fa
Feedback

فریب کلاهبرداران را نخورید! تل‌متریو این کانال‌ها را شناسایی و برچسب‌گذاری می‌کند 👉 برای مشاهده برچسب، اشتراک تهیه کنید 👈

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

رفتن به کانال در Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

نمایش بیشتر
1 307
مشترکین
+124 ساعت
-27 روز
-1330 روز
آرشیو پست ها
photo content

Maafisa wa Idara ya Huduma ya Wanyamapori (KWS) siku ya Jana Ijumaa walifanikiwa kumuua mamba aliyemla mtoto wa miaka 11 katika kijiji cha Manyuru, kaunti ndogo ya Ndhiwa. Katika tukio hilo, mtoto huyo, Felix Odongo wa Gredi ya Pili alikuwa anachota maji na wenzake Mto Kuja wakati alipovamiwa na mamba huyo. Mama mzazi wa mtoto huyo, Janet Auma alisema alikuwa nyumbani wakati mkasa huo ulipotokea. “Nilitaka ale kwanza kabla kwenda mtoni lakini alisisitiza kwamba lazima amalize kazi za nyumbani kwanza kabla ya kula,” alisema mama huyo ilikuwa siku ya Alhamisi. Akiwa nyumbani, mama huyo anasema alisikia mayowe mtoni. Mayowe hayo yalikuwa ya watoto wengine waliokuwa wanaita kuomba msaada baada ya mwenzake kukamatwa na mamba huyo. Alipofika kwenye mto, Bi Auma anasema aliona mamba huyo akiogelea na kutoweka na mwanawe. Alikimbia kando kando ya mto kujaribu kumwokoa mtoto wake. “Nilijawa na mshtuko usioelezeka nilipoona mamba huyo akiyoyomea majini na mwanangu,” alihadithia akiwa na majonzi mengi. Hapo siku ya Jana Ijumaa, maafisa hao walifanikiwa kumpata mamba huyo baada ya majaribio kadhaa ya kumpiga risasi bila mafanikio awali. Wakazi walifurika kumwona mamba huyo alipotolewa mtoni na huzuni ilijaa zaidi pale alipokatwa tumboni mwili wa mtoto huyo ulipotolewa.

photo content

Umevaa vizuuuri mwenyewe…umependeeeeza…kumbe unatembelewa na kunguni kwenye shati lako daaaah.. 🤣🤣🤣🤣noma sana… Tuache uta
Umevaa vizuuuri mwenyewe…umependeeeeza…kumbe unatembelewa na kunguni kwenye shati lako daaaah.. 🤣🤣🤣🤣noma sana… Tuache utani Mjomba…wewe unapataje usingizi kwenye geto lenye kunguni...🤔🤔🤔🤔hebu tupe uzoefu wako…. Huyu mwamba anauwezo mkubwa wa kustahimili hatari dhidi ya maisha yake. Maana yake ni kwamba … unahitaji zaidi ya aina 1000 za kemikali za sumu ili kumtokomeza mdudu huyu. Watafiti wanadai kadri unavyompulizia kemikali za sumu, ambazo zinaweza kuua wadudu wengine, ndivyo ambavyo kunguni hutafuta mbinu mpya za kuimarisha kinga yake dhidi ya sumu hizo. Sasa itakuwaje…🤔🤔🤔🤔! Watafiti wanashauri kutafutwa mbinu tofauti na mpya ya kukabiliana na kunguni pasina kutumia sumu, kama vile kutafuta wadudu wengine wanaoweza kutumia kunguni au mayai yao kama chakula. Wataalamu nchini Marekani wamebaini kunguni hupenda rangi nyeusi na nyekundu na huchukia njano na kijani kibichi. Ning’ate sikio mjomba… wewe unatumia mbinu gani kupambana na kunguni nyumbani kwako? CHANZO : BBC/ IPP Media/USA Today/The Journal

Tupo kwenye mwezi wa Wapendanao Mama Kenaya @officialnandy anaamini kama nyinyi ni Couple ya Wapendanao na hamna time ya kupi
Tupo kwenye mwezi wa Wapendanao Mama Kenaya @officialnandy anaamini kama nyinyi ni Couple ya Wapendanao na hamna time ya kupiga umbea kidogo na mpenzi wako basi hamja-bond vizuri. Kupitia mahojiano yake na XXL ya# CloudsFM, Nandy amefunguka ambavyo yeye na mume wake @billnass wanavyowasema watu. Nandy anasema kuwa sio tu stori mbaya za umbea wanazowaongea watu lakini pia hata kama ni stori nzuri au nyimbo nzuri ikipita kwenye anga zao basi kijiwe chao cha umbea lazima kiwe na kikao cha dharura kuzizungumzia😁. Vipi, kwa upande wenu ikoje? Wewe na mpenzi wako huwa mnapiga umbea, au nyie hivyo sio vitu vyenu? Dondosha comment yako.

photo content
+3

KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://yo
+9
KUTOKA MITANDAONI Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK

Pichani ni mjane Maria Ngoda aliyehukumiwa miaka 22 jela kwa kukutwa na vipande vya nyama ya swala, baada ya hukumu hiyo kuzu
Pichani ni mjane Maria Ngoda aliyehukumiwa miaka 22 jela kwa kukutwa na vipande vya nyama ya swala, baada ya hukumu hiyo kuzua gumzo walijitokeza mawakili kumsaidia kukata rufaa ambayo imeanza kusikilizwa jana.

Ronaldo aunga mkono chalenji ya Manara na Zaylissa Pichani mke wa Ronaldo akimfanyia maseji ya miguu mme wake Tutafute ela vi
Ronaldo aunga mkono chalenji ya Manara na Zaylissa Pichani mke wa Ronaldo akimfanyia maseji ya miguu mme wake Tutafute ela vijana aisee wakubwa wanafaid Aloooooooh 😋😋😋😋

⚠️🥰 Batuli mwigizaji maarufu Bongo akiwa Maka Picha zaidi kwenye comments section
+1
⚠️🥰 Batuli mwigizaji maarufu Bongo akiwa Maka Picha zaidi kwenye comments section

SERIKALI KUANZISHA SOMO LA UCHAMBUZI WA MICHRI Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inakusudia kuanza kufundisha somo la Uchambuzi wa Michezo katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo-Malya na Vyuo vingine kwa kuzingatia uhitaji wa somo hilo nchini ili kuongeza ajira na utaalamu katika eneo hilo. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma Februari 1, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa jimbo la Mlalo, Lushoto Mhe. Rashid Abdallah Shangazi aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuendeleza wachambuzi wa soka nchini ili wawe na utaalamu wa kutosha katika kazi hiyo. "Uchambuzi katika michezo ni sehemu ya mada zinazohusiana na michezo husika ambazo zipo katika sheria zinazotawala michezo. Serikali itaangalia mahitaji ya soko katika kipindi cha kuhuisha mitaala na kuzingatia eneo la uchambuzi ambalo sasa limeiletea heshima michezo kupitia wachambuzi nguli na mahiri waliopo" amesisitiza Mhe. Mwinjuma. Ameongeza kuwa somo hilo la uchambuzi halitahusisha soka pekee bali pia michezo mingine ikiwemo Ngumi ambayo ni miongoni mwa michezo inayotangaza vyema Taifa la Tanzania na kutoa ajira.

photo content

"Kuolewa mimi saivi bado wakati wangu haujafika, naamini wakati ukifika nitaolewa tu, na sio kwamba siolewi kwasababu sipo ka
"Kuolewa mimi saivi bado wakati wangu haujafika, naamini wakati ukifika nitaolewa tu, na sio kwamba siolewi kwasababu sipo karibu na Mungu, mbona kuna mabinti kibao wapo karibu na Mungu lakini bado hawajaolewa, wanashinda makanisani lakini hawapati wanaume wa kuwaoa, kwahiyo mimi nafikiri ni wakati na maamuzi, sasa hivi mimi natafuta pesa na niko karibu na Mungu sijawahi kumkimbia"- Linah Sanga, Msanii wa muziki Tanzania. Toa maoni

"Leo Nimejifunza Somo Kubwa Sana, Kwenye Maisha Yako Hapa Duniani Unahitaji YES Moja Yenye Kibali Na Mamlaka Nayo Inatoka Kwa
"Leo Nimejifunza Somo Kubwa Sana, Kwenye Maisha Yako Hapa Duniani Unahitaji YES Moja Yenye Kibali Na Mamlaka Nayo Inatoka Kwa MWENYEZI MUNGU Tu, Ukibahatika Kuipata Hizi NO Za Watesi Ambao Hawakumbuki Hata Kumshukuru MUNGU Kwa NEEMA Na BARAKA Zake Juu Yao Kamwe Hawawezi Kukumbuka Wema Wala Fadhila Zako, Hakikisha Unapata Kibali Chenye Mamlaka Sahihi" - amesema Batuli mwigizaji wa Kibongo

Akielezea usiku huu katika kipindi chake 88.9 Wasafi FM "Lavidavi", Diva ameeleza na kuweka wazi mtu ambaye ana moyo wake "Ku
Akielezea usiku huu katika kipindi chake 88.9 Wasafi FM "Lavidavi", Diva ameeleza na kuweka wazi mtu ambaye ana moyo wake "Kuna mtu nampenda sana hakuna namna naweza elezea jinsi ninavyompenda , huyu mtu ni heaven sent wangu , nampenda kuliko maelezo yuko katikati ya moyo wangu na mtu huyo si mwengine bali bibi yangu Stella George Gumbo. alinipenda alinilea alinidekeza, kama watoto wengine ambao hawakuwa na mama, bibi yangu alikuwa mama yangu alikuwa kila kitu chake I love her so much it hurts" - amesema Diva Mtangazaji huyo maarufu amesisitiza kwamba ata-dedicate mwezi huu season of love kwa ajili ya bibi yake

Zawadi watakazopewa Wachezaji wa Timu ya Angola 🇦🇴 endapo watafanikiwa kuifunga Timu ya Taifa ya Nigeria 🇳🇬 hapo kesho na
Zawadi watakazopewa Wachezaji wa Timu ya Angola 🇦🇴 endapo watafanikiwa kuifunga Timu ya Taifa ya Nigeria 🇳🇬 hapo kesho na kufuzu nusu fainali ya (AFCON) 2023. - iPhone 15, Internet bure, kupiga simu na kutuma ujumbe (sms) kwa mwaka mzima. - Dola 250,000 sawa na Shilingi milioni (636) - Gari Toa maoni yako

"Kuhusu tuhuma za kulelewa kwa Lukamba mimi sijui kwasababu wakati niko nae nilikuwa simlei, mimi ni Mtanga natakiwa kulelewa
"Kuhusu tuhuma za kulelewa kwa Lukamba mimi sijui kwasababu wakati niko nae nilikuwa simlei, mimi ni Mtanga natakiwa kulelewa sio kulea. Mimi sijawahi kumlea mwanaume hata hiyo pesa ya kumlea mwanaume sina, mimi kwakweli kwangu alikuwa anatimiza majukumu yake kama mwanaume ya kunilea mimi kama mke wake na mtoto wetu" "Hao wanawake zake wengine wanaosema hivyo mimi sijui kama ni kweli au laah!! kunaweza kuwa kuna ukweli au uongo" amesema Shuu Mimi Mke wa kwanza wa Lukamba ambaye wamezaa Mtoto mmoja lakini baadae walikuja kuachana. Kabla hawajaachana na Shuu Mimi, akiwa ndani ya ndoa Lukamba aliongeza mke wa pili ambaye ni Cecy ambapo vilianza vibwengo vya mke mdogo na mkubwa kisha baadae Shuu Mimi akaamua kuachia ngazi akamuacha Lukamba na Cecy ambao nao hawakumaliza muda mrefu waliachana kila mtu akaendelea na maisha yake, hata hivyo Lukamba alijitosa kwenye mahusiano mengine na Mwanadada aitwae Pendeza ambaye pia wameachana siku kadhaa zilizopita na ndiye aliyejitokeza na madai ya kumlea Lukamba.

Neema Kenge (39) Mkazi wa Mtaa wa Mgonahazeru Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amejikuta njia panda baada ya watoto wake watatu kati ya 15 kukatishwa masomo kwa ujauzito, huku waliowafanya vitendo hivyo wakitoweka kusikojulikana. Mmoja wa watoto Subira Simoni (19), ambaye ni Mtoto wa tatu katika familia ya mama Neema amesema alilazimika kukatisha masomo yake akiwa kidato cha pili, baada kurubuniwa na kupata ujauzito ambapo kwasasa ana mtoto mwenye umri wa miezi miwili na tayari ana ujauzito wa wiki mbili. Katika hali ya kushangaza, Regina Simoni Mwenye umri wa miaka kumi na 17 na mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 nao wamejikuta wakikatisha masomo yao kwa kupatiwa ujauzito na kwa pamoja wameliomba jeshi la Polisi kuwakamata waliohusika kuwapa ujauzito na kutoweka lakini pia wakawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kutokana na changamoto wanazo kumbana nazo ikiwemo hali duni ya maisha. Jirani wa Neema, Bea Joseph amesema Familia hiyo inakumbwa na changamoto nyingi kutokana na idadi kubwa ya watoto na hali duni ya maisha ya wazazi wao hivyo kama kuna mtu ataguswa asisite kutoa msaada. Baada ya kupata taarifa kuhusu familia hiyo, Jeshi la Polisi Morogoro kupitia kwa Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Morogoro Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Pendo Mashurie alilazimika kufika, ili kuona namna ya kutoa msaada huku akikiri kuwepo kwa familia hiyo na kuahidi kuwatafuta waliohusika na kuwaomba wadau mbalimbali kutoa msaada, ili kuinusuru famila hiyo. Neema ambaye ni mama wa nyumbani anajishughulisha na ufanyaji wa usafi katika nyumba za watu, ili aweze kupata kipato cha kuihudumia familia yake, huku mumewe akijushulisha na kazi ya ulinzi.