NENO LA MUNGU NI UZIMA
Ir al canal en Telegram
Neno la Mungu, maombi na ushauri
Mostrar másEl país no está especificadoReligión y espiritualidad75 525
970
Suscriptores
Sin datos24 horas
+97 días
+2830 días
Carga de datos en curso...
Canales Similares
Nube de Etiquetas
Sin datos
¿Algún problema? Por favor, actualice la página o contacte a nuestro gerente de soporte.
Menciones Entrantes y Salientes
---
---
---
---
---
---
Atraer Suscriptores
septiembre '24
septiembre '24
+31
en 0 canales
agosto '24
+47
en 0 canales
Get PRO
julio '24
+54
en 0 canales
Get PRO
junio '24
+70
en 0 canales
Get PRO
mayo '24
+78
en 0 canales
Get PRO
abril '24
+74
en 0 canales
Get PRO
marzo '24
+46
en 0 canales
Get PRO
febrero '24
+56
en 0 canales
Get PRO
enero '24
+97
en 0 canales
Get PRO
diciembre '23
+61
en 0 canales
Get PRO
noviembre '23
+27
en 0 canales
Get PRO
octubre '23
+49
en 0 canales
Get PRO
septiembre '23
+14
en 0 canales
Get PRO
agosto '23
+9
en 0 canales
Get PRO
julio '23
+21
en 0 canales
Get PRO
junio '23
+18
en 0 canales
Get PRO
mayo '23
+28
en 0 canales
Get PRO
abril '23
+35
en 0 canales
Get PRO
marzo '23
+26
en 0 canales
Get PRO
febrero '23
+33
en 0 canales
Get PRO
enero '23
+31
en 0 canales
Get PRO
diciembre '22
+392
en 0 canales
| Fecha | Crecimiento de Suscriptores | Menciones | Canales | |
| 22 septiembre | +1 | |||
| 21 septiembre | +3 | |||
| 20 septiembre | +1 | |||
| 19 septiembre | 0 | |||
| 18 septiembre | +1 | |||
| 17 septiembre | +3 | |||
| 16 septiembre | +2 | |||
| 15 septiembre | +1 | |||
| 14 septiembre | 0 | |||
| 13 septiembre | +1 | |||
| 12 septiembre | +1 | |||
| 11 septiembre | 0 | |||
| 10 septiembre | +2 | |||
| 09 septiembre | +1 | |||
| 08 septiembre | +1 | |||
| 07 septiembre | 0 | |||
| 06 septiembre | 0 | |||
| 05 septiembre | +2 | |||
| 04 septiembre | +3 | |||
| 03 septiembre | +4 | |||
| 02 septiembre | +1 | |||
| 01 septiembre | +3 |
Publicaciones del Canal
MAMBO YAFUATAYO YATAKUSAIDIA KUPATA KIBALI CHA MUNGU.
1. Kuwa na uhusiano mzuri na Mungu kwa kuhakikisha unakuwa na maisha yenye ushuhuda mzuri. Ikimbie dhambi maana dhambi inavunja uhusiano wa Mungu na mwanadamu, (Isaya 59:1-3)
2. Kuwa na bidii kwa ajili ya Mungu, kuwa na bidii ya ibada, vipindi vya mbalimbali vya kanisani, shughuli au kazi za kanisa.
3. Mheshimu na kumthamini kiongozi aliyewekwa na Mungu kukuongoza. Maana amewekwa kukuongoza kwa makusudi maalumu, utakapomdharau unakuwa unadharau kusudi la Mungu.
Usijali umri wake au hali yake, bali kwasababu amewekwa na Mungu, basi mheshimu.
Hii ni kwa viongozi wa ngazi zote, awe Askofu, Mchungaji, wazee wa kanisa, shemasi na viongozi wa idara na vikundi vyote kanisani.
4. Upendo; wajali, wathamini watu wote, wenye hali ngumu na wenye hali nzuri, usimdharau mtu yeyote wala kumchukia mtu yeyote, maana kumpenda Mungu kunaanza kwa kuwapenda watu wengine, (1Yohana 4:20)
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria.
| 2 | BADO UPO GIZANI KAMA UNA VITU HIVI:
1. Chuki kwa wengine.
1 Yohana 2:9.,10.,11.
"Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho."
Hata kama unakwenda kanisani unasema umeokoka lakini unawachukia wengine, basi tambua kuwa bado upo gizani na ni mtumishi mzuri wa shetani, maana chuki ni mpango wa shetani wala siyo mpango wa Mungu. Maana Mungu anaagiza tupendane maana Mungu ni pendo na pendo latoka kwa Mungu.
(a) Ni unafiki mkubwa kujionyesha unaabudu huku ukiwa umejaza chuki ndani yako dhidi ya wengine.
Warumi 12:9-10.
"Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu."
(b) Huna Roho Mtakatifu ndani yako maana upendo ni tunda la Roho,(Wagalatia 5:22)
Roho Mtakatifu hazai chuki ndani ya mtu, bali huzaa upendo.
Ni kujidanganya kusema unampenda Mungu wakati unawachukia wengine, (1Yohana 4:20)
2. Kutokusamehe wanaokukosea.
Tabia ya Mungu ni kusamehe na hivyo watoto wake tunapaswa kuwa na roho ya kusamehe, maana tunapowasamehe wengine, tunapata kibali cha kusamehewa makosa yetu kwa Mungu.
Mathayo 6:12
"Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu."
Mathayo 6:14-15
"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. "
Usiposamehe maana yake unajizibia nafasi ya kusamehewa na Mungu dhambi zako, maana yake KUTOKUSAMEHE TU NI DHAMBI maana yake uko upande wa shetani, maana yake upo gizani.
Hivyo jitafakari katika vipengele hivyo, je upo kwenye NURU YA MUNGU au upo kwenye GIZA LA SHETANI? Chuki zako na kutokusamehe kwako kutakupeleka jehanum ya moto wa milele.
Mungu akubariki sana.
Lazaro Zakaria | 0 |
| 3 | KAMA HUWEZI KUSEMA MBELE ZA WATU KUWA UMEOKOKA.
1. Haujaokoka huwa unaenda kanisani kujionyesha kwa mchungaji na watu. Lakini kwa Mungu hauna nafasi.
Marko 8:38.
"Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu."
2. Maisha yako hayana ushuhuda mzuri unaogopa kusemwa na watu kuwa haujaokoka kwasasababu ya matendo yako.
Ushuhuda wako mbaya mbele za watu unakufanya ushindwe kuwashuhudia na kuwahubiri watu habari za wokovu.
Warumi 1:16.
"Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."
Hivyo basi kuwa na msimamo wa maisha katika wokovu, ukiamua kumfuata Yesu basi achana na mambo yatakayokufanya ushindwe kumtangaza Kristo, na mambo yenyewe ni dhambi.
Mungu akubariki!
Lazaro Zakaria | 0 |
| 4 | USIRUHUSU TATIZO LIKUANGAMIZE FANYA UAMUZI UTAKAOKUSAIDIA KULITATUA.
2Wafalme 7:3-16
Ni habari ya watu wenye ukoma wanne waliotengwa nje ya kwasababu ya ukoma wao ili wasiwaambukize wengine. Lakini pamoja na udhaifu wao walifanya mambo ambayo yalikuwa na msaada mkubwa katika nchi yao iliyokuwa inakabiliwa na njaa kubwa sana kiasi kwamba watu walikula hadi mavi ya njiwa.
MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WATU HAWA.
1. Tathmini hali yako.
Unapokuwa katika changamoto au tatizo lolote unatakiwa kufanya tathmini hali uliyo nayo, uwezo ulio nao, kipi ufanye ili kutatua tatizo lako.
2 Wafalme 7:4.
"Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu."
Walitathmini ukubwa wa tatizo walilokuwa nalo na wakagundua pamoja na ukoma wao, lakini tatizo kubwa kwao ni njaa, wakirudi mjini hakuna chakula watakufa, wakibaki pale watakufa pia, nafuu yao ikawa ni kwenda kwa maadui maana pengine wanaweza kuwaacha hai wakawapa chakula kama ni kufa hata pale watakufa tu.
Usikae na kulalamika na kulaumu, haitakusaidia maana hutapata jibu la tatizo lako zaidi sana utaendelea kuumia.
2. Fanya uamuzi utakao kusaidia bila kujali utakuwa mgumu kiasi gani.
Kuwa na uthubutu wa kufanya hata kama inaonekana ni vigumu, kuogopa kwako kutakufanya uendelee kuteseka na kubaki hivyo ulivyo.
2 Wafalme 7:4b.
".....Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu."
Haukua uamuzi rahisi kwao, maana saa nyingine Washami wangehisi wametumwa kuwapeleleza na kuwahada.
Lakini uamuzi wao mgumu ndiyo uliwasaidia wakapata chakula wakaishi.
Hakuna kitu kizuri kinachopatikana kwa urahisi, ni lazima maamuzi magumu yafanyike ili kukipata.
3. Chukua hatua ya utekelezaji wa maamuzi yako.
Na hapo ndipo utaona Mungu akikutokea na kukusaidia kufanikisha maamuzi yale uliyoyaamua na kukusaidia kutatua tatizo.
Wale wenye ukoma walipoanza safari ya kwenda kwenye jeshi la Washami ndipo Mungu alionekana kwao akiwasaidia.
2 Wafalme 7:5-7.
"Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao."
Mungu anataka wewe uamue nini kifanyike ili aweze kukusaidia, kuna mambo Mungu hawezi kumlazimisha mtu kufanya, bali mtu anatakiwa aamue yeye mwenyewe.
Mfano mtu anawezakuwa anaumwa, asipoamua yeye mwenyewe kuomba uponyaji Mungu hawezi kuponya, mwingine ana tatizo la kutokupata mtoto, asipochukua hatua ya kuanza kuomba kupata mtoto na kuwaona wataalamu wa afya kwakweli hawezi kupata mtoto.
Hivyo pale utakapoanza kufanya ndipo utakapomuona Mungu akikusaidia, ukikaa kimya uwe na uhakika hautamuona Mungu akikusaidia, ukiwa mtu wa kulaumu na kulalamika, uwe na uhakika hautapata matokeo yoyote ya maana.
4. Usijidharau kwasababu ya udhaifu wako, Mungu anaweza kumtumia yeyote hata aliye dhaifu kufanya kazi yake kwa ajili ya wengine.
Kama aliwatumia watu wenye ukoma kuwafukuza maadui wa nchi yao hata wewe anaweza kukutumia kuwa kuwalinda watu wengine, kama kupitia wakoma mji ulipata chakula, basi hata kwako wewe anaweza kukutumia kuwa sababu ya furaha kwa watu wengine. Usijidharau bali jipe thamani.
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria | 0 |
| 5 | MTU AKIFA HAKUNA KINACHOWEZA KUBADILIKA KWAKE.
Hakuna ukweli wowote kuwa mtu akifa katika dhambi anaweza kuombewa msamaha na waliobaki hai akasamehewa dhambi zake. Ukweli ni kwamba mtu akishafariki hana analoweza kufanya au akafanyiwa ikabadilisha hukumu yake.
Waebrania 9:27.
"Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu"
1. Mtu anaanda mahali pake baada ya kufa akiwa hapa duniani.
Yesu mwenyewe alitoa mfano wa tajiri na maskini Lazaro, baada ya kufariki kila mmoja alienda sehemu yake, tajiri aliingia kwenye mateso moja kwa moja, na Lazaro kwenye uzima.
Luka 16:22-23.
"Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake."
2. Mtu akifa hata akiomba hawezi kukubaliwa wala maombi yake hayawezi kusikika kwasasababu nafasi yake inakuwa imekwisha. Wala hawezi kupata msaada wowote ule. (Luka 16:24-26)
3. Mtu akifa hawezi kuwa na msaada na msaada wowote kwa watu walio hai.
Yule tajiri alipokufa aliwaombea ndugu zake lakini haikusaidia.
Luka 16:27-,29.
"Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28. kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. 29. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. "
Maana yake ni kuwa mfu hawezi kuomba wala kumuombea mtu. Hivyo mtu yeyote aliyekuf hana msaada wowote kwa aliye hai. Inashangaza kuona kuna baadhi ya jamii, dini, madhehebu huomba kwa watu waliokufa wawasaidie, wanaomba kwa watu wanaowaita watakatifu fulani, nikwambie tu alimaliza kazi yake akiwa hapa duniani. Ana hesabu yake mbele za Mungu. Kunawatu wanaenda kuomba kwenye makaburi ya watu mashuhuri, hapo mnaabudu mizimu na masanamu. Tumeagizwa kuomba kwa Jina la Yesu tu.
3. Kumuombea Marehemu hakuwezi kubadilisha hukumu yake.
Ufunuo wa Yohana 14:13.
"Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao. "
Matendo ya mtu akiwa hai ndiyo ushahidi mkubwa unaotumika kumhukumu mtu, maana yanamfuata hadi atakapohukumiwa.
Hivyo sala za kuwaombea marehemu ni kudanganyana, haziwezi kumsaidia kabisa. Huu utaratibu iliwekwa ili kufarijiana katika dhambi kuwa hata akifa kwenye dhambi anaweza kuokolewa kwa sala za wachungaji, padre, ndugu nk. Huo ni uongo hakuna kitu kama hicho.
Mtu anatengeneza njia yake akiwa hapa duniani. Akifa ni hukumu tu. Maneno pumzika kwa amani, Rest in pieace, Mungu mpokee mpendwa, hayana msaada wowote. Badilisha mwenendo wako ukiwa hai, ukifa katika dhambi utahukumiwa adhabu ya milele.
Mungu akubariki sana.
Lazaro Zakaria | 0 |
| 6 | FIKIRA NA MAWAZO YANATAKIWA YA MTII KRISTO.
"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;" (2Wakorintho 10:3-5)
Unapomsikia mtu yeyote anasema jambo lolote lile, tambua kuwa lile jambo limeanzia kwenye mawazo. Pia umuonapo mtu anafanya jambo lolote lile, nalo tambua kuwa limeanzia kwenye mawazo na fikra zake.
Hapo sasa ndipo pa kujiuliza swali, huyo mtu anatamka au kufanya matendo ya aina gani? Maneno au matendo ayafanyayo mtu humtambulisha mtu yule alivyo ndani ya roho yake.
Jiulize hapo ulipo unawaza nini?
Unawaza nini kuhusu maisha yako?
Unawaza nini kuhusu hizo changamoto unazozipitia?
Unaweza nini kuhusu huo ugonjwa unaokusumbua?
Mawazo yanaweza kukufanya ushinde, au ushindwe, upone ugonjwa au usipone.
Kwahiyo basi, kwa Mkristo ili aweze kuishinda vita dhidi ya shetani ni lazima kila wakati amtafakari Yesu, alitafakari Neno la Mungu kila wakati. Neno la Mungu linasema hivi, "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana." (Yoshua 1:8)
Watu wengi siku wanashindwa kuendelea mbele kiroho na kimwili kwasababu ya mambo wanayoyatafakari kila wakati usiku na mchana. Biblia inatuambia tukilitafakari Neno la Mungu ndipo "UTAKAPOIFANIKISHA NJIA YAKO, KISHA NDIPO UTAKAPOSITAWI SANA."
Kutafakari Neno la Mungu, kunamfanya mtu ajenge na kukua Kiroho kwasababu huko ndiko anakopata chakula cha roho, ndiko anakopata maarifa ya kutosha jinsi ya kumuomba Mungu, jinsi ya kumtumikia Mungu, jinsi ya kumshinda shetani na majaribu yake.
Sasa wengi wanashindwa kwasababu mioyo yao imejaa mambo ya kidunia zaidi, kila wakati wanawaza uzuri wa dunia na masumbufu yake badala ya kuwaza yale yaliyo ya Mungu kama Neno la Mungu linavyosema.
"Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo." (Wafilipi 4:8)
Pia Neno la Mungu linasema, "Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi." (Wakolosai 3:1-2)
Kwahiyo ili Mkristo aweze kuishi maisha matakatifu yenye mafanikio ya Kiroho na kimwili, ni lazima aamue kumruhusu Yesu Kristo kuyatawala mawazo yake kila wakati, kwa:
(a)kusoma Neno na kulitafakari Neno la Mungu,
(b)kuomba na kukemea roho zote chafu zinazopandikiza mawazo machafu ndani ya mtu.
(c) Kuepuka kuona, kusikiliza, mazungumzo na kutenda mambo ambayo yatakufanya uyatafanya uyatafakari zaidi kuliko Yesu Kristo.
Vile unavyomtafakari zaidi Yesu Kristo zaidi mara kwa mara ndivyo unavyomfanya awe karibu yako. Na unavyoyatafakari mambo ya duania zaidi na maovu ndivyo unavyomfanya Yesu awe mbali na wewe.
Yafanye mawazo na kila fikira yako imtii Kristo.
Mungu akubariki sana.
Lazaro Zakaria | 0 |
| 7 | UAMINIFU KWA MUNGU UNAKUPA UJASIRI WA KUZUNGUMZA NA MUNGU.
Mtu akiwa mwaminifu kwa Mungu anakuwa na mahusiano mazuri na Mungu, hivyo anakuwa na nafasi kubwa ya kusikilizwa na Mungu.
Hezekia alipopewa ujumbe na Isaya kuwa atengeneze mambo ya nyumba yake, maana hatapona ugonjwa bali atakufa. Alizungumza na Mungu kuhusu maisha yake.
2 Wafalme 20:2-3.
"Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA akasema, Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. "
Tunajifunza mambo yafuatayo.
1. FANYA MAMBO YATAKAYOKUFANYA UMKUMBUSHE MUNGU.
Hezekia alifanya mambo mazuri, ambayo alimkumbusha Mungu jinsi alivyofanya katika maisha yake ambayo yalikuwa mema, na Mungu alipoona kuwa ni mema alikubaliana na Hezekia.
2. ISHI MAISHA YA UAMINIFU AMBAYO YATAKUPA UJASIRI WA KUZUNGUMZA NA MUNGU.
Hezekia alipata ujasiri wa kuzungumza na kumkumbusha Mungu kwasababu alikuwa mkamilifu kwa Mungu, makosa ya nyumba yake ndiyo yalitaka kusababisha afe. Lakini kwa upande wake alikuwa mwaminifu na mkamilifu, ndiyo maana anasema, "Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. "
Nina hakika angekuwa mtu muovu, Mungu asingesikia maombi yake, bali Mungu alisikia na kumuongezea umri wa miaka 15, (2Wafalme 20: 4-6)
Huo unatakiwa kuwa mfano mzuri kwetu kuwa tukiishi maisha ya uaminifu na kumpendeza Mungu, tutamuomba atasikia maombi yetu na tukiwa kwenye matatizo atatusaidia na kutuokoa.
Lakini tukiwa kinyume na mapenzi ya Mungu,
1. Hatuwezi kuwa na mahusiano mazuri na Mungu, (Isaya 50:1-3)
2. Hata tukiomba lolote hawezi kutusikia, (Yohana 9:31)
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria. | 0 |
| 8 | JE, UNAFURAHI AU UNAUMIA UNAPOONA MTU ANAPOTEA KWA KUMWACHA MUNGU?
Je, unaona ni kawaida tu unapoona mwingine anapata shida na matatizo?
Katika mfano wa mwanampotevu kuna jambo tujifunze kutoka kwa ndugu yake, (Luka 15:11-32)
Baada ya ndugu yake kurudi kutoka katika upotevu wake, baba yao alifurahi na kufanya sherehe kubwa sana, lakini ndugu yake alichukia na kumlaumu baba yake.
Luka 15:28-30
"Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona."
Mambo kadhaa ya kujifunza kutoka kwenye mistari hiyo.
1. Kuna watu hawahangaiki kuwatafuta wengine waliopotea katika imani. Wakiona mtu ameanguka katika dhambi, ameacha kuhudhuria ibada wanaona ni kawaida, wanasema shauri yake atajijua mwenyewe, hiyo siyo jambo analolitaka Yesu. Bali anataka tutafutane sisi wenyewe.
Je, mpendwa huwa unachukua hatua gani baada ya kuona mwenzako amepotea katika imani? Je, unakaa na kurizika kuwa haikuhusu? Saa nyingine Mungu anakusemesha kabisa kuwa unatakiwa kumsaidia lakini unaona haikuhusu.
Hiyo siyo kazi ya viongozi peke yao, siyo ya mchungaji peke yake, bali ni yetu sote. Na hapo ndipo ndipo tutakuwa tumeonyesha upendo halisi.
2. Kuna watu hawapendi wengine wajirudi na kupata mema wanayostahili kupata. Wakiona mtu amerudi katika hali nzuri wanaumia kama yule ndugu yake alivyolaumu kuwa kwanini baba yake amempokea wakati alimfanyia mabaya?
Hata kanisani kuna watu huumia sana kuona mtu aliyekuwa ametenda shambi amerudi na kutubu, huanza kulaumu na kuhesabu mambo mabaya ambayo aliyoyafanya zamani na kuona kuwa wao pekee ndiyo wanastahili kuwa kanisani kwasababu ni watakatifu.
Kitu ambacho siyo sawa kabisa, maana Yesu alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea na siyo walio watakatifu.
Pia haifai kujihesabia haki kuwa wewe ni mwema sana, kuwahukumu tu wengine kuwa hawafai ni dhambi tosha kabisa ya kukufarakanisha na Mungu.
Tambua kuwa baba yao alikuwa anaumia sana kwa mtoto wake kupotea, ndivyo Mungu anaumia sana kuona watu wako kwenye dhambi ndiyo maana aliamua kufanya ukombozi kwa kumtoa Yesu awe sadaka ya ukombozi wetu, (Yohana 3:16)
Hivyo basi:
1. Tuumie tunapoona wenzetu wanaopotea na kuwaonea huruma.
2. Tuwatafute wenzetu wanapotea na kuwarejeza kwa Mungu.
3. Tufurahi wenzetu waliopotea wanaporejea na kuungana nasi, maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria. | 0 |
| 9 | Faida tatu za kusamehe.
1. Kiroho; ili usamehewe na Mungu ni sharti kwanza uwasamehe waliokukosea, (Mathayo 5:14-15)
2. Kiafya; msamaha utakupa amani ya moyo kiasi kwamba magonjwa ya moyo na preasure yatakuwa mbali na wewe.
3. Utastawi kijamii na kiuchumi maana utakuwa na nafasi ya kufanya mambo ya maendeleo badala ya kushughulikia watu waliokukwaza au kukukosea.
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria | 0 |
| 10 | ADUI HUTUMIA UDHAIFU WA MTU ILI AWEZE KUMSHINDA.
Kila mtu ana uimara wake na udhaifu wake, na siyo rahisi mtu kushindwa kama hajashambuliwa kwenye udhaifu alio nao, uimara wa mtu huondolewa kwa kutumia udhaifu wake.
Kwa mfano Samsoni alikuwa ni mtu mwenye nguvu nyingi sana ambazo adui zake walitafuta namna ya kumshinda lakini walishindwa hadi walipopata siri ya nguvu zake, na siri za nguvu zake zilijulikana kwa udhaifu wake. Na udhaifu wa Samsoni ulikuwa upendo wake kwa mwanamke ambaye hakujua kuwa ni mtego wa adui dhidi yake, (Waamuzi 6:16-22)
Samsoni nguvu zilimwishia baada ya kukatwa nywele zake, na hapo adui akamshinda.
Pia Ayubu pamoja ya kuwa hakushindwa, lakini adui alijaribu kutafuta udhaifu wake lakini, hakuweza, kwasababu yeye alidhani Ayubu uimara wake upo kwenye mali zake lakini kumbe haikuwa hivyo, (Ayubu 1:9-10)
Pia Danieli wabaya wake walijaribu kutafuta udhaifu wake waweze kummaliza lakink pia walishindwa.
Kwahiyo ndivyo ilivyo hata katika maisha ya kawaida, kuna adui mwanadamu ili aweze kukushinda ni lazima atafute wapi palipo ma udhaifu wako ili aweze kukushambulia na kukumaliza, hivyo unatakiwa kuwa makini sana kwa kila jambo na kila wakati usimruhusu mtu yeyote ajue udhaifu wako wowote ule, iwe ni kwa maneno au kwa vitendo.
Pia shetani hawezi kukushambulia bila kutumia udhaifu wako, ni lazima atafute upenyo wowote apandikize jambo baya ambalo litakuondoa katika uwepo wa Mungu kama alivyofanya kwa Samsoni. Anaweza kutumia maneno ya ushawishi au matendo.
Jitahidi sana kutokuingia katika mtego wa shetani kwa kufanya dhambi yeyote, na ukitambua kuwa kuna dhambi yeyote ile basi fanya toba haraka sana, maana dhambi ndiyo mlango mkubwa sana anaoutumia shetani kuweka udhaifu kwa mtu ili apate kumshambulia kwa urahisi.
Kuwa makini sana na maneno unayotamka, maana maneno huwa yanabeba ujumbe wa nguvu sanana kusimamiwa katika ulimwengu wa roho, epuka mizaha (Zaburi 1)
Usijiapize kwa jambo lolote lile, ukiwa na hasira usitamke maneno yoyote yale maana shetani hutumia sana hiyo nafasi.
Kwahiyo jitahidi sana mpendwa kutokuonyesha udhaifu wako, jiimarishe kwa ibada, Neno la Mungu na maombi.
Mungu akubariki sana! Ameni.
Lazaro Zakaria. | 0 |
| 11 | MAOMBI 07
Kuomba kwa bidii bila kukata tamaa kuna kupa nafasi ya kupata matokeo makubwa kwa kile uombacho.
1 Wathesalonike 5:17.
"ombeni bila kukoma; "
Yakobo 5:16-18.
"Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. 17. Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18. Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. "
Kule kuomba kwa bidii kunaonyesha nia na shauku ya hitaji lako, kwahiyo ile bidii yako ya kuombea lile jambo kunamfanya Mungu akufanyie hitaji lako.
Luka 18:7.,8.
"Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia haki upesi."
Kwahiyo usikate tamaa unapoona huapati matokeo kwa haraka katika jambo unaloliombea, endelea kuomba hadi utakapoona matokeo, maana kwa wakati wake BWANA anatakujibu.
Mungu akubariki sana.
Lazaro Zakaria | 0 |
| 12 | MAOMBI 06
Maombi ni njia ya kumuepusha mtu na majaribu.
Mathayo 26:41
"Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu."
Shetani humwekea mtu mitego mbalimbali ili aweze kumuangusha na kumuondoa katika imani ya kumwamini Mungu na kumtumikia.
Mtu anapoomba, Mungu huyaepusha majaribu yote ambayo yalikuwa yamemlenga kiasi cha kumuangamiza.
Pia hata kama majaribu yatamkuta basi anatiwa nguvu ya kuvumilia na kuyashinda majaribu yaliyo mpata.
Usiache kuomba, omba kila siku ili Mungu akupe uwezo wa kuyashinda majaribu.
Mathayo 6:13
"Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu."
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria | 0 |
| 13 | MAOMBI 05
Maombi ni njia ya kupata hitaji lako kutoka kwa Mungu.
Mathayo 7:7 -8
"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
Hata katika maisha ya kawaida tu ili mtu aweze kupata kitu kilichopo kwa mtu ni lazima amuombe. Vivyo hivyo ili mtu apate kutoka kwa Mungu anatakiwa aombe.
Yohana 16:24
"Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu."
Maisha ya kumtegemea Mungu yanawezekana kwa njia ya kuomba. Mtu asieomba hutumia akili zake mwenyewe na kukosa mwongozo wa Roho Mtakatifu katika maamuzi na wengi hujikwaa katika maamuzi yao kwasababu ya kukosa mwongozo wa Roho Mtakatifu.
Mungu akubariki sana! Ameni
Lazaro Zakaria | 0 |
| 14 | MAOMBI 04
Maombi ni miongoni mwa njia ya kuonana na Mungu.
Yeremia 29:12 -13
"Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote."
Moyo wa kumtafuta Mungu kwa njia ya maombi hutegemea sana kiwango cha upendo wako kwa Yesu, upendo wa Yesu kwako pamoja na ufunuo uliopo ndani yako kwa njia ya Neno.
Mithali 8:17
"Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona."
Fanya maombi kwa bidii na utamuona Mungu katika maeneo mbalimbali katika maisha yako.
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria | 0 |
| 15 | Basi nikawa naomba Mungu alikuwa ananisaidia niweze kugundua hila na udanganyifu ambao watu walikuwa wanatengeneza ili wakauze mafuta kwa ajili ya magendo.
Wakati ule ulikuwa ukija kuomba mafuta tulikuwa tunawaambia waje na kadi za magari. Sasa kuna kadi ya gari ambazo unakuta magari yako juu ya mawe lakini kadi inalipiwa.
Lakini ukichukua mafuta yale wanaenda kuuza kwa njia ya magendo. Basi alikuja mtu mmoja na gari. Nilimwambia gari yako ni mbovu lakini yeye alikataa na akawa mkali kweli. Basi nikampigia simu OCD wa ile wilaya nikasema naombeni nitumieni traffic ili akakague gari la huyu mtu akililikuta ni zima nitampa mafuta ila kama ni bovu simpi.
Basi yule mtu akasema naomba ndugu yangu Mwakasege tusaidiane. Alipoona napiga simu namna hiyo akanyanyuka pole pole huku akisema “sijui anajuaje…sijui anajuaje…”.
Ukiombea mfumo, mfumo utakuwa rafiki yako (utakulinda, utakutetea, n.k) kwa sababu Mungu yupo upande wako na kukusaidia katika mtego uliowekewa. Kwa hiyo lazima kuwe na mkakati wa kuombea uwepo wa Mungu uwepo mahali.
Katika haya maeneo ninayokuambia lazima ufahamu kuwa Habakuki alipoona Mungu anakuja huku akiwa amebeba utukufu wake, alipambana ajue namna ya kuupokea na kuutunza na mtu asipojua hivyo atapata shida.
Mungu akutengenezee nafasi hata kama uko mwenyewe hakikisha unatunza siri za ofisi usimshirikishe kila mtu huku ukisema mnaziombea kwa sababu kuna mambo ndani ya mfumo hayatakiwi kutoka nje hata kama unamwambia mtu mwingine asiyekuwepo ofisini kwako, hutakiwi kumwambia tatizo lililoko mweleze kile ulichokibeba na liombee hapo ofisini (tenga muda wa kuombea kazi yako).
Wapo watu wanaona aibu kiasi ambacho ukimwambia aombe anapata shida kuwa watu wasimwone anaomba; ujue hiyo ni hofu kutoka kwa shetani ili asipokee kile Mungu amemkusudia. Mungu anatakusaidia namna ya kuomba na kwa muda sahihi sawasawa na mazingira yako ya kazi. Unaweza usipate umuhimu wa kumwomba Mungu wakati unapita nyakati ngumu sana au za raha maishani ndani ya mifumo.
Mfano:
Kuna mwaka nilikuwa Canada nikiwa na rafiki yangu mmoja Mganda tukihubiri katika miji kadha wa kadha, tulikaribishwa kanisa moja la Kianglikana (Church of Canada) ilikuwa kijijini katika jimbo mojawapo kule na wenyeji wote walikuwa wazungu (weupe) ila sisi wawili ndio weusi (ila mimi nilikuwa mweusi zaidi) kiasi ambacho watoto wanashangaa kumwona mtu mweusi live na watoto wengine wakanisogelea wakigusa ngozi waone kama ni rangi au vipi.
Mtoto mmoja akasema:
Mtoto: Nikuulize swali?
Mwakasege: Uliza.
Mtoto: Kule kwenu mnakaa kwenye nyumba?
😀😀😀
Ilipofika wakati wa kutoa sadaka tukatoa sadaka ghafla mchungaji wa pale alienda kwenye kikapu cha sadaka na kutoa sadaka zetu halafu akaturudishia huku akisema “hawa majamaa ni matajiri sana hakuna haja ya kuwasaidia”. Tukamwambia HAPANA, SISI HATUTOI KUWASAIDIA ILA TUNAMPA MUNGU, TUKACHUKUA ZILE SADAKA NA KUZIRUDISHA KWENYE KIKAPU.
LEO NATAKA TUOMBE MAOMBI HAYA:
🔸Kwa wale ambao wana uhuru wa kuomba maombi nyumbani lakini wakifika kazini wanakosa tena msukumo wa kuomba au ukiwa mwenyewe unaomba ila tu ukiwa na wengine huombi. Nataka niombe kwa ajili yako ili Mungu akupe upako wa kuomba.
🔸Pia wale wanaopata nafasi ya kuomba ila kila wakitaka kuomba sababu ya kutokuomba inakuja na hiyo sababu mtu anaikubali na kuomba kunakata kabisa. Nataka niombe kwa ajili yako
Ila tuanze na kuombea na kutoa sadaka halafu tuombe kwa ajili ya agenda za maombi hapo juu
(PATA LINK YA NAMBA ZA SADAKA NA YA SOMO HILI YOUTUBE PALE JUU MWANZONI MWA SOMO).
×××××××°°°°×××××°°°°××××××××
Ubarikiwe sana kufuatilia semina hii na hapa ndio tumefika mwisho wa semina Singida, endelea kutufuatilia kwenye semina na makongamano maeneo mengine ndani ya nchi yetu Tanzania na nje ya nchi.
UMEBARIKIWA | 0 |
| 16 | AINA YA TATU
KUOMBA KWA BIDII
Maana yake ni kuomba kwa kutokukata tamaa yaani kuombea kitu ambacho huoni mabadiliko yake kwa haraka. Kuna tofauti ya kuomb akwa juhudi kwa bidii.Juhudi ni kuomba kwa kutaka matokeo ambayo unakuwa unayahitaji. Lakini bidii ni kuombea kitu hata kama kinachelewa kuja uendelee kuomba.
Ukisoma Luka 18:1 unaona Biblia inasema imetupasa kumwomba Mungu siku zote ili tusikate tamaa. Kama unaombea mfumo usikate tamaa kuombea mfumo. Omba mpaka pale Mungu atakaposema inatosha. Ila endelea kuombea mfumo.
Biblia inasema kwa habari za Eliya kuomba kwa bidii.Hii unaipata katika Yakobo 5:16-18
Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
Biblia inatufundisha stamina ya wewe kuendelea kuomba bila kukoma ili kupata matokeo ambayo yanatakiwa. Hii haina maana mazingira hayatakusumbua yatakusumbua ila wewe utajitia moyo kwa Bwana. Hata kama kuna watu ambao wanaleta mzaha kaa nao mbali sawa sawa na Zaburi 1.
Habakuki alipomaliza mstari wa 2, aliposema katika ghadhabu alisema kumbuka rehema. Mstari wa tatu Mungu alikuja. Katika mwisho wa mstari wa pili na mwanzo wa mstari wa tatu Biblia haituambii kuwa ni muda gani ulipita. Yaani ni siku moja au wiki au mwaka.
Mungu akija ili kujibu maombi yako inafuta kabisa uchungu wako wa kuchelewa. Maana Mungu hachelewi wala hawahi; anakuja kwa ratiba yake na ndio maana utendaji wa mifumo ni kwa ajili ya muda.
AINA YA NNE
KUOMBA KWA KUDUMU
Kuomba kwa kudumu maana yake ni kuomba ili kutunza utukufu wa Mungu au udhihirisho wa Mungu au uwepo wa Mungu.
Wakolosai 4:2
Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani
1 Thesalonike 5:17
ombeni bila kukoma
Kwa maana hiyo dumu katika kuomba. Sasa je kama kitu umepata kwanini uendelee kuomba? Katika Hababuki 3:3 Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Mahali popote penye utukufu wake una udhihirisho wa Mungu. Huo utukufu wa Mungu unatakiwa ukae kila siku usizimike.Akina Musa walipewa jukumu kuhakikisha moto hauzimiki katika madhabahu. Sadaka kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha kuwa moto hauzimiki katika madhabahu.
Mambo ya Walawi 6:8-13 Moto katika madhabahu haukutakiwa kuzimika kabisa. Na ile ilikuwa ni ishara ya kuwa Mungu analirudia kanisa lake na kuleta tena utukufu wake kwa kanisa. Kila wakati kumbuka tona ya Warumi 3:23 Wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Katika Biblia, hii ni tiba ya kukuongezea utukufu wa Bwana. Maandiko yanasema utukufu wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko ule wa kwanza.
Kwa hiyo uwepo wa Mungu unatakiwa uwepo kila mahali na katika mifumo ambayo tunaishi. Kwa hiyo tuendelee kujifunza kuomba ili kudumu katika maombi. Danieli alikuwa anaomba mara tatu kutwa ili Mungu aweze kuwepo katika mfumo.
Yale maombi ambayo aliyokuwa anaomba mara tatu kutwa na ndio alikuwa anatawala mifumo. Hata Nebukdneza alipokorofisha Mungu alisema adhabu hii imekuja kwa ajili ya walinzi akaja akapewa nyakati saba za kukaa porini kwa nyakati saba.
Kwa hiyo weka imani yako katika matendo na jifunze kuombea mifumo ambayo inakuhusu. Anza hata na hatua chache hata maneno mawili ombea kazi mifumo. Anza pole pole na katika hatua kwa hatua ufalme wa Mungu utatawala.
Wakati ule nafanya kazi ofisi zetu zilikuwa zinafunguliwa saa moja na nusu. Lakini mimi nilikuwa naenda saa moja kamili. Nusu saa ilikuwa ni kwa ajili ya kuomba na kufanya Bible study yangu. Wakati ule kulikuwa na shida ya mafuta.
Mkurugenzi wa wakati ule alikuwa amenipa kazi ya kusimamia mafuta. Na wakati ule ilikuwa ni shida sana. Nilikuja kuelewa namna ile kazi ilivyokuwa jaribu sana na lile suala langu la kuomba kila siku nusu saa lilinisaidia sana kwa namna gani. | 0 |
| 17 | Ukisoma Esta 4:13-14. Hapa unaona kwa Mfalme Ahusero aliyekuwa mume wa Esta. Mara ya kwanza mke wake alikuwa ni Vashti. Wakati ule mfumo wa kazi ulikuwa unatawala hata ndoa yake.
Maana ilikuwa ni kikao cha Cabinet lililoitishwa kujadili ndoa ya mfalme na hawakuwa wazazi wa pande mbili. Maana walisema je kama kwako itakuwa hivi itakuwaje, kwa hiyo toa tangazo kwa nchi nzima ili hamna mwanamke kuja kwako ni mpaka umenyooshea fimbo yake.
Kwa hiyo alimwambia Mordekai kuwa asimuone Esta kakaa pale lakini ndoa yangu iko salama. Lakini Mordekai alisema Esta usijue kama utapona kama wewe usipoomba maana utaangamia wewe na Wayahudi wote. Maana wewe uliujia ufalme huu majira haya. Shetani aliweka mkakati wake akatega mtego na akamtoa Esta kwenye mfumo mwezi mmoja kabla.
Kwa hiyo Esta alisema ombeni kwa ajili yangu kwa ajili ya siku tatu. Kwa hiyo jifunze kuomba kimkakati yaani kimfumo. Habakuki kitu cha kwanza alichofanya ni kuomba toba, alalafu alisema naogopa. Maana alikuja kugundua kuwa kuna kitu hakijakaa sawa kwake katikati kabla ya mfumo. Ndio maana alisema ee Bwana katikati ya ghadhabu kumbuka rehema.
Esta alikuwa anaombewa kwa ajili yake ili aweze kusimamia kusudi la Bwana. Maana japo Esta alikuwa na kila kitu lakini alikosa kusimamia kusudi la Bwana.
Hababuki aliomba kwa ajili ya toba maana katika maombi yake. Na ndio maana alisema katika ghadhabu kumbuka rehema.
Mathayo 6:33 Maandiko yanasema Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Mambo yanazunguzwa hapa ni ule nini uvae nini.Kwa hiyo tanguliza masilahi ya ufalme wa mbinuni. Je mbinguni wanakutazamaje wewe? Kule mbinguni unasomake?
Eliya alipochoka Mungu alimwambia nimekuelewa rudi nyumbani. Kuna mtu mwingine atakuja amalizie kazi. Kazi yake ilikuja kumalizwa na Elisha. Ule mfumo wa Ahabu ulimvuruga na kumtoa katika mfumo. Maana alipewa ale chakula ili aweze kuendelea na safari. Lakini alipokuwa chakula kwa mara ya pili alikuwa chakula na kilimsaidia. Japo hakumalizia kazi ambayo Mungu alimpa.
AINA YA PILI
MAOMBI YENYE JUHUDI
Maombi yenye juhudi ni maobi yenye kiu kubwa ya kutaka kujibiwa maombi yako.
Matendo ya Mitume 12:5
Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake . Hapa utaona kuwa wakati uke wa Herode alimkamata Yakobo na akamuua na baadae akamata Petro ndipo walianza kuomba kwa juhudi.
Kwa hiyo jifunze kuomba maombi kimkakati na omba kwa hati ya dhahura pale itakapobidi. Maana katika mahali popote pale kuna dhahura. Kwa hiyo je wewe una haraka kiasi gani katika mfumo?
Habakuki alilalamika sura ya kwanza na sura ya pili. Baada ya pale sura ya pili mstari wa pili. Mungu alikuja kumjibu na mpaka mstari wa 20 alipomaliza kusikiliza majibu ya Mungu. Ndipo unaanza kuona Mungu anasema Bwana nimesikia habari zako na nimeogopa. Baada ya pale alianza kutetemeka. Alisem ee Bwana fufua kazi yako katikati ya miaka.
Je alibeba kitu gani moyoni mwake. Kinywa kinasema kile ambacho kinaujaza moyo. Kwa hiyo utamjua mtu wa maneno ambayo anasema. Kama unafuatilia vizuri mashindano ya formula one. Unaona wanajua kabisa kuwa katika mashindano yake gari kama inakuwa imekimbia kilimota kadhaa wanajiandaa kubadilisha tairi.
Lakini wanakuwa wamejipanga kila kitu ndani ya dakika mbili au tatu unaona tairi wamebadilisha kila kitu. Na gari inaondoka mara moja. Lengo kuu ni kuwamfanya mshiririki ili aweze kushinda. Wale hawashindi kwa kukimbia bali ni kwa ajili ya muda.
Mungu anaposema kuwa badilisha mfumo wako na namna ambayo unaomba lakini unachukua muda mrefu kuomba na unaanza kubadilika kuomba. Inakuwa ngumu sana kuweza kubadilika na mfumo wako umejaza chuki.
Biblia inasema jua lisichwe moyoni mwako usiwe na uchungu. Maandiko yabasema katika Habakuki kuwa wakigeuzwa kuwa samaki huwa wanawekewa na roho ya uasi ndani yao. Mtu akikasirika hata kama alikuwa anakupenda anageuka kuwa mwasi wakati huo huo. Ila kanuni unayoitumia kubadilika ndio ambayo itafanya wewe uweze kubadilika.
Habakuki alisema ee Bwana fufua kazi yako katikati ya miaka kwenye ghadhabu kumbuka rehema. | 0 |
| 18 | Luka 17:20-21
“Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
Tunapookoka Yesu anaingia ndani yetu naye anaingia ndani yetu.
Saa nyingine unakasirika ufe lakini Mungu hakuui hii ni kwa sababu alijiweka wakfu kwa ajili yetu sasa unataka uende wapi? Kama Eliya alivyojaribu kutaka kufa lakini Mungu akasema ana njaa tu ale, aendelee na kazi yake.
Lazima tuishi kwa imani yaani ni kumtegemea Mungu aje:
Matendo ya Mitume 17:28
“Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu.”
Lakini tulipomkataa aliondoka katikati ya wanadamu lakini sasa hivi anakuja katikati yetu sawa na:
Habakuki 3:2-3
“Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema. Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.”
Maana yake Mungu aje ajidhihirishe sio atulie kwani akitulia ni kama hayupo (utukufu wake kuondoka).
Kwa wale wanaoenda na mifumo, wanajua mifumo inaenda na nyakati. Na mifumo ikifa Mungu anafufua vitu ambavyo vimekufa na hawezi kunyamaza na anakuongoza kwa neno lake katika uwezo wa Roho Mtakatifu. Mifumo iliumbwa kwa neno na unapotembea humo ndani unapewa neno.
Changamoto ni hii watu wanakuwa na mzigo wa kuomba wanapopata shida ila wakati wa amani hawana shida na maombi. Na wengine wanawategemea wataalam kuwasaidia kwenye vitu fulani Je! Siku wanaokusaidia hawapo utafanyeje? Hakikisha unajua namna ya kuenda pamoja na Mungu kwa kumtegemea.
Kama unamtegemea Mungu, maombi yanakuwa sehemu ya maisha yako (maombi yanakuwa ni mfumo wa maisha) na si kitu cha mara moja moja.
Ukisoma kwenye Biblia utaona watu waliokuwa wanaenda kwa Yesu walienda kuponywa sio kwamba walienda kwenye maombi ili kuponywa kwa hiyo wakienda kuponywa hawaridhiki na maombi wasipoponywa.
Kushiriki maombi ya kuponywa ni kwamba utaridhika hata kama hujaponywa.
Huyu ndugu alikuwa kwenye aligundua namna ya kuomba kwake maana mara ya kwanza alikuwa anaomba kwa kutazama tatizo lakini sasa alianza kuomba kwa kumtazama Mungu. Maana unaweza ukaenda hospitali kutibiwa na kwenda kuponywa.Kwa mfano ukienda hospitali kutibuwa hata usipopona hamna shida maana wewe unaangalia unaenda tu kutibiwa. Ila aliyeenda kuponywa huwa anaridhika pale alipopata huduma na akapona.
Pia kuna tofauti kwa aliyekwenda kusoma na kufaulu. Huyu ambaye anakwenda kusoma hajali kama atafaulu au asipofaulu.Kuna mtu mwingine unaweza ukamuuliza je wewe unafanya kazi. Atakujibu vizuri kabisa kuwa anafanya kazi. Lakini hataweza kukuambia matokeo ya ile kazi ambayo anafanya.
Kwa mfano ukienda kumuuliza daktari kuwa unafanya kazi gani atasema mimi ni daktari lakini hatakuambia kuwa taaluma yake imetibu magonjwa mangapi na wagonjwa wangapi. Kuna watu wanakimbia ili mradi lakini katika Biblia inasema ukimbie ili uweze kushinda.
Usipojua tofauti kati ya maombi ya Habakuki namna alivyokuwa anaomba mwanzo alikuwa anaomba kwa kuangalia matatizo. Lakini baada ya kutazama vema alianza kuomba kwa kuangalia maono ambayo Mungu kampa. Jibu halikuwa kwenye kulalamika bali ni kwenye maono.
Kama ukiondoka katika maono hamuwezi fika mahali maana utakuwa unafanya kazi ili upate mshahara. Nilipokuwa naangalia kitabu cha Habakuki katika mstari wa pili nimeona kuna aina sita za maombi ambazo Habakuki aliomba katika mfumo.
AINA SITA ZA MAOMBI AMBAZO HABAKUKI ALIOMBA
AINA YA KWANZA
MAOMBI YA KIMKAKATI
Kwa hiyo usiombe kwa hasira au kiholela. Kwa mfano ikitokea jambo limekukwamisha unaoata hasira na unapata hasira kubwa. Ndani yako kunajaa chuki, huzuni na maneno mengi. Lengo lake kukudhoofisha kuomba. Maana yake kila ukianza kuomba utaanza kulalamika. Wana Israel walipewa adhabu kwa kulalamika. Watu wengi huwa hawatubu kwa kulalamika kwao. Kwa hiyo nasisitiza sana kuomba kimkakati. | 0 |
| 19 | 5️⃣ SEMINA YA NENO LA MUNGU - UWANJA WA BOMBADIA / PIPOZ - SINGIDA MJINI : NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE
SIKU YA TANO : 21 JULAI, 2024
SOMO : “KUONDOA MAZUIO KATIKA MIFUMO YANAYOZUIA KUFANIKIWA KWAKO”
LINK YA SOMO HILI YOUTUBE: 👇🏼
https://www.youtube.com/live/IF0VICcW5NM?si=dmG5uhDM5KS37fex
NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA: 👇🏼
https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda
TEMBELEA AKAUNTI/KURASA ZETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII (Facebook, YouTube, Instagram na Telegram): 👇🏼
https://bit.ly/MwakasegeCDMM-Media
UTANGULIZI
MALENGO YA SOMO
Katika somo hili tuna lengo kuu moja:
🔴 Kuhakikisha kuona mifumo inatumika kufanikisha na si kukwamisha kama Mungu alivyokusudia.
Yeremia 29:11
“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho (baadaye).”
Mathayo 26:27-28
“Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”
Luka 4:5-8
“Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.”
LEO NATAKA TUANGALIE KITU/KIPENGELE KINGINE:
KUFANYA MAOMBI KAMA NJIA MOJAWAPO YA MUNGU KUKUONDOLEA MAZUIO KATIKA MIFUMO
Tuanze na
Habakuki 1:1
“Ufunuo aliouona nabii Habakuki.”
Ni mstari wenye maneno manne tu yenye nguvu. Habakuki aliandika hiki kitabu baada ya kuona haya yote ambavyo mtu wa kawaida hawezi kuviona. Nami namwomba Mungu uone maono kwa namna hii alivyoona Habakuki.
Halafu nataka tulinganishe hii mistari miwili ya:
Habakuki 2:1
“Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu.”
Na
Habakuki 3:1
“Sala ya nabii Habakuki.”
Sura ya pili unaona Habakuki ameingia kwenye zamu yake ya utumishi lakini analalamika ila sura ya tatu ameingia kwenye sala isiyo na malalamiko.
Tukiona kwenye mioyo yetu (rohoni) kama alivyoona Habakuki kwenye moyo wake, tutaona ndani ya mifumo alichoona halafu tutabadilika kile tulichokibeba tunapoombea mifumo. Kama hivi:
Habakuki 3:2
“Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.”
Na ukianza kusoma Habakuki 2:2-20 Mungu anaongea na Habakuki na Mungu akampa majibu mengi hapo la kwanza likiwa ni kuwa na maono. Bila kuwa na maono hata utendaji wa unachofanya hauendi sawasawa.
Kitu kingine alichoona ni hasira ya Mungu ukiona hasira ya Mungu kwa jicho la binadamu unaweza ukadharau lakini ukiona kwa jicho la Mungu utajipanga sawasawa.
Ukisoma Habakuki 2:6-20 utaona maneno "OLE WAKE" na yametokea mara sita. Ole zilikuwa nyingi ila neno "MWENYE HAKI WANGU" lilikuwa moja tu; inaonyesha Mungu alikuwa ana hasira sana juu ya mambo yaliyoko kwenye mifumo. Tazama hasira ya Mungu kwa jicho la Mungu, utakaa sawasawa.
Mwenye haki akiwa kwenye mifumo ataishi kwa imani yake. Lakini baada ya ole hizo kutolewa na Mungu Habakuki alikuja kugundua lile halikuwa tatizo la kawaida bali ni la kiroho. Kama alitakiwa kuishi kwa imani hawezi kuishi peke yake yaani anapaswa kuwa na imani na Mungu kimfumo.
Watu wengi sana waa uhusiano na Mungu kwa ajili ya kwenda mbinguni na si kwa ajili ya kuishi duniani ndio maana hawajali namna ya kuishi na Mungu duniani ila wanajitahidi sana kukung'uta dhambi ili dhambi isiwakwamishe kwenda mbinguni.
Kuna ufalme wa Mungu kwenye sehemu mbili yaani mbinguni na duniani. Kuna ufalme tunatakiwa kuuingia na Yesu mwenyewe alisema tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Hakusema tubuni kwa maana safari ya kwenda mbinguni imekaribia. Yesu alimaanisha sisi kuingia katika ufalme wa Mungu na ufalme wa Mungu kuja hapa duniani na kuingia ndani yetu. | 0 |
| 20 | MAOMBI 03
Katika maombi tunapata uthibitisho wa Neno la Kristo na makusudio yote yanadhihirika kwa kuomba.
Ayubu 22:27
"Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako."
Fanya maombi kila mara ili lile neno lililokusudiwa na Mungu kwako lipate kuthibitika kwako.
Mungu akubariki sana!
Lazaro Zakaria | 0 |
