuendelea mbele, na hii ndio sababu ya kwanini watu wengi wanabaki kwenye ndoa zenye unyanyasaji na uonevu.” Alisisitiza Flaviana ambaye muda mwingi anaishi Marekani na kuja Tanzania mara kwa mara kikazi na kusaidia wasichana walio katika mazingira magumu
1 307
⚠️😳 "Siwezi na sipendi kutafuna vitu vigumu kwasababu sijalelewa hivyo maana wazazi wangu walinidekeza. Na naamini nitapata mwanaume ambaye hapendi kutafuna vitu vigumu kama mimi ili twende sawa" - Halima Kopwe, Miss Tanzania.
