E-PLUS MEDIA
رفتن به کانال در Telegram
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
1 307
"Suala la akina Mdee sasa hivi sisi tunachosubiri waondolewe bungeni. Nimekwisha mwandikia barua spika na imepelekwa. Kwahiyo, kwa sasa umma, vyombo vya habari ni kumuuliza spika popote pale alipo baada ya kuwa amepokea barua ya CHADEMA." - John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA
1 307
Klabu ya TJ Tatran ya nchini Slovakia inajivunia kuwa na moja ya uwanja wa kipekee duniani unaitwa Cierny Balog wenye njia ya reli inayopita karibu na sehemu ya kuchezea.
Cierny Balog, mji mdogo wa Slovakia wenye watu wapatao 5,100, umekuwa sehemu ya watalii.
Mnamo mwaka wa 2015, video ilionesha treni likitipia karibu na wachwazaji waliokuwa uwanjani na kuwaacha watu wengi kwenye mshangao.
Je tukio la mara moja tu, au kweli kulikuwa na treni iliyokuwa ikipita mara kwa mara kwenye uwanja?
Uwanja wa Cierny Balog ulijengwa miaka ya 1980, wakati ambapo reli iliyopita uwanjani hapo haitumiki. Haijulikani kwa nini manispaa ya mji huo ilichagua eneo hilo kujenga uwanja wa mpira.
Mambo yalibadilika mwanzoni mwa miaka ya 1990, Ulipoanza ukarabati wa njia hiyo ya treni. Mnamo 1992, ilifunguliwa tena kama reli ya urithi kwa watalii (yani reli ya zamani)
Watalii wanaotaka kuvutiwa na uzuri wa milima ya Lower Tatras wakiwa ndani ya treni wanaweza kununua tikiti za treni ya zamani ambayo inapita kwenye mstari wa urefu wa kilomita 17 kati ya Chvatimech na Vydrovo, kupitia uwanja wa Cierny Balog ni moja wapo ya mambo muhimu ya safari.
1 307
Wanafunzi 72 wamehitimu mafunzo ya uhudumu wa ndani ya ndege ( cabin crew) yaliyotolewa na Kituo cha Mafunzo cha Air Tanzania (ATTC) Jijini Dar es salaam na kufanya idadi ya Wanafunzi waliopatiwa mafunzo toka kuanzishwa kwa kituo hicho miaka 10 iliyopita kufikia 600.
Kwenye mahafali hayo yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi amesema maombi ya kujiunga na kozi ya uhudumu wa ndani ya Ndege katika Kituo hicho yameongezeka maradufu na kusema maombi yaliyopokelewa September 2023 pekee ilikua ni zaidi ya Watu 500 lakini wakapatikana 72 tu baada ya mchujo.
Matindi amesema mojawapo ya kozi mpya zilizoanzishwa kwa kuzingatia maombi ya Wadau ni mafunzo ya huduma bora kwa Wateja na kusisitiza kuwa sifa inayokipa nguvu Kituo hicho kuendelea kuwa shindani ni uwepo wa Wakufunzi wabobezi, Wanafunzi kupata fursa ya mafunzo kwa vitendo kwenye Taasisi kubwa za Serikali na binafsi zenye vifaa vya kisasa pamoja na idadi kubwa ya Wahitimu kupata ajira ndani na nje ya Nchi.
Miss Tanzania Halima Kopwe ambaye pia ni mmoja wa waliowahi kusoma kwenye Kituo hicho, amesema miongoni mwa sababu zinazofanya maombi ya wanaotaka kujiunga na Kituo hicho kuwa mengi ni uzoefu na umahiri wa Wakufunzi wa Kituo hicho pamoja na hadhi yake Kimataifa. #MillardAyoUPDATES
1 307
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameivunja Bodi ya Shirika la Umeme TANESCO na amemteua Dkt. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya akichukua kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli.
Rais Samia ameivunja Bodi hiyo kufuatia Balozi Meja Jenerali Simuli ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda jana December 18, 2023. #MillardAyoUPDATES
1 307
#HABARI: Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini (LATRA), imeonyesha sampuli ya sare zitakazotumiwa na Madereva pamoja na Makondakta wa daladala zitakazotoa huduma katika stendi mpya ya daladala ya Mwenge, iliyopo Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
.
Sare hizo ni shati la mikono mirefu la rangi bluu bahari pamoja Suruali nyeusi.
Nini maoni yako??
1 307
IDRIS SULTAN AINGIA KWENYE ORODHA YA DUNIA KWA KUINGIZA PESA NDEFU KUPITIA INSTAGRAM
Mchekeshaji @idrissultan ndiye Mtanzania pekee ambaye ametokea kwenye orodha ya mastaa wa dunia ambao wametengeneza pesa ndefu kupitia mtandao wa instagram mwaka 2021 (Instagram Rich List), kwa mujibu wa tovuti ya #HopperHQ.
Idris Sultan mwenye jumla ya wafuasi 7M yupo kwenye nafasi ya 108, akitajwa kutoza kiasi cha ($42,800) TZS. Milioni 99.2 Ku-post Tangazo la Biashara.
1 307
"Tunamshukuru Sana Rais Samia Suluhu Hassan amewekeza sana katika elimu na imelipa kwa sasa hivi ukiona elimu ya sekondari ya Serikali sio ya wakati ule. Sasa hivi ukiona utajua ni private. Na kwenye matokeo shule za Sekondari zinafanya vizuri zaidi kushinda private"
🗣️ Batilda Salha Burian, RC Tabora.
1 307
“Kule tulikokuwa tunabomoa [Madanguro] tuliwakuta Dada Poa. Hakuna Dada Poa hata mmoja tuliyemkamata [..] na kwa mantiki hiyo, hakuna tuliyemtuma akakamate hao Dada Poa.” – Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
1 307
Kampuni ya moja nchini China imewataka wafanyakazi wake kukimbia maili 2 (3.2km) kila siku ikiwa wanataka kupata posho kubwa zaidi.
Kampuni hiyo yenye lengo la kuimarisha afya za wafanyakazi wake imefungamanisha posho wanazopata kwa mwaka kwa idadi ya maili wanazokimbia kila mwezi.
1 307
Ufunuo 13:11
Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
1 307
#HABARI Watu wawili wamefariki (mtoto wa miezi sita na mama mtu mzima) na wengine takribani 50 wamejeruhiwa katika ajali ya gari dogo aina ya tata liliokuwa linatoka Kigogo Freshi kuelekea Mloka kupitia Kisarawe baada ya kupinduka na kuingia kwenye Mto.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amebainisha hayo alipofika hospitali ya wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwapatia pole na kuwajulia hali majeruhi hao usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe disemba 19. 2023.
Adha akithibitisha kupokea majeruhi na miili ya waliofariki mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya kisarawe Dkt.Risasi Rajabu amesema baadhi ya majeruhi waliopata majeraha madogo wamesha waruhusu na wengine wanaendelea kuwapatia huduma pamoja na saba wamewapatia rufaa ya kwenda hospitali ya rufaa Muhimbili.
Ajali hiyo imetokea jana desemba 18 majira ya saa nane mchana.
CHANZO #EastAfricaRadio
1 307
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam Jude Thaddaeus Ruwai'chi ametoa wito kwa Jamii hususani waumini wa Kanisa hilo kuwa watulivu na wafuatilie kwa makini tamko lililotolewa hivi karibuni na na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis huku wakibaki na uwelewa na msingi wa mafundisho sahihi ya Kanisa hilo
Akizungumzia mjadala ulioibuka hivi karibuni unaodai kuwa Papa Francis amebariki Ndoa za Jinsia moja Askofu Ruwai'chi ameeleza kuwa tamko la Baba Mtakatifu limehusu Baraka, Baraka ambazo mtu yeyote anaweza kuomba isipokuwa yule anayeomba Baraka hizo asiwe na mategemeo ambayo yanakinzana na msimamo na misingi ya Kanisa
Amesema bahati mbaya iliyopo ni kwamba Mazingira ambayo mafundisho ya Baba Mtakatifu Yametolewa kuhusu hiyo Baraka yametekwa na Watu kwenye Jamii na kwenye mitandao ambao kimsingi hawalitakii mema Kanisa Katoliki
"Kimsingi akija mtu kwangu kwa mfano akisema naomba Baraka, sifahamu kama ni Shoga au sio Shoga mimi nitambariki lakini endapo wanakuja Watu wawili wananiambia Sisi ni Mashoga tunaomba utubariki nitawauliza ninyi niwabariki katika lipi?, na nitashindwa kuwabariki katika Ushoga wao nitawashauri, nitawaelekeza kutafuta namna ya kukabili changamoto yao lakini mimi kama mimi sitaweza kuwabariki katika misimamo na mielekeo ya Kishoga" -Askofu Ruwai'chi
Ameendelea kusisitiza kuwa hakuna Baraka yoyote ambayo itatengua mafundisho ya msingi kuhusu ndoa ambapo ndoa ya Wakatoliki ni muunganiko kati ya Mume na Mke na muunganiko huo ufanyike katika nia iliyo sahihi na si kinyume cha hapo kwa kuwa ndoa inalenga kushirikiana na Mungu katika kazi ya uumbaji
1 307
FULL VIDEO NA MATUKIO MAZIMA UTAYAPATA KWA KU BONYEZA HAPA KWENYE INSTAGRAM LINK:-https://instagram.com/e_plus_media?utm_medium=copy_link
FACEBOOK PAGE FOLLOW:-https://www.facebook.com/eplusmediatv/
1 307
Master J ambaye ni Mmiliki wa Studio ya kurekodi muziki ya MJ Records, amesema kuwa ataanza kufuatilia haki zake kwa Wasanii aliowatayarishia nyimbo zao miaka ya nyuma (zamani). Mtayarishaji (Producer) huyo amesema zamani hakufuatilia kwa sababu hakuwa na njaa ya kugombana na Wasanii ila kwa sasa anahitaji Pesa, hivyo Wasanii wajiandae.
Toa maoni yako
1 307
PAPA FRANCIS ABARIKI NDOA YA JINSIA MOJA
Baba Mtakatifu Papa Francis ametoa Idhini kwa mapadri huko Vatican kubariki ndoa za jinsia moja
"Mwenyezi Mungu kamwe hamkatai yeyote anayemwendea, hakika ni baraka inawapa watu njia ya kuongeza imani yao kwa Mungu. Ni uzao wa patakatifu roho ambayo ni lazima iendelezwe na sio kuzuiwa"- hii ni kulingana na waraka uliotolewa na ofisi ya mafundisho ya Vatikani.
Ikumbukwe kuwa Padri huyo Oktoba mwaka jana alibariki ndoa ya wapenzi wa jinsia moja ikiwa ni kuashiria mabadiliko kutoka kwa uamuzi wa mwaka 2021 ambao ulikuwa unazuia uamuzi huo.
1 307
"Nashukuru sana kwa kushinda Tuzo ya kutangaza Utamaduni na hii nilistahili na nitaendelea kutangaza Uswahili ili uende duniani na huku tukidumisha Lugha adhimu ya kiswahili. Watu wanautafsiri uswahili kama ni tusi lakini mimi nimebaki katika Uswahili wangu"- Madebe Lidai
