E-PLUS MEDIA
Ir al canal en Telegram
1 307
Suscriptores
+124 horas
-27 días
-1330 días
Archivo de publicaciones
1 307
"TFF INAPASWA KUTOA MAJAWABU".
The Most Tanzanian inform player, Tanzanian Icon Katika Soka la Wanawake,Nyota zaidi na anayelipwa fedha nyingi zaidi ya Wachezaji Wote wa Soka la Wanawake katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Mshindi wa Tuzo Ya Outstanding in Women Sport Kwenye Tuzo za Women in Sport, Art and Culture Awards 2023 (WISAC) zilizotolewa Novemba 3 Jijini Dar es salaam, huyu hapa Ni "Clara Luvanga".
Clara anakipiga kunako Timu ya Wanawake ya Al Nasri ya Ligi kuu ya Saudi Arabia,ikumbukwe Al Nasri ya Wanaume ndio anayochezea Nyota Mahiri wa soka Duniani Cristiano Ronaldo.
Clara Luvanga ambaye Zamani alicheza Yanga Princess kabla kuhamia Hispania na Kisha Al Nasri,Msimu Huu anaongoza kwa Magoli Huko Saudi Arabia akiwa na Magoli 6 katika Mechi 5,
Pamoja na kufunga Magoli yote Manne Katika Ushindi wa 4-1 wa Tanzania ya Vijana Dhidi ya Cameroon ya Vijana Huko Cameroon Mwaka Jana na tukafuzu Kombe la Dunia la Vijana kwa Mara ya kwanza Lakini Nyota huyu Mahiri wa Tanzania jina lake halimo katika Orodha ya Wachezaji walioitwa katika Kikosi Cha Timu ya Taifa ya Tanzania -Twiga Stars kitakachoingia kambini Tarehe 22 Mwezi Huu.
Walioitwa ni Julieath Singano(FC Juarez- Mexico) Enekia Kasonga(Eastern Flames- Saudi Arabia)Diana Lucas -Ameds FK( Uturuki) Opa Clement (Besiktas-Uturuki) na Aisha Masaka (BK Hancken - Sweden).
Je Tatizo lipo Wapi, TFF inapaswa kujibu Hilo.
Pio Pius.
1 307
KUTOKA MITANDAONI
Kwa habari zaidi SUBSCRIBE kupitia YOUTUBE channel yetu kwa ku bonyeza hapa chini.👇.kwenye link
https://youtube.com/@E-PlusMediaTv?si=JjehK80_nkzrHGNK
1 307
⚠️ Mama yake Burna Boy kwenye ubora mpya
Mama Burna Boy ambaye jina lake halisi ni Bosi Ogulu yeye ndie meneja wa mwanae(Burna Boy) katika kazi zake za muziki
Mama Burna Boy yupo kwenye ndoa tangu mwaka 1990, yeye na mume wake wamejaaliwa watoto watatu ambao ni Burna Boy(32) na wadogo zake wenye miaka 30 na 29
Mama Burna Boy ni msomi wa degrees za vyuo vikuu hasa katika lugha za kigeni na tafsiri za lugha, anazungumza vizuri lugha 6 ambazo ni kiingereza, kifaransa, kiitaliano, Kijerumani na Kiyoruba na Pijini english ya Nigeria.
Kwa miaka kumi alifundisha Kifaransa katika chuo kikuu cha elimu Hartcourt, Nigeria pia aliwahi kuwa mtafsiri lugha katika Federation of West African Chambers of Commerce
Aliamua kuacha kazi huko kwingine na kuamua kujikita zaidi kiwanda cha muziki alikoona kuna maslahi zaidi hasa kumsimamia mwanae ambapo Burna Boy mwenyewe ndie alimuomba mama yake awe meneja wake baada ya kuona ana uwezo mkubwa katika hilo
Mwaka 2021 Bilboard ya Marekani katika orodha yao ya Internationa Powers Players List kutambua mchango wake kwa anachokifanya katika ulimwengu muziki ambapo mwanae kwasasa sio tu superstar mwenye mafanikio katika muzika bali ameweza kukubalika hata kidunia ikiwemo America na Ulaya
Picha akiwa na mume wake kwenye comments section
1 307
Pichani ni mchezaji Romeo Lukaku akiperuzi katika simu yake kwenye benchi katika kipindi cha pili cha mchezo wao, Ubeligiji dhidi ya Azerbaijan.
Katika mchezo huo wa jana Ubeligiji iliibuka na ushindi wa bao 5 kwa 1, na Lukaku alifunga goli 4 kati ya hizo 5.
Akitumia dakika 37 pekee kupachika mabao hayo. Nafikiri hapo Mwanetu alikuwa anaangalia kama bloggers wamekwisham-post! 😀
1 307
Watu ambao kawaida hupata mapumziko kwa kulalala mchana wanaweza kuwa na ubongo mkubwa!
Kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la Afya ya usingizi 'Sleep Health', limeeza kuwa watu ambao kawaida hulala mchana walikuwa na ubongo ambao ulikuwa mkubwa kwa kiasi sawa na miaka 2.6 hadi 6.5 ya uzee ikilinganishwa na watu ambao hawakuwa wakilala mchana!.
Matokeo hayo yanapendekeza kwamba kulala mchana kunaweza kufanya kazi nzuri katika kuchelewesha mchakato wa kupungua kwa ubongo kunaoktokea kutokana na ongezeko la umri.
M-tag rafiki yako ambae anapenda kulala mchana, umfikishie hizi good news! 😀
1 307
Wataalamu nchini Uingereza wapo kwenye majaribio ya kifaa kipya kitakachuruhusu watazamaji kuonja chakula moja kwa moja kutoka kwenye televisheni pindi wanapotazama vipindi vya mapishi.
1 307
Kikawaida siku ya ‘birthday’ mwenye sherehe ndio hupaswa kuzawadiwa lakini Rais wa Makampuni ya GSM Ghalib Said Mohammed kwa upendo wake ameamua kubadilisha mazoea na kutoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya milioni 137 kwa Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam.
Katika hafla fupi iliyofanyika Hospitalini hapo, Ghalib alishiriki kula chakula na Wageni maalum wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, Rais wa TFF Wallace Karia na Rais wa Yanga Hersi na kukata keki.
Ghalib ni Mfanyabiashara anayeheshimika na kukubalika na Watu wengi Nchini Tanzania Kutokana na uzalendo wake kwa Taifa, moyo wake wa kusaidia wengine pamoja na uwekezaji wa kimapinduzi alioufanya kwa Club ya Yanga ulioleta matokeo mazuri uwanjani hadi kupelekea Mashabiki zake kuingia kwenye orodha ya Mashabiki wenye furaha zaidi Barani Afrika.
1 307
Tanzania inakadiriwa kutumia takribani Sh5.6 trilioni kila mwaka kutokana na gharama za matibabu ya magonjwa, muda wa uzalishaji mali kupotea kwa sababu ya kuuguza au kuugua magonjwa yanayotokana na kujisaidia nje.
Kwa mujibu wa Taarifa ya hali ya uchumi iliyotolewa na Benki ya Dunia (Tanzania Economic Update) ya mwaka 2023 imeonesha hiyo ni gharama ambayo nchi imekuwa ikiipata kutokana na hali duni ya huduma za maji na vyoo.
Hayo yamesemwa jana Jumapili, Novemba 19, 2023 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipotoa tamko kuhusu Siku ya Choo duniani huku akihamasisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi ya choo bora kama njia muhimu ya kudhibiti magonjwa yatokanayo na kinyesi cha binadamu.
1 307
"Ukikitumia kipaji vizuri kinakupa maisha ukikitumia vibaya kinakupa msongo wa mawazo ndiyo maana leo wakina Ronald wanaishi vizuri kwasababu walikitumia kipaji kuwa ajira, kwahiyo tuna changamoto kubwa ya wasanii wa Tanzania kuwa na afya ya akili" Steve Nyerere, Msanii wa Filam
1 307
BBC inasema: Trump anataka kuiondoa Marekani katika muungano wa NATO iwapo atashinda uchaguzi ujao (Basi nini kitatokea kwa Ukraine)
Imechapishwa: 05 Novemba, 2023 09:35
Donald Trump atafanya nini ikiwa ataingia madarakani kwa muhula wa pili
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anafanya kampeni za kuwa mgombea katika uchaguzi ujao wa rais wa Marekani. Kwa sasa Trump ndiye mgombea anayeongoza kwa uteuzi wa chama cha Republican. ikiwa mgombea wa chama hicho atathibitishwa, ataingia kwenye vita vya uchaguzi na Rais wa sasa Joe Biden mnamo Novemba mwaka ujao.
Trump alishindwa na Biden, kiongozi wa Chama cha Kidemokrasia katika uchaguzi wa rais wa 2020.
Wakati huu, hataki kuendelea kujaribu makosa. trump anatazamia kurekebisha makosa ya muhula wake wa kwanza madarakani na kusonga mbele. Kwa sababu hii, Trump na chama chake wanapanga watakachofanya iwapo wataingia madarakani kwa muhula wa pili, huku kukiwa na shughuli nyingi za kampeni za uchaguzi.
Kuangalia tovuti ya kampeni ya Trump, mikutano yake mbalimbali ya kampeni, na mazungumzo na wafanyakazi wa karibu hutoa mwanga wa mipango yake ya muhula wa pili.
Iwapo atashinda uchaguzi ujao, atakuwa Rais wa 47 wa Marekani. akimaanisha idadi hiyo, mpango ambao Trump atautekeleza atakapoingia madarakani unaitwa 'Ajenda 47'.
Mark Lotter alikuwa mmoja wa wafanyikazi wa kampeni ya Trump wakati wa muhula wake wa kwanza ofisini. Bado yuko karibu na Trump.
bahati nasibu na wafanyikazi wengine wanahisi kuwa upungufu katika maandalizi ya muhula wa kwanza hauwezi kudumishwa wakati huu. Hata hivyo, baadhi ya mipango ya Trump kwa muhula wa pili inaonekana kuwa ya kipuuzi; Kwa mfano, akipata muhula wa pili madarakani, serikali itawekeza katika kujenga magari yanayoruka. pia kuna baadhi ya mipango yenye utata; Kwa mfano, watu wasio na makazi watahamishwa hadi kwenye kambi za mahema mbali na miji. Wanapaswa kukaa katika kambi hiyo hadi tatizo litatuliwe. baadhi ya mipango ya Trump inapingana moja kwa moja na utamaduni; K
1 307
Unaweza ukavaa tu kama swaga lakini mavazi mengi duniani huwa yanamaana wenzetu Wana utamaduni wa kuvaa kwa kumaanisha ila sisi huku kibongo bongo tunajivalia tu 🤣🤣 mfano mzuri ni hiki kilemba Cha Palestina au 'keffiyeh' kinatumika kama nembo ya mshikamano na harakati za Palestina. Vazi la kitamaduni - mara nyingi huzungushwa kwenye kichwa au shingo ya mfuasi kwa mitindo tofauti - ina majina tofauti kulingana na nchi: Inaitwa "shemagh" huko Jordan na Syria na "ghutra" katika nchi za Ghuba.
Pamba nyeusi tofauti kwenye kilemba cha pamba nyeupe inaaminika kuwa na umuhimu wa ishara.
Miundo kwenye keffiyeh inasemekana kujumuisha alama hizi tatu zinazowakilisha Palestina:
Dress how you want to be addressed .
1 307
UTATA KISA CHA UGOMVI WA MR NICE NA DUDU BAYA 👇👇👇
Tukio lililo wahi kuwashangaza na kuwashitua wengi ni tukio lilitokoewa January 2004. Pale Dudu Baya alivyo vamia stejini na kuanza kumshushia kipondo Msanii mwenzake Mr Nice licha ya kuwa na walinzi wengi (security) ukumbini hapo lakini hawakuweza kumzuia Dudu Baya kutekeleza shambulio hilo. Watu wengi hatuwahi kujua kwamba wawili hao walikuwa wanaukaribu ama urafiki wengi tulijuwa watu WA karibu wa Mr Nice alikuwa Mtunis, Ben Kinyaiya, Rey Kigosi huku upande wa Dudu Baya tuliwajua Darskendo. Baada ya tukio hilo wanahabari na watu mbali mbali walihangaika kujuwa chanzo cha ugomvi huo lakini kwa kiasi kikubwa zikawa hadithi tu kwani pia wawili hao hakuna aliewahi kuwa tayar kuzungumza ukweli juu ya tukio hilo japo kidogo Mr Nice kwenye wimbo wake wa Rafiki aligusia kwambali juu ya ukaribu wake na Dudu Baya, Chakushangaza zaidi ni jinsi kesi hii ilivyo kufa kirahisi bila kwenda hata mahakamani iliishia Polisi tu baada ya Dudu Baya kukamatwa na kuswekwa lumande kwa muda mrefu na baadae Eric Shigongo akaja kumtoa. Ni wazi kuna jambo kubwa limejificha juu ya tukio hili zikaibuka tetesi kwamba kisa cha ugomvi huo ni Tajiri wa kipindi hiko Merey Balhabou aliekuwa mmiliki wa sheri za TOT, wanadai Dudu Baya na Mr Nice walikuwa wakipishana kwenye korido za ofisi za tajiri huyo
