E-PLUS MEDIA
Ir al canal en Telegram
1 307
Suscriptores
+124 horas
-27 días
-1330 días
Archivo de publicaciones
1 307
"Yanga wana timu nzuri inayoweza kuimaliza Al-Ahly ila kwa kutumia mfumo wa (4-2-3-1) wakiwa hawana mpira, lakini wanaposhambulia wanaweza kubadilika na kutumia (4-3-3) ili kurahisisha mashambulizi"
"Al-Ahly wanacheza tofauti wanapokuwa nyumbani na ugenini. Kwa kuwa Yanga ataanzia nyumbani, ndiyo wanahitaji kucheza hii mechi kwa kuhitaji matokeo mazuri lakini wanatakiwa kuwa makini kwani wapinzani wao wanapenda sana kucheza soka la kushambulia"
"Kama Yanga watatumia mfumo wa (4-3-3) wakati wa kushambulia utawafanya kuwa na idadi nzuri kule mbele katika mashammbulizi yao ambapo itawapa wakati mgumu mabeki wa Al-Ahly ambao hawana utulivu sana"
"Al-Ahly hawana kasi sana ya kukimbia kurudi nyuma kujilinda, hili lazima Yanga walitumie kwa kucheza mpira wa kasi ili wafike langoni kwao kuwapa presha mabeki wao"
"Yanga ina wachezaji bora, ila ina wachezaji (3) wenye ubora zaidi, Aziz Ki, Pacome, Max. Kama wakiamka vizuri siku ya Mchezo wanaweza kuwa hatari katika lango la Al-Ahly" - Robertinho 🇧🇷, aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Simba SC via MwanaSpoti.
Ukihitaji matangazo ya biashara yako au Promotion ya nyimbo zako, filamu, mitandao yako ya kijamii (facebook na YouTube), njoo inbox 📥
Toa maoni yako
#MvanoSports
#MvanoMtangaeaji
#M32
1 307
Mista Champagne Vs Kajala
Niambie umeona nini kwenye picha hizi mbili. Kwa waliosoma Cuba tumeelewa tayari 😂😯
NB : Comenti fupi fupi
1 307
Mtangazaji wa Wasafi FM @oscaroscarjr amefanikiwa kutunukiwa shahada ya uzamili ya sanaa katika mawasiliano ya umma (Masters Degree of Arts in mass Communication) toka katika chuo kikukuu cha cha Dar es Salaam.
1 307
Kijana Mmoja ambaye jina lake halijafahamika wala Makazi yake amekutwa amejinyonga katika nyumba ambayo haijamalizika ujenzi iliyopo mtaa wa Madizini kata ya Lizaboni
Wakizungumza na Wasafi Media George Oddo Diwani wa kata ya Lizaboni na Cathbert Mwinuka ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Madizini wamesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Novemba 30 2023 huku wakidai mtu huyo ambaye amevalia jezi ya Timu ya Simba hafahamiki katika mtaa huo
"Ni kweli tukio hili limetokea hapa kwetu lakini huyu mtu kwetu ni mgeni hafahamiki na hajulikani katokea wapi pia hata chanzo cha kujinyonga kwakwe hakuna anayetambua" wameiambia Wasafi Media.
1 307
Mchezaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Aurelien Tchm ameuchagua wimbo wa msanii wa Tanzania, Harmonize unaoitwa Single Again kama wimbo wake pendwa wa Afro beat
Aurelien Tchm amemjibu shabiki kupitia Instastory ambapo shabiki huyo alitaka kufahamu wimbo pendwa Afro beat kutoka kwa mchezaji huyo ndipo akauchagua Single Again wa Harmonize.
1 307
Diamond Platnumz ameonekana akipiga goti na kumvisha pete ya uchumba mrembo, Peace Hyde.
Peace Hyde ni mtayarishaji wa vipindi vya televisheni kutoka Ghana.
Tukio hili linazidi kuwaacha wengi na maswali.
1 307
kuelekea siku 16 za kupinga ukatili.....wanawake wanashauriwa kuchunga midomo yao....katika kupambana na ukatili
Neno gani alikuambia Mwanamke/Mkeo husahau Mpaka Leo?
1 307
KAULI YA "SIKUMPENDA RUSHAYNAH" YAMPONZA HAJJI MANARA.
Hajji Manara amejikuta kwenye wakati mgumu wa kushambuliwa na wadau mbalimbali na hii ni baada ya kusema kwamba alimuoa Rushaynah ili kumkomoa Rubynah ambaye alikuwa mkewe kwa wakati huo na sio kwamba alimuoa kwasababu alimpenda.
Kwenye mahojiano yake na Mashamsham ya Wasafi fm, Hajji alisema kati ya mnyororo wa ndoa zake tano alizowahi kuzitumikia aliwapenda wanawake wengine wote isipokuwa Rushynah ambaye alimuoa kama kipozeo, fimbo ya kumchapia mkewe ambaye kwa wakati huo alikuwa akimsumbua.
Kauli hiyo ya Manara imechukuliwa kama udhalilishaji kwa wanawake na sio udhalilishaji tu bali ni udhalilishaji uliopitiliza kwasababu hata kama ni kweli hakumpenda Rushynah hakupaswa kutamka hilo tena kwenye media kubwa, angebaki nalo moyoni asingepungukiwa kitu. Wapo walioomba ikiwezekana akamatwe kwa udhalilishaji huo na wapo ambao awali walimuona Rushynah kama ndiye mwenye makosa lakini baada ya kauli hiyo ya Manara watu wengi wameungana na Rushynah.
Kwa upande wako una mtazamo gani juu ya kauli ya Hajji Manara?
1 307
"Ukija nyumbani kwangu kwenye friji langu hakukosi chocolate, biscuits na maziwa, napenda vitu vyenye nutrition kwa sababu pia mimi ni mtu wa mazoezi sana. Mimi huwa naamka saa saba au saa nane mchana na nikiamka chakula changu pendwa nitatanguliza ndizi na parachichi"- Chris Mziwanda
1 307
Kutoka Group la Wahenga (Enzi Hizo)
MOHRA ni filamu Kali sana ya kihindi imetoka 1994 Kwangu ni best na nyimbo zake tamu waliobahatika kuiona watakua mashuhuda kama Bado itafute humu Kuna wakali kama Akshay Kumar, Sunil Shetty,Nasseruddin Shah,Raveena Tandon na wengineo .Nasseruddin anajifanya kipofu anamtumia Sunil mShetty kufanya mauaji kila akiua mwamba anaweka X kwenye picha ya mhusika ila badae inagundulika kuwa Nasseruddin anaona sio kipofu half ni jambaz la hatar so Akshay Kumar ambae ni askar Wana ungana na Sunil Shetty kummaliza jamaa haikua rahisi daah bonge la muvi unaikumbuka hii muhenga.
1 307
Ukiwahitaji hawa Wasanii wa Afrika kwenye show yako, jiandae na kiasi hicho cha fedha 👇
NB : Thamani ni kwa dola ya Kimarekani.
1 307
"Futi sita na ushee hiyo, ukija na kitanda chako cha futi tano au sita yenyewe unamlaza mkunjo wa samaki. Ni Twiga flani aliyenyooka na mwendo wake unafanana na Kangaroo wa Prince William wa UK, shingo yake imenikumbusha Beyonce aliposhinda zile Grammy nyingi miaka ile"
"Hakujui Uturuki wala India lakini shepu yake ni ya Kistaa, namuona kabisa new Staa mjini, imagine Bugati ndio nimpeleke zile ruti zangu za kufa mtu, itakuwaje? yale mavocation ya Bugati tour. Simtabirii lakini anaenda kushika nchi soon, ajiandae tu kuanza kupigwa vita ya mtandao, uzuri kaka yako ni gwiji huku nitakulinda na kukuhifadhi kwa gharama kubwa"
"Yes, siwezi kuacha kumlinda new celebrity wa nchi, asiyejua hata jaribu na koboa face, ni rangi ya peponi hii ni colour ya Makka, tena orijinal. Naanza kumpenda huyu dada yangu, anything can happen, mambo ya kuficha-ficha siwezi kabisa kwanza friji langu lenyewe bovu namficha naniliu, no baby"- ameandika Hajji Manara.
Toa maoni yako
1 307
"Tanzania ndio nchi pekee ambayo ukianza kuhifadhi pesa zako kwenye kibubu ikifika elfu 50 ni kosa, mjomba kashameza shoka huko vijijini. Nimeanza kusevu pesa nimefikisha elfu 50 simu kibao zinaanza kuingia na zote ni za shida kibao!! kuanzia familia mpaka ukoo, kwani hii ni Tanzania tu au na nchi zingine ziko hivyo?"- Mama Nairo
1 307
⚠️🕊 Ama kweli ajali haina kinga, mwanadada huyo pichani baada ya kufanyiwa Send-Off Marehemu alikuwa anaelekea Kilimanjaro kwa ajili ya harusi yake iliyopangwa kufanyika 2/12/2023 (Jumamosi). Kwa bahati mbaya wakapata ajali mbaya maeneo ya Mwanga.
Ajali hiyo imemchukua bibi harusi mtarajiwa (Bi Rehema), mama yake mzazi na dada wa kazi.
Hakika wapumnzike kwa amani na waliobaki Mungu awatie nguvu, hasa wazazi na mume Marehemu.
1 307
LEO NITASEMA UKWELI KUHUSU ALIKIBA; BARAKA THE PRINCE
"Mimi sio Malaika, mimi sio Mtume wala mimi sio Yesu au Manabii, kinachonishangaza kuhusu mashabiki wa msanii wenu plus wadau na watangazaji walio nyuma ya mgongo wake. Ukimzungumzia msanii wao wanakuja juu, ukikwepa pia kumzungumzia wanakuja juu, so watu kama hawa niwaweke katika kundi gani?"
"Sasa basi, leo ni siku ya kuzungumza ukweli wote na kama unajua ukweli wangu huwa unakukera please zima data kwa siku tatu maana najua ukweli wa leo nitakukera mno, nimechoka kulimbikiziwa ubaya kila siku na baadhi ya panya Road wadogo wadogo wenye nia na madhumuni mabovu juu ya career yangu. Nimechoka kuonekana mbaya hata kama nimekosewa mimi, aiseee leo ni siku ya kuongea ukweli hadi Media, watangazaji wanaonifanyia figisu tangu mwaka 2016, ninazo listi zao na matukio yote plus ushahidi, leo nitakuwa live saa 8:00 pm kupitia Instagram page na YouTube yangu"- ameandika Baraka the Prince.
Maamuzi hayo ya Baraka yamekuja baada ya siku za hivi karibuni kususia mahojiano na moja ya chombo cha habari, na kususia huko kulikuja baada ya kuulizwa swali kuhusu Alikiba. Kitendo cha yeye kuondoka katikati ya mahojiano kiliwaibua mashabiki na wadau wa Muziki ambao waliandamana kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuanza kumporomoshea matusi huku wengi wakidai ana dharau, kujisikia na kwa staili hiyo hawezi kufika popote.
