es
Feedback

¡No caigas en manos de tramposos! Telemetrio encuentra y marca estos canales 👉 Si quieres ver la etiqueta, suscríbete 👈

E-PLUS MEDIA

E-PLUS MEDIA

Ir al canal en Telegram

Get the latest news,videos,and more everyday.

Mostrar más
1 307
Suscriptores
+124 horas
-27 días
-1330 días
Archivo de publicaciones
CHILLAH: NAMCHUKIA SANA ALIKIBA - Q Chillah akiongelea kuhusu Alikiba kuwa na Kiburi amesema Umwinyi ukizidi sana huwa ni Tat
CHILLAH: NAMCHUKIA SANA ALIKIBA - Q Chillah akiongelea kuhusu Alikiba kuwa na Kiburi amesema Umwinyi ukizidi sana huwa ni Tatizo ni vyema Alikiba akaitumia kalama yake ya Muziki kutoathiri Kizazi sababu Ufalme ni suala la Kisayansi, kitamaduni na kurithishana Kimila. Amesema hajawahi kufanya Collabo na Alikiba wala hana ukaribu naye, yeye huwa haombi Collabo bali anaombwa Collabo. Aidha, Q Chillah amesema hapendi kuulizwa mambo ya Alikiba kwa sababu ni kumuuliza Upumbavu wa Wapumbavu, anataka aulizwe kuhusu Nyimbo zake zinazotarajia kutoka mwaka huu. Amesisitiza kuwa hakuna msanii yeyote anayemuweza kwa kuimba hapa nchini akiwemo Christian Bella na wengine wote wanaojiona wakali

"Kwa sasa mimi ni Kungwi tena ni somo haswaa, nimewafunda wanawake wengi hata 400 wanafika. Lakini pamoja na kuwa Kungwi mkub
"Kwa sasa mimi ni Kungwi tena ni somo haswaa, nimewafunda wanawake wengi hata 400 wanafika. Lakini pamoja na kuwa Kungwi mkubwa mimi pia nimeachika kwenye ndoa mbili na sasa sina mtu nipo single, nawambiaga masomo wangu kuwa wafuate maneno yangu wasifuate matendo yangu"- Bi Rehema Majuto, Kungwi maarufu Tanzania. Toa maoni yako

"Kiukweli sadaka zinatolewa ili ziliwe, hatuna account ya Mungu hapa kwamba mkitoa leo tutaenda kuposti ziende mbinguni. Mwam
"Kiukweli sadaka zinatolewa ili ziliwe, hatuna account ya Mungu hapa kwamba mkitoa leo tutaenda kuposti ziende mbinguni. Mwambie jirani yako acha ujinga! sisi ndio meno yake, sisi ndio meno ya Mungu tunakula kwa niaba"- Pastor Daniel Mgogo, Mchungaji. Toa maoni yako

"Nilikuwa nampenda sana mume wangu, nilikuwa sitaki kumpoteza lakini majaribu yalizidi ndoa yangu ikasambaratika. Usicheze na jaribu la ndoa, kuna watu wakiona mtu hayupo kwenye ndoa wanahisi mtu hapendi ndoa. Kwa binadamu mwenye akili timamu hakuna mtu ambaye hapendi mahusiano yake ilimradi hakutafutiwa alijitafutia mwenyewe" "Hakuna mtu anayetamani stress za ndoa, ila adui anajua chanzo cha baraka ni ndoa ikiwa na amani, ili baraka iondoke kwenye familia lazima ndoa iharibike, kwahiyo adui anaipiga ndoa kwasababu anajua penye ndoa ya amani pana kila kitu kizuri. Ndoa yangu ilipoanza kuwa ngumu nikashangaa mume wangu akabadilika, ile sura nzuri niliyokuwa naiona ya mume wangu ikapotea akawa sio yule tena yani sijui alikuwa ananiona kama kituko cha namna gani" "Lakini zaidi ya yote changamoto nyingine nilianza kupata kwenye vyombo vya habari, kipindi kile kulikuwa na gazeti la KIU walikuwa wanaandika makala yangu mpaka wanasema itaendelea toleo lijalo. Kwahiyo kila nikipita njiani nilikuwa nakutana na habari zangu kila kona kwenye magazeti, nilikuwa napewa matukio ya ajabu na ya kutosha, na kilichotokea ni kwamba Waandishi walimfuata jamaa yangu akiwa na hasira halafu tayari alikuwa na mwanamke mwingine, kwahiyo alizungumza yote akaongeza na chumvi za kutosha" "Lengo lake kubwa lilikuwa ni kunishusha na kunipoteza kabisa, alikuwa anawaambia waandishi kuwa nataka nimpoteze Bahati kwasababu nimempa umaarufu halafu ameleta mbwembwele. Kwahiyo mimi ndoa nilikuwa naitaka sana lakini kwa bahati mbaya nilikuwa napata mimba nikizaa watoto wakikaa siku chache wanakufa, akawasikiliza ndugu na marafiki zake wakamwambia ajaribu sehemu nyingine, sasa kwenye kujaribu ikawa sio kujaribu tena ni vurugu, nikaamua kuondoka na hapo ndipo vita ilipoanzia"- Bahati Bukuku, Mwimbaji wa muziki wa Injili Tanzania. Ikumbukwe kuwa Bahati Bukuku aliachana na Mume wake aitwaye Daniel Basila ambaye walifunga ndoa mwanzoni mwa miaka ya 2000. Toa maoni yako

photo content

"Vijana wa siku hizi hawana adabu kabisa, yani Vijana wadogo lakini wanapata nguvu ya kunitongoza eti mama nimekuelewa, ni wa
"Vijana wa siku hizi hawana adabu kabisa, yani Vijana wadogo lakini wanapata nguvu ya kunitongoza eti mama nimekuelewa, ni washenzi wanaenda na ule msemo wa "ukipata limama likomoe" wamkomoe nani? mie? wakija wakiniambia mama nimekupenda nawaambiaga asante hauko peke yako. Mimi mpaka kuwa hapa nimejitunza, situmii kilevi chochote na kwenye yale mambo yetu ya kitandani natumia kiasi"- Khadija Kopa, Msanii wa muziki wa Taarab Tanzania. Toa maoni yako

"𝗔𝗡𝗚𝗔𝗟𝗜𝗘𝗡𝗜 𝗠𝗪𝗘𝗭𝗜 𝗠𝗨𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗢 𝗝𝗨𝗠𝗔𝗧𝗔𝗧𝗨 𝗦𝗜𝗞𝗨 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗔𝗕𝗔𝗡𝗜 29" Samaha Mufti Dr. Abubakar
"𝗔𝗡𝗚𝗔𝗟𝗜𝗘𝗡𝗜 𝗠𝗪𝗘𝗭𝗜 𝗠𝗨𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗢 𝗝𝗨𝗠𝗔𝗧𝗔𝗧𝗨 𝗦𝗜𝗞𝗨 𝗬𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗔𝗕𝗔𝗡𝗜 29" Samaha Mufti Dr. Abubakar Zubeir Ali Mbwana amewataka waislamu wa Tanzania kutazama Mwezi kwa Makini siku ya Jumatatu tarehe 11.3.2024 sawa na Shaabani 29. "Mkiona Mwezi popote mlipo kote nchini toeni taarifa haraka iwezekanavyo kwenye ofisi ya Bakwata ya karibu ili funga ya Ramadhani ianze Jumanne 12.3.2024. ikiwa hautaandama Jumatatu tutatimiza siku 30 za shaabani na kuanza funga Jumatano 13.3.2924" amesema Mufti Akiongea na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake jijini Dar es salaam Mufti amewataka Masheikh kuendeleza utaratibu wa kutoa Darsa misikitini na kuwataka waislamu kusikiliza dasra hizo. Aidha amewataka waislamu wazidishe dua na ibada mbalimbali ambazo zina malipo makubwa ndani ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani. ....... Dr. Harith Nkussa Mwandishi Maalum wa Mufti Saa sita na dkk 30 Mchana Alhamisi 7.3.2024 Bolisa Kondoa. Chanzo @ Harith Nkusa

Msanii aliyetamba na ngoma ya imekaa vibaya na tumbo joto Abdul Miraji maarufu kama Kali P amesema hataki tena kusikia masual
Msanii aliyetamba na ngoma ya imekaa vibaya na tumbo joto Abdul Miraji maarufu kama Kali P amesema hataki tena kusikia masuala ya muziki kwani katika upande wa dini yake ya kiislam ni jambo hilo ni haramu. Kali P amesema ameamua kumrudia Mungu na sasa hivi ana takriban miaka 12 ameingia Kwenye dini na ameachana na masuala ya muziki. “Katika dini yetu ya Uislam muziki ni haramu ndio maana mimi nikajitoa kwa sababu ya kumuogopa Mungu, kama ujumbe kuna njia ya watu kuwafikishia ila sio muziki, siku ambayo naacha muziki nafsi yangu ilisema sipendi tena muziki.” Aidha msanii Kali P ameongeza kusema “Kipindi nafanya muziki nilikuwa na miaka 22, Nyimbo zangu zikipigwa najisikia vibaya na sina habari nazo tena, atakayeimba atakuwa anajichochea moto mwenyewe, muziki utaratibu halali wa kutafuta riziki. Kali P sasa nafahamika kwa jina la Shekh Abdul Miraji na anapatikana maeneo ya Kitunda, Dar es Salaam. CC : Smile FM Toa maoni yako

Wanaimaliza siku kuu ya akina Mama Duniani.
Wanaimaliza siku kuu ya akina Mama Duniani.

photo content

KUTOKA MITANDAONI Jiunge ukurasa wetu wa what's up hapa kwenye link.👇 https://whatsapp.com/channel/0029VaD9yM1D8SE3Brlapz1l
KUTOKA MITANDAONI Jiunge ukurasa wetu wa what's up hapa kwenye link.👇 https://whatsapp.com/channel/0029VaD9yM1D8SE3Brlapz1l

KUTOKA MITANDAONI Jiunge ukurasa wetu wa Telegram..👇 https://t.me/EplusmediaTv
KUTOKA MITANDAONI Jiunge ukurasa wetu wa Telegram..👇 https://t.me/EplusmediaTv

photo content
+5

photo content
+9

KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media
+9
KUTOKA MITANDAONI Follow ukurasa wetu wa Threads👇 https://www.threads.net/@e_plus_media

H.Baba anadai Mtoto wake wa kike aitwaye Tanzanite aliyemzaa na Mwigizaji wa filamu Florah Mvungi anafanana na Irene Uwoya ambaye ni Mpenzi wake wa zamani. "Maswali yenu ya DM kunifatafata nimemuuliza na mimi huyu mtoto kwanini anafanana sana na Uwoya kila anavyokuwa ananishangaza. ntamuuliza mshikaji wangu Uwoya na kwanini Krish na Tanzanite wanataka kufanana hivi kuna nini hapa au duniani wawili wawili Asante UWOYA asante FLORAH huyu TANZANITE sijui au mimi nilibaki na chembe chembe za UWOYA kwanini hivi? Asante Mungu Nina mbegu kali za watoto wazuri sigawi mbegu hovyo tafadhali nimemzaa Uwoya uku tuongee ukweli huyu mtoto ni TANZANITE kweliii… " "Mwanangu umefanana sana na Uwoya au mimi naona vibaya mtanisamehe sana huyu(Tanzanite) ndie mtoto pekee alizaliwa na nyota yake ya kupendwa sio yakulazimisha Asante FLORAH huyu mtoto kanifundisha kitu inabidi nichunge sana mbegu zangu zina afya bora nakutengeneza watoto wazuri warefu. uuuu Kuna mtu kanuna kusikia hivyo atatukana ndio hivyo sijui nifanye biashara yakupandikiza mbegu kama unataka mtoto kama huyo unanilipa nakupa mbegu unapeleka uko naona kama bora nifanye hivyo au mnasemaje walimwengu? " - H.Baba, Msanii wa muziki. Ikumbukwe kwamba kipindi H.Baba anafanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Flava aliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Irene Uwoya mara baada tu ya kumaliza kushiriki Miss Tanzania kisha wakuachana. Baadaye H.Baba akafunga ndoa na Florah Mvungi aliyewahi pia kuwa Miss Pwani na kushiriki Miss Tanzania, walipata Watoto wawili akiwemo Tanzanite huyu anayedaiwa kufanana na Uwoya lakini ndoa yao ilivunjika. Hii si mara ya kwanza kwa H.Baba kuzungumzia Irene Uwoya kwenye mitandao ya kijamii na amekuwa akifanya hivyo mara nyingi lakini Uwoya hajawahi kuzungumzia wala kujibu chochote kile kuhusu H.Baba. Toa maoni

photo content

Diamond Platnumz akutana na Mdogo wake Alikiba, AbduKiba kwa mara nyingine tena.
Diamond Platnumz akutana na Mdogo wake Alikiba, AbduKiba kwa mara nyingine tena.

Mama Mzazi kasema ana miaka (12) ila Wanazengo hawataki kuamini 😂, Wastara Juma amefunguka hayo 👇 "Asbunalaahu waneeima li wakili MUNGU akulinde na hasadi za midomo mibaya na macho mabaya mrembo wangu mtoto wangu mim mlezi ni mimi niliyezaa ni mimi. kwa kuwasaidia tu na midomo yenu na macho yenu kama wachawi waliochelewa kuwanga nyie watu wachache wabaya fitna wenye midomo mibaya yenye harufu kama choo cha gest bubu MUNGU wasamehe tu maana mtoto hamjamuona miaka afu mnaanza kuhukumu kujiuliza na kujijibu wenyewe mzazi wa huyu binti ni Wastara Juma na Sajuki, kwa kuwasaidia wee fitna angalia picha no 2 na 3 no editing akiwa na miaka 11 ni mrefu kanizidi mim jee sasa miaka 12 unategemea anakuaje au mlitaka agande tu asikue but kumleta kwenu binti yangu ni kwa ajili kumwish na sio kufundishana mavazi mapicha umri na kumropokea mineno ya kise,... kwenye siku yake ya kuzaliwa na hamjui tofauti ya picha make up na editng wala no make up natural wengine waseme photolab sasa photolab sawa hiyo sura mnayoiona hapo ya baba zenu au acheni bana kusema watoto wa watu na kuwatia nuksi tu kwenye siku yake ya furaha wakati kuna wengine mnaocoment ujinga wakati mnaujua uchungu wa mtoto mlishamanuka hospital mkazaa kwa uchungu ukisema cha mwenzio fikiria na kwako kiukweli mim sipendi kuona mtu ananyoosha kidole kwa mtoto wangu yoyote ninachukia sana na ukinipitia karibu naweza kukufyonza damu huku nakuangalia usoni asante wenye kumuwish bint yangu kwa wema. asanteni pia nyie mnaropoka kama wachawi mliolishwa usembe leo nitawakera sana tu bado ndio nimeanza" - Wastara Juma, Mwigizaji wa filamu Tanzania. Ikumbukwe kwamba huyu Binti ndiye yule aliyemzaa na Juma Kilowoko maarufu Sajuki ambaye ni marehemu kwa sasa. Toa maoni

photo content