fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
MIMI NDIO TAJIRI WATOTO WANGU WATAFUTE PESA ZAO Nyota wa zamani wa #NBA , #ShaquilleRashaunO'Neal amewachana watoto wake sita
+2
MIMI NDIO TAJIRI WATOTO WANGU WATAFUTE PESA ZAO Nyota wa zamani wa #NBA , #ShaquilleRashaunO'Neal amewachana watoto wake sita kuwa Pesa alizonazo na Utajiri alionao sio wao bali ni wa kwake hivyo na wao wajitafutie pesa zao. Mpaka sasa #Shaq anakadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Sh.Trilioni 1 na anaamini kuwa pesa hizo amezitafuta yeye na sio watoto wake kauli yake kwa watoto wake ni "Sisi sio Matajiri, Mimi ni Tajiri" kauli ambayo watoto wake hawapendezwi nayo.

Muonekano mpya wa Eric Omondi 🤔.
Muonekano mpya wa Eric Omondi 🤔.

Osaka, Japan 🇯🇵. May 2023.
Osaka, Japan 🇯🇵. May 2023.

Wachezaji wa timu ya wanawake ya Ivory 🇨🇮 Club, Athletico FC of Abidjan iliyoshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika wanawa
Wachezaji wa timu ya wanawake ya Ivory 🇨🇮 Club, Athletico FC of Abidjan iliyoshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika wanawake.

"Bado sina mtoto na nasubiri ndoa ndiyo tuanze kutengeneza familia ila sasa hivi tupo kwenye mipango ya kufunga ndoa" @tarimo
"Bado sina mtoto na nasubiri ndoa ndiyo tuanze kutengeneza familia ila sasa hivi tupo kwenye mipango ya kufunga ndoa" @tarimoloveness491

Utafiti umeeleza kuwa zaidi ya theluthi moja (asilimia 35) ya wanawake walioolewa au wanaoishi na wenza wa karibu wamewahi ku
Utafiti umeeleza kuwa zaidi ya theluthi moja (asilimia 35) ya wanawake walioolewa au wanaoishi na wenza wa karibu wamewahi kufanyiwa ukatili wa kimwili, ikilinganishwa na asilimia 4 ya wanawake ambao hawajawahi kuolewa. Miongoni mwa wanawake walioachika, kutengana au wajane, asilimia 50 wamewahi kufanyiwa ukatili wa kimwili.

Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, imeyafutia usajili mashirika 9, ikiwemo Taasisi ya Mo Dewji Foundation, in
Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, imeyafutia usajili mashirika 9, ikiwemo Taasisi ya Mo Dewji Foundation, inayomilikiwa na mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohamed Dewji. Taarifa iliyotolewa Bodi hiyo imeeleza kwamba mashirika hayo yameomba kufutiwa usajili kwa hiyari. Mo Foundation ilikuwa ni mmoja wa wadhamini wa klabu ya Simba na nembo yake ilikuwa ikikaa nyuma ya jezi za klabu hiyo.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema bangi ni dawa haramu inayoongozwa kwa kupatikana na kutum
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema bangi ni dawa haramu inayoongozwa kwa kupatikana na kutumiwa zaidi nchini ikifuatiwa na heroin, mirungi na cocaine na hivi karibuni methamphetamine ambapo amesema dawa hizo zina madhara ya kiafya ikiwemo Mtu kuona visivyokuwepo na kupelekea kufanya vitu visivvyofaa kwenye Jamii. Akiongea Jijini Dar es salaam leo, Kamishna Msaidizi wa Kinga na Huduma za Jamii DCEA, Moza Makumbuli amesema bangi ni miongoni mwa vileta njozi ambapo humfanya Mtumiaji kuhisi, kuona au kusikia vitu visivyokuwepo au tofauti na uhalisia. Makumbuli amewataka Watanzania kujiepusha na matumizi ya bangi na dawa nyingine za kulevya kwakuwa zina madhara huku akishangaa Watumiaji wa mitandao kutofurahia pale madhara ya bangi yanaposemwa au bangi ikikamatwa “Suala la bangi ni mtihani inaonekana wengi wanatumia, hata ukiangalia habari mfano ile ya biskuti za bangi mtandaoni comment za Watu ni kama vile wanaona bangi inachelewa kuhalalishwa, bangi haifai tujiepushe kutumia”

Mtangazaji Nguli Salim_kikeke ametangaza rasmi kujiunga na @dstvtanzania ambapo atakuwa anaendesha kipindi kinachoitwa #SupaS
Mtangazaji Nguli Salim_kikeke ametangaza rasmi kujiunga na @dstvtanzania ambapo atakuwa anaendesha kipindi kinachoitwa #SupaSoka na kutangaza Mechi za England kwa Lugha ya Kiswahili.

"Sijui kufua, kupika nitajaribu"- Madam Ritha "Nataka kubadili dini nitoke kwenye Ukristo niwe Muislam, na sitabadili kwasaba
"Sijui kufua, kupika nitajaribu"- Madam Ritha "Nataka kubadili dini nitoke kwenye Ukristo niwe Muislam, na sitabadili kwasababu ya mwanaume, ni mimi mwenyewe nimeamua kwasababu napenda mambo ya Kiislamu. Kufua sijui na hii itakuwa ngumu kidogo kwangu kwasababu dada yupo ananifulia, lakini pia kuna mashine za kufulia ila kupika niko vizuri kiasi"- amesema Ritha

#HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikano wa Afrika Masharkiki wa Tanzania, January Makamba, amesema amepata ahadi ya bina
#HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikano wa Afrika Masharkiki wa Tanzania, January Makamba, amesema amepata ahadi ya binafsi kutoka kwa Waziri wa mambo ya nje wa Israel Israel ya kusaka wanafunzi wawili wa Kitanzania ambao walipotea mwezi mmoja uliopita wakati wa kuanza tena kwa mapigano na Palestina. Serikali ya Israel imewataja wahitimu wa kilimo Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga kati ya mamia ya mateka wanaoshikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas huko Gaza tangu Oktoba 7, wakati walipofanya shambulio dhidi ya eneo la Israel, kusababisha mfululizo wa mashambulizi ya kulipiza kisasi yenye umwagaji damu. Mamlaka ya Tanzania bado haijathibitisha rasmi uwezekano wa utekaji nyara, wakisema tu kwamba wanafunzi wawili kati ya raia wake wa takriban 260 nchini Israel hawajulikani walipo tangu shambulio la Hamas.

Haji Mnoga,Ben starkie,Simon msuva na Kwesi kawawa tayari wamewasili nchini Tanzania kujiunga na kambi ya timu ya taifa kujia
+1
Haji Mnoga,Ben starkie,Simon msuva na Kwesi kawawa tayari wamewasili nchini Tanzania kujiunga na kambi ya timu ya taifa kujiandaa na michezo ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Morocco na Niger. Picha na TFF

"Mimi nawashauri Kajala na Paula brand muda mwingine inaweza ikawa nzuri kuihusisha na biashara lakini kuna muda mwingine bra
"Mimi nawashauri Kajala na Paula brand muda mwingine inaweza ikawa nzuri kuihusisha na biashara lakini kuna muda mwingine brand haiwi nzuri kuihusisha na biashara, mimi ningefarijika sana kama wangefungua biashara yao bila kuhusisha brand zao. Kwasababu kwenye brand zao kuna watu wanawakubali na kuna watu wasiowakubali, Sina uhakika kana biashara yao itafanya vizuri kwasababu wameihusisha na brand zao moja kwa moja" "Tusipepese macho, Kajala na Paula kuna sehemu wamefanya vizuri lakini pia kuna sehemu jamii iliwaona kama watu wa ajabu. Kwahiyo kuna watu wanaweza kwenda dukani kwao kununua nguo lakini kuna wengine hawatotamani hata kusogea, mimi ningetamani kama watafungua biashara nyingine huko mbeleni waitofautishe biashara na brand zao, waipe jina tofauti na majina yao au wajifanye kama ni mabalozi wa hilo duka wanamupromoti mtu lakini kumbe linakuwa ni duka lao, watauza sanaa"- Mwijaku

msee akakamulia na ndimu kwenye supu 😅
msee akakamulia na ndimu kwenye supu 😅

Kuna Kitu KINAKUJA! ........C.E.O Wa Zamani wa SimbaSc ,Barbara Gonzalez akiwa Sambamba na RAIS Wa Heshima Wa SimbaSc ,Mo Dew
Kuna Kitu KINAKUJA! ........C.E.O Wa Zamani wa SimbaSc ,Barbara Gonzalez akiwa Sambamba na RAIS Wa Heshima Wa SimbaSc ,Mo Dewj . Guess What!!

"Kuna siku nilivaa kigodoro nikakipangilia ukiniangalia utasema kalio la Zari the Boss Lady, M'baba akapagawa na mimi akaanza
"Kuna siku nilivaa kigodoro nikakipangilia ukiniangalia utasema kalio la Zari the Boss Lady, M'baba akapagawa na mimi akaanza kunitongoza kila nikimkataa ananipiga na elfu 10, nikasema hapa nitayazua yule baba akawa ananifata kila kona nikasema huyu asiniponze. Nikaenda kulivua nikarudi alivyoniangalia akaniambia mama mimi sikupenda sura yako nililipenda kalio kwahiyo sikutaki" "Nikamwambia baba samahani niache, naishi alivyoniumba Mwenyezi Mungu na uzuri wangu wa asili. Wanaume ndio wanatuponza sisi wanawake kwasababu wao ndio wanatushawishi tuhangaike. Mijanaume inayopenda makalio mimi naona ni mishamba tu kwasababu wewe mwanaume mzima uliyekamilika huwezi kunyanyapaa wanawake kwa kuwabagua vimbaumbau na kuwapenda wenye shepu"- Zai Kijiwenongwa

Wachezaji wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” wakiendelea na mazoezi kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia vs Niger na Mor
+4
Wachezaji wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” wakiendelea na mazoezi kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia vs Niger na Morocco , mazoezi yamefanyika uwanja wa JKT, Kunduchi

Miss Nairobi 1966. #Kenya..
Miss Nairobi 1966. #Kenya..

DEE KIPENZI CHA WATU TIKTOK AFARIKI DUNIA. Ukiingia Tiktok leo kumejaa majonzi, simanzi na maombolezo, ni baada ya kuja kwa t
DEE KIPENZI CHA WATU TIKTOK AFARIKI DUNIA. Ukiingia Tiktok leo kumejaa majonzi, simanzi na maombolezo, ni baada ya kuja kwa taarifa kwamba Dee mtoto ambaye alikuwa kipenzi cha watu kwenye mtandao wa Tiktok amefariki dunia baada ya kupata ajali ya bembea. Yeye na Dada yake Kamamaa walijizolea umaarufu kutokana na vituko vyao ambavyo vimekaa kwenye muundo wa maigizo. "Assalam Aleykum, innah lillah wa innah illaihi rajiun. Leo alfajiri tumempoteza mtoto wetu Dee kwa ajali ya bembea, naomba dua zenu tupo katika wakati mgumu. Tulimpenda ila Mungu kampenda zaidi"- imesema familia Moja ya ndoto kubwa za Dee ilikuwa ni kukua haraka ili awe Rubani amsaidie mama yake. "Mamaaa mimi nataka kuwa mkubwa haraka nina ndoto zangu nyingi, mimi nataka kukua ili niwe Rubani haraka ili nikusaidie wewe utakapokuwa hauna pesa💔"-Aliwahi kusema Dee. Ama kwa hakika inauma lakini tumuombee 🙏

photo content
+7