fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
MUONEKANO WA JUU WA UWANJA WA AMAAN 🏟️🙌🏾!! Baadhi ya picha zinazoonesha Muonekano wa Juu wa Uwanja Mpya na Wa Kisasa wa AM
+2
MUONEKANO WA JUU WA UWANJA WA AMAAN 🏟️🙌🏾!! Baadhi ya picha zinazoonesha Muonekano wa Juu wa Uwanja Mpya na Wa Kisasa wa AMAAN Zanzibar, uliojengwa na Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar Chini Ya Mhe Rais @dr.hmwinyi . 📸: @baba_nahya1 / @shiva_maphoto

Pichani ni Hajji Manara na mfirisi wake
Pichani ni Hajji Manara na mfirisi wake

Moja ya nadharia kuhusu historia ya Boxing Day ni kwamba ilianza katika karne ya 17 nchini Uingereza ambapo waajiri waliwapa
Moja ya nadharia kuhusu historia ya Boxing Day ni kwamba ilianza katika karne ya 17 nchini Uingereza ambapo waajiri waliwapa sanduku la zawadi wafanyakazi na wahudumu wa majumbani kama ishara ya shukrani kwa kufanya kazi mwaka mzima pamoja na kutoa zawadi kwa wahitaji.

KESI INAYOMKABILI MBUNGE WA BABATI MJINI YAFUTWA. Mahakama ya wilaya ya Babati imefuta shauri la jinai lililofunguliwa na wakili Peter Madeleka dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul la kumfanyia shambulio la mwili Hashim Ali. Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 27,2023 na Hakimu Mkazi wilaya ya Babati Victor Kimario baada ya mwendesha mashtaka wa serikali kuona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo na ameiondoa kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) Cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022. Nje ya mahakama wakili upande wa mlalamikaji Peter Madeleka amesema wanakusudia kukata rufaa kwa kuwa hawajaridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama.  Madeleka akiwa na mawakili wengine Thadei Lister na Peter Masanja walifungua kesi dhidi ya Mbunge Paulina Gekul wakidai alimfanyia kitendo hicho Hashim Ali kwa kumuingizia chupa sehemu ya haja kubwa. Upande wa mshtakiwa uliwakilishwa na wakili Ephraim Kisanga. #Haki jamiiforums

photo content

KAMA MAMA KAMA MWANA Pichani ni Diana Kimari pamoja na mwanae wa kike. Kimari ni miongoni mwa wanawake ambao hutumika msemo m
KAMA MAMA KAMA MWANA Pichani ni Diana Kimari pamoja na mwanae wa kike. Kimari ni miongoni mwa wanawake ambao hutumika msemo maarufu kwamba (Amejizaa) hii ni kutokana na kufanana kindaki-ndaki na mtoto wake.

KISA NYUMBA YA WOLPER MASHABIKI WAIVAMIA PAGE YA DIDA SHAIBU WAKIMNANGA "KIKO WAPI?" Baada ya Staa wa Filamu nchini, Jackline Wolper kuonyesha picha ya mjengo wake hapo jana (kwa njia ya video) mjengo ambao umewaacha watu wengi vinywa wazi hususani mashabiki ambao pengine hawakutarajia Wolper kumiliki mjengo wa aina hiyo kutokana na kuaminishwa kuwa msanii huyo amekuwa akiishi maisha feki hana kitu. Dida Shaibu ni miongoni mwa watu ambao waliwahi kumsema vibaya Wolper kwamba hana nyumba huku akijinadi kwamba yeye anamiliki nyumba kadhaa hapa Dar es salaam. Ambapo pia tuliona Wolper alimjibu Dida kuwa asijigambe sana kwasababu nyumba ambayo yeye anaiona kubwa na kuwasimanga wenzake, yeye ndio nyumba ya kulala dada wa kazi. Baada ya Wolper kuposti nyumba hiyo, mashabiki wameenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa Instagram wa Dida Shaibu wakimchokonoa kila mmoja kwa neno lake huku maneno ya kejeli yakitawala zaidi wakimuuliza kuwa (kiko wapi?). Hizi ni baadhi ya hizo komenti za mashabiki kwa Dida Shaibu "Dida Wolper anakuita kwenye page yake" "Dida umeona Kasri la Wolper?" "Dada dida wameufananisha mjengo wako na wa Wolper, umeona?" "Umeona nyumba kule? Usinene ukamala dada umedhalilika" "Kiko wapi? Kujifanya gwiji mpambanaji Wolper kakukomesha ikisimama nyumba yako na ya Wolper nyumba yako inaonekana kama jiko" "Dida unavyoongea kitu usimalize maneno dada, ona watu wanavyokushona kisa nyumba ya Wolper, sema ulijimaliza mnooo Mungu ni wa wote sio wa mmoja".

photo content

Ungekua ww ungefanyaje
+1
Ungekua ww ungefanyaje

"Huu uwanja duniani ni wa pili kwa Afrika ni uwanja wa kwanza kwenye viwango vya FIFA, tunakushukuru sana na tunaahidi tutaul
"Huu uwanja duniani ni wa pili kwa Afrika ni uwanja wa kwanza kwenye viwango vya FIFA, tunakushukuru sana na tunaahidi tutaulinda" Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.

Anaandika mtangazaji na mchambuzi wa michezo nchini #OscarOscarjr "Tanzania Bondia ni Mwakinyo tu. Hata kama anaringa. Hata k
Anaandika mtangazaji na mchambuzi wa michezo nchini #OscarOscarjr "Tanzania Bondia ni Mwakinyo tu. Hata kama anaringa. Hata kama anajisikia. Ndiyo Bondia wetu Bora tupende au tusipende." Nini maoni yako?

HII HAPA HISTORIA FUPI YA BAHATI BUKUKU "SPONSA ALINISAIDIA KUREKODI ALBUM YANGU YA KWANZA". "Kwa majina yangu naitwa Bahati Bukuku, nimezaliwa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya mwaka 1981 hospital ya Igogwe, ni Mnyakyusa kwa baba na mama. Mimi ni mtoto wa 13 katika watoto 14 ambao watoto saba walifariki lakini watoto saba wapo hai. Nilisoma shule ya msingi Muungano iliyopo mkoani Mbeya nimemaliza mwaka 1996 Nimesoma shule ya Meta Sekondari lakini kwa bahati nzuri au mbaya sikufanya vizuri shuleni, nilikuja Dar es salaam kwa lengo la kulisiti mitihani yangu ya kidato cha nne. Kihistoria mimi niliokoka nikiwa darasa la sita shule ya msingi Muungano, kuanzia darasa la kwanza mpaka la sita nilikuwa naishi kwa wokovu wa wazazi wangu, lakini nilipofika darasa la sita nikaamua kuokoka mimi kama mimi bila kushinikizwa na mtu yoyote. Nikiwa nasubiri kulisiti mitihani yangu ya kidato cha nne hapa Dar es salaam kwa bahati mbaya wazazi wangu walichelewa nikajikuta nalisiti Ndoa badala ya shule. Nilivyofika tu hapa Dar nilikuwa na mambo yangu mawili kichwani, nalisiti lakini naimba, nilikuwa naimba kanisani mimi kama mimi. Katika harakati za kuimba huku na kule ndio nikapata sponsa ambaye baadae alikuja kuwa mume wangu. Sponsa alinisaidia kurekodi na kwa bahati nzuri niliporekodi tu Album yangu ya kwanza (Yashinde Mapito) Mungu akatenda muujiza, Sponsa alikuwa ananipenda lakini alishindwa kuniambia akawa anatumia pesa kuzungumza na mimi, akawa anamtumia rafiki yangu kuniletea zawadi mimi nilikuwa nashangaa tu naletewa zawadi na rafiki yangu, nguo, pesa ya kusuka, cheni ya dhahabu lakini sikujua kwanini jamaa alikuwa ananipatia. Alijitoa sana kwangu na hakuonyesha tamaa, licha ya watu wengi kunikatisha tamaa kutokana na sauti yangu lakini yeye alisimama na mimi na hakika alinisaidia sana. Nilianza kurekodi wimbo wangu wa (Ikulu ya Mbinguni) lakini kwa bahati mbaya ulifanya vibaya na watu waliousikiliza wengi walinikatisha tamaa kuwa siwezi na asilimia kubwa walikuwa ni waimbaji niliokuwa nawakuta studio. Kuna watu wachache walikuwa wananitia moyo na wakanipa nguvu ya kurekodi Nyakati za Mwisho, Yashinde mapito na nyimbo nyingine kadhaa ambazo baada ya kurekodi tu zilifanya vizuri watu wakazishambulia, nikatafutwa na Mhindi aliyekuwa anasambaza kwa kipindi hicho tukauziana na alinipa pesa nyingi ambayo sikuwahi kuishika na huo ndio ukawa mwanzo wangu wa kuishi katika umaarufu na kumtumikia Mungu. Baadae baada ya kuwa maarufu wanaume wengi walijitokeza kutaka kunioa, ndipo Sponsa akaniambia ukweli kuwa hawezi kukubali wanaume wengine wanioe wakati yeye ananipenda na ndiye aliyeniwezesha nikawa Bahati Bukuku. Basi kwakuwa jamaa alikuwa na pesa nikaamua kumkubali maana ukiangalia yeye alikuwa na pesa mimi nilikuwa sina kitu, tulikuwa levo mbili tofauti, alikuja kujitambulisha kwa wazazi tukafunga ndoa"- Bahati Bukuku Hata hivyo miaka kadhaa baadae, Bahati na huyo mume wake (Daniel Basila) walikuja kutengana kwa vita kubwa ambapo baada ya kutengana Daniel alianza kufanya jitihada za kutaka kumshusha Bahati ili apotee kabisa kwenye ulimwengu wa umaarufu, ambapo alimtengenezea stori mbalimbali kwenye magazeti lakini pia aliwatumia Ray Kigosi na Johari kutengeneza Filamu ambayo ilielezea maisha machafu ya Bahati Bukuku. Hata hivyo Bahati hakuwahi kujibu mashambulizi ya mume wake isipokuwa alitoa Album nyingine iliyobebwa na wimbo (Waraka wa Amani) Chanzo hasa kikubwa cha ndoa ya Bahati Bukuku na Daniel Basila kuvunjika ni Bahati alikuwa anazaa watoto kisha wanakufa. Ambapo ndugu walimshauri Daniel aachane na Bahati atafute mwanamke mwingine ambaye atakuwa anazaa. Na hii ni kwa mujibu wa Bahati mwenyewe.

photo content

Pichani ni Cristiano Ronaldo akiwa na mama yake mzazi baada ya kushinda kombe lake la kwanza kwenye mashindano ya mpira shuleni Ronaldo amekulia familia maskini na shuleni hakuwa na akili darasani, baba yake mzazi alikuwa mlevi kupindukia huku mama yake mzazi akijihusisha na biashara ndogo ndogo mtaani. Anaeonekana pichani nyuma mwenye ndevu nyingi ni baba yake mzazi ambaye unaambiwa aliwahi kumwambia "kama hutosoma kwa bidii na kufaulu masomo sidhani kama utafanikiwa maishani maana umasikini wangu pia ni kwasababu sikusoma". Ronaldo alimjibu baba yake kwamba uwezo darasani sina ila naamini ipo siku kupitia kipaji changu nitafanikiwa na kuwatoa kwenye umasikini. Baada ya miaka kadhaa Mungu alimuinua kupitia kipaji chake na sasa ni mwanasoka tajiri zaidi ulimwenguni. Siku za karibuni akihojiwa Ronaldo alisema baada ya kufanikiwa alitamani kumuonesha baba yake mzazi kwamba sasa amefanikiwa ila kwa bahati mbaya baba yake huyo alifariki dunia wakati Ronaldo akiwa kwenye hatua za mwanzo za soka lake. Funzo: Kamwe usikate tamaa Mungu yupo ipo siku atabadili historia yako, usikate tamaa 2024 ukawe mwaka wako🙏

photo content

Haya tujuane leo #wewe unaamini katika chama kipi cha siasa kuelekea chaguzi za mitaa 2024 na mkuu 2025?
Haya tujuane leo #wewe unaamini katika chama kipi cha siasa kuelekea chaguzi za mitaa 2024 na mkuu 2025?

photo content
+7

KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://yo
+9
KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK

Thamani ya nguo zilizovaliwa na mchezaji wa klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia na Ureno, Cristiano Ronaldo. ⌚ Saa inagharimu $
Thamani ya nguo zilizovaliwa na mchezaji wa klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia na Ureno, Cristiano Ronaldo. ⌚ Saa inagharimu $100,000 kutoka kwa Hublot 🧥 Shati inagharimu $2,800 kutoka kwa Gucci 🕶️ Miwani hiyo inagharimu $77 kutoka Belvoir&Co's

Wachezaji wa Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wakielekea Zanzibar kwaajili ya mchezo maalumu wa kirafiki kufungua uw
+3
Wachezaji wa Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wakielekea Zanzibar kwaajili ya mchezo maalumu wa kirafiki kufungua uwanja wa Amaan Desemba 27, 2023 dhidi ya Zanzibar Heroes.